Zitto Kabwe More Than Meets the Eye!

Zitto ni MwanaCCM mwaminifu kupitia CHADEMA, ndiyo maana wanampigania ili waweze kufanikiwa malengo yao.

Baadhi ya wanaomtetea ndani ya chama bila shaka ni mtandao wake

siku njema mkuu, maneno makali sanaaa.
 
Wadau mtakubaliana nami kuwa baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumvua nyazifa zote za uongozi Mh. Zubery Zitto Kabwe kumekuepo maneno mengi na mijadala isiyoisha kumuhusu yeye. Baadhi ya watu wamemtetea na wengine kumponda. Kitu cha kushangaza sana ni hili swala la baadhi ya viongozi au wanasiasa wa vyama vingine kumpigania mithili ya kwamba ni mwanachama mwenzao katika vyama vyao. Nimekua nikijiuliza mfano ni kwa nini baadhi ya wanachama au viongozi wa chama tawala wanamtetea sana. Au ni kwanini baadhi ya watu wanaponda chadema na kusema imemuonea? Kuna nini hapa? Mbona hao hao wanaoponda uamuzi wa Chadema kumvua uongozi Zitto na vyama vyao kwa kipindi fulani vimefanya hivyo hivyo na watu hawakupiga kelele? Hebu ngoja niweke mifano michache hapa:
1. CCM muda si mrefu sana umepita walimvua uongozi Mh. Mansor Yusuf Himidi Mbunge wa Mjini Magharibi huko Zanzibar lakini watu hawakupiga kelele hivi!
2. CUF walimvua uongozi na uanachama Mh. Hamadi Rashid Mbunge wa Wawi lakini watu hawakupiga kelele hivi?
3. NCCR Mageuzi walimsimamisha Mh. David Kafulila Mbunge wa Kigoma Kusini lakini watu hawakupiga kelele hivi!

Sasa kwa nini Zitto ? Na kwanini Chadema ndio ionekane mbaya sana kwa swala hili?
TAFAKARI! TOA JIBU!

Ishu ya Zitto imeisha sasa turudi kwa kapuya. vipi polisi wamemhoji? au bado wanagwaya
 
Jamani hawa wanasiasa wetu tuwe tunawaangalia na family background zao inaweza kuwa chanzo!!!
 
Pamoja na mjadala kufungwa ndani ya chama na Bos Slaa, bado JF imejaa posts zinazomhusu Zito. Kwa kiasi fulani Umaarufu wa CHADEMA umeongezeka na hali hii itaendelea kupanda kulingana na matukio tunayoyatarajia, ikiwemo kuvuliwa uanachama, KUB Bungeni kumjadili nk. Kwa upande mwingine Hoja nyingine za watanzania kama vile kupanda kwa umeme hazina mvuto kabisa labda mpaka UPEPO huu upite. Naamini pia kuwa kwa sasa Zito atakuwa akiandikwa sana (hot NEWS) na Magazeti yatafanya biashara sana huku picha yake ikipamba kurasa za mbele!!
Matukio haya huenda yakatoa taswila nzuri kwa wale wasio wavivu wa kutafakari au wenye uelewa mzuri katika kusoma alama za nyakati tukielekea 2015.
Anyway tuendelee kuiombea Tanzania na bunge leo linaloanza kikao leo angalau UtOKEE upepo mwingine ili tuachane na hadithi za ZIto.. Zisiwe ngumi lakini...... KWA FAIDA YA Tanzania tuitakayo... wasalaam ...AMEN!
 
Hiki chama nikikisikia siku hizi nahisi kama nakutana na nyani hakina maaana yoyote kwenye jamii ya watanzania.
 
Wadau mtakubaliana nami kuwa baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumvua nyazifa zote za uongozi Mh. Zubery Zitto Kabwe kumekuepo maneno mengi na mijadala isiyoisha kumuhusu yeye. Baadhi ya watu wamemtetea na wengine kumponda. Kitu cha kushangaza sana ni hili swala la baadhi ya viongozi au wanasiasa wa vyama vingine kumpigania mithili ya kwamba ni mwanachama mwenzao katika vyama vyao. Nimekua nikijiuliza mfano ni kwa nini baadhi ya wanachama au viongozi wa chama tawala wanamtetea sana. Au ni kwanini baadhi ya watu wanaponda chadema na kusema imemuonea? Kuna nini hapa? Mbona hao hao wanaoponda uamuzi wa Chadema kumvua uongozi Zitto na vyama vyao kwa kipindi fulani vimefanya hivyo hivyo na watu hawakupiga kelele? Hebu ngoja niweke mifano michache hapa:
1. CCM muda si mrefu sana umepita walimvua uongozi Mh. Mansor Yusuf Himidi Mbunge wa Mjini Magharibi huko Zanzibar lakini watu hawakupiga kelele hivi!
2. CUF walimvua uongozi na uanachama Mh. Hamadi Rashid Mbunge wa Wawi lakini watu hawakupiga kelele hivi?
3. NCCR Mageuzi walimsimamisha Mh. David Kafulila Mbunge wa Kigoma Kusini lakini watu hawakupiga kelele hivi!

Sasa kwa nini Zitto ? Na kwanini Chadema ndio ionekane mbaya sana kwa swala hili?
TAFAKARI! TOA JIBU!

Hakuna cha kutafakari hapa...ufisadi na uvivu wa kufikiri kwa wana chadomo ndio unapelekea kuchagua namna ya kujadili suala hili.

Kwa mtu mwenye busara angehoji hivi:-

...........Ni kwa nini Zitto Kabwe anaungwa mkono na hata wasio wana chadomo (wakiwepo hao mnaolazimisha kuwa ni wana ccm...ni sijui ni kwa utafiti gani )

Hao unaojaribu kuwalinganisha na Zito ni ukosefu wa shukurani na nidhamu kwa mtu kama Zitto....ni sawa na kulalama kuwa kwa nini vyombo vya habari vinalalamika kwa C Ronaldo kukosa heshima ya mwanasoka bora wa dunia huku ukitolea mfano wa mchezaji wa timu ya Kanjibai Fc ya india (kama ipo)kutopewa kipaumbele na vyombo vyao vya habari kwa kunyimwa nafasi inayofanana na hiyo huko nchini kwao.

Kwa maelezo rahisi ni kuwa...hizo habari za kina Hamadi, Mansor na Kafulila waeleze wanaohusika nao....Zitto ni wa taifa zima sio wa chadomo pekee.
 
Mwanasiasa imara,hutuliza mambo yanapoenda mrama,hasa pale hisia za watu zinapoambatana na mtu badala ya CHAMA,kama hivi sasa inavyojionesha ya kuwa Mh. ZITTO,kuwa ana watu wake wanao mwamini sana kuwa ndio shujaa wao.nakushauri kijana mwenzangu ZZK,watulize hao wafuasi wako,waambie mimi si maarufu kuliko chama,Chama ndicho kimenifikisha hapa,.okoa wimbi la wanachama kutimkia kizani tena,kubali kuonywa na kuonyeka.ama la sivyo ukishindwa kufanya hivyo Ondoka nao anzisha Chama chenu ,itakuwa bora kuliko kukalia mbeleko unayo dhani imetoboka.

CHADEMA ITADUMU,AKINA ZITTO,MBOWE NA SLAA WATAPITA,KAMA SI UMRI ,historia itawahukumu kwa matendo yao.peoples power.
 
Inawezekana kabisa una hoja, ila umeiua hoja yako mwenyewe kwa kufanya uchambuzi wa upande mmoja (biased analysis) ambao bila shaka yoyote hitimisho lako litaegemea upande mmoja. Kwa nini nasema hivyo; ni kwa kuwa uchambuzi wako umeegemea katika maelezo na utetezi unaoaminika umetoka kwa mtuhumiwa Mh. Zitto Zuberi Kabwe!

