Zitto kuaga wabunge wenzake leo - Machi 19, 2015

Zitto kuaga wabunge wenzake leo - Machi 19, 2015

Status
Not open for further replies.
Zzk Ndio mwenye Akili timamu na mwenye kupambanua mambo ndani ya chadema yote. Walio baki ni mbulula tuu hasa wale viongozi Wa juu ni wachumia tumbo
Angalia itakavyo polomoka kwenye uchaguzi ujao na hamta amini

Sasa CHADEMA ikiporomoka si raha yenu.

Shida iko wapi

Tuacheni CHADEMA tulivyo....Hiki chama watu wamekufa kwa kukipigania leo wapuuzi wachache walete upuuzi wao na tuwanyamazie...Big No
 
nam dedicate wimbo wa you can hate me now By Nass ,no turning back
 
tutaondoka wengi tu hili limefanywa kwa chuki tu hakuna sababu za kumfukuza zitto.tunajua ni chuki dhidi yake Kwa sababu ana upeo mkubwa na ushawishi kushinda viongozi.na mlijua suala hili lingepelekwa baraza kuu zitto angewapiga chini mmeamua kutumia ubabe.hii haikubaliki hata kidogo.nasema chedema tutaondoka wengi Zitto usijali tuko na wewe mpaka mwisho.

Mkuu tupo pamoja..Hatuwezi kukubali kushiriki dhambi hii.
 
ZZK mpaka jana alikuwa hajapewa barua na chama kwa kufukuzwa kwake ( kwa mjibu speaker). Katibu mkuu alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa utaratibu wa kufukuzwa kwa zzk kilikuwa s kipaumbele cha chama kwa wakati huu....bila shaka kulikuwa na utaratibu wa kufuatwa..probably na hicho kikao unachosema. Kabla ya barua hiyo kutoka zzk anatangazs kuaga wabunge wezake! Hii ni kama si zzk kufuata ratiba zake ili ajoin act before 28/03 election?

Ongeza na zako....hii ndo siasa. Fuata mnaotaka kumfuata. Chadema iko imala kuelekea Oct na dola tunachukua.

ipo imara.
ZZK na LOWASSA ndio wakuu wa ACT
 
Kama Kijana Zitto Leo anawaaga Wabunge Wenzie,akisimama kuongea akumbuke ushauri mwema kwake kuwa Sasa ni muda wa yeye kuweka siasa pembeni na kwenda chini kabisa kuanza kujifunza Mama Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano.Zitto kama atajifunza kwenda ngazi ya chini ya kuanza kujifunza HOW MAMA TANZANIA WORKS, basi miaka mitano ijayo yan 2020/25 basi atakuwa na ufahamu mzuri sana na wenye ufahamu yakinifu wenye nidhamu, uzalendo, werevu, subira, usikivu na hata ujitambuzi binafsi wa kumenage stress na kuepuka mihemuko na jaziba hasa anapokutana na changamoto zinazohitaji maamuzi yenye utulivu zaidi na si mihemuko na bashasha.

Ni muda sasa kama kweli anataka kuwa Zitto wa Manufaa Kwa Taifa, ni muda wa kwenda nje ya siasa na kukaa daraja la kawaida la maisha ya Watanzania ambako kutampa fursa ya kuwa Mchezaji aliyekaa jukwaa la Watazamaji Uwanja wa Taifa huku akiangalia Timu ambazo alipata kuzichezea [Political Parties] zikimenyana na yeye kupima na Kutathimini [Evaluation & Analysis] juu ya kinachoendelea katika ujenzi wa Taifa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Its a time for Zitto to have a stake in having his own Estate in Building the so called Tanzania outside politics. Ujenzi wa Taifa kupitia uzio nje ya sura ya siasa ni mgumu sana na muhimu sana kwa mtu mwenye kuipenda kweli Tanzania.So on your Mark!!!! Get Ready!!!! Paaa Huku nyuma sahau vyombo vya HABARI acha kabisa vijembe na kwa kuwa ni kizazi cha dotcom basi kwenye FB yako ni wakati mwafaka wa kuachana na posts za kisiasa na tuanze kuona michango yenye HAIBA ya ukomavu wa Intellegent person na sio Zitto Mwanasiasa.

Ukisikia habari za wanasiasa zipe kisogo subilia Kuevaluate na Analysis. Utajifunza mengi na utafunguka mengi kiasi kuwa utaona aibu kwa yale ambayo wewe uliyoyafanya, kwa hiari yako , au pasipo kujua kuwa umechezeshwa kucheza mziki wa wachagua wimbo....kama kweli unatoka huko utakuwa umesogea hatua kubwa sana.Ila Go and shut Up...Zitto na kama bado uko kwenye ulingo wa siasa kwa 2015/2020 basi Kwisheny Forever...Gone Gone Forever Katika Ulimwengu wa Siasa Za Tanzania na hata wale wa dilisha la mwisho jicho la Taifa nao Watakutupa Pia.

