Wanabodi,
Zitto Kabwe mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Chadema na Naibu Katibu Mkuu (Bara), Naibu Kiongozi Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma.
Kwa mujibu watu wa karibu wa Zitto Kabwe, yupo tayari kuishi na kufa akiwa kwenye mapambano kama ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi, ambaye ni kipenzi chake alianza mapambano na aliyekuwa Mfalme wa Ethiopia Haile Mariamu, akiwa na umri wa miaka 19 na hatimaye kufanikisha mapambano yake ya kuingia Ikulu akiwa na umri wa miaka 36.
Wafuasi wa Zitto Kabwe wametoa onyo kwa Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho kuwa mkakati wowote mchafu wa kutaka kumkwamisha Zitto kugombea urais wakati ndiye anayekubalika utakigharimu chama hicho kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 wafuasi wa Zitto ambao wengi ni kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Tanga, Mtwara, Lindi, Singida, Pwani, Ruvuma, wanapinga mkakati wa Mbowe na Dr Slaa kutaka kumzuia endapo watathubutu kumzuia basi wataamua kuwapigia kura wagombea wa vyama vingine lakini si Chadema.
Zitto Kabwe inasemekana ndiye ambaye anaungwa mkono na karibu vijana wote wa nchi hii walioko ndani na nje ya Chadema, na hasa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, Itakumbukwa mwaka 2010 wakati wa kampeni za ubunge jimboni kwake Zitto Kabwe aliwaambia wapiga kura wake wampe muhula wa mwisho mwaka 2015 hatagombea tena ubunge bali atagombea urais ili aweze kuwatumikia Watanzania wote kwa ujumla wao.