Zitto Kabwe ndani ya Karatu

Zitto Kabwe ndani ya Karatu

ZZK at Karatu
380097_477385475615488_686482092_n.jpg
 
Mag3, ruttashobolwa, Shardcole KOMBAJR, Adoya, Nicholas, Ukwaju, Zaha, Mungi, Crashwise Molemo,

Zitto Kabwe

Narudia, mwaka 2015 sitagombea Ubunge. Nitafanya kampeni ya Urais, ama mimi kama mgombea wa chama changu CHADEMA au kama mpiga debe wa mgombea wa chama changu. Miaka 10 ya Ubunge inatosha na kwa ngazi hiyo ni vema niwaachie wengine wasukume mbele gurudumu la maendeleo ya Jimbo na mkoa wetu. Huu ndio uamuzi wangu wa mwisho na nimeshawaeleza wananchi wa Jimbo langu na mkoa wa Kigoma toka mwaka 2005.

:violin:

Ritz
Kama watu tusioegemea upande wo wote habari hii inasomeka hivi;
Tangazo la Zitto Kabwe kipindi hiki ni cha mwisho kuwa mbunge na kusisitiza kwamba hatagombea tena ubunge ila Urais au kumwunga mkono mgomea urais atakayepitishwa na Chama chake Chadema, kuna siri nzito ambayo hapendi kuitoa ila kuna bomu ambalo analijua kabla au wakati wa uchaguzi ujao laweza kulipuka.

Tujuavyo Zitto Kabwe ni kijana mdogo sana, kwamba hana nia ya kugombea ubunge tena, je, anakusudia kujiondoa katika siasa au kuna kitu kingine anachokusudia katika siasa? Ndege mjanja hunasa katika tundu bovu, dalili sasa zinaanza kujionyesha wazi. Wengi tutakuja kuyaelewa mambo haya baadaye wakati wenye upeo wa kusoma ishara za nyakati tayari wanaona kiza kilivyo ndani ya kijana huyu kwa matamshi yasiyolenga malengo ya muda mrefu katika utendaji anaotazamiwa katika jamii ya watanzania. Ujanja ujanja si dhana ya uadilifu katika utumishi wa umma.

Naweza kutafsiri tamko lake kama ifuatavyo:

  1. Ana wasiwasi wa kutopita tena jimboni kwake uchaguzi ujao kama haja tekeleza aliyoahidi, au kunachipukia wapya wenye mvuto kwa wananchi.
  2. Amekuwa na matarajio ya nafasi ya juu, anapotafiti maoni ya wengi anaelekea kutopita kirahisi kugombea urais.
  3. Hali ilivyo ana wasiwasi uwezekana uchaguzi wa viongozi wa kitaifa ujao nafasi hiyo ya unaibu Katibu Mkuu ikaenda kwa mwanachama mwingine.
  4. Amerubuniwa na CCM kupitia serikali dau kubwa ili aisambaratishe Chadema.
  5. Anasubiri Katiba mpya asipokubaliwa na Chadema atasimama kama mgombea binafsi wa Urais.
  6. Hana msimamo kisiasa muda mwingi ameonekana kutaka kuwa kinyume cha chama chake na kujitahidi kurudi tena kundini, mguu mmoja nje na mguu mmoja ndani.
  7. Ameenda kupima upepo jimboni kwa Dr. Slaa kama anakubalika, kwani anachofanya yeye sasa ni kupima kukubalika kugombea urais badala ya dhana ya kukiimarisha chama matawini.
  8. Je, anaweza kuwa mmoja wapo wa walioficha mabilioni huko Uswiss? Wengi wa wagombea Urais kwa ridhaa yao huwa wanajiandaa kwa hali na mali ikiwepo pesa za kufanyia kampeni.

Kuna mengi ya kujiuliza, hawa ndugu zetu rahisi mno kushawishika kama akina Kaburu, Yule wa NCCR Mageuzi ambaye kabla alikuwa Chadema na wengineo.

Jambo la msingi katika uongozi ndani ya jamii ni mshikamano wa viongozi, kuwa na kauli ambazo zinapata baraka katika vikao vyao.

Kupitia vyombo vya habari kutangaza mbio za kugombea urais pasipo kufuata utaratibu wa chama nadhani ni kukosa maadili ya chama. Itakapopitishwa mgombea binafsi hilo litawezekana kwa vile yuko huru na hahitaji baraka za vikao vya chama ila mashabiki idadi inayokubaliwa kumwidhinisha ili aweze kusimama kivyake. Hili la kuzidi kung'ang'ania nafasi ambayo wakati ukifika ana nafasi wazi ya kufanya kisha kusubiri chama kubariki au kumpisha mwingine, inaonekana jinsi wanasiasa walio wengi walivyojikita katika matarajio binafsi badala ya kuunganisha nguvu za kujenga taswira ya mageuzi ya kweli kijamii badala ya mtu binafsi.

Mageuzi katu hayatafanikiwa katika jamii kwa mtu binafsi hata awe rais, ila ni jamii iandaliwe, ielewe na ishirikishwe ndipo nguvu ya mabadiliko inapoweza kushika kasi yake.
 
Karatu wamemkubali Zitto raia wamepanda mpaka juu ya miti.

Maneno ya Zitto, kama una akili utamwelewa, Sasa nyinyi CCM endeleeni kufurahia mnachofurahia juu ya Zitto. Mwisho wa siku yatawatokea puani...

"Narudia, mwaka 2015 sitagombea Ubunge. Nitafanya kampeni ya Urais, ama mimi kama mgombea wa chama changu CHADEMA au kama mpiga debe wa mgombea wa chama changu. Miaka 10 ya Ubunge inatosha na kwa ngazi hiyo ni vema niwaachie wengine wasukume mbele gurudumu la maendeleo ya Jimbo na mkoa wetu. Huu ndio uamuzi wangu wa mwisho na nimeshawaeleza wananchi wa Jimbo langu na mkoa wa Kigoma toka mwaka 2005''
 
Anaweza kuwa rais mzuri (kama atapitishwa na chama na kuchaguliwa na watanzania walo wengi) lakini anaonekana kuwa a little bit lenient!!!!. Ni wakati muafaka kwa CDM kuwekeza hilo vuguvugu Unguja, Pemba na Tanga kwa nguvu zote na kupunguza nguvu huku ambako tayari wanakubalika!!!!
 
Ritz
Kama watu tusioegemea upande wo wote habari hii inasomeka hivi;
Tangazo la Zitto Kabwe kipindi hiki ni cha mwisho kuwa mbunge na kusisitiza kwamba hatagombea tena ubunge ila Urais au kumwunga mkono mgomea urais atakayepitishwa na Chama chake Chadema, kuna siri nzito ambayo hapendi kuitoa ila kuna bomu ambalo analijua kabla au wakati wa uchaguzi ujao laweza kulipuka.

Tujuavyo Zitto Kabwe ni kijana mdogo sana, kwamba hana nia ya kugombea ubunge tena, je, anakusudia kujiondoa katika siasa au kuna kitu kingine anachokusudia katika siasa? Ndege mjanja hunasa katika tundu bovu, dalili sasa zinaanza kujionyesha wazi. Wengi tutakuja kuyaelewa mambo haya baadaye wakati wenye upeo wa kusoma ishara za nyakati tayari wanaona kiza kilivyo ndani ya kijana huyu kwa matamshi yasiyolenga malengo ya muda mrefu katika utendaji anaotazamiwa katika jamii ya watanzania. Ujanja ujanja si dhana ya uadilifu katika utumishi wa umma.

Naweza kutafsiri tamko lake kama ifuatavyo:

  1. Ana wasiwasi wa kutopita tena jimboni kwake uchaguzi ujao kama haja tekeleza aliyoahidi, au kunachipukia wapya wenye mvuto kwa wananchi.
  2. Amekuwa na matarajio ya nafasi ya juu, anapotafiti maoni ya wengi anaelekea kutopita kirahisi kugombea urais.
  3. Hali ilivyo ana wasiwasi uwezekana uchaguzi wa viongozi wa kitaifa ujao nafasi hiyo ya unaibu Katibu Mkuu ikaenda kwa mwanachama mwingine.
  4. Amerubuniwa na CCM kupitia serikali dau kubwa ili aisambaratishe Chadema.
  5. Anasubiri Katiba mpya asipokubaliwa na Chadema atasimama kama mgombea binafsi wa Urais.
  6. Hana msimamo kisiasa muda mwingi ameonekana kutaka kuwa kinyume cha chama chake na kujitahidi kurudi tena kundini, mguu mmoja nje na mguu mmoja ndani.
  7. Ameenda kupima upepo jimboni kwa Dr. Slaa kama anakubalika, kwani anachofanya yeye sasa ni kupima kukubalika kugombea urais badala ya dhana ya kukiimarisha chama matawini.
  8. Je, anaweza kuwa mmoja wapo wa walioficha mabilioni huko Uswiss? Wengi wa wagombea Urais kwa ridhaa yao huwa wanajiandaa kwa hali na mali ikiwepo pesa za kufanyia kampeni.

Kuna mengi ya kujiuliza, hawa ndugu zetu rahisi mno kushawishika kama akina Kaburu, Yule wa NCCR Mageuzi ambaye kabla alikuwa Chadema na wengineo.

Jambo la msingi katika uongozi ndani ya jamii ni mshikamano wa viongozi, kuwa na kauli ambazo zinapata baraka katika vikao vyao.

Kupitia vyombo vya habari kutangaza mbio za kugombea urais pasipo kufuata utaratibu wa chama nadhani ni kukosa maadili ya chama. Itakapopitishwa mgombea binafsi hilo litawezekana kwa vile yuko huru na hahitaji baraka za vikao vya chama ila mashabiki idadi inayokubaliwa kumwidhinisha ili aweze kusimama kivyake. Hili la kuzidi kung'ang'ania nafasi ambayo wakati ukifika ana nafasi wazi ya kufanya kisha kusubiri chama kubariki au kumpisha mwingine, inaonekana jinsi wanasiasa walio wengi walivyojikita katika matarajio binafsi badala ya kuunganisha nguvu za kujenga taswira ya mageuzi ya kweli kijamii badala ya mtu binafsi.

Mageuzi katu hayatafanikiwa katika jamii kwa mtu binafsi hata awe rais, ila ni jamii iandaliwe, ielewe na ishirikishwe ndipo nguvu ya mabadiliko inapoweza kushika kasi yake.
Zitto Kabwe atangaza kung’atuka

zitto.jpg

Mheshimiwa Zitto Kabwe.

Kutoka gazeti 'lao' la Tanzania Daima
na Samuel Mwanga, Maswa

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ametangaza kung’atuka katika wadhifa wake mwaka 2010.

Kabwe alitangaza adhima yake hiyo jana, wakati akiongea na waandishi wa habari katika Hoteli ya Greenbeach mjini Maswa mkoani Shinyanga.

Alisema amefikia uamuzi huo bila kushinikizwa na mtu yeyote na ameamua kutangaza mapema ili kutoa nafasi kwa wanaotaka kugombea nafasi hiyo, ili wajiandae.

Kabwe alisema anatamani kufanya kazi za kitaalamu, hasa zinazohusu taaluma yake baada ya kuwa mwakilishi wa wananchi kwa kipindi cha miaka mitano.

“Tangu nimalize masomo yangu chuo kikuu, ni kipindi cha mwaka mmoja tu niliofanya kazi kisha nikachaguliwa kuwa mbunge, hivyo nina hamu ya kufanya kazi nyingine mbali na hii ya uwakilishi,” alisema Kabwe.

Alisema uamuzi wake wa kuachana na ubunge hauhusuni na masuala ya siasa ambayo iko katika damu yake.

Kabwe alisema kamwe hataachana na siasa bali baada ya kuachana na ubunge, ataendelea kufanya kazi za kuiimarisha CHADEMA ambayo imemfikisha katika mafanikio aliyonayo sasa.

Aliahidi kuendelea kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa uaminifu na kushirikiana nao kuondoa kero mbalimbali zinazowakabiri pamoja na kutimiza ahadi zake alizozitoa wakati wa kuomba kura.

Kabwe alionya kuwa kazi ya ubunge si lelemama kama baadhi ya watu wanavyofikiria, bali ni ngumu na inayohitaji uvumilivu wa hali ya juu.

“Nimeifanya kazi hii ya ubunge kwa muda wa mwaka mmoja sasa, si kazi ya lelemama, ni lazima ujitolee kweli kuwatumikia watu, kwani kila tatizo linapotokea jimboni wananchi wanakutazama wewe mbunge,” alisema Kabwe.

Kabwe ni miongoni mwa wabunge vijana wa CHADEMA ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa vyama vingi wa mwaka 2005 alifanikiwa kuwashinda wagombea wa vyama vingine vya siasa.
 
Wajinga hao wamezoea kuwekana wakaskazini sasa safari hii ni zamu ya kigoma.
Watake wasitake.
Waulize mbowe keshagombea akashindwa,slaa nae pia akachemka,
Sasa kinachowasumbua wasimpe zitto nae atupe karata zake ni nini kama sio dhambi ya ukanda na udini?
Suala siyo kumpa wala kutompa Bob! suala ni kauli gani unatoa wapi? Sasa na Mbowe, Slaa, Mnyika, Mdee, Sugu, nk wakienda kwa wananchi/wanahabari wakitoa kauli kama hizo itakuaje? Mbona hata nyie wa CC Mabwepande mna utaratibu? Mbona hata huyo C*F bibiye wenu wana utaratibu? hakuna mropokaji? ZZK ni pandikizi na hana nafasi! tuko tayari kupoteza wanafiki na mapandikizi wote na kuanza moja!!
 
Dah! Kweli hii ndo JF yani watu majungu tu alafu eti chama kimoja? Hebu acheni jamani hayo majungu mnayopigana na kuchafuana ninyi kwa ninyi kwani nyie wote ni wamoja na mnaunganishwa na CHADEMA na adui yenu mkuu sio Zitto, slaa au Mbowe bali adui yenu ni CCM, sasa inabidi mbadilike kwani haya mabandiko mnayoyaandika hapa na matusi juu ni kujiharibia sifa,

acheni jamani ushabiki wa watu na internal chuki kwani zitakiangamiza chama.

watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa yao.
 
Sasa tunaomba mtuwekee na hotuba yake kama kuna mwenye nayo,ili tujadili hoja na si matusi na chuki tu humu ndani.JF ni kisima cha fikra na si majungu,uzandiki,maneno machafu na yenye kuchochea chuki.Tunashukuru kwa picha,sasa tupeni hotuba.
 
Ndani ya chama kila mmoja ana haki ya kuomba kuwa Raisi!
 
Namshauri apite Kata zote zenye Madiwani wa CCM.Kama kweli ameamua kujiunga na M4C
 
:ranger: leo naona kundi la zitto lipo juu zaidi kwa vijembe kuliko siku zote, inaonekana jamaa wamejipanga kwa lolote humu ndani.
 
Akiropoka uraisi hapo karatu............ PLEASE NAOMBA KICHAPO CHA UHAKIKA; WAIRAQ NAWAAMINIA, HUYU MTU ANATAFUTA MANENO M4C INARATIBA YAKE KARATU ANATAFUTA NINI? ..............ATAJIFANYA ANAFAFANUA KAULI YAKE NAKUANZA KUMSIFIA SLAA....
Mkuu, usisumbuke kufikiri kuhusu kauli ya zzk kuhusu urais, wakati utafika chama kitamsimamisha mgombea kitakachoona anafaa. Aliyosema ni maoni yake, na nadhani ni vema isichukuliwe kama kauli ya ajabu sana. Acha jamaa aifurahishe nafsi yake...Na kumbuka kuwa kauli yake siyo final... Hii ndio demokrasia, ni muhimu kuvumiliana.
 
:ranger: Leo naona kundi la zitto lipo juu zaidi kwa vijembe kuliko siku zote, inaonekana jamaa wamejipanga kwa lolote humu ndani.

naona ni kundi kubwa sana,sijui mafunzo wamepatia wapi au ni alshabab wa somalia
 
namshauri apite kata zote zenye madiwani wa ccm.kama kweli ameamua kujiunga na m4c

bila shaka zitto ameamua kufanya kazi,swala la kumwambia aanzie wapi ni kufanya kazi isiyokuhusu.nashukuru ameanzia jimboni kwa dr.slaa.
M4c ya chadema imesimama kwa sasa,na sio lazima wote wawe kweye m4c
 
Unaweza kutuwekea hotuba yake mkuu?
 
Back
Top Bottom