Zitto Kabwe: Kama ningepata mamlaka ningefanya tofauti

Zitto Kabwe: Kama ningepata mamlaka ningefanya tofauti

Katika kila mawazo yako utoayo Kuna ujenzi wa taifa!! Mimi huwa Ni msikilizaji hodari wa hoja zako!! Mkuu na ndo role modal wangu uliyefanya nifatilie siasa tokea unachukua ubunge wa kigoma!! Ila Sasa mtani wangu Kuna tatizo hapa!! Business idea is always sweet when you think it @ the future!! But it become bitter when your idea came into action!! Nimesoma waraka wako!! Unatia moyo saana! Na unaonesha Ni jinsi gani umeumiza kichwa! Katika kutafakuri mambo amaizing!!
Swali ni je? Tokea umekuwa mbunge mawazili wote waliopita hamjawahi kuwa marafiki? Nimeuliza kwa sababu Hilo wazo labda lingewafikia kama private idea! Nje ya bunge mkiwa mnapata chakula!!
Labda pia lingewafikia kama ungewaita Hao mawaziri ukawaelezea kama ulivyoelezea hapa sisi tusiokuwa na elimu tukaelewa! Maana ukilifikisha bungeni kwa njia ile mnayotumia I think ndo maana viongozi hawalipitishi kwa maana bungeni wabunge wote mnaonesha kukinzana tu hata kwenye hoja za maana!! Mara upande mmoja unatoka Nje! Mara upande mwingine wao Ni mwendo wa ndiyooo!!
Na je Katika kuchimba hizo vanadium na chuma umeme up utakaotumiwa?? Je? Umeme unaozalishwa Tanzania unaweza kutosheleza hayo machimbo na kuyeyusha hizo materials mpaka zikawa final product? Na je investment itagharimu kiasi gani? Umetaja ndege, na umetaja rufiji hydroelectric power! Je unaona sio muhimu?
Mwisho mimi naona Katika kuwaza kwako umewaza vyema 150% na [HASHTAG]#ningefanyatofauti[/HASHTAG] inatakiwa iwe jawabu letu sisi!! Ibadilishe iwe [HASHTAG]#nitafanyatofauti[/HASHTAG]. Unaweza kufanya tofauti ukiwa mbunge kwa kutafuta investors from abroad ukawapa hizo ideas wakafanya feasibility study! Then ukawakabidhi mikononi mwa serikali!! Hiyo ndo tunaweza ita [HASHTAG]#ningefanyatofauti[/HASHTAG].

Kwasababu usipochaguliwa kuongoza nchi idea yako itaishia hapo??
Mwisho nakuomba radhi kama Kuna sehemu sijatumia lugha mbadala! Eg matusi
 
NingefanyaTofauti

Na Zitto Kabwe

KWA miaka mingi nimekuwa mtu ninayeamini katika kujipa muda wa upweke na kutazama dunia iliyonizunguka na kujiuliza maswali ama kunihusu mimi binafsi au kuhusu nchi yangu na Afrika. Waingereza wangesema self reflection lakini ninapenda kutumia neno la lugha ya Kiswahili; kutafakari. Ninaamini kwamba ni muhimu kwa kiongozi kupata muda huu muhimu.

Siku chache zilizopita, nilijipa muda huo wa utulivu kwa ajili ya tafakari. Swali kuu nililokuwa nikijiuliza ni hili; kwamba kama ningekuwa nimepewa mamlaka ya kuongoza Tanzania nini ningefanya tofauti na wanaoongoza sasa?

Katika tafakari hii nilikumbuka safari niliyofanya wilayani Ludewa mwaka 2011 kukagua na kutoa nguvu kwa uwekezaji wa kimkakati wa uchimbaji wa madini ya chuma na makaa ya mawe na kuweka msingi wa viwanda mama nchini kwetu. Unaweza soma chapisho la blogu ya safari hiyo hapa An Eye Opener Week-long Visit to South Tanzania 1500MW Electricity Complex. Nadhani ningeanza na mradi huu kabla ya kitu kingine chochote. Nina sababu za kufikia hitimisho hilo.

Mchuchuma na Liganga ni nini?

Madini ya chuma na makaa ya mawe ndio msingi wa maendeleo ya viwanda duniani kote. Nchi yetu ina madini haya yote kwenye eneo moja, wilayani Ludewa mkoa wa Njombe. Hakika Mungu alitupenda, maana aliumba dunia na akaisanifu Ludewa na kuiweka Tanzania ili iwe chanzo cha viwanda mama.

Katika eneo la Mchuchuma kuna mashapo yenye tani bilioni 1.2 makaa ya mawe yenye uwezo wa kuzalisha Umeme 600MW kwa miaka 150. Makaa hayo pia hutumika kuyeyusha chuma na kuzalisha chuma cha pua. Vilevile eneo la Liganga lina mashapo ya madini ya chuma tani bilioni mbili ambayo ndani yake kuna madini yenye thamani kubwa ya Titanium na Vanadium.

Ujenzi wa kilometa moja ya reli unahitaji chuma cha pua (steel) chenye ubora wa hali ya juu kiasi cha tani 40 mpaka 60. Tanzania tunajenga kilomita 1200 za reli kwa sasa hivi na baadaye zitaongezeka kwa vipande vya Tabora - Kigoma, Kaliua - Mpanda - Karema, Uvinza - Musongati na miradi mingine kama Mtwara - Mbamba Bay, Ruvu - Tanga, Tanga - Musoma - Kigali nk. Kwahiyo basi, Tanzania itahitaji sio chini ya tani 500,000 za chuma cha pua (steel) katika kipindi cha miaka michache ijayo.

Afrika nzima inajenga reli za kisasa na zote zinahitaji chuma kwa ajili ya kujenga njia za reli. Kenya na Ethiopia wamemaliza hatua za kwanza za reli zao ambapo Kenya imeshajenga kilometa 485 kutoka Mombasa mpaka Nairobi na Ethiopia kilometa 760 kutoka Addis Ababa mpaka Djibouti. Miradi yote hii mataruma ya reli yameagizwa kutoka nje na kuletwa Afrika na hivyo kuzalisha ajira huko kwenye nchi hizo (ambazo mataruma hayo yamezalishwa ).

Fedha za miradi hii zitakwenda nje ya nchi, Waafrika hawatafaidika kabisa. Tanzania nayo inakwenda njia hiyo hiyo licha ya kwamba ina madini ya chuma na makaa ya mawe ya kuzalisha chuma cha pua ambacho huzalisha mataruma ya reli na bidhaa nyingine kadha wa kadha za ujenzi wa reli. Tanzania ingeamua, ingeweza kulisha miradi yote ya reli chuma kutoka Ludewa katika nchi za Kongo, Zambia, Angola, Uganda na Rwanda ambao wote wana miradi ya ujenzi wa reli na wamepanga kuagiza chuma kutoka China na kwingineko.

Bei ya tani moja ya chuma kwenye soko la dunia ni dola za Marekani 600 mpaka 1000. Kwa hiyo Tanzania ikizalisha chuma tani milioni moja tu kwa mwaka, inaweza kupata mapato ya fedha za kigeni kati ya dola milioni 600 mpaka dola bilioni moja kwa mwaka. Kwa mashapo yaliyopo Tanzania, tunaweza kuzalisha kiwango hicho cha chuma kwa miaka zaidi ya 2000 na chuma cha Ludewa kisiishe.

Kwa hakika mahitaji ya chuma yatakuwa ni makubwa na tunaweza kuzalisha na kuuza nje mpaka tani milioni tano kwa mwaka. Hivi sasa nchi ya Australia ndio inaongoza duniani kwa kuuza chuma kingi zaidi. Mwaka 2017 waliuza tani milioni 49 za chuma na kupata dola za marekani bilioni 49.

Jambo kubwa sana ambalo Tanzania imebahatika ni kwamba mashapo ya chuma yana madini mengine yenye thamani kubwa zaidi. Kwa mfano Vanadium ya Ludewa inauzwa tani moja dola 50,000 katika soko la dunia. Katika kila tani milioni moja ya chuma kutoka Ludewa, kuna tani 80,000 ya Vanadium. Tukiuza madini haya tunapata fedha za kigeni dola za kimarekani bilioni nne kwa mwaka.

[HASHTAG]#NingefanyaTofauti[/HASHTAG]

Unapokuwa na mamlaka ya uongozi wa nchi unakumbana na changamoto nyingi sana na moja ya changamoto ni kuamua uanze na nini katika vipaumbele vya nchi ili kupiga hatua za kimaendeleo. Kiongozi mwenye maarifa huanza na mambo ambayo yatamwezesha kupata rasilimali fedha ili atekeleze majukumu mengine. Ni dhahiri hapa Tanzania tuna changamoto ya miundombinu ya usafirishaji, reli, barabara na hata usafiri wa anga.

Viongozi wetu wa sasa wameamua kuanza na hayo kwa kutumia fedha za kodi au mikopo ghali yenye riba kubwa kutoka mabenki ya biashara ya nje. Wameanza na ujenzi wa reli wa dola bilioni saba, ununuzi wa ndege wa zaidi ya dola bilioni moja ( Dreamliner ‘Terrible Teen’) imenunuliwa kwa dola milioni 224 na hata ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Rufiji maarufu kwa jina la Stiglers Gorge litakalogharimu dola bilioni 3.5.

Yote haya yanahitaji kukamua kodi wananchi na kuchukua mikopo inayokuza Deni la Taifa. Yote haya yanasababisha mzunguko wa fedha nchini kuwa mdogo kwa sababu fedha zinatoka nje ya nchi kulipia wakandarasi na kununua malighafi kama chuma.

Ningekuwa na mamlaka ningeyafanya haya yote, lakini kabla ya kufanya hayo, ningeanza kwanza kwa kufanya jambo moja kubwa ambalo lingenipa fedha za kufanya hayo. Ningefanya tofauti.

Ningeanza na mradi wa Mchuchuma na Liganga kwa kuhakikisha kuwa uwekezaji unaanza mara moja na uzalishaji wa chuma na makaa ya mawe unafanyika bila kuchelewa. Ningehakikisha kuwa ndani ya miaka 2 tunaanza uzalishaji wa chuma, Vanadium na Titanium.

Mauzo ya Vanadium peke yake ni sawa na dola bilioni nne kwa mwaka ambapo kwa kuwa haya ni bidhaa ambatana na chuma maana yake 80% ya mapato haya yangekuwa ya nchi. Kwa hiyo mwaka wa kwanza tu wa uzalishaji ningeweza kupata dola bilioni 3.2. Kwa fedha hizo, tungejenga reli kuanzia Dar mpaka Dodoma kwa mara moja bila kuungaunga na kubakia na chenji ya dola bilioni moja ambazo ningeweza kujenga hospitali tano kubwa kama Mloganzila katika kanda tano za nchi; Mbeya, Mtwara, Mwanza, Kigoma na Arusha.

Ningeweza kujenga vyuo vya VETA kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa nchini ( Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji ) kwani unahitaji shilingi bilioni 750 tu kujenga vyuo hivyo vilivyokamili na vifaa vya kutosha vijana kupata mafunzo.

Ningeweza kujenga vyuo vikuu vipya vitatu aina ya UDOM kwani UDOM moja ina thamani ya shs bilioni 800 tu. Haya ni mapato ya mwaka wa kwanza tu. Kumbuka kuwa tunaweza kuendelea kuchimba chuma tani milioni moja kwa mwaka kwa miaka 2000!

