Zitto Kabwe: Kama ningepata mamlaka ningefanya tofauti

Zitto Kabwe: Kama ningepata mamlaka ningefanya tofauti

Nimesoma kwa makini tafakari ya Zitto Kabwe (Mb), Nilichogundua ni kwamba vipaumbele vya namna ya kufikisha Taifa la Tanzania kwenye uchumi wa FOUR ASIA TIGERS (Hong Kong, Singapore, Taiwan na South Korea) ita-wezekana tu pale tutakapo kuwa na sera ya nchi na si sera ya CCM, sera ya CHADEMA & CUF. Au mbaya zaidi utashi wa mtu mmoja ambaye maamuzi yake tu ndio yatakuwa mwongozo wa Taifa. Mfano miradi yote mikubwa anayoifanya Raisi ina tija kwa Taifa, ipo miradi ambayo tija itaonekana baadaye sana lakini itaiacha nchi kwenye hali mbaya ya uchumi kwa sasa sababu inatekelezwa kwa kasi kubwa tofauti na ukuaji wa uchumi wa nchi yetu. Lakini kama miradi hiyo ingewekwa kwenye sera ya nchi haikuwa na lazima kuisha ndani ya miaka mitano au kumi. Hivyo kila kiongozi anayeingia madarakani angekuwa na wajibu wa kuendeleza sera za nchi kama nchi kwa kutumia mikakati yake. Hivyo Zito Kabwe(Mb) una mikakati mizuri nadhani ungeishauri serikali ukiwa bungeni. Pia mbunge wa eneo hilo ana deni kwa watanzania maana amekalia mali ghafi ambazo zinaweza kuliokoa taifa, aishauri serikali
 
Hili kupanga mipango kamambe na kuanza utekelezaji kwa vishindo, halafu mambo yanaishia kati na hakuna mrejesho, niliwahi kulizungumza hapa [URL="https://www.jamiiforums.com/threads/faida-na-hasara-za-maamuzi-ya-zimamoto-tuletewe-mrejesho-isije-kuwa-tunatwanga-maji-kwenye-kinu.1130858/#post-18033876"]Faida na Hasara za Maamuzi ya Zimamoto: Tuletewe Mrejesho Isije Kuwa Tunatwanga Maji Kwenye Kinu!.[/URL]

Na sio kosa tuu la serikali kutotoa mrejesho, bali hata sisi wananchi, hatuna utamaduni wa kuhitaji mrejesho.

Tena sisi waandishi wa habari wa Tanzania, we are part of the problem, kila siku tunaitwa wakati wa utiaji saini na uzinduzi wa miradi kwa mbwembwe huku tukifungashiwa zile bahasha zetu nene nene, tunaridhika na kusubiria kuitwa tena. Tulipaswa kuomba the roadmaps za miradi zenye kuonyesha milestones achievements ili kila baada ya muda tuipitie hiyo miradi kupata mrejesho na kilichofanyika.

Hata kwenye siasa it's the same, JK alipoingia madarakani ile 2005, walijiandikisha watu milioni 21, waliopiga kura ni watu milioni 12. Uchaguzi wa 2010, wakajiandikisha watu milioni 23, lakini waliojitokeza kupiga kura ni watu milioni 8 na yeye kuchaguliwa rais kwa kura milioni 5 tuu!. Hadi tunaingia uchaguzi wa 2015, kulikuwa hakuna mrejesho wowote wa why watu wanajiandikisha kupiga kura, halafu hawajitokezi kupiga kura.

Tungekuwa na utamaduni wa kuhoji mrejesho, haingewezekana taifa litumie kiasi kikubwa cha fedha namna iile kwenye mchakato wa katiba, alafu akaibuka mtu na ku abandon kwa hoja kuwa sio kipaumbele chake!, halafu akaibuka na vipaumbele vyake na kutumia kiasi kikubwa cha fedha bila kuidhinishwa na Bunge, na tunaangalia tuu na sana sana tunashangilia!.

P.
 
Smart people don’t start many bar fights. But stupid people don’t build many hydrogen bombs.
 
Mda aliotumia kuandaa hili kwanini asitumie kuandaa desa ni jinsi gani kama mbunge atawasaidie ili wanufaike na zao la chikichi?

Bila kupinga ushauri wako. Zitto ni mtu ambaye anajua mambo mengi kwa wastani mzuri sana. Ukija kwenye kilimo huwa anajua, ukienda kwenye uchumi humu anafahamu vyema, ukiingia kwenye siasa, huku anafahamu mpaka za kimataifa. Ukienda kwenye michezo pia anafahamu na tunaina michango yake.

Kwa sasa hapa nchini zao la michikichi Zitto analizungumzia kuliko kiongozi yoyote. Zitto pia nilimuona akizungumzia gas kwa undani. Zitto iwapo atakuwa rais wetu huko mbeleni nina hakika atakuw rais bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania na africa kwa ujumla. Iwapo atagombea hiyo 2020 na mshindani wake kuwa Magufuli ni dhahiri ataacha mwangwi mkubwa kuliko alioacha Slaa 2010 alipogombea na JK. Na ninakuhakikishia atasababisha Magufuli na ccm yake kuwa na wakati mgumu na hata kubadilisha mambo mengi kwani Magufuli ni mdhaifu linapokuja suala la siasa za ushawishi.
 
