acheni chuki binafsi wana JF, kubalini kuwa Zitto ana mchango mkubwa ndani ya CDM na nadhani ni yeye na Dr. Slaa ndio wanaoongoza kuifanya CDM leo iwe tishio. Nani atabisha.? Zitto ameleta hamasa kubwa kwa vijana kupenda CDM kuliko mwingine yeyote. Kama yeye ni pandikizi la CCM, kulikuwa na haja gani aijenge chadema wakati ilikuwa haijulikani.? Mapandikizi ni wale wanaodandia chama kikiwa kimeshakomaa. Zitto kajiunga na chama wakati ana miaka 16 na chama kilikuwa hakijulikani, na amekua nacho na ameshiriki kukijenga. Ni mpumbavu gani duniani apoteze muda wake kujenga nyumba halafu aanze kuibomoa? Mkubali msikubali, zitto ni jembe la chadema na hakuna wa kumtoa sababu hana hatia yeyote na ndio atakibeba chama 2015. Acheni kuwa na wivu na ubaguzi usio na msingi.