Zitto katoa wapi pesa za kufanya 'private investigation' Uswisi?

Zitto katoa wapi pesa za kufanya 'private investigation' Uswisi?

Kwenye hili sakata Zitto ni"remote cotrol" tena sio "universal" aliyeshikilia ya television na dvd player ni watu tofauti.

Wakishindwa kwenye hili lazima 2015 watimuliwe vumbi.Watajuta kwanini wamekuwa wanaendekeza siasa za "kuuma na kupuliza"
 
Kufanya utafiti wa wizi kama huu wa viongozi wetu si lazima uwe na pesa. Unaweza kuwa na watu ndani ya benki ima Uswisi au hapa nyumbani ambao wanajua mambo ya wakubwa wakukupa habari. Hii inaweza kusababishwa ima na uzalendo wao au kutaka kuwakomoa kutokana na sababu wanazojua. Mfano mdogo ni jinsi wizi unavyofichuliwa kwenye idara na wizara serikalini. Magazeti yanayojua kazi ya uchunguzi ima hujenga urafiki na watendaji makini au wenye kuyashabikia kwenye taasisi au kununua hata habari toka kwa watu wadogo wanaoona madudu yanayotendeka. Mfano, wafagiaji wengi kwenye maofisi ya mawaziri wanaweza kuwa source nzuri. Madereva wao hata marafiki kuanzia nyumba ndogo hata washirika. Namna nyingine ya kupata habari ni kuzipata toka usalama wa taifa. Kwa wataalamu wa masuala ya usalama na upelelezi, kuna njia nyingi zisizo hata hitaji pesa. Hivyo Zitto kwa nafasi yake anaweza kupata taarifa muhimu kuhusiana na hao majambazi. Yeye si kichaa kusema atajaribu kuibua majina. Muhimu ni kuweka nukta na kumkumbusha pale atakapoonekana kutotaja majina.
 
Hata ya EPA, maswali ya hivi yaliletwa, baadaye ikagundulika kuwa ni ukweli.

Pamoja na methodology, na gharama alizotumia, suala la msingi ni kuwa aliyosema ni ya kweli au si ya kweli.

Nafurahi kuwa mwanasheria mkuu ameunda kikosi kazi kinachoshirikisha Usalama wa Taifa na Interpol kuhakiki ukweli wa madai ya Zito. Hilo ndilo la muhimu.

zanzibar huru, ukijua ametoa wapi pesa, ukweli wa madai utaupeleka wapi?

Hilo la mwanasheria mkuu kuunda kikosikazi huna haja ya kushukuru , unayakumbuka ya Mwanyika na Hosea kwenye Richmond ?
 
37.jpg
Kutinga kwenye mambo kama haya na "Super Rich" ni ushamba wa hali ya juu hakuna tofauti na wale wanaokwenda disco na Ipad
 
Mjamaa wa kweli ni yule ambaye yupo tayari kuitu,ikia nchi yake kadri awezavyo kwa manufaa ya wananchi wa nchi yake pasipo kuhesabu atalipwa nini. Mwl. Nyerere
 
Acha wivu wewe, Zitto ana hela, mbona huwa anakodi ndege ya Tanapa mara kwa mara kwenda jimboni Kigoma? Kama asingekuwa hela angewezaje? Lakini pia kwa kazi hii ya kuzuia wizi na ufisadi lazima
kuna vikwazo, hata huyu mleta hoja anaweza kuwa kikwazo, anaweza kuwa ametumwa na
wenye mapesa Uswis kukwamisha mkakati zanzibar huru
 
Last edited by a moderator:
mleta uzi amejipembua kama mmoja kati ya watu wanaofikiri kinyume na hili linalofanywa na zito, isitoshe hakuna zaidi ya hofu inayokusumbua, ngoja uchunguzi ukamilike ili mkaangwe vizuri,
kazi nzuri zito achana na watu wenye wivu
 
  • Thanks
Reactions: PhD
Pesa ikishaenda kwa kwa wazungu huwa hairudi kama huamini jiulize huyu jamaa GENERAL SANI ABACHA aliiiba zaidi ya 5 billion USD

Wazungu wamerudisha kiasi gani Nigeria?

Walirudisha milioni 600 tu. Nyingine zote waliweka kibindoni. Chezea Waswiss weye?
 
chezea Kabwe Zitto wewe, ni dealer maker. Akiona pesa inampungua anatafuta dili la kumwingizia fedha. Mnakumbuka ile ishu ya madini alipoteuliwa na raisi kwenye kamati ya uchunguzi? Na hii ishu ya mabillion ya uswiss yatamtoa tu. Niulize yatamtoa vp nikuelezee?
 
we ni zaidi ya mbea. Yote hayo yanakuhusu nn?

Afadhali umemjibu huyo chaumbea, kazi yao ni kukatisha tamaa wenzao wanaojaribu kuiokoa nchi hii.Hoja hapa sio zitto kapata wapi pesa za uchunguzi, hoja ni uchunguzi ufanyike hayo makuwadi ya ufisadi yajulikane.
 
mleta uzi amejipembua kama mmoja kati ya watu wanaofikiri kinyume na hili linalofanywa na zito, isitoshe hakuna zaidi ya hofu inayokusumbua, ngoja uchunguzi ukamilike ili mkaangwe vizuri,
kazi nzuri zito achana na watu wenye wivu

tena unaweza ukakuta aliyeleta uzi huu yumo CDM , wivu na husda tu
 
Mkuu maswali meeeeengiiii! Ila umesahau swali moja tu! Je, kamshirikisha mkeo? Watu wengine bwana!
 
Pesa ikishaenda kwa kwa wazungu huwa hairudi kama huamini jiulize huyu jamaa GENERAL SANI ABACHA aliiiba zaidi ya 5 billion USD

Wazungu wamerudisha kiasi gani Nigeria?

sani_abacha_nigeria.jpg

Huyu kaibia Kenya zaidi ya usd 40 billion

Daniel+Arap+Moi.jpg



Pesa zimefishwa kwenye banks hizi hapa na hakuna hata senti 5 iliyorudishwa kenya:

pesa zingine ziko humu:
288795.jpg

121018044059-goldman-sachs-greg-smith-story-top.jpg


na kama anazo pesa za kutosha pesa ananazo zitaka zito ziko address hii hapa NEW YORK:

740 PARK AVENUE (le Mutuz na watu wa NYC wanaweza ku confirm nani anakaa humo...na ina a way wako connected na hao ambao Zitto kaambiwa wana accounts Uswisi)
article-2030131-0D921DA000000578-272_468x533.jpg

data=Ay5GWBeob_WIPLDYoIWcfVXxvZu9XwJ55OX7Ag,vuq4wY6_rhE9kyirukO5hCd508h6iM4AKGKaXQncoGUe8PU8DFZteEaWSEzBQu-6VZch5ykWdmdCiNFc8olQQiIdNEAtKEyVZA5caBOydwnRIIaLqN93m0gi_sh5I_vcq75ddw

Walirudisha milioni 600 tu. Nyingine zote waliweka kibindoni. Chezea Waswiss weye?

end thread

hakuna pesa inayokwenda kwa mzungu na kurudi tena africa
 
Mimi sioni tatizo Zitto kuhamua kufuatilia mwenyewe. Kafanya hivyo kwa kuwa serikali ya CCM haiko tayari kufuatilia. Acha aendelee, hata akishindwa haikuhusu we mtoa mada fisadi. Katika mchakato wake sidhani kama kakuomba wewe hata senti 1. In Zitto we trust
 
zanzibar huru Kama habari uliyoisema kuwa Zitto kaweka private investigators ili kuchunguza hizo pesa za wizi huko Uswisi, hili ni jambo la jema ambalo watanganyika wenye kuipenda nchi hii tunamuunga mkono! Wewe endeleza harakati zenu na UAMSHO mpate Zanzibar huru mnayoitaka mdomoni, huku kimatendo mnaendelea kujibaraguza
 
Last edited by a moderator:
Baada ya muda si mrefu mtafahamu huyu mtu aitwaye ZITTO ZUBERI KABWE hasa anafanyia nani kazi. Mpaka sasa wengi hamjafahamu nani hasa anamfanyia kazi. Mnadhani ni upinzani au CDM.
 
Kinachotakiwa ni kumpa support watu wakiwa na mawazo kama ya mleta uzi maana yake tayari tunajigawa makundi kuangalia hayo mambo ya kapata wapi ela badala ya kufuatilia ela zilizofichwa. Mleta uzi asihofu lengo kuu ni kufuatilia fedha zilizofichwa hivyo basi mawazo yako ni ya mwisho baada ya zoezi kufanyika ndipo watu wahoji hayo mambo ya zito. Na ndio maana hata MKAGUZI MKUU WA SERIKALI huwa anahoji matumizi ya fedha baada ya kuwa ela zimeshatumika na si kabla ya matumizi maana itakuwa kama anawafundisha namna ya kutumia
 
Kinachotakiwa ni kumpa support watu wakiwa na mawazo kama ya mleta uzi maana yake tayari tunajigawa makundi kuangalia hayo mambo ya kapata wapi ela badala ya kufuatilia ela zilizofichwa. Mleta uzi asihofu lengo kuu ni kufuatilia fedha zilizofichwa hivyo basi mawazo yako ni ya mwisho baada ya zoezi kufanyika ndipo watu wahoji hayo mambo ya zito. Na ndio maana hata MKAGUZI MKUU WA SERIKALI huwa anahoji matumizi ya fedha baada ya kuwa ela zimeshatumika na si kabla ya matumizi maana itakuwa kama anawafundisha namna ya kutumia
 
Back
Top Bottom