Zitto katoa wapi pesa za kufanya 'private investigation' Uswisi?

zanzibar huru

JF-Expert Member
May 28, 2012
218
225
37.jpg


Hivi mshahara na marupurupu yake yote kwa mwezi ni kiasi gani?

Ana biashara zipi alizo declare kama mbunge

all in all Zitto ana worth kiasi gani?

Sasa tujishajumuisha cha kujiuliza maswali yafuatayo:

1. Je kuna umuhimu gani yeye kwenda?
2. CHADEMA na uongozi wake wameshirikishwa kwenye hili au ni CRUSADE ya Zitto na ego yake?
3. Gharama za HOTELI, CHAKULA, MAWASILIANO, USAFIRI, WA NDEGE NA TAXI analipia nani? je zinaweza kufikia kiasi gani per day?
4. Je serikali ya Uswisi itampa ulinzi?
5. Je kaishirikisha Ubalozi wa Tanzania Geneva?
6. Je kaishirikisha Wizara ya mambo ya nje?
7. Je kaishirikisha Usalama wa Taifa
8. Je kaishirikisha wizara ya sheria?
9. Je kaishirikisha wizara ya utawala bora?
10.Je kaishirikisha OECD
11.Je kaishirikisha EU
12. Je kaishirikisha wizara ya fedha?
13. Je kaishirikisha BOT?
14. Je kazishirikisha hizo benki zilizofanya transfer?
15. Je kaishirikisha PCCB ?
16. Je kaishirikisha INTERPOOL?
17. Je kaishirikisha wizara ya fedha ya USWISI?
18. Je kaishirikisha BENKI KUU YA USWISI?
19. Je kaishirikisha POLISI YA USWISI?
20. Je kashawaandikia watuhumiwa barua za kujieleza? na alipoandika barua aliandika kama nani?
21. Je akikuta watu washamaisha hizo pesa kwenda nchi 30 duaniani ataendelea na ziaya yake kwenda kwenye hizo nchi zote?
22. Je akikuta kuwa hakuna pesa ata refund pesa alizopewa na chama au?
24. Je anategemea kutumia gharama za kiasi gani kwenye hii CRUSADE yake?
25. Atataumia legal jurisdiction zipi kwenye huu mpango wake?
26. Hivi wananchi wa jimbo lake watasemaje kuhusu huu mpango wa mbunge wao kufanya ziara ya muda mrefu kwenye hizo Tax havens ambazo anajua fika hatopata kitu?

Huyu ni mbunge kijana ana anaonekana anapenda kujionyesha kuwa ana mawazo mbadala lakini sasa naanza kupatwa na question marks kuhusu huu mpango wake wakati tunajua fika kuwa huhitaji kwenda Uswisi kujua kama Tanzania ina mafisadi.

Kama akitaka tumwone serious angeanza na TRA/TPA ili kujua kwa nini tanzania inapoteza minimum BILIONI 300 per day kutokana na uozo uliopo pale bandari na TRA
 

George Smiley

JF-Expert Member
Oct 24, 2011
471
225
Sasa sidhani kama Zitto ataelewa maana ya hii picha au alisoma historia yake. Jinsi ilivyo ikifika Easter mwakani tutajua kama anasoma vitabu na kuelewa au na yeye anataka kuwa na library kubwa ya vitabu kama swahiba yake.

trojan-horse2.jpg
 

George Smiley

JF-Expert Member
Oct 24, 2011
471
225
Kazitoa Uswisi

Kwa hesabu za haraka haraka tuu tena kwa conservative estimates itabidi Zitto awe na minimum 4 million usd.

na hiyo sio guarantee kuwa atapata kujua who did what, when and where. In short wenzake nijuavyo washahamisha pesa kwenda kwenye layers of more than 30 corporations, foundations and trusts tena kwa majina ya wengine na makampuni mengine.

Kingine Zitto lazima ajue kuwa uchumi wa nchi hizo unaendeshwa kwa pesa za wizi ndio maana wazungu walifanya colonialism kwani wako driven by plunder.

Na pia asitegemee kuwa hao mambalozi wa nchi hizo wanavoongea naye na mikutano yake nao wao wana interest saaaana na Tanzania. Hao wako huku Tanzania kulinda interests zao including modern day plunder ya makampuni yao namshauri angeanza kusoma kitabu vifuatavyo:

124894886.JPG
102042413.jpg
103051357.jpg
166845544.JPG
102674984.jpg
103182277.jpg
 

Mwanaukweli

JF-Expert Member
May 18, 2007
4,783
2,000
Hata ya EPA, maswali ya hivi yaliletwa, baadaye ikagundulika kuwa ni ukweli.

Pamoja na methodology, na gharama alizotumia, suala la msingi ni kuwa aliyosema ni ya kweli au si ya kweli.

Nafurahi kuwa mwanasheria mkuu ameunda kikosi kazi kinachoshirikisha Usalama wa Taifa na Interpol kuhakiki ukweli wa madai ya Zito. Hilo ndilo la muhimu.

zanzibar huru, ukijua ametoa wapi pesa, ukweli wa madai utaupeleka wapi?
 

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,147
2,000
Umeielewa vizuri hoja ya Zitto kweli? Hebu kasome upya gazeti la mwananchi utajua Zitto ameongea nini. Wakati mwingine msipende sana kukurupuka tu na kuanza kushambulia vitu bila kuelewa. Zitto anasema kama investigation itafanywa kwa kutumia mfumo wa kiserikali kwa maana ya kushirikisha serikali ya Tanzania na Uswis, process yake itakuwa ni ndefu na inaweza kuwa ngumu. Lakini kama mkifanya private investigations, (kwa mfano selikali ya Tanzania itumie inteligensia yake ku-investigate ni akina nani wana pesa huko, ni kiasi gani na walizipataje), mnaweza kutoka na majibu mazuri kabisa. Maana kwenye private investigation hamuhitaji kuishirikisha serikali ya Uswis, mtadeal na wahusika moja kwa moja na wahusika wenyewe ndiyo watakaowapa access kwenye account zao za nje.

"Zitto alisema uchunguzi utakaofanywa utafuata mfumo wa uchunguzi binafsi na kubainisha kuwa, kufuata mfumo wa kiserikali kunaweza kuwa na vikwazo vingi. “Sisi hatufuati mfumo wa kiserikali, mfumo wa kiserikali ndiyo una masharti hayo. Sisi tunafuata mfumo wa uchunguzi binafsi,” alisema Zitto. Quoted from Mwananchi.

Halafu idea ya Zitto kuwa sehemu ya hiyo investigation si yake, bali ni ya mwanasheria mkuu ambaye ameunda kikosi kazi cha kufanya hiyo investigation. Ni mwanasheria ndiye anayependekeza Zitto awe kwenye hiyo team. sasa sielewi hapa Zitto anasekamwa kwa lipi? Na hilo haliihusu CHADEMA bali linamhusu Zitto kama mtu binafsi. sanasana ataomba tu ruhusa kwa bosi wake.
 

George Smiley

JF-Expert Member
Oct 24, 2011
471
225
Hata ya EPA, maswali ya hivi yaliletwa, baadaye ikagundulika kuwa ni ukweli.

Pamoja na methodology, na gharama alizotumia, suala la msingi ni kuwa aliyosema ni ya kweli au si ya kweli.

Nafurahi kuwa mwanasheria mkuu ameunda kikosi kazi kinachoshirikisha Usalama wa Taifa na Interpol pamoja na zito mwenyewe kuhakiki ukweli wa madai ya Zito. Hilo ndilo la muhimu.

zanzibar huru, ukijua ametoa wapi pesa, ukweli wa madai utaupeleka wapi?

edited
 

George Smiley

JF-Expert Member
Oct 24, 2011
471
225
kwa wana JF mnao lilia katiba mpya ije na transparency nadhani mleta hoja yuko right.

Ingekuwa ni ulaya nadhani maswali yangekuwa zaidi ya hayo.

lakini nafurahi kuona wana JF wanauliza maswali ambayo watu wengine hawapendi yaulizwe. GREAT THINKERS ambao wana GREAT MINDS....
 

George Smiley

JF-Expert Member
Oct 24, 2011
471
225
.....Kama akitaka tumwone serious angeanza na TRA/TPA ili kujua kwa nini tanzania inapoteza minimum BILIONI 300 per day kutokana na uozo uliopo pale bandari na TRA

Pesa ikishaenda kwa kwa wazungu huwa hairudi kama huamini jiulize huyu jamaa GENERAL SANI ABACHA aliiiba zaidi ya 5 billion USD

Wazungu wamerudisha kiasi gani Nigeria?

sani_abacha_nigeria.jpg
 

Jangakuu

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
513
250
zanzibar huru What is uswisi , hata mimi na mshahara wangu wa graduate engineer , nina uwezo wa kwenda uswisi na kukaa kule mwezi mzima bila tatizo, sasa zito ni mbunge na alipwa msharahara zaid ya mimi, after all hawezi kwenda bila kuwashirikisha uongozi wa chadema, coz anaenda kwa manufaa ya watanzania, hatuna wasiwasi na zitto tumuombee , mapigano mema dhidi ya mafisadi. My God bless Zitto!!!
 
Last edited by a moderator:

George Smiley

JF-Expert Member
Oct 24, 2011
471
225
Huyu kaibia Kenya zaidi ya usd 40 billion

Daniel+Arap+Moi.jpgPesa zimefishwa kwenye banks hizi hapa na hakuna hata senti 5 iliyorudishwa kenya:

pesa zingine ziko humu:
288795.jpg

121018044059-goldman-sachs-greg-smith-story-top.jpg


na kama anazo pesa za kutosha pesa ananazo zitaka zito ziko address hii hapa NEW YORK:

740 PARK AVENUE (le Mutuz na watu wa NYC wanaweza ku confirm nani anakaa humo...na ina a way wako connected na hao ambao Zitto kaambiwa wana accounts Uswisi)
article-2030131-0D921DA000000578-272_468x533.jpg

data=Ay5GWBeob_WIPLDYoIWcfVXxvZu9XwJ55OX7Ag,vuq4wY6_rhE9kyirukO5hCd508h6iM4AKGKaXQncoGUe8PU8DFZteEaWSEzBQu-6VZch5ykWdmdCiNFc8olQQiIdNEAtKEyVZA5caBOydwnRIIaLqN93m0gi_sh5I_vcq75ddw
 

Saracen

Senior Member
Apr 14, 2011
148
195
kwa wana JF mnao lilia katiba mpya ije na transparency nadhani mleta hoja yuko right.

Ingekuwa ni ulaya nadhani maswali yangekuwa zaidi ya hayo.

lakini nafurahi kuona wana JF wanauliza maswali ambayo watu wengine hawapendi yaulizwe. GREAT THINKERS ambao wana GREAT MINDS....

mambo mengine bora watu wayaache tuu yatapita na upepo
 

chicco

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
748
225
fitina na majungu tu.so we ulitaka aende prezida wenu mtembezi ndo ufurahi?hivi mbona hamuishi kumtafuta ubaya zzk?yaani badala ya kumpongeza mtu ambaye anajaribu kutusaidia tunamponda?mbona wengine wanaenda kwa ziara za kubembea tu hamuhoji wamepata wapi pesa za kuwapeleka huko?
 

Mwakalinga Bujo

JF-Expert Member
Oct 22, 2008
2,721
2,000
  • Hakuna jambo lisilokosa kasoro/mapungufu machoni/moyoni mwa mwanadamu .Muhimu ni kutumia akili na maarifa mbadala kuyabainisha hayo mapungufu/kasoro
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom