King Kong III
Platinum Member
- Oct 15, 2010
- 63,160
- 95,900
Imekaa vizuri sana hiyo,Tanzania tumejaliwa natural resources za kutosha,inashangaza kwanini tunaendelea kuwa ombaomba.
Nilikuelewa sana na ndiyo maana nakuambia kumlinganisha mbunge mtu mmoja tu asiye na dola wala vyanzo vya mapato hata kupanga bajeti ya jimbo lake na serikali dudu kubwa ni kutojitendea haki mwenyewe!!
Well. Hoja yako kutokuwa na taarifa na afanyayo ktk jimbo lake haina maana kwa sababu zifuatazo:
1. Elewa kazi na majukumu ya mbunge. Kubwa kabisa ni kuwa sauti ya kuwasemea wananchi wa jimbo lake (kuwakilisha). Kwa lugha rahisi kabisa mbunge huwa ni "link" kati ya wananchi na serikali
2. Zitto Kabwe mbunge wa Kigoma Mjini ni miongoni mwa wabunge walioifanya kazi hii (ya ku - link wananchi na serikali) kwa umaridadi usio mithirika. Sina hakika kama hili hulioni ama hujawahi kuliona. Na sina hakika wataka uone nini zaidi ya hili!!
3. Amefanya nini jimboni kwake? Hili ni swali awezaye kujiuliza mtu asiye na ufahamu wa kutosha tu dhidi ya kazi na majukumu ya mbunge. Nakushauri, iulize serikali imefanya ni jimboni kwa Zitto Kabwe na Tanzania kwa ujumla...
Ndiyo. Serikali ndiyo yenye dola, inakusanya kodi na kupanga matumizi yake. Kazi ya mbunge ktk hili ni kuomba na kushauri tu na hili wabunge wanafanya sana. Kama huoni, basi hili ni tatizo lako ndugu yangu Kalamu1....
4. Sina hakika kama ni kazi ya mbunge kujenga shule, vituo vya polisi, kuajiri walimu, kujenga barabara, reli, madaraja, kununua madawa na kupeleka mahospitalini nk....
Kama nilivyokuambia hapo awali mbunge anachoweza kufanya ni kuhamasisha wananchi kushiriki ktk shughuli za maendeleo zilizo ndani ya uwezo wao mf. Kilimo ili wapate chakula, kuibua miradi ya maendeleo ambayo mwisho wa siku ni lazima tu wapate support ya serikali ktk kuikamilisha kupitia mfumo wa kibajeti....
Sasa unadhani Zitto Kabwe kama mbunge kama mbunge ktk jimbo lake hafanyi hili kwa kushirikiana madiwani wa eneo lake?
Kukusaidia tu ni kuwa, you don't need any evidence ktk hili.
Ushahidi nambari one ambao ni sharti ukuijie kichwani mara moja kabla ya ku - argue ni huu: YEYE NI MBUNGE na ni mwakilishi wa watu na hata sasa yuko jimboni kwake baada ya kikao kirefu cha bunge la bajeti ya 2018/2019!!
Kwa hiyo ndiyo ule uamuzi kuwa mwanasiasa afanye siasa ktk jimbo lake tu unautaka utumike hata kwenye fikra?Mda aliotumia kuandaa hili kwanini asitumie kuandaa desa ni jinsi gani kama mbunge atawasaidie ili wanufaike na zao la chikichi?
Umeng'ang'ania 'kazi za mbunge-----" na hapo hapo unaeleza 'umenielewa' nilichoeleza! Siwezi kubishana kihivyo.
umenifanya nikumbuke jamaa yangu aliyekuwa anakosoa walioko uwanjani wakisakata kabumbu, alipewa nafasi baadaye ili akarekebishe makosa ila alichofanya alienda kuboronga kuliko aliyetolewa.Ni rahisi sana kusema lakini sio kutenda.
Turudishe mpira kwako Mbunge wa Kigoma mjini: Huko kwako umefanyaje nje ya sera ya serikali kuu?
Wewe ni mzushi na muongo mkubwa.Lini nimewahi kuwa shabiki wa CCM? Tangu nimepata akili na kuanza kufuatilia siasa za nchi hii huwa nashangaa sana kuona mtu anajitambulisha kuwa ni mfuasi wa CCM chama ambacho viongozi wake wengi kwa miaka mingi wanatuhumiwa kwa kashifa karibu kila siku alafu leo eti leo mimi niwe mpenzi wa CCM.Wewe ulikuwa CCM na ulihama na baba yako Lowassa tuambie ulipokuwa CCM ulifanya cha maana kipi na sasa uliko umefanya kitu gani cha kukumbukwa? Au kwa kuwa umebanwa kwenye ufisadi wako ndiyo maana una bwabwaja tu!! Mtapata taabu sana awamu hii...!!
No! Mjadala wa terrible teens ni tofauti na huu. Please tungefarijika kama ungemjibu hoja zinazohusiana na alichosemaZitto vipi zile "terrible teens" ulizozivalia njuga?
Zitto huwa nakubaliana nae sana lakini kwahili hapana tunahitaji reli kwa haraka yeye anasema tuanze na kujenga viwanda vyachuma nisawa na umefikiwa na magonjwa ya kipindupindu alafu dawa ipo kwa jirani unasema mgonjwa asipewe mpaka nitengeneze dawa yakwangu Leo tunanunua chuma kesho tutatengeneza chakwetu tutauzia wengine ndio biashara nakumbuka mzee mwinyi aliwahi kusema biashara nikununuliana nakuuziana uchumi haujengwi kwa wivu naninunue kwake tunahitaji reli haraka tuondoe mizungukoZitto my brodah!!!
Haya unayoyasema ni mambo mazuri sana ambayo yanaonyesha kuwa umefanya tafiti ya kina kwa kiwango chako.
Nije kwenye hoja ya msingi, hivi je kimewh kuwa na national priority kwenye serikal hii ya CCM zaid ya wakati ule wa uongozi wa mwalim?
Kipindi nakua nilikuwa najua vipaumbele vya taifa ilikuwa ni kuondoa ujinga umaskin na maradhi. Kila mtu alibeba vipaumbele hivi na kuvivaa shingoni. Bibi afya alikuwa anapata majumban kukagua usafi hadi wa nyumban na chooni, bwana shamba alikuwa anashinda shambani kutuelekeeza hata jinsi ya kuchuma kahawa. Madarasa ya elimu ya watu wazima tuliyashuhudia vipindi vya region kuelimisha umma kuhusu vipaumbele hivi vilikuwa vingi na vya Kila wiki.
Baada ya mwl haya yalidumu kwa muda mfupi tuu yakatoweka.
Kwasasa nimekuwa nikishuhudia aina ya viongozi ambao wanakuja na ndoto zao wanamaliza muda wao ndoto hazijatimia.
Kasheshe ni kwa serikal hii ya awamu ya tano, yaan imebidi overspend kwa k7fanya investment kwenye more of luxurious goods kuliko kwenye production. Viwanda vinavyopigiwa kelele ni vya cherehani na ususi wa nywele vikienda mbali sana ni vya maji. Ndio ww unakuja kuongelea swala la makaa ya mawe na chuma???
Kwa kipaumbele gani tulicho nacho?
Ni uzalishaji, ukuzaji mtaji wa kitaifa, elimu, afya ama ni ubabe??
Hapana, Zitto anahoja tatizo hujamsoma vizuriZitto huwa nakubaliana nae sana lakini kwahili hapana tunahitaji reli kwa haraka yeye anasema tuanze na kujenga viwanda vyachuma nisawa na umefikiwa na magonjwa ya kipindupindu alafu dawa ipo kwa jirani unasema mgonjwa asipewe mpaka nitengeneze dawa yakwangu Leo tunanunua chuma kesho tutatengeneza chakwetu tutauzia wengine ndio biashara nakumbuka mzee mwinyi aliwahi kusema biashara nikununuliana nakuuziana uchumi haujengwi kwa wivu naninunue kwake tunahitaji reli haraka tuondoe mizunguko
Hapa kuna tatizo kweli kwa wananchi wetu na nina shaka Wabunge wetu kama wanaelewa tofauti ya Dira au Sera za Kitaifa na Sera za vyama["1000 digits, post: 27676781, member:Kumbuka kuwa Kwa wenzetu walioendelea kuna Sera ya Taifa ambayo inajengwa na wataalam.Kwetu Sera inatengenezwa na wanasiasa wa chama kimoja.
Inaonekana una stress zaidi yake mkuu.Una stress we jamaa. Suala la maji kigoma mjini limeishia wapi?
Kutwa alikuwa akiuza sura vyombo vya habari wenzie ripoti wakitoa wanaipeleka bungeni ambako ndiko unatakiwa kupelekwa sio media kama zitto alivyokuwa akifanyaUngefanyaje mkuu,maana PAC siku hizi haisikiki kabisa kama kipindi alichokuwepo Zitto mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.