mchukiaufisadi
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 546
- 193
Hakubaliki kwa sababu aligombea uenyekiti wa chadema taifa2009 na kumpinga mkurugenzi wa chagga development manifestal na pia anahoji kwa nini chama kinaendeshwa kikampuni zaidi mpaka uwe mchaga ndo unatapa nafasi
Wakuu heshima mbele,
Hoja ya Zitto kuwakilisha Upinzani ina mashiko lakini hoja nyingine inaibuka ni nani amemtua kuwakilisha upinzani? Maana tunavyojua ki Protocal ilipaswa Ikulu iiombe ofisi ya Spika Mbunge mmoja kutoka kambi ya Upinzani ashiriki kwenye msiba kwa niaba ya upinzani. Hata hivyo, Spika nae asingekuwa na mandate ya kuteua Mwakilishi kutoka kambi ya Upinzani. Ilipaswa ashushe dokezi chini hadi kwenye Ofisi ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani ndiye ateue Mbunge wa Kuwakilisha.
Sasa kama Jina la Zitto limetoka moja kwa moja kutoka Ikulu lazima watu wahoji. Kunani Zitto? Kwa nini asiwe Lissu au Nassari au Silinde au Wenje nk? Je uteuzi wa Zitto kwenda Ethiopia ulikuwa na baraka za Ofisi ya Spika na Kiongozi wa Upinzani? Haya ndiyo maswali ya kujiuliza, Mimi, wewe na wengine.
TUMBIRI (PhD in Progress at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd[/SUP] Overall Best Student in Form Six National Exams)
tumbiri@jamiiforums.com
Huyu jamaa simpendi kama nini sijui. Kajamaa kana mambo ya kishamba kinoma sana haka. Halafu dizaini kama ushamba na ulughalugha bado haujamtoka. Kana tabia za kujikweza na kujiona kako bora kuliko wenzako. Mi natamani hata katimuliwe tu Chadema kama vipi.
tatizo la zuberi zitto ndani ya chadema ni hilo jina lake.
Kichuguu,Inawezekana amekwenda kama sehemu ya ujumbe wa Tanzania kutoka vyama vya upinzani. Nadhani wenzake huko CDM watakauwa na taarifa. JK na ZK wana commonalities fulani kisiasa kwani wote walianza ambitions za kisiasa wakiwa wangali wadogo sana na walipopata nafasi hizo wakaanza kwa kushupalia makampuni ya madini kabla hawajanyamaza kama vile makampuni hayo hayapo tena.
Hivi yule "Zoka" ni wa ikulu?ama ni Ghondi?anyways RIP Zenawi.
Sizani kama ni sahihi kukandia kila jambo linalofanywa na Zitto. Kufanya hivyo tutakuwa hatumjengi ,ana mabaya yake na mazuri pia.Ameenda kutuwakilisha hivyo ni vyema tukapunguza hisia na chuki zenye mtazamo hasi.
WAKUU!
Namshangaa huyu Mh. Zitto Z. Kabwe. Wakati wa mkutano wa M4C Morogoro tuliambiwa angehudhuria. Baadae mawasiliano kati yake na Makamanda waliokuwa kwenye harakati za ukombozi yakapotea. Leo hii katia timu Addis na Mkulu.
Makamanda, hii ime kaa je? wakati Makamanda wengine wakiendeleza harakati za kuwakomboa waTanzania huyu Mh. mbona yupo beneti na Magogoni sana?
Ni kuuliza tu Makamanda.
Tatizo la Zitto siyo kusafiri na Kikwete, tatizo ni kwa nini yupo benet sana na Viongozi kwa CCM kuliko viongozi wake ndani ya Chama? Nyie mnasema siasa siyo chuki wala uadui mbona Dk Slaa, Mnyika na Lema wanawindwa kwa sababu za kisiasa? Iweje na JK nae analindwa na msafara kama siasa siyo uadui? Acheni kupotosha. Siasa ina create maadaui na kama usipojipanga vizuri huchukui round. Ndiyo maana Dk Slaa anatembea na Bastola na Board Guard wa kutosha!
TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
Kaka TUMBIRI hapo chini ni cv au vitu gani?
Wakuu, nasikitika kusema kwamba wana JF wengi waliochangia uzi huu wamechangia kwa jazba, wengine kwa kuunga mkono na wengine hata kwa kupongeza.
Lakini mtoa mada amekuja kwa kutoa taarifa ya uwepo wa Mhe. Zitto katika msafara wa Mhe. Rais kuelekea katika mazishi ya Mhe. Zenawi, lakini pia ameongeza na swali, hii imekaaje?
Matarajio yangu yalikuwa, wana JF wangekuja na ushahidi wa aidha CDM imemruhusu akiwakilishe au kajiamulia mwenyewe nk.
Sasa majibu kama siasa si uadui, anafanya kazi ya kitaifa au anachukua uzoefu na mengine kama hayo yanatoka wapi?
Tafadhali mwenye taarifa kamili atujuze, amekwenda kwa baraka za nani? Bunge, Serikali, CDM, Jimbo lake au binafsi?
M4C movement for chaga na yeye ni muha wa kigoma sasa unataka akafanye nini huko?
acheni majungu watoto wa mtei. mbona hamsemi ni kosa gani kafanya kwa kuhudhuria mazishi?
TUMBIRI (PhD in Progress at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd[/SUP] Overall Best Student in Form Six National Exams)
tumbiri@jamiiforums.com
Sizani kama ni sahihi kukandia kila jambo linalofanywa na Zitto. Kufanya hivyo tutakuwa hatumjengi ,ana mabaya yake na mazuri pia.Ameenda kutuwakilisha hivyo ni vyema tukapunguza hisia na chuki zenye mtazamo hasi.