Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 52,737
- 165,199
Taarifa zilizosambaa bungeni ni kuwa, mbunge wa Kigoma kaskazini, Zitto Kabwe anakusudia kuaga wabunge wenzake leo.
Taarifa zinasema Zitto alitaka kufanya hivyo kabla ya kukabidhiwa barua na chama chake tangu siku ya jana ila alitulizwa na spika Makinda.
Pia,gazeti la Nipashe linaripoti kuwa siku 8 zamsubiri zito ACT.
===================
Chanzo:Mtanzania
Taarifa zinasema Zitto alitaka kufanya hivyo kabla ya kukabidhiwa barua na chama chake tangu siku ya jana ila alitulizwa na spika Makinda.
Pia,gazeti la Nipashe linaripoti kuwa siku 8 zamsubiri zito ACT.
===================
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), leo anatarajiwa kuaga rasmi bungeni na kujiuzulu nafasi yake ya ubunge.
Uamuzi huo wa Zitto umekuja baada ya kuwa katika mkakati wa muda mrefu wa kuondoka kwa heshima ndani ya Bunge ambapo ameitumikia nafasi ya ubunge kwa vipindi viwili.
Juma lililopita, Zitto aliwaaga wananchi wa jimbo lake kuwa hatagombea tena ubunge, akisema ataendelea kuwatumikia akiwa sehemu nyingine.
Jana, baada ya kuahirishwa kwa Bunge, mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, alikuwa na mazungumzo ya muda mrefu na Spika wa Bunge, Anne Makinda. Mazungumzo yao hadi sasa hayajajulikana.
Zitto, alisema ataongea leo jioni kabla ya kuahirishwa kwa Bunge na kuweka msimamo wake juu ya kinachoendelea kuhusu ubunge wake.
"Aliyekwambia hajakosea, nimeishi na watu vizuri siwezi kuondoka tu bila kufanya consultations (kushauriana), nimefanya consultation kwa kuzungumza na Spika wa sasa, Spika aliyepita waziri mkuu wa sasa na waziri mkuu aliyepita.
"… Mzee Said Arfi Makamu Mwenyekiti mstaafu wa Chadema na washauri wangu wa karibu, nitaongea leo jioni kabla ya Bunge kuahirishwa na kuweka wazi msimamo wangu wa kinachoendelea kuhusu ubunge wangu," alisema Zitto.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili hivi karibuni, Zitto alisema hatima yake ya kisiasa baada ya kutimuliwa Chadema itajulikana juma hili.
"Ni nini kinachokuja baada ya hapo tutakijua vizuri wiki ijayo (wiki hii). Hatujajua kama Chadema wameandika barua kwa Spika ili kutangaza kuwa jimbo liko wazi, kama wameandika tutakaa kujua ni nini cha kufanya," alisema.
Kuhusu kuhamia chama cha ACT, Zitto alisema: "Tusitake kuvuka daraja kabla ya kufika sehemu ya kuvukia, tusubiri muda ufike."
Machi 10, mwaka huu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kilitangaza kumvua rasmi uanachama Zitto.
Hatua hiyo ya Chadema ilikuja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutupa kesi iliyofunguliwa na Zitto dhidi ya Bodi ya Udhamini ya chama hicho na Katibu wake, Dk. Willibrod Slaa.
Kesi hiyo ilitupwa na Jaji Richard Mziray baada ya kupitia hoja za mapingamizi matano yaliyowasilishwa na mawakili wa Chadema.
Baada ya kutolewa kwa uamuzi huo wa mahakama, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, alizungumza na waandishi wa habari na kusema tangu Zitto alipokishtaki chama hicho mahakamani, kwa mujibu wa kanuni na maadili ya viongozi wa chama hicho, alishajifukuzisha uanachama.
"Kwa mujibu wa kanuni zinazohusu maadili ya viongozi ya chama chetu, kanuni ya 10 inaeleza kuwa pale mwanachama anapokishtaki chama mahakamani, anakuwa amejifukuzisha uanachama," alisema Lissu.
Kutokana na hali hiyo, Lissu alisema tangu walipowachukulia hatua aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na Mjumbe wa Kamati Kuu, Profesa Kitila Mkumbo, walishamalizana na Zitto bali kilichokuwa kimebaki ni kusubiri uamuzi wa mahakama.
Alisema kwa mujibu wa Katiba ya chama chao, Kanuni ya Maadili ya Wabunge na Madiwani, Zitto si mwanachama wa Chadema na wala si mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Chanzo:Mtanzania