well, labda nianze kwa kueleza maana za maneno haya mawili kama ninavyo yaelewa Kisha nitaeleza alichokifanya zitto na wenzake nikutu gani.
Uhaini- ni njama zakuuondoa utawala halali kwa nguvu yakimapinduzi nje ya utaratibu sahihi wauchaguzi na KABLA YA WAKATI WA UCHAGUZI.
Usaliti- ni vitendo vinavyo fanywa na mtu wa ndani mtu aliye aminiwa na siri za ndani, anapotoka kwa makusudi na kwasiri nakufanya mambo ilikunufaisha kundipinzani ilihali akiendelea na kundi lake kanakwamba hafanyi vitendo hivyo vya kuliuza kundi lake.
Sasa kwakutumia tafsiri zote hizi simuoni zitto kama muhaini wala msaliti, ninachokiona ni mtu ambaye amekosea utaratibu, kwakushiriki kwenye waraka wenye kutoa shutuma dhidi ya viongozi wenzake nje ya utaratibu wa katiba ya chama.
sio mhaini kwasababu ile ilikua mikakati tu yanamna ya kushinda kwenye uchaguzi halali wakati ukifika.
Sio msaliti pia kwakua hakuna ushaidi unao onyesha zitto akitoa siri wala kufanya vitendo kwaajili ya chama kingine nakukiumiza chadema ilihali akiwa chadema bado.