Zitto katoa wapi pesa za kufanya 'private investigation' Uswisi?

Zitto katoa wapi pesa za kufanya 'private investigation' Uswisi?

WEzi wachukuliwe hatua kwanza...halafu ndo tutafute majibu ya maswali hayo!!
"End justifies the means"
 
Kwa mujibu wa maelezo ya Zitto kutoka Star TV;
5 & 6 amesema Uswisi ni moja kati ya nchi zinazotoa misaada kwa Tanzania kwahiyo serikali waongee nao wawasaidie katika hili, pia ikiwezekana kuwa na mkataba wa transparency kati ya nchi hizi mbili ili taarifa ziwe wazi.

Zitto anaishi dunia gani?

Uswisi ni mmoja katii ya nchi zilizokuwa zinatoa msaada Kenya, je walirudisha kiasi gani kati ya 10 billion USD alizoiba Moi wa Kenya?

Nigeria ambayo civil society yake ni more active na rigorous kuliko hawa wazugaji wetu walifuatilia weee zile pesa zilizochukuliwa na Abacha lakini hakuna hata senti moja ya maana iliyo rejeshwa.


Je mmesahau pesa za RADA serikali ya UK ilivyotusumbua kuzirejesha?

Zitto anazungumzia transparency lakini ilitakiwa awe transparent kwanza kuhusu huu mpango wake kwa kujibu maswali:

a) Je kuna sheria gani imekiukwa na watanzania kufungua akaunti Uswisi na kwingineko?

b) Je ana uthibitisho gani kuonyesha kuwa walio na akaunti uswisi waliziiba toka kwa umma?

c) Je akiwataja watu majina na wengine wakawa hawana hatia atatoa wapi pesa za kuwalipa wakimshitaki?

d) Je tatizo lake ni watu kuwa na akaunti uswisi au kutolipa kodi Tanzania au vipi? Inabidi Zitto awe clear na objective yake hapa.

13 &14 amesema kisheria mtu yeyote akihitaji kuhifadhi au kuhamisha fedha nje lazima awe na kibali cha gavana na kwa kuanzia BOT itoe list ya hao waliopewa vibali kufungua akaunti nje.

Hii si kweli, mimi wakati nasoma Uganda nilifungua akaunti kule bila kibali cha BOT, na suala la kuhamisha pesa si lazima mtu atumie local banks kufanya hivyo. Unless Zitto anazungumzia kitu kingine tusichokijua. Ndio maana nataka nione hiyo video ya interview yake kwani inaweza kutumika baadae kwenye ushahidi.
21 amesema traces zote zitapatikana kuanzia pale mchakato ulipoanzia (yani BOT) kwenda kwenye hizo akaunti na hata zikihamishwa itaonekana zilipoelekea japo amesema kazi haitakuwa rahisi ila watanzania wasipende mambo marahisi.

If this is the case ataona trace BOT na sidhani kama BOT wanaweza kutoa hizo taarifa bila kuagizwa na legal authority kama mahakama. Pia hata kama pesa zilionekana zimetoka Zitto ataona pesa za akina Bakhressa, Mengi, Mo Dewji, Zakaria, OILCOM na wengineo ambao wanazo kila haki ya kufungua akaunti kokote kule wanakopenda duniani. So kuwa na paper trail toka BOT haimaanishi anything in this case.
at the end of the day yeye ndiye ameleta allegation sasa burden of proof iko kwake yeye alete ushaidi.
25 amesema ajenda hii sio yake kama Zitto yeye katumika tu kuiwakilisha kwasababu yupo kwenye nafasi ya kutumia platform ya bunge, kuna vijana wakitanzania ambao ni waandishi wa habari za kichunguzi wenye connections Uswisi Joburg na kwingineko, pia wabunge wa ndani na nchi nyingine ndio wameshirikiana katika hili sakata

Zitto is deluded na anaishi kwenye dunia ya kufikirika kama anategemea hawa waandishi wetu na media uchwara ya Tanzania kama wanazo akili na resources za kufuatilia pesa Uswisi. Kufuatilia mambo madogo madogo hapa Tanzania wanashindwa ndio wawe na hiyo akili ya investigative journalism? TSJ inatutolea ma graduates ambao wamepata marks za GOOGLE & WIKIPEDIA media owners tulio nao hawana tofauti sana na shigongo ambaye walau naweza kusema yeye anajijua anataka nini.

Mfano Editor in chief wa Tanzania Daima hajui mji wa DAVOS uko wapi sasa kweli kuna safari ya kwenda Geneva hapo?
Ukweli ni kuwa mtandao wa JAMIIFORUMS unafanya more for online media in Tanzania kuliko media houses zote Tanzania. That's a fact.

Kama majibu ya Zitto ni haya then kashafeli kwa sababu mleta hoja aliuliza maswali very technical na naona majibu ya Zitto yamekuwa too simplistic.