Kwa haraka haraka niseme sijaona umechambua vipi tuhuma alizoelekezewa; kwa mfano kupokea pesa kutoka serikali inayoongozwa na chama pinzani, kuzigawa pesa hizo kwa baadhi ya watu ndani na nje ya chama wanaoaminika ni mamluki, kuwa na mawasiliano ya siri na taasisi nyeti za usalama mawasiliano yanayothibitisha mipango ya siri ya kukihujumu chama, n.k.

Pengine ungejaribu kuzichambua tuhuma zinazomkabili angalau nusu yake, ukaleta uchambuzi wa utetezi alioutoa kwa kila tuhuma aliyoelekezewa, kisha ukatoa hitimisho (conclusion) binafsi ningeona thread yako iko neutral kama nilivyo neutral (sina upande) katika kinachoendelea ndani ya CDM lkn sina upande katika siasa za nchi hii, bali kukweli wa moyo wangu nina upande katika maslahi mapana ya nchi yangu na watu wake.
 
comrades habari,

Siasa za upinzani nijuu ya hoja tofauti na mawazo mbadala ilikuleta ufanisi bora zaidi katika nchi hiyohiyo moja. Kwaio hoja hapa ni kuboresha ufanisi wa serikali ilikuboresha maisha ya kila siku ya mwananchi wa sasa na vizazi vijavyo.

Hapa swala si uadui na uhasimu tu na chuki zilizo jengwa juu tofauti ya rangi za bendera zetu.

Upinzani sio maana yake uwe adui wa kila mtu ilimradi tu yuko upande wa pili., Laah hasha sivyo hata kidogo.

Kuwa mpinzani haimaanishi huwezi kukubaliana na hoja sahihi za mtu wa upande wapili, Actually ilikuwa mpinzani makini unahitaji kuaminiwa na upande wako lakini na upande wapili pia.,

Tatizo ninalo liona hasa changamoto anayokumbana nayo ng. Zitto, ni ule uswahili, ubinafsi, USHAMBA wa watu wengine ndani ya chama wanao mtazama nakushindwa kumuelewa tu., wanadhani zitto anafanya anayoyafanya ilikupata sifa nakusahau kwamba kiongozi makini huhitaji kuweka misingi wakati mwingine., Lazima afanye gestures (kwakumaanisha kabisa) zinazo onyesha unachokiamini ilikujenga misingi sahihi kwa wale unao waongoza.

zipo hoja kwamba mbona zitto anaaminika na serikali ya CCM kuliko wengine, anahongwa!,.

Sasa niseme tu wasi, Zitto kuaminika na watawala is a BIG plus to the change movement.

Namimi nafkiri amefanikiwa kujenga imani kwao si kwa Usaliti ila kwa kazi nzuri ambayo ameifanya so far, kwa professionalism aliyo ionyesha so far.,
Sasa
Kama aliyo yaeleza hapa JF kwenye threads kadhaa alizo ziandika kujitetea kuhusu maswala kama lile la kuamua kutogombea ubunge mwaka 2010, Na kama ni kweli yale aliyo yaeleza kua amefanya bungeni, na kwenye chama, na michango yake ndani na nnje ya nnchi ameyafanya., na kama ni kweli mipango aliyoieleza ni kwasababu alizozieleza hapa na sivinginevyo, na mtazamo alioueleza hapa ndio mtazamo wake halisi.

Basi mimi sioni shida hata kidogo, namuona mtu mwenye uwezo,Nia na sababu ya kufanya mabadiliko ya kweli kwenye siasa zetu, actually na muona mtu mwenye the right mentality for leadership.., if this is what his heart is. then, I think THERE ACTUALLY MIGHT BE MORE TO THIS PARTY STRIFE THAN MEETS THE EYE.

