Inawezekana kabisa una hoja, ila umeiua hoja yako mwenyewe kwa kufanya uchambuzi wa upande mmoja (biased analysis) ambao bila shaka yoyote hitimisho lako litaegemea upande mmoja. Kwa nini nasema hivyo; ni kwa kuwa uchambuzi wako umeegemea katika maelezo na utetezi unaoaminika umetoka kwa mtuhumiwa Mh. Zitto Zuberi Kabwe!
Kwa haraka haraka niseme sijaona umechambua vipi tuhuma alizoelekezewa; kwa mfano kupokea pesa kutoka serikali inayoongozwa na chama pinzani, kuzigawa pesa hizo kwa baadhi ya watu ndani na nje ya chama wanaoaminika ni mamluki, kuwa na mawasiliano ya siri na taasisi nyeti za usalama mawasiliano yanayothibitisha mipango ya siri ya kukihujumu chama, n.k.
Pengine ungejaribu kuzichambua tuhuma zinazomkabili angalau nusu yake, ukaleta uchambuzi wa utetezi alioutoa kwa kila tuhuma aliyoelekezewa, kisha ukatoa hitimisho (conclusion) binafsi ningeona thread yako iko neutral kama nilivyo neutral (sina upande) katika kinachoendelea ndani ya CDM lkn sina upande katika siasa za nchi hii, bali kukweli wa moyo wangu nina upande katika maslahi mapana ya nchi yangu na watu wake.