Zitto Kabwe More Than Meets the Eye!

Zitto Kabwe More Than Meets the Eye!

Hii kazi chafu huku mitandaoni hazitamwokoa Zitto

Mark my word!!
 
Last edited by a moderator:
Bora CCM itawale kuliko kuwa na Chadema yenye muono wa CCM.

Kuondoka kwa Zitto itakuwa fundisho kuu ktk kuheshimu taratibu tulizojiwekea.
 
Hilarious with a serious meaning.

yeah well, that's your take, I respect it., you have a right to your own opinion. I Must not remind you though that its a right your own "opinion" NOT your own "facts"
 
Hilarious with a serious meaning.

yeah well, that's your take, I respect it., you have a right to your own opinion. I Must not remind you though that its a right to your own "opinion" NOT your own "facts"
 
Character X, naomba nikuulize jambo moja tu; kama leo uchaguzi huru ungefanyika Chadema na upande wa MM, M1, M2 na M3 usiibuke kidedea, unadhani huo upande ungekubali kubaki ndani ya Chadema chini ya uongozi ule ule walioushutumu kwenye waraka na kupanga njama za siri kuuondoa madarakani?
 
Last edited by a moderator:
If Zito tried to bring a leadership change not through election but an internal coup. There are two options with the coup plotting if caught in the game expulsion is a logical conclusion and if successful the previous leadership will either smart up and remain in the party. A coup is an option taken when voluntary removal can be difficult or some agreement has been breached. Margaret Thatcher was ousted from the party leadership when she became too authoritarian. Now is the current leadership clique based to warrant a coup or is power lust that drove the manifesto plot. So my comrade if Zito was caught in the manifesto plot there is no way but showing him the door out of leadership else it will lead to management problems. The CC hasmade the correct decision if proven. So far Zito has to see if he can revive his political future within or out of CDM.
 
Najiuliza haya matamko ya viongozi hewa wa CDM wanajipambanua kuwa ni viongozi wa CDM wakiwa either walishafukuzwa au si viongozi kabisa wa chama.

Na cha ajabu ni magazeti ya chama tawala na serikali yakiongozwa na Habari leo, Jambo leo, uhuru, majira.

Sasa najiuliza kama Zitto hausiki katika haya kwanini hatoi tamko ya kulaani au kutakana hayo??

P
 
kwani hukuona waliondaa press conference walikuwa wana ccm?indiketa zinaonyesha Zito na unafiki wake umefikia mwisho
 
Wadau mtakubaliana nami kuwa baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumvua nyazifa zote za uongozi Mh. Zubery Zitto Kabwe kumekuepo maneno mengi na mijadala isiyoisha kumuhusu yeye. Baadhi ya watu wamemtetea na wengine kumponda. Kitu cha kushangaza sana ni hili swala la baadhi ya viongozi au wanasiasa wa vyama vingine kumpigania mithili ya kwamba ni mwanachama mwenzao katika vyama vyao. Nimekua nikijiuliza mfano ni kwa nini baadhi ya wanachama au viongozi wa chama tawala wanamtetea sana. Au ni kwanini baadhi ya watu wanaponda chadema na kusema imemuonea? Kuna nini hapa? Mbona hao hao wanaoponda uamuzi wa Chadema kumvua uongozi Zitto na vyama vyao kwa kipindi fulani vimefanya hivyo hivyo na watu hawakupiga kelele? Hebu ngoja niweke mifano michache hapa:
1. CCM muda si mrefu sana umepita walimvua uongozi Mh. Mansor Yusuf Himidi Mbunge wa Mjini Magharibi huko Zanzibar lakini watu hawakupiga kelele hivi!
2. CUF walimvua uongozi na uanachama Mh. Hamadi Rashid Mbunge wa Wawi lakini watu hawakupiga kelele hivi?
3. NCCR Mageuzi walimsimamisha Mh. David Kafulila Mbunge wa Kigoma Kusini lakini watu hawakupiga kelele hivi!

Sasa kwa nini Zitto ? Na kwanini Chadema ndio ionekane mbaya sana kwa swala hili?
TAFAKARI! TOA JIBU!
 
Wana JF,

Katika mkutane wake na waandishi wa habari baada ya kuvuliwa uongozi ndani ya CHADEMA zito alitamka kuwa wananchi kwanza halafu vyama baadaye. Je huu usemi wa Zito una ukweli wowote? Hebu tujikumbushe kama Zito akiwa mbunge na mwenyekiti wa kamati alishawahi kuongelea mambo kadhaa yanayohusu maslahi ya wananchi.

La kwanza ni kuuawa mara kwa mara kwa wananchi wanaozunguka mgodi wa north Mara. Je, Zito aliongea nini?

La pili ni kuuawa kwa Mwangosi, Kutekwa na kuteswa kwa Dr. Ulimboka na Kibanda, nini ilikuwa kauli ya Zitto?

La tatu ni malimbikizo ya mishahara ya walimu na wafanya kazi serikalini. yeye akiwa msimamizi wa hesabu za serikali angeweza kutumia nafasi yake kujua ni kwa nini wafanyakazi hawalipwi haki zao na kusimamia serikali kuzilipa. Tukumbuke kuwa maslahi ya wafanyakazi ndiyo yanaifanya elimu inadidimia.

Akiwa kama mwenyekiti wa mashirika ya Umma alitakiwa kuingilia na kutolea tamko mgogoro wa wafanyakazi na PPF. Yeye kakaa kimya!

Hayo na mengine mengi yananifanya niamini kuwa mara nyingi kauli za Zitto si za dhati.
 
Umefikiri critically na kizalendo!watanzania wote ni ndugu, tusiamini katika hoja ya ushindi kama ya ushabiki wa yanga na simba, bali ktk hoja ya kumtoa mtanzania ktk umaskini. Kinachoibomoa Chadema ni uchu wa madaraka tu.Vyama za siasa haviangalii asilimia kubwa ya watanzania ambao si wanachama wa chama chochote Ndio tunaopiga kura ya maamuzi ya mstakabali wa nchi yetu.hizi ni kura ambazo hazitabiriki.Chadema tunaihitaji sana kuweka uwiano wa maamuzi ya nchi hii hivyo isijiamini kwa hatua iliyofikia maana hata NCCR mageuzi ilikuwepo na ilikuwa na nguvu mpaka Mwl Nyerere ilimbidi arudi majukwaani.Chadema wakae meza moja na Zito maana ukweli haupingiki hoja zake Bungeni ndio zimeifanya ikapewa imani na watanzania.

.Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Panya anavuta mkwanja toka gambani,Hata mwandiga wanalijua hili
 
Zitto ni MwanaCCM mwaminifu kupitia CHADEMA, ndiyo maana wanampigania ili waweze kufanikiwa malengo yao.

Baadhi ya wanaomtetea ndani ya chama bila shaka ni mtandao wake
 
Ndugu yangu Zitto ni mwanasiasa mchumia tumbo, bila kuelezwa hayo ya ndani kabisa wewe jaribu kuangalia tu nyendo zake wakati wote wa harakati za viongozi wa CDM ktk kuimarisha chama yeye alikuwa anafanya nini... bora ukamfadhili m....kuliko Zitto wao
 
wanamtetea kwasababu wanamuamini. Na wanahisi anatendewa isivyo haki

CCM ni chama tawala. Wanamtetea Zitto ambaye anapaswa kuwapinga kwa mambo mengi. Hii inaingia akilini? Yaani mpinzani wako uone anaonewa pale anapowajibishwa kwa usaliti? Ha ha haaa! Ni sawa na jirani aje juu kwa kuwa umemrudisha kijijini ndugu ambaye haaminiki akiwa mjini. Ukiona hivyo alikuwa anamwibia sukari na vitunguu kama hupo nyumbani. Kama CCM wameumia sana na wanaona Zitto ni jembe, kwa nini hawamchukui akasaidiana na vijana kuhakikisha chama kinabaki madarakani? Watetezi wa Zitto walikuwa wanapata indani wa CDM. Mbona hawakumtetea hivyo Kafulila na Hamadi? Halafu si hao hao walipingana na Mansuri na kumtema? Hii ajabu kweli kweli. Zitto ni mwanachama na hawezi kuwa juu ya chama. Mambo hujadiliwa kwa uwazi na siyo kwa kupinduana. Time will come when Zitto will realise he was been used and that time is just around the corner.
 
Zitto kabwe kama nilivyo mimi ninaeandika thread hii, nimwanachama halali wa chama cha demokrasia na maendeleo ana HAKI ya kuchaguliwa kushika nafasi yoyote katika chama. Kama mkakati wake na wenzake ungefanikiwa na akawa mwenyekiti halali basi angekuwa amefanikiwa ku exercise HAKI yake anayopewa na katiba zote mbili- ya CHADEMA na ya Jamuhuri ya Muumgano wa Tanzania.
Tatizo pekee la andiko lile nipale lilipo Toa shutuma na kueleza madhaifu ya mwenyekiti HALALI wa chama nje ya utaratibu wa vikao kama katiba inavyoelekeza, hilo ni KOSA! nanimesema na Zitto amesema pia kwamba atafuata taratibu zote kama atakavyo elekezwa na kamati kuu, ili kulifikisha jambo hili mwisho wake.,

Ndugu Character X, nimependa analysis yako na ninaona unasogea karibu kulekea kwenye Haki na Ukweli. Mimi nina haya yafuatayo.

1. Hakuna ushahidi wa Kumlink Zitto na huo Waraka.
Iwapo CC ya Chadema ilimtia Hatiani Kitila kwa kukiri kuhusika na huo Waraka, Basi ingetumia angalau testimony hiyo hiyo ya Kitila kusema kwamba Zitto hahusiki na huo waraka. Angalau basi CC ingekuja na Azimio la kuchunguza kuona kama Zitto kweli anahusika nao au hahusiki nao, hiyo ingekuwa Fair.

2. Ninavoona mimi ni kwamba ndani ya roho yako kuna chembe chembe nyingi za Justice, lakini pia unaipenda Chadema sana, kiasi kwamba umetambua CC imekosea, lakini ili kukikinga chama kisiyumbe zaidi umeamua kujaribu kuwa balanced, kwa kuyakubali matokeo ya CC lakini at the same time unafahamu kwamba zille accusations dhidi ya Zitto ni dubious accusations. SIMAMIA HAKI NA UKWELI NDUGU YANGU, USIKUBALI KUWA VUGUVUGU.

3. Ule waraka umeanalyse strength za Mbowe na weakness zake, na pia ukiusoma vizuri umeanalyze Strength za Zitto na weakness zake. HAWA NI WATU WALIOKUWA WANAFANYA ANALYSIS YA KISOMI KUANGALIA UWEZO WA KUCHAGULIWA WAMTAKAYE AU POSSIBILITY YA KUTOKUCHAGULIWA KWAKE, KWA ANALYSIS HIYO HAWAKULENGA KUMCHAFUA MBOWE WALA ZITTO, BY THE WAY WARAKA WENYEWE ULIKUSUDIWA KUWA KWA AJILI YA INSIDERS WA MKAKATI WA USHINDI, NA WALA HAUKUKUSUDIWA KUENEZWA KWA WANACHAMA, KWA HIVYO HOFU YA KUMCHAFUA MWENYEKITI CHAMANI NI YA KIZUSHI. KAMA WANGEUVUJISHA KWA WANACHAMA USINGEKUWA TENA KUWA NI MKAKATI WA USHINDI KWA MAANA MBINU ZAO ZINGEKUWA ZIMEANIKWA WAZI!.

NDUGU CHARACTER X, SIMAMIA UKWELI TUJENGE UPINZANI WA UKWELI!
 
Back
Top Bottom