comrades habari,
Siasa za upinzani nijuu ya hoja tofauti na mawazo mbadala ilikuleta ufanisi bora zaidi katika nchi hiyohiyo moja. Kwaio hoja hapa ni kuboresha ufanisi wa serikali ilikuboresha maisha ya kila siku ya mwananchi wa sasa na vizazi vijavyo.
Hapa swala si uadui na uhasimu tu na chuki zilizo jengwa juu tofauti ya rangi za bendera zetu.
Upinzani sio maana yake uwe adui wa kila mtu ilimradi tu yuko upande wa pili., Laah hasha sivyo hata kidogo.
Kuwa mpinzani haimaanishi huwezi kukubaliana na hoja sahihi za mtu wa upande wapili, Actually ilikuwa mpinzani makini unahitaji kuaminiwa na upande wako lakini na upande wapili pia.,
Tatizo ninalo liona hasa changamoto anayokumbana nayo ng. Zitto, ni ule uswahili, ubinafsi, USHAMBA wa watu wengine ndani ya chama wanao mtazama nakushindwa kumuelewa tu., wanadhani zitto anafanya anayoyafanya ilikupata sifa nakusahau kwamba kiongozi makini huhitaji kuweka misingi wakati mwingine., Lazima afanye gestures (kwakumaanisha kabisa) zinazo onyesha unachokiamini ilikujenga misingi sahihi kwa wale unao waongoza.
zipo hoja kwamba mbona zitto anaaminika na serikali ya CCM kuliko wengine, anahongwa!,.
Sasa niseme tu wasi, Zitto kuaminika na watawala is a BIG plus to the change movement.
Namimi nafkiri amefanikiwa kujenga imani kwao si kwa Usaliti ila kwa kazi nzuri ambayo ameifanya so far, kwa professionalism aliyo ionyesha so far.,
Sasa
Kama aliyo yaeleza hapa JF kwenye threads kadhaa alizo ziandika kujitetea kuhusu maswala kama lile la kuamua kutogombea ubunge mwaka 2010, Na kama ni kweli yale aliyo yaeleza kua amefanya bungeni, na kwenye chama, na michango yake ndani na nnje ya nnchi ameyafanya., na kama ni kweli mipango aliyoieleza ni kwasababu alizozieleza hapa na sivinginevyo, na mtazamo alioueleza hapa ndio mtazamo wake halisi.
Basi mimi sioni shida hata kidogo, namuona mtu mwenye uwezo,Nia na sababu ya kufanya mabadiliko ya kweli kwenye siasa zetu, actually na muona mtu mwenye the right mentality for leadership.., if this is what his heart is. then, I think THERE ACTUALLY MIGHT BE MORE TO THIS PARTY STRIFE THAN MEETS THE EYE.
Ninachosema hapa ni kitu gani, Zitto kujenga kuaminiwa na seeikali ya CCM hakutakiwi kumaanisha ni msaliti, nandio maana hoja zake nyingi bungeni zimefanyiwa kazi na kuboresha shuguli za bunge na serikali kwa ujumla, wakati hoja za wengine hata pale ambapo hua nzuri na zenyenguvu kabisa hukataliwa bila hata kusikilizwa.
Baada ya kusema hayo mengi niliosema, ninaomba kumalizia kwakusema, Mh. Zitto anahitajika CHADEMA sikwasababu bila yeye CHADEMA haiwezekani kuendelea HAPANA HATA KIDOGO!