Hayo yangekuwepo tungeyasikia tu,sasa kusema watu wanapiga noti na wakati taarifa za upigwaji hizo noti hazipo,kwanini tusiseme unapiga ramli?

Kilichofanyika ni kudhibiti vyombo vya habari visitangaze hayo mambo ya upigaji. Mpaka sasa kuna 1.5t imekosa majibu ya uhakika na hii ni kwa mujibu wa ripoti ya CAG. Hizi 1.5tni nyingi kuliko huo upigaji uliopigiwa kelele enzi za JK.

Udhibitisho wa upigwaji wa hizo 1.5t, ni pale lugha gongana ziliposhamiri kwa viongozi waandamizi wa serekali na ccm. Walidanganya 200b ilipelekwa Znz lakini baada ya kubanwa wakakiri hazikwenda na serekali ya Znz ndani ya baraza la wawakilishi lilikiri kutokupokea hiyo hela. Kamati ya PAC ilitarajiwa kutoa ripoti ya hiyo hiyo hela ndani ya bunge lililopita lakini hilo halikufanyika, na halikufanyika sio kwa bahati mbaya bali ni nguvu toka kwa mtuhumiwa namba moja kwani alijua haiba yake inaenda kuchafuka. Kinachofanyika sasa ni kuhakikisha huo uchafu hauripotiwi na vyombo vya habari na sio kwamba upigaji haupo. Na rushwa pia ipo kama kawaida. Ambacho hakipo ni uhuru wa vyombo vya habari na serekali imejitoa kwenye open government basi.
 
Kitaturu, ninakubaliana kabisa na haya uliyoyaeleza hapa kuhusu kazi za mbunge katika uwakilishi wa jimbo. Nisipokubaliana na wewe ni nini nafasi ya mbunge kama kiongozi wa wananchi jimboni kwake. Sijui kama utanielewa utofauti ninaouzungumzia hapa juu ya kofia hizi mbili anazoweza kuzivaa mbunge. Maendeleo ya jimbo ni zaidi ya kutegemea pesa inayotolewa na serikali, na hata wafadhiri uliowataja.

Hata hivyo, katika kukurupuka kunijibu mimi, umeamua kutoweka maanani kauli yangu ya kuwa sina taarifa ya anayoyafanya Zitto jimboni kwake na kwa sababu hiyo nisingeweza kumhukumu kwa hilo.

Nilikuelewa sana na ndiyo maana nakuambia kumlinganisha mbunge mtu mmoja tu asiye na dola wala vyanzo vya mapato hata kupanga bajeti ya jimbo lake na serikali dudu kubwa ni kutojitendea haki mwenyewe!!

Well. Hoja yako kutokuwa na taarifa na afanyayo ktk jimbo lake haina maana kwa sababu zifuatazo:

1. Elewa kazi na majukumu ya mbunge. Kubwa kabisa ni kuwa sauti ya kuwasemea wananchi wa jimbo lake (kuwakilisha). Kwa lugha rahisi kabisa mbunge huwa ni "link" kati ya wananchi na serikali

2. Zitto Kabwe mbunge wa Kigoma Mjini ni miongoni mwa wabunge walioifanya kazi hii (ya ku - link wananchi na serikali) kwa umaridadi usio mithirika. Sina hakika kama hili hulioni ama hujawahi kuliona. Na sina hakika wataka uone nini zaidi ya hili!!

3. Amefanya nini jimboni kwake? Hili ni swali awezaye kujiuliza mtu asiye na ufahamu wa kutosha tu dhidi ya kazi na majukumu ya mbunge. Nakushauri, iulize serikali imefanya ni jimboni kwa Zitto Kabwe na Tanzania kwa ujumla...

Ndiyo. Serikali ndiyo yenye dola, inakusanya kodi na kupanga matumizi yake. Kazi ya mbunge ktk hili ni kuomba na kushauri tu na hili wabunge wanafanya sana. Kama huoni, basi hili ni tatizo lako ndugu yangu Kalamu1....

4. Sina hakika kama ni kazi ya mbunge kujenga shule, vituo vya polisi, kuajiri walimu, kujenga barabara, reli, madaraja, kununua madawa na kupeleka mahospitalini nk....

Kama nilivyokuambia hapo awali mbunge anachoweza kufanya ni kuhamasisha wananchi kushiriki ktk shughuli za maendeleo zilizo ndani ya uwezo wao mf. Kilimo ili wapate chakula, kuibua miradi ya maendeleo ambayo mwisho wa siku ni lazima tu wapate support ya serikali ktk kuikamilisha kupitia mfumo wa kibajeti....

Sasa unadhani Zitto Kabwe kama mbunge kama mbunge ktk jimbo lake hafanyi hili kwa kushirikiana madiwani wa eneo lake?

