Zitto: Mkoa wa Kilimanjaro unapendelewa na Serikali

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Leo wakichangia mpango wa maendeleo wa miaka 5 baadhi ya wabunge akiwemo Zitto Kabwe,Amesema serikali imekuwa ikipendelea mkoa wa Kilimanjaro kwa miaka mingi na kuisahau baadhi ya mikoa mingine.

Zitto ameyasema hayo baada ya mbunge wa Rombo Joseph Selasini kuomba mwongozo kwa Chenge na kusema,Serekali inatoa tamko gani kwa hii tabia ya wabunge kuona mkoa wa Kilimanjaro unapendelewa?

Mwenyekiti wa bunge ameiagiza serikali itoe tamko juu ya suala hilo,Maana linaweza kuligawa taifa na kuleta mtafaruku.

Hivi mi najiulizaga,maendeleo ya Kilimanjaro ni ya asili au ni ya upendeleo?
 
Kama anamaanisha kweli aanze na kuilaumu Serikali ya Kikoloni!
 
Waziri Maghembe akabwa koo
BY SHARON SAUWA
25th April 2013
Email
Print

Waziri wa Maji, Profesa Jummanne Maghembe.
Wabunge wamempa wakati mgumu Waziri wa Maji, Profesa Jummanne Maghembe, baada ya kumtuhumu kuwa anajipendelea kutokana na kupeleka Sh. bilioni 32 katika miradi ya maji kwenye wilaya ya Mwanga anayotoka huku fedha za uchangia wa miradi ya maji katika vijiji 10 kwa kila halmashauri nchini ikitengewa Sh. bilioni 13 tu.

Aidha, Waziri huyo amebanwa na Mbunge wa Mwibara, Khangi Lugola (CCM), akitaka athibitishe ukweli wa taarifa alizosoma katika bajeti yake ya mwaka 2013/14 aliyoiwasilisha jana kwamba bomba lenye urefu wa kilometa 23.5 limetandazwa katika wilaya ya Bunda, mkoani Mara.

Hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iliyosomwa na Mbunge wa Viti Maalum, Cecilia Pareso, ilisema katika hotuba ya bajeti ya mji wa Same-Mwanga, mradi umetengewa Sh. bilioni 32 na kati ya fedha hizo, Sh. bilioni 20.6 ni fedha za ndani.

“Na katika miradi yote ya maendeleo ya mwaka huu ya maji hakuna mradi mwingine wowote ambao umetengewa kiasi kikubwa cha fedha za ndani, isipokuwa mradi wa kuboresha huduma za maji katika jiji la Dar es Salaam ulitengewa Sh. bilioni 43,” alisema Pareso.

Alisema kambi hiyo inataka kupata maelezo ya kina kama fedha zinaweza kutolewa wakati upembuzi yakinifu haujatolewa kwa miradi husika.

“Je, ni kwanini maeneo mengine yanashindwa kupatiwa fedha kwa kigezo kuwa upembuzi yakinifu bado mshauri hajakamilisha?” alihoji.

Alisema suala hilo linapaswa kutolewa maelezo ya kina ili kuondoa manung’uniko ya dhana ya upendeleo katika miradi ya maji na hasa huo ambao ni kwenye wilaya anayotoka Waziri Maghembe kutengewa fedha kabla ya upembuzi yakinifu kukamilika.

“Jambo hili ni hatari sana na hasa ikizingatiwa kuwa mradi huu haukuwa kwenye mpango wa bajeti wa mwaka 2012/2013, sasa leo fedha zinaondolewa kwenye miradi mingine na kurundikwa kwenye wilaya anayotoka Waziri wa Maji au ni nini kilipelekea mgawanyo huo wa fedha?” alihoji.
 
Kilimanjaro (hasa Uchagani)kweli ukienda kila barabara kubwa zinazoenda kwenye majimbo zina lami, pia kuna umeme kwa kitu kama 70% hivi, maji safi ni kama 80% hivi, zahanati na shule zipo karibia kila kijiji, japkua nyingi zimejengwa na wananchi wenyewe
lakini kitu cha ajabu kuliko vyote hawa ndio watu ambao hawaipendi CCM, eti haijfanya kitu miaka 50
 