Acha kuropoka na hizi kauli zako uzitunze vizuri itakuja kuyakumbuka maneno yako haya kama ni yasingi mda huu
 
mkuu tupo pamoja..hatuwezi kukubali kushiriki dhambi hii.

tutaondoka wengi tu hili limefanywa kwa chuki tu hakuna sababu za kumfukuza zitto.tunajua ni chuki dhidi yake kwa sababu ana upeo mkubwa na ushawishi kushinda viongozi.na mlijua suala hili lingepelekwa baraza kuu zitto angewapiga chini mmeamua kutumia ubabe.hii haikubaliki hata kidogo.nasema chedema tutaondoka wengi zitto usijali tuko na wewe mpaka mwisho.

mtamfuata zzk nyinyi na waume zenyu pekeeenu
 
mi nadhani kwa kuwa zitto ni mwanasiasa ambaye CCM wamempenda sana kwa nini wasimchukue. inapotokea Yanga ikamfukuza mchezaji kwa madai kuwa anahujumu Team kwa kupeleka mbinu za ushindi kwa team pinzani na kusababisha team kupoteza ushindi halafu Simba wakaja kumtetea kuwa Yanga wanafanya kosa sana kumfukuza wangebaki naye tu hapo inaleta mashaka. mi nadhan kama ni mchezaji mzuri Simba wamchukue kimya kimya awe wao na pia wamfanye awe kapteni wa team yao au kama ni Kipa basi adakie team yao. mi sina tatizo na zitto. katiba ya CDM inasemaje tujiulize? lakini pia hii inaonesha kuwa hakuna aliye mkuu kuliko chama CCM walianzisha suala la kuvuana gamba.. wakatishiana nyau na sasa bado wapo. ok waliwahi afukuza akina Kolimba, Kombe, Daud Balali na Malima. watu wamesahau.... sana kuwa hawa pia walifukuzwa kwa namna yao na CCM ambayo hiyo ndiyo inayotumika CCM . mi nashauri CCM wamchukue Zitto na pia wafurahie maana kama CDM imepoteza mtu mzuri basi ni faida kwao. waache kuajiri watu wa kujifanya wanampenda zitto ili kumpa kichwa na yule bwana kwa kutochanganya na za kwake anajikuta anajiharibia future yake. Zitto hawez kuwa Rais kwa Hulka yake mi nawaambia. atabaki kuwa mwanasiasa wa kwenye JF, FAcebook, TWITTER na Vijiwen. anaweza kuwa anajua kujenga hoja lakini Hekima za uuongozi hana kuwa kiongozi sikujenga hoja mbna mi nawafahamu watu wabishi sana laini hawawezi kuongoza hata kidogo. Tundu Lissu ni mtu mwenye akili na mwenye uwezo mkubwa sana katika sheria na kujenga hoja lakini HAwezi kuwa Rais, Prof Lipumba ni Msomi mzuri wa Uchumi lakin he will never be a president. haya mambo yapo tunaye Rais ambaye kichwan is mzuri lakini ndo Rais.

mkuu upo right kabisa, nakupa Heko.
 
sheria ndio imemvua zitto uanachama sio mh.Lissu! Zitto alishafuatiliwa sana ndio maana w
chama kikafikia uamuzi huo

mbona mitaa tunakaa na majizi na mijambazi mingi tu tunalolifanya ni kwamba unaishi nalo kiakili unless otherwise umikosea au kulichomea police police wataliambia nani amechoma hv balaa kukuangukia /walipaswa kuishi nae kiakili tu ndani ya cdm
 
Hapo ndipo unapoujua unafiki wa Zitto,anaaga wabunge wenzake kwani lini alipewa barua ya kumfukuza Chadema??ni lini alipambiwa na bunge siyo mbunge?? ni lini barua ya tume ya uchaguzi ilienda bungeni kutoa taarifa Zitto siyo mbunge tenaa?? Hapo ndipo utajua Ziotto kwenye kila anlofanya anatafuta huruma ya watanzania,amepiga hesabu zake na kuona hawezi kwenda kugombea ACT akiwa bado mwanachama wa Chadema ameamua kujifanya kuachia ili aweze kwenda ACT. Kweli heri mchawi kuliko mnafiki'
 
mbona mitaa tunakaa na majizi na mijambazi mingi tu tunalolifanya ni kwamba unaishi nalo kiakili unless otherwise umikosea au kulichomea police police wataliambia nani amechoma hv balaa kukuangukia /walipaswa kuishi nae kiakili tu ndani ya cdm

Kuishi naye ki akili? kumbuka binadamu mwenzao yule, bora wajeruhike waanze upya kuliko kuishi na nyoka mwenye sumu huku nje akijitanabali ni kondoo mpole!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom