Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,590
- 8,726
Kama anamaanisha kweli aanze na kuilaumu Serikali ya Kikoloni!
Maendeleo ya Kilimanjaro hayajatokana na wakoloni Bali watu wake ....kumbuka hawa walikuwa na Native Gorverment " chagga council " ambayo ilikuwa na mandate kamili ha kuwaletea watu Maendeleo ...serikali ya mkoloni ilikuwa ikitoa allocations Kama serikali inavyofanya Sasa lakini tofauti "serikali " ya Kikimanjaro ilikuwa inaenda mbali zaidi kutoza Kodi kwenye mazao ....na kuweza kwa kutumia fedha zake yenyewe ..kujenga
Barabara za lami
Mifereji ya asili
Kuhudumia shule ( wanafunzi walipata chakula,madaftari,uniforms, bure kwa kutumia Kodi za kahawa ")
Kujenga Kasri Palace
Kujenga Legislative Assembly ( bunge ) la kisasa
Kuweka Mfumo Rasmi wa "mahakama"
Kuwa na walinzi wake
Kusomesha wanafunzi nje ya Nchi
Kujenga hotel Kati Ya kisasa kuliko zote wakati huo Afrika mashariki "kncu" ...pia ndio lift ya kwanza
Kujenga Chuo cha ushirika
Kujenga Kituo cha utafiti wa kahawa ..
Kujenga shule ya secondary ya Kisasa kuliko zote "lyamungo" ambayo ilikuwa kila chumba anakaa mwanafunzi mmoja au wawili ....na ilikuwa na facilities za kimataifa ikiwamo Bwawa la Kuogelea .
Kuwa na Akiba ya fedha za kigeni nje .....
Etc
Hayo yote yalifanywa na wananchi wenyewe kupitia Native Gorverment Kabla ya uhuru .....iweje Leo kuanza kuwaonea watu hawa kusema wanapendelewa?????????
Kilimanjaro ,Mji wake wa Moshi ilikuwa the same line as Nairobi Kabla ya Uhuru ........watu walikuwa wanatoka Nairobi Kuja kula raha moshi ....Native Gorverment ya Kilimanjaaro ilikuwa ni ya pili yenye nguvu Afrika mashariki baada ya Buganda ....iweje ionekane walipendelewa........zaidi wazee wengi wanaona MAENDELEO YA KILIMANJARO YAMESIMAMA AU KWENDA TARATIBU...KAMA YANGEENDA KWA KASI ILE BASI LEO HII SIJUI WATU WANGESEMAJE....
TAZAMA HATA MKOA WA TANGA HUU ULIKUWA MANISPAA KABLA HATA YA DAR ES SALAAM LAKINI NAO WAKASIMAMA .....NI LAZIMA TUWE WAKWELI