Nimejaribu kupitia mtandao wake LAKINI nimeshangaa mpaka sasa haja upload hiyo interview yake kule star TV

as I type naendelea ku search on you tube inawezekana anayo YOUTUBE CHANNEL ambayo assistants wake wamepost videos and video blogs zake ili niiitazame kwa undani zaidi.
 
Mkuu George Smiley nimejitahidi kuwakilisha nilichokisikia, kama ulivyosema ni vizuri ukapata hiyo video umsikie mwenyewe moja kwa moja.

Pia alisema kwa sasa tumuacha mwanasheria mkuu na kikosi kazi alichounda wafanye kazi yao mpaka April mwakani watakapokabidhi comprehensive report
 
Last edited by a moderator:
Sasa sidhani kama Zitto ataelewa maana ya hii picha au alisoma historia yake. Jinsi ilivyo ikifika Easter mwakani tutajua kama anasoma vitabu na kuelewa au na yeye anataka kuwa na library kubwa ya vitabu kama swahiba yake.

trojan-horse2.jpg

Kwakweli anaweza asiikumbuke (kama aliwahi kukutana nayo) !!! Huyo ni TROJAN HORSE........

Tukiitafsiri kwa kiswahili chetu; ni sawa na kusema KIKULACHO KINGUONI MWAKO.....(ni tasfisi yangu kwa upeo wangu mdogo)
 
Kwakweli anaweza asiikumbuke (kama aliwahi kukutana nayo) !!! Huyo ni TROJAN HORSE........

Tukiitafsiri kwa kiswahili chetu; ni sawa na kusema KIKULACHO KINGUONI MWAKO.....(ni tasfisi yangu kwa upeo wangu mdogo)

Trojans walilichukua hilo dude (horse) ikiwa kama ishara ya ushindi wa vita dhidi ya wagiriki na kuliingiza kwenye mji wao. Usiku jamaa waliokuwa ndani wakatoka na kufanya madhara makubwa sana na ikawa ndio mwisho wa vita iliyodumu kwa mda mrefu.

kama nimemsoma vizuri mtoa mada ana maana unaweza chukua kitu kama ushindi kumbe ni mbinu ya adui kupata access flani ambayo baadaye atakuja kukuletea (wewe au chama) anguko kuu..
 
Mkuu George Smiley nimejitahidi kuwakilisha nilichokisikia, kama ulivyosema ni vizuri ukapata hiyo video umsikie mwenyewe moja kwa moja.

Pia alisema kwa sasa tumuacha mwanasheria mkuu na kikosi kazi alichounda wafanye kazi yao mpaka April mwakani watakapokabidhi comprehensive report

1. Interestingly kaambiwa itabidi na yeye awe mjumbe wa hiyo task force

2. Ile estimate yangu ya awali kuwa by Easter tutaona mengi naona ilikuwa close..give or take April report ikiwa tayari magogoni wataikalia na kuondoa vya kuondoa then watawapa watu report ya diluted version by then itakuwa ni August...na kama ujuavyo a week in politics can be very long lakini 6 months?

well...bado nasubiri ripoti ya majina ya MWEMBE YANGA na majina ya WAUZA UNGA na bila kusahau zinginezo zilizotayarishwa mwaka huu.
 
  • Thanks
Reactions: KXY
More than a million bucks(usd)lol!

Duh!We ni mfukunyuzi!

Hiyo picha umeitoa wapi?Yuko na nani hapo kushoto kwake?,Maana niliowatambuwa hapo ni Lady Jay D,huyo mdada mwingine looks familiar lakini simjui.

Pia kitabu alichonacho ndugu Zitto ni cha Russel Simmons kinachoitwa "Super Rich",haya bana,miye siwawezi nyie.Nadhani ndugu Zitto anapenda kujisomea kama alivyowahi kusema.

Kwamba anataka kuwa super rich akiwa kiongozi...Mhn ,mhn mhn...Kaazi kweli kweli!Viongozi wa nchi masikini bana!
e2.jpg

BTW hicho kitabu aliweka kama mbwembwe ama kitu gani?Maana mkuu huwa ana act very humble humu!Ama ni super rich?CTFU!

Matatizo ya watu kudandia mambo wasiyoyajua, sasa mtu aliyeileta hii picha inahusikaje kwenye uzi huu?
Well, kwa ajili JF imegeuka jukwaa la kupiga soga basi ngoja niwasaidie kama hivi:
Kushoto ni madam Ritta, kulia ni Maria Sarungi na Lady JD
Hiyo ilikuwa ni siku ya jumamosi tarehe 1 Dec kwenye Red Ribbon Fashion Galla pale Serena Hotel, na hicho kitabu mnachokipigia kelele kilikuwa kinanadiwa na Mhe. Zitto alifanikiwa kukinunua kwenye mnada ule ambao madhumuni yake ni kusaidia watoto yatima waathirika wanaolelewa na Tanzania Mitindo house.
Hii picha itakuwa imetolewa kwenye blog ya michuzi
 
Kazitoa Uswisi

Mzee katika suala la ulinzi shirikishi (rejea IGP Mwema) hoja ya msingi mtu anatumia vipi nafasi yake kudhibiti uhalifu au kusaidiana na dola kukomesha uhalifu. Kipaumbele si maswali kwamba amepata wapi maguvu mithili ya baunsa hadi kukamata mhalifu wa miraba minne. Au unajiuliza amekula ugali mkubwa kiasi gani hadi akamate mhalifu baunsa. Mission ni kukamata kwanza mhalifu mengine baadaye.
 
Kazi ipo kwa watanzania kwa kutetea wizi hawajui kitu chenye faida kwao
 
Moi wa Kenya aliiba zaidi ya 10 billion wazungu walirudisha kiasi gani?

Abacha wa Nigeria aliiba 4 billion usd je wazungu walirudisha kiasi gani ya hicho?

Mubutu pesa alizoiba Zaire wazungu walirudisha kiasi gani?
Nilisema hayo kwasababu ulisema ni muhimu kuzuia ndani,nikasema kuzuia ndani hakuwezekani kama hawatatajwa na kuwa held responsible,so sijui tunapishana wapi?
 
na hicho kitabu mnachokipigia kelele kilikuwa kinanadiwa na Mhe. Zitto alifanikiwa kukinunua kwenye mnada ule ambao madhumuni yake ni kusaidia watoto yatima waathirika wanaolelewa na Tanzania Mitindo house.
Kitabu gani kimepigiwa kelele?
 
That is POLITICAL BEHAVIOR hivyo baadhi yetu tunaojitambua huwa hatudanganywi
 
Jambo lipi la maana na lipi sio la maana ni relative, na kila mtu ana tafsiri yake kutokana na uelewa wa ni lipi ni jambo la maana na lipi sio la maana, wewe umetumia kigezo gani kuita hoja ya mtoa mada ya kipumbavu? Unajuaje kama anajua zaidi ya unavyojua kwamba labda Bw. Zito Kabwe haya yote anayoyafanya ni show tu? unauhakika gani na hilo mpaka uiite hoja yake ni ya kipumbavu?

Je kesho ukija kusikia kwamba Bw. Zito Kabwe naye anaakaunti huko Uswisi na hayo yote alikuwa anafanya ili kupoteza ushahidi ambao labda ungemfunga yeye mwenyewe bado utaita hoja ya mtoa mada ya kipumbavu?

Nataka tu kuweka sawa hapo kwenye kuiita hoja hoja ya mwingine ya kipumbavu!

well said

zitto naye ana vijisenti huko lakini mbio zake si kwa ajili ya kujiokoa yeye tu lakini uwezekano upo kuwa anataka kuficha baadhi waliomtuma...political game...watz mtakaa kuchezewa mpaka lini...tangu jambo hili limeanza hatuoni tu..hatufungui macho
 
Support aliyonayo Zitto ni Kubwa mno, wazee wengi ndani ya ccm wanampa moral and material support. Inakuumiza sana, kuona ameling'ang'ania hili. Mengi mno yanakuja. Biblia inasema"...niombe nami nitakuonesha mambo magumu usiyoyajua."
Mikesha ya watakatifu ya kila Desemba 31 imeanza kutoa majibu. Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka , Mungu wa Yakobo akiombwa anajibu. Farao alijaribu kuzuia mpango wa Mungu aliishia kupigwa. Hayo ndiyo yanaenda kutokea TZ.
Kilio cha watanzania kimefika mbinguni, na Mungu, BWANA wa Majeshi amejibu! HALELUYAAAAA! Kwa Jina la Yesu wa Nazareti watanzania wanatoka vifungoni mwa waabudu mizimu, watambikao, wanaoutambikia mwenge wa uhuru.
 
Moi wa Kenya aliiba zaidi ya 10 billion wazungu walirudisha kiasi gani?

Abacha wa Nigeria aliiba 4 billion usd je wazungu walirudisha kiasi gani ya hicho?

Mubutu pesa alizoiba Zaire wazungu walirudisha kiasi gani?
Its just the matter of time,huwa zinarudishwa...
The case of frozen funds linked to former Nigerian dictator Sani Abacha took Switzerland five years to return the money to Nigeria.
Swiss gov't bares $1B frozen funds from Arab Spring countries | GantDaily.com

Hata pesa za Mobutu ilikuwa the same,kinachotakiwa ni Taifa kudai na kupeleka ushahidi kuwa pesa zilizowekwa huko zilipatikana kinyume na maadili.

Na kama muda mwingi ukipita bila ya serikali husika kudai, huwa wanazirudisha kwa wanafamilia wao.

So nashangazwa sana na wasiwasi wako mkuu.
 
Nyie zungumze mambo yote yale. Lakini mimi nina wivu, itakuwaje Zitto awe sandwiched na warembo kwenye hiyo picha?
 
Nyie zungumze mambo yote yale. Lakini mimi nina wivu, itakuwaje Zitto awe sandwiched na warembo kwenye hiyo picha?
He's single,powerful,and he's got money,whats up with you?!lol!
 
Back
Top Bottom