Leo wakichangia mpango wa maendeleo wa miaka 5 baadhi ya wabunge akiwemo zitto kabwe,Amesema serekali imekuwa ikipendelea mkoa wa kilimanjaro kwa miaka mingi na kuisahau baadhi ya mikoa mingine.
Zitto ameyasema hayo baada ya mbunge wa Rombo Joseph selesini kuomba mwongozo kwa Chenge na kusema,Serekali inatoa tamko gani kwa hii tabia ya wabunge kuona mkoa wa Kilimanjaro unapendelewa?Mwenyekiti wa bunge ameiagiza serekali itoe tamko juu ya swala hilo,Maana linaweza kuligawa taifa na kuleta mtafaruku.
Hivi mi najiulizaga,maendeleo ya Kilimanjaro ni ya asili au ni ya upendeleo?
Hayo maneno hakuyasema Zitto,yamesemwa na mbunge wa viti maalumu kutoka CCM,ndipo Mh Selasini akaomba muongozo ambao ulitolewa na Chenge.Kimsingi Chenge alitoa ushauri kwamba serikali inajitahidi kuboresha huduma nchi nzima,hapo ndipo Mh Zitto alieleza namna ambavyo mkoa wa Kigoma upo nyuma na kumtaka Chenge asiwapake mafuta.Mwisho alisimama Mh J.Milya naye akaeleza jinsi Simanjiro ilivyonyuma.
 
huyo maghembe aliyewekwa kiti moto kwa upendeleo wa jimbo lake la mwanga, alipita kwenye ubunge wa jimbo lake wake kwa mbinde balaa, na kesi ipo mahakamani kua alilazimisha kutangazwa mshindi
 
real G,

..ungewalaumu wale ambao ccm haijawafanyia chochote lakini wanaipa kura asilimia 80 mpaka 90.
hawa ndio nawashangaa na mimi pia, wachaga ukizingua kidogo wanakupiga chini, hata kama uliwafanyia nini, Selasini pale Rombo wangemtema ila hawawezi kuchagua CCM ndio maana bado yupo,
 
Kilimanjaro kweli ukienda kila barabara kubwa zinazoenda kwenye majimbo zina lami, pia kuna umeme kwa kitu kama 70% hivi, maji safi ni kama 80% hivi, zahanati na shule zipo karibia kila kijiji, japkua nyingi zimejengwa na wananchi wenyewe
lakini kitu cha ajabu kuliko vyote hawa ndio watu ambao hawaipendi CCM, eti haijfanya kitu miaka 50
Umesema asilimia kubwa ya maendeleo ni wao wenyewe...hivi kuna maendeleo bila elimu? Basi kumbe maendeleo hayo ni juhudi ZAO.
wengine igeni basi.sisiemu haijawahi leta maendeleo sehemu yoyote nchu hii toka Uhuru.
 
Umesema asilimia kubwa ya maendeleo ni wao wenyewe...hivi kuna maendeleo bila elimu? Basi kumbe maendeleo hayo ni juhudi ZAO.
wengine igeni basi.sisiemu haijawahi leta maendeleo sehemu yoyote nchu hii toka Uhuru.
ila umeme, maji na barabara, waishukuru serikali
 
na wana bidii sana.imeandikwa mkono wa mwenye bidii utafanikiwa.
Nakumbuka miaka ya nyuma sana sehem nyingi zikiwa hazina umeme nikienda kilimanjaro Mwanga Usangi Ugweno nakuta umeme ni milimani sana 90s sasa kwanini mkoa usiendelee" waige mfano waache kulalamika lalamika hakuna upendeleo ni kupenda kwenu tu.
 
hawa ndio nawashangaa na mimi pia, wachaga ukizingua kidogo wanakupiga chini, hata kama uliwafanyia nini, Selasini pale Rombo wangemtema ila hawawezi kuchagua CCM ndio maana bado yupo,

..kitu kingine ni MOBILITY ya wananchi wa maeneo mbalimbali ya Tz.

..Wachaga wanaongoza kwa kuhama Kilimanjaro kwenda kutafuta fursa maeneo mengine ya Tz.

..sasa watu wanalalamika kuwa Wachaga wanapendelewa, wakati Wachaga wenyewe wanakimbia Kilimanjaro.

..kuna haja ya kubadili mentality ya wa-Tz. Kama eneo unaloishi halina fursa au serikali imesahau kupelekea maendeleo basi ni vizuri mtu akahama kwenda kuishi kule kwenye huduma nzuri.

..Chukulia mfano Marekani. Obama amezaliwa Hawaii, amesoma New York, amekwenda kufanya kazi Chicago/Illinois. Alipokuwa anagombea Uraisi alikuwa anajulikana kama the junior senator frm Illinois.
 
Back
Top Bottom