Ninachosema hapa ni kitu gani, Zitto kujenga kuaminiwa na seeikali ya CCM hakutakiwi kumaanisha ni msaliti, nandio maana hoja zake nyingi bungeni zimefanyiwa kazi na kuboresha shuguli za bunge na serikali kwa ujumla, wakati hoja za wengine hata pale ambapo hua nzuri na zenyenguvu kabisa hukataliwa bila hata kusikilizwa.

Baada ya kusema hayo mengi niliosema, ninaomba kumalizia kwakusema, Mh. Zitto anahitajika CHADEMA sikwasababu bila yeye CHADEMA haiwezekani kuendelea HAPANA HATA KIDOGO!

Character X,
Maneno mazuri ya mtu mwenye fikira ambazo zinaonekana adimu sana siku hizi humu JF. Kwa kifupi naona kuna matatizo mawili tu ndani ya CHADEMA;
  1. Mtazamo wa Mbowe wa kuijenga CHADEMA unategemea uwepo wa migongano na CCM ikiwa ni pamoja na vurugu kama zile za Arusha n.k., iwe ya halali au la. Wakati Zitto/Kitila n.k. wanaona hizo ni siasa za kizamani. Wanaona wakati wa kutumia ubongo zaidi umefika badala ya kuburuza mashabiki wao kwa mambo ya kijinga umeadia. Hivyo wanaona CDM inahitaji msomi mwenye mtazamo huo na sio Mbowe.
  2. Kuna viongozi ambao madaraka yameshanza kuwanogea (Mbowe n.k.) na hawako tayari kuyaachia, kwa hiyo wanajaribu kutumia kila njia kubakia nayo. Hii ni pamoja na kujaribu kuwaondoa viongozi maarufu wenye nia na uwezo wa kumpindua Mbowe. Na katika kufanya hivyo, upendeleo (nepotisim), ukabila, pesa n.k. vimetumika.
Kwa hiyo kwa mtazamo wangu, tatizo la CHADEMA sio Zitto au Kitila, bali ni
Mbowe asiyetaka kubadilika au kuachia madaraka. Kwa hiyo, yeyote anayekitakia mema CHADEMA na taifa kwa ujumla, hana budi kumshinikiza Mbowe ili ang'atuke ili chama kiweze kuwa na mabadiliko.
 
Mjadala umefungwa na tunasubiri siku ziishe haya yote unayohubiri yatapata muafaka!!!!!!!

You never step on a snake and relax on there!!!!
 
Hakuna cha kutafakari hapa...ufisadi na uvivu wa kufikiri kwa wana chadomo ndio unapelekea kuchagua namna ya kujadili suala hili.

Kwa mtu mwenye busara angehoji hivi:-

...........Ni kwa nini Zitto Kabwe anaungwa mkono na hata wasio wana chadomo (wakiwepo hao mnaolazimisha kuwa ni wana ccm...ni sijui ni kwa utafiti gani )

Hao unaojaribu kuwalinganisha na Zito ni ukosefu wa shukurani na nidhamu kwa mtu kama Zitto....ni sawa na kulalama kuwa kwa nini vyombo vya habari vinalalamika kwa C Ronaldo kukosa heshima ya mwanasoka bora wa dunia huku ukitolea mfano wa mchezaji wa timu ya Kanjibai Fc ya india (kama ipo)kutopewa kipaumbele na vyombo vyao vya habari kwa kunyimwa nafasi inayofanana na hiyo huko nchini kwao.

Kwa maelezo rahisi ni kuwa...hizo habari za kina Hamadi, Mansor na Kafulila waeleze wanaohusika nao....Zitto ni wa taifa zima sio wa chadomo pekee.

What do you mean taifa zima? Hakuna chama cha taifa zima. Zitto is a perfect child of two worlds- ya upinzani na chama tawala the reason why anakuwa msaliti. Either he belongs to the ruling party or to the opposition. If he is in both worlds he must be a traitor. You cannot serve two masters.
 
Sijui kwa nini anahangaika na kukomalia chadema wakati anasema hakuna democrasia, aondoke aende chama chenye hiyo democrasia
 
Mwanasiasa imara,hutuliza mambo yanapoenda mrama,hasa pale hisia za watu zinapoambatana na mtu badala ya CHAMA,kama hivi sasa inavyojionesha ya kuwa Mh. ZITTO,kuwa ana watu wake wanao mwamini sana kuwa ndio shujaa wao.nakushauri kijana mwenzangu ZZK,watulize hao wafuasi wako,waambie mimi si maarufu kuliko chama,Chama ndicho kimenifikisha hapa,.okoa wimbi la wanachama kutimkia kizani tena,kubali kuonywa na kuonyeka.ama la sivyo ukishindwa kufanya hivyo Ondoka nao anzisha Chama chenu ,itakuwa bora kuliko kukalia mbeleko unayo dhani imetoboka.

CHADEMA ITADUMU,AKINA ZITTO,MBOWE NA SLAA WATAPITA,KAMA SI UMRI ,historia itawahukumu kwa matendo yao.peoples power.
Zitto alishawatuliza kitambo wafuasi wake. Sema tu kuwa watu wanajitambua na wamechoka kuonewa. Aidha, wanachama hao wa chadema wanaendeleza ile dhana inayotekelezwa na viongozi na wafuasi wa chadema kuwa hawataacha mpaka kieleweke. Hivyo wanachama na wafuasi wa zitto hawachaacha kupigania haki mpaka kieleweke
 
Mwanasiasa imara,hutuliza mambo yanapoenda mrama,hasa pale hisia za watu zinapoambatana na mtu badala ya CHAMA,kama hivi sasa inavyojionesha ya kuwa Mh. ZITTO,kuwa ana watu wake wanao mwamini sana kuwa ndio shujaa wao.nakushauri kijana mwenzangu ZZK,watulize hao wafuasi wako,waambie mimi si maarufu kuliko chama,Chama ndicho kimenifikisha hapa,.okoa wimbi la wanachama kutimkia kizani tena,kubali kuonywa na kuonyeka.ama la sivyo ukishindwa kufanya hivyo Ondoka nao anzisha Chama chenu ,itakuwa bora kuliko kukalia mbeleko unayo dhani imetoboka.

CHADEMA ITADUMU,AKINA ZITTO,MBOWE NA SLAA WATAPITA,KAMA SI UMRI ,historia itawahukumu kwa matendo yao.peoples power.
Kwani wewe ndani ya chadema mpaka uanze kutupigia kelele kwenda zako hiki chama ni cha mnowe na slaa wengine wafagiaji tu tena usirudie kuzungumza habari za chadema mwenye uhuru wa kuongea ni mbowe na slaa peke yao wengine kimya.
 
Sijui kwa nini anahangaika na kukomalia chadema wakati anasema hakuna democrasia, aondoke aende chama chenye hiyo democrasia
Njia nzuri ya kurekebisha mambo si kukimbia matatizo. Ni kuyarekebisha kupitia mfumo na taasisi iliyopo. Zitto kakilea chadema mpaka kimekuwa. Wengine wameingia cdm wakati zitto akiwa anakipigania. Sema chadema kimekuja kuharibiwa na hawa wachaga ambao wanakumbatia ukabila na ukanda kwenye chama hiki
 
Sijui kwa nini anahangaika na kukomalia chadema wakati anasema hakuna democrasia, aondoke aende chama chenye hiyo democrasia
Na wewe unaikomalia chadema ya nini ondoka na wewe hatukutaki wanachama kama wewe ni mzigo jitoe nenda kwenye lichama lenu.
 
Back
Top Bottom