Tungeamua kuzalisha tani milioni tano kwa mwaka maana yake mapato ya Vanadium peke yake kwa mwaka yangekuwa dola bilioni 16 ambazo ni sawa na kumaliza reli yote mpaka Kigoma na Mwanza na kuiwezesha Air Tanzania kuwa na ndege kubwa na ndogo sawa na Shirika la Ndege la Ethiopia na hata kuzalisha umeme zaidi ya 10,000MW ndani ya miaka mitano kwa kutumia makaa ya mawe, geo thermo, gesi asilia, upepo na jua – yote hayo bila kuathiri hifadhi ya Selous.

Kwa kuzalisha tani milioni tano kwa mwaka tungezalisha chuma, Vanadium na Titanium kwa miaka 400 mpaka kumaliza mashapo yote tuliyonayo. Kwanini hatuwekezi Mchuchuma na Liganga?

Kungoza nchi kunahitaji MAARIFA. Hakika [HASHTAG]#NingefanyaTofauti[/HASHTAG]
Mawazo Mazuri kama haya yanadhaurilwa kisa tu ushauri umetoka kwa upinzani
 
Ni rahisi sana kusema lakini sio kutenda.

Turudishe mpira kwako Mbunge wa Kigoma mjini: Huko kwako umefanyaje nje ya sera ya serikali kuu?
Kwa bajeti ipi na vyanzo gani vyama mapato. Au umesahau Kigoma ilipo pata ufadhili wa OGP ikatishiwa kufutwa halmashauri. Ok welcome Luiche Irrigation scheme.hold on
 
Tatizo ni moja, mfumo wetu wa kujitawala una matatizo.
Mkuu Nguruvi 3, nakuona unavyokuwa diplomatic kwa kusema Tanzania tuna tatizo moja tuu la mfumo wetu wa kujitawala ndio wenye matatizo!. The reality tatizo sio mfumo tuu ndio wenye matatizo bali hata baadhi ya watawala wetu ni tatizo!.

Hili la ukosefu wa Dira ya taifa, lilizungumzwa vizuri sana na Prof. Shivji wakati wa mchakato wa katiba ana akasema wazi wazi bila kumung'unya maneno
Prof. Shivji Aukosoa Mchakato wa Katiba Mpya!- Aliponda Bunge la Katiba!. Watch ITV/TBC-1!.

Hivyo Mkuu Nguruvi3, sema tuu mahali tatizo haswa lilipo!.

P.
 
Ndugu yangu Pascal Mayalla
Nakubaliana nawe kuhusu tatizo la MFUMO na WATU wanaoongoza hiyo Mifumo.

Huku ndani ya Utumishi wa Umma kuna shida ya Viongoz wenye maono na mkakati wa kulitoa hili Taifa hapa lilipo.

Kwa Raslimali hizi tulizojariwa, inahitajika Uzalendo, Uthubutu na Uongozi mahiri.

Kwa SISI tulio NDANI ya Utumishi wa Umma, tumeona 100% JemedariM kwa kweli ana vitu hivyo, tatizo kwa chini yake ni kama Wasaidiz wameshikwa Ganzi. Hawana maono ya Rais (wameshindwa kutafsiri) wala mikakati madhubuti.

[HASHTAG]#Mwaka[/HASHTAG] huu, JPM akishanipa NAFASI ya kuongoza Taasisi ya Umma nitafanya tofauti sana na Watendaji wengine.

Tuzidi kuomba Uzima na Rehema ya Mungu wetu
 
Kusikika kulikuwa na Tija gani wakati huo? Kulimsaidia nini Mtanzania wa kawaida?
Kwa hakika NINGEFANYA TOFAUTI na alichofanya Zitto Kabwe. Shame on him!
Muda utaongea.
Hata kujiita majina ya kingonongono kunashabihi namna yako ya kufikiri. KUSIKIKA ndio maana halisi ya kuibua yaliyojificha.

Usimtaraji asiyeshika kodi yako kukununulia kipande cha lami, kazi yake ni kusema na kusema na kusema tena hadi yule mwenye kapu la taifa anyooshe mkono kutibu tabu za wenye wamiliki wa kapu
 
Ndugu yangu Pascal Mayalla
Nakubaliana nawe kuhusu tatizo la MFUMO na WATU wanaoongoza hiyo Mifumo.

Huku ndani ya Utumishi wa Umma kuna shida ya Viongoz wenye maono na mkakati wa kulitoa hili Taifa hapa lilipo.

Kwa Raslimali hizi tulizojariwa, inahitajika Uzalendo, Uthubutu na Uongozi mahiri.

Kwa SISI tulio NDANI ya Utumishi wa Umma, tumeona 100% JemedariM kwa kweli ana vitu hivyo, tatizo kwa chini yake ni kama Wasaidiz wameshikwa Ganzi. Hawana maono ya Rais (wameshindwa kutafsiri) wala mikakati madhubuti.

[HASHTAG]#Mwaka[/HASHTAG] huu, JPM akishanipa NAFASI ya kuongoza Taasisi ya Umma nitafanya tofauti sana na Watendaji wengine.

Tuzidi kuomba Uzima na Rehema ya Mungu wetu
Unataraji wafanye nini hao unaowalaumu ikiwa kila kitu kinaamiliwa kwa siasa badala ya taaluma?

Unajua mapato ya halmashauri yameminywa na miradi huko inadhorota?
 
Mawazo Mazuri kama haya yanadhaurilwa kisa tu ushauri umetoka kwa upinzani
Tatizo ni njia ambayo wapinzani wameamua kuitumia kufikisha mawazo mazuri mbele ya mhimili wa serikali (Bunge). Wazo na mchakato ni mzuri na ndio maan rais sio hapendi ushauri ila ile style ya kuita media na kuiponda tu serikal haipo njema kabisaaaaaaa. BADILIKENI HAPO MTAFAIDI USHAURI WENU.
 
Waulize ccm walioshika hatamu wanajua akili yao inachowaza mm sijawahi waelewa.Uliza mtu yeyote je hajapata maendeleo kwa sababu ya reli sgr/dreamliner kutokuwepo?jamii yetu inazalisha washika hatamu wa aina yake
Au kuna mtu ameshindwa kwenda Marekani kwa sababu ya kukosa usafiri.
Au mzungu ameshindwa kuja Afriaka Mashariki kwa sababu ya kukosa usafiri.
Hivi ni mzungu gani akitaka kuna Tanzania atashindwa kwa sababu ya Ndege ya umma?
Kama wazungu walikuaja Afrika kwa Majahazi watashindwa Leo kwenye madege maelfu yanayopita anagani na kufiaka kila nchi.

Mbona Hatuna Meli za mizigo na mizigo inapakuliwa pale bandarini masaa 24?
 
Maiti mwenyewe. Zitto mchumia tumbo kama wengine mradi wa maji toka mwaka 2013 mpaka leo hii haujulikani kukamilika lini.

Nimesoma comments zako kazaa, baada ya hii nimebaini tatizo ni uwezo wako wa kupambanua mambo.
 
Unataraji wafanye nini hao unaowalaumu ikiwa kila kitu kinaamiliwa kwa siasa badala ya taaluma?

Unajua mapato ya halmashauri yameminywa na miradi huko inadhorota?
Comrade
Sikubalian na hoja yako
Mtendaji mwenye kuwajibika na maono hajafungwa mikono
 
Katika kila mawazo yako utoayo Kuna ujenzi wa taifa!! Mimi huwa Ni msikilizaji hodari wa hoja zako!! Mkuu na ndo role modal wangu uliyefanya nifatilie siasa tokea unachukua ubunge wa kigoma!! Ila Sasa mtani wangu Kuna tatizo hapa!! Business idea is always sweet when you think it @ the future!! But it become bitter when your idea came into action!! Nimesoma waraka wako!! Unatia moyo saana! Na unaonesha Ni jinsi gani umeumiza kichwa! Katika kutafakuri mambo amaizing!!
Swali ni je? Tokea umekuwa mbunge mawazili wote waliopita hamjawahi kuwa marafiki? Nimeuliza kwa sababu Hilo wazo labda lingewafikia kama private idea! Nje ya bunge mkiwa mnapata chakula!!
Labda pia lingewafikia kama ungewaita Hao mawaziri ukawaelezea kama ulivyoelezea hapa sisi tusiokuwa na elimu tukaelewa! Maana ukilifikisha bungeni kwa njia ile mnayotumia I think ndo maana viongozi hawalipitishi kwa maana bungeni wabunge wote mnaonesha kukinzana tu hata kwenye hoja za maana!! Mara upande mmoja unatoka Nje! Mara upande mwingine wao Ni mwendo wa ndiyooo!!
Na je Katika kuchimba hizo vanadium na chuma umeme up utakaotumiwa?? Je? Umeme unaozalishwa Tanzania unaweza kutosheleza hayo machimbo na kuyeyusha hizo materials mpaka zikawa final product? Na je investment itagharimu kiasi gani? Umetaja ndege, na umetaja rufiji hydroelectric power! Je unaona sio muhimu?
Mwisho mimi naona Katika kuwaza kwako umewaza vyema 150% na [HASHTAG]#ningefanyatofauti[/HASHTAG] inatakiwa iwe jawabu letu sisi!! Ibadilishe iwe [HASHTAG]#nitafanyatofauti[/HASHTAG]. Unaweza kufanya tofauti ukiwa mbunge kwa kutafuta investors from abroad ukawapa hizo ideas wakafanya feasibility study! Then ukawakabidhi mikononi mwa serikali!! Hiyo ndo tunaweza ita [HASHTAG]#ningefanyatofauti[/HASHTAG].

Kwasababu usipochaguliwa kuongoza nchi idea yako itaishia hapo??
Mwisho nakuomba radhi kama Kuna sehemu sijatumia lugha mbadala! Eg matusi
Kumbuka kuwa Kwa wenzetu walioendelea kuna Sera ya Taifa ambayo inajengwa na wataalam.
Kwetu Sera inatengenezwa na wanasiasa wa chama kimoja.
Lakini pia Mipango ya serikali inatengenezwa na mawaziri wa wizara husika ambao ni wanasiasa.
Pia ukumbuke nchi yetu Checks and Balance haijakaa vizuri au haipo kabisa. Kuna usiri mkubwa.

Wazo la Zito liko clear kabisa, na kwa nchi yoyote inayohitaji manedeleo endelevu inajenga uchumi wake wa ndani kwanza kwa kutumia rasilimali za ndani ili iweze kuuza nje.
Makaa ya mawe na madini ya chuma yanaweza kutumiwa na wazalishaji wote wa vyuma kuanzia wakubwa na wadogo,

Ni ukweli usiopingika kuwa kama unazalisha mfano Chuma kwa wingi kabisa barani Afrika na kuiuza kwa bei ya chini Utasababisaha nchi zote za Jirani zije kununua chuma Tanzania kuanzia Nondo mpaka mataruma ya Reli.
Utakua na wageni wengi sana na magari na malori mengi sana yanayoingia na kutokana kwa ajili ya kubeba nondo ndani na nje ya nchi.
Miradi iliyopo ni mizuri na ni mikubwa sana lakini tuangalie kuwa zitafanya mzunguko kiasi gani wa fedha za ndani na zile za nchi.

Unauliza kuhusu umeme wakati Zito amebainisha vyema kabisa kuwa angezalisha mpaka KW 10000 kwa kutumia ,umeme wa upepo,makaa ya mawe,geothermal, gesi n.k amnavyo vyote vipo kwa kiwango kikubwa sana.

Ni kweli kuwa Zito alukua na nafasi ya kuwashauri mawaziri lakini ni lazima Kenya au nchi yoyote lakini tuangalie kuna suala la maslahi binafsi katika miradi mikubwa has a yenye manunuzi mengi toka nje.
Kule nchini za ulaya wanaita Teni percent.
Hii IPO sana.
Ukimuunganishia mtu biashara ya bilioni zaidi ya 500 kwa zile nchi za wenzetu ambao watendaji nao wana mapungufu kama binadamu basi kuna namna ile shukrani ya pekee itawekwa hata kwa rafiki au ndugu wa mbali ili isionekane kuwa mtu amepewa mshiko.
Hili watendaji wengi wanalifahamu na wanacheza nalo kwenye nchi za wenzetu huko mbali. Sijui huku kwetu wao ikoje. Siwezi kusema moja kwa moja.

Hata hivyo bado serikali ina Muda wa kufanyia kazi maoni ya watu yenye muelekeo wa kujenga uchumi wa viwanda.
 
Mda aliotumia kuandaa hili kwanini asitumie kuandaa desa ni jinsi gani kama mbunge atawasaidie ili wanufaike na zao la chikichi?

kiukweli kuna vitu vya kumulaum Zitto ila siyo katika zao la michikichi. wewe umelisikia na kulizungumzia kwasababu yeye alianza kulipigia kelele, Ashukuriwe Mungu ni kama serikali imemsikia maana sasa lipo mawazoni mwa Waziri mkuu(Nimemsikia mara kazaa Waziri mkuu akizungumzia Wawese na Alizeti).
 
Mianya ipi iliyozibwa wee uko humu unamwaga Povu watu wanapiga Noti eti Mianya imezibwa
Hayo yangekuwepo tungeyasikia tu,sasa kusema watu wanapiga noti na wakati taarifa za upigwaji hizo noti hazipo,kwanini tusiseme unapiga ramli?
 
Tuna safari ndefu sana kutoka hapa tulipo chini ya CCM na viongozi wake.

Viongozi hawa wanawaza zaidi kuchukua fedha kutoka hazina kufanya mambo yatakayowapa umaarufu wa kisiasa kuliko kuwaza kufanya mambo yatakayotengeneza fedha za kupeleka hazina kisha ndio wazitumie kuleta maendeleo.
Wewe ulikuwa CCM na ulihama na baba yako Lowassa tuambie ulipokuwa CCM ulifanya cha maana kipi na sasa uliko umefanya kitu gani cha kukumbukwa? Au kwa kuwa umebanwa kwenye ufisadi wako ndiyo maana una bwabwaja tu!! Mtapata taabu sana awamu hii...!!
 
Zitto napata ujasiri nikijua bado tuna watu kama wewe. Hakika vipaumbele vyetu vya namna ya kuvuka tulipo bila madhara makubwa tumekosea. Ningekuwa kwenye mamlaka haraka ningekuita ikulu uje tukae nikueleze niliyonayo nawe unieleze uliyonayo kwa ajili ya kuijenga Tanzania lakini sasa tumebaki na siasa chafu tu za kupora ushindi na kubambikia kesi wapinzani.
Zitto nasubiri siku nitakayopiga kura kukuchagua kama rais wa nchi hii. Naisubiri siku hii
 
Hayo yangekuwepo tungeyasikia tu,sasa kusema watu wanapiga noti na wakati taarifa za upigwaji hizo noti hazipo,kwanini tusiseme unapiga ramli?
...wee endelea kubeba marobota ya Fulana na Kofia Ukiwa unasubiri ..kuambiwa ....kwaakili kama hizo kwanini usiwe zawadi yao maana wanataka watu wanaofikiri kama wewe...pole ndugu yangu kwa taarifa tu watu wanapiga Noti
 
Hata kujiita majina ya kingonongono kunashabihi namna yako ya kufikiri. KUSIKIKA ndio maana halisi ya kuibua yaliyojificha.

Usimtaraji asiyeshika kodi yako kukununulia kipande cha lami, kazi yake ni kusema na kusema na kusema tena hadi yule mwenye kapu la taifa anyooshe mkono kutibu tabu za wenye wamiliki wa kapu
Naona Gyno wako amekuvuruga kweli kweli.
 
Back
Top Bottom