Mkuu Mvaa Tai, the motive behind ni nia dhalimu iliyofichika ya mleta mada ili kutengeneza reaction fulani kwa mada yake!.
Hebu msome hapa!.
"Kwa mujibu watu wa karibu wa Zitto Kabwe", yupo tayari kuishi na kufa akiwa kwenye mapambano " Huu ni uzushi tuu, hakuna watu wowote wa karibu na ZZK, bali ameisoma makala ya ZZK kuhusu Zenawi na sasa anaitumia kumjengea chuki ZZK ili kuwatia hofu wana Chadema kuwa ZZK yuko tayari kupambana hadi kufa ili kuwa mgombea wa Chadema!.
"Wafuasi wa Zitto Kabwe wametoa onyo kwa Mbowe" Huu pia ni uzushi, hakuna mfuasi yoyote aliyetoa onyo lolote kwa yeyote!.
"mkakati wowote mchafu wa kutaka kumkwamisha Zitto kugombea urais" - Huu pia ni uzushi ili kuonyesha kuna mkakati wa kutaka kumkwamisha ZZK kugombea!
" ZZK ndiye anayekubalika" Hakuna survey yoyote iliofanyika kuthibitisha kuwa ZZK ndiye anayekubalika!
"wafuasi wa Zitto ambao wengi ni kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Tanga, Mtwara, Lindi, Singida, Pwani, Ruvuma" Huu pia ni uzushi kwa lengo la kuwaaminisha watu kuwa ni kweli Chadema kina ukabila, hivyo kujenga dhana kuwa ukiondoa kanda ya Kaskazini, wafuasi wengine wote wa Chadema wa mikoa yote hiyo ni wafuasi wa ZZK!.
"mkakati wa Mbowe na Dr Slaa kutaka kumzuia ZZK" huu pia ni uzushi, hakuna mkakati wowote wa kiongozi yoyote wa Chadema kumzua mwanachama yoyote kugombea nafasi yoyote!.
"endapo watathubutu kumzuia basi watamuua kuwapigia kura wagombea wa vyama vingine lakini si Chadema" huu pia ni uzushi wa tisha toto ili kujenga hoja kuwa ushindi kwa Chadema 2015 ni kupitia kwa ZZK pekee, bila ZZK hakuna ushindi kwa Chadema!
"Zitto Kabwe inasemekana ndiye ambaye anaungwa mkono na karibu vijana wote wa nchi hii walioko ndani na nje ya Chadema, na hasa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini," huu pia ni uzushi wenye lengo la kumjengea chuki ZZK!.
Itakumbukwa mwaka 2010 wakati wa kampeni za ubunge jimboni kwake Zitto Kabwe aliwaambia wapiga kura wake wampe muhula wa mwisho mwaka 2015 hatagombea tena ubunge" Ni kweli ZZK aliomba mhula wa mwisho ila sio kweli aliaga ili akagombee urais bali alipanga kuingia kwenye a totally diferent venture away from politics!.
Lengo ni "ill motives"!.
Pasco.
NB: Pasco wa jf, sio mwanachama, mfuasi au mshabiki wa Chadema, bali kama mwanahabari, ninayo direct access kwa top leadership ya Chadema, kama ilivyo kwa CCM, CUF na vyama vingine vyote, na nimeiunga mkono presidential bid ya ZZK kupitia Chadema, kwa CCM naiunga mkono presidential bid ya EL, kwa CUF, Prof. Lipumba ndie mgombea urais wa kudumu wa CUF bara na Maalim kule Zanzibar ila naunga mkono bid ya Jussa kumpokea Maalim, 2020!.