Kukusaidia tu ni kuwa, you don't need any evidence ktk hili.

Ushahidi nambari one ambao ni sharti ukuijie kichwani mara moja kabla ya ku - argue ni huu: YEYE NI MBUNGE na ni mwakilishi wa watu na hata sasa yuko jimboni kwake baada ya kikao kirefu cha bunge la bajeti ya 2018/2019!!
 
Zitto , baada ya kusoma bandiko lako yapo ninayokubaliana nawe na nisiyokubaliana nayo

Nianze kwa nisiyokubaliana nayo.
Kauli kwamba 'ningepewa mamlaka ningefanya abcd' si sahihi.

Kauli hiyo inatoa 'uhalali' wa mwingine kusema nina mamlaka nafanya abcd

Pengine ungesema ningepewa mamlaka ningeshauriana na wenzangu kuhusu abcd

Utamaduni wa kushaurian umetoweka na Mwalimu. Ukirudi nyuma, kulikuwa na mipango ya maendeleo ya kitaifa 'vision' kuanzia ule wa mwaka 1963 na kuendelea.

Mipango hiyo imeacha alama unazoweza kuziona kote nchini hadi leo.
Si barabara, maji, umeme,Shule, Hospitali, viwanda, kilimo n.k.

Kwasababu ya kupoteza vision ya kitaifa, mipango ya maendeleo imekuwa kama hadithi
Nimeshangaa tumeondoka kwenye gesi ya Mtwara katika miaka 2 tu sasa ni stigler gorge

Nauliza, tulikuwa na vision ya kitaifa kuhusu nishati? Na kama ilikuwepo ni ya miaka mingapi?Na kwa utaratibu gani tumeweza kubadili gia ghafla kiasi hicho?

Pili, tulipoacha reli kama ile ya kaskazini ikaota nyasi tulikuwa na vision ya kitaifa ya infrastructure? Kama ilikuwepo kwanini tunarudi kwenye reli tena ikiwa tuliachana nayo?

Tatizo ni moja, mfumo wetu wa kujitawala una matatizo.
Hatuna sera za kitaifa kama dira, tunasera za vyama.

Hivi ni vitu viwili tofauti ingawa hatujui. Sera za kitaifa zinaeleza 'vision' ya taifa
Kwa wenzetu sera za kitaifa hazibadiliki hata kama mifumo ya kisiasa inabadilika.

Sera za vyama zinabadilika katika kueleza tunafikiaje malengo ya dira ya Taifa 'vision'

Hili utaliona Bungeni Ulipo.
Masuala ya kitaifa yanajadiliwa kivyama, utapataje vision ya taifa kwa mfumo huo?
Mipango ya maendeleo inafikishwa na kujadiliwa kivyama tena bila tathmini ya uliopita

Kutokana na mfumo mbovu unaoanzia bungeni, hakuna mijadala ya sera za nchi
Ubovu huo unapelekea kuwepo kwa Elimu kwanza, Kilimo kwanza, Viwanda kwanza n.k. kwa kofia ile ile uliyosema 'ningekuwa na mamlaka, au nina mamlaka nitafanya abcd'

Ningekuwa au nina, si mbadala wa tungefanya . Kwa hilo unadhani tutafanikiwa?

JokaKuu Pascal Mayalla

"Nuggets" kama hizi ni nadra kuziona siku hizi. "Nguruvi3" mmoja wa 'Greats', mfikirishaji ndani ya jukwaa. I salute you ndugu. 28 million posts, na nyingi ya hizo zikiwa 'dhahabu' tupu sio mchezo ati!
 
Kilichofanyika ni kudhibiti vyombo vya habari visitangaze hayo mambo ya upigaji. Mpaka sasa kuna 1.5t imekosa majibu ya uhakika na hii ni kwa mujibu wa ripoti ya CAG. Hizi 1.5tni nyingi kuliko huo upigaji uliopigiwa kelele enzi za JK.

Udhibitisho wa upigwaji wa hizo 1.5t, ni pale lugha gongana ziliposhamiri kwa viongozi waandamizi wa serekali na ccm. Walidanganya 200b ilipelekwa Znz lakini baada ya kubanwa wakakiri hazikwenda na serekali ya Znz ndani ya baraza la wawakilishi lilikiri kutokupokea hiyo hela. Kamati ya PAC ilitarajiwa kutoa ripoti ya hiyo hiyo hela ndani ya bunge lililopita lakini hilo halikufanyika, na halikufanyika sio kwa bahati mbaya bali ni nguvu toka kwa mtuhumiwa namba moja kwani alijua haiba yake inaenda kuchafuka. Kinachofanyika sasa ni kuhakikisha huo uchafu hauripotiwi na vyombo vya habari na sio kwamba upigaji haupo. Na rushwa pia ipo kama kawaida. Ambacho hakipo ni uhuru wa vyombo vya habari na serekali imejitoa kwenye open government basi.

Na kwa kuwa vyombo vya habari havina uhuru wa kuyaeleza madