Zitto Kabwe: Bajeti haijajibu changamoto za watu

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
ACT Wazalendo wamefanya uchambuzi wa Bajeti Kuu iliyosomwa siku ya Alhamisi June 15, 2023, uchambuzi uliowasilishwa na Msemaji wa Sekta ya Fedha na Uchumi ACT Wazalendo Esther Thomas na Naibu wake Juma Hamad jana tarehe Juni 17, 2023.

Wakati akihitimisha zoezi hilo Zitto Kabwe alisema hayo ndio maelezo yao kuwa, Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2023/2024 haijajibu changamoto za watu badala yake imetoa unafuu mkubwa kwa watu wenye uwezo (vibopa), imetoa unafuu mkubwa sana kwa watu wa sekta binafsi, wafanyabiashara na kuwaacha watu wa kawaida (wanyonge), akihaidi kuwa wataendelea kupigia kalele bajeti hii ilenge kuwanufaisha wanachi wote.

Kubwa zaidi kwenye uchambuzi huu wa Bajeti Kuu ya Serikali, ACT wametoa jibu la namna gani ya kutatua tatizo la Bima ya Afya kwa Wote kwa kupitia mfumo wa hifadhi ya jamii.

Hili litafanywa kwa kutenga 2% ya pato la taifa la sasa kugharamia hifahi ya jamii, itakayowezesha kila Mtanzania kuwa na bima ya afya kwa wote, bima ambayo siyo ya vifurushi wala matabaka, bima ambayo utalipa kulingana na uwezo wako wa kipato lakini utapata huduma kulingana na mahitaji yako, tofauti na ilivyo sasa unalipa kutokana na kipato chako na unapata huduma kutokana na kipato chako.

Pia ACT wametoa pendekezo kwa magari yote yanayotumika kwa shughuli za Serikali kufungwa matenki ya gesi ya asilia (Compressed Natural Gas) ili kupunguza matumizi ya mafuta, ambapo itasaidia kupunguza kiwango cha mafuta yanayoagizwa kutoka nje, lakini pia itapunguza gharama za serikali zinazotumiwa katika kuagiza mafuta ambapo serikali itaokoa kiasi cha fedha cha Tsh. Bilioni 500 ambacho ni kiasi cha fedha kinachohitajika kuwekeza MSD ili kuwa na mtaji utakaowezesha kuagiza dawa kwa ajili ya Watanzania.

Mwisho Zitto atoa wito kwa Rais Samia kuwa mfano, kwa kuhakikisha gari zake zinafungwa matenki ya CNG (gesi asilia), ambako yeye akianza hakuna mtu nchini achaacha kufata.

 
Hakuna bajeti itajibu changamoto zetu kamwe na sababu kubwa ni kuwa walipa kodi ni wachache sana.
Siku ikifika walipakodi sajiliwa ni 10mil hapo ndio angalau, ila kwa walipakodi 4mil na wenye TIN 1.8 hapo tusahau
 
Back
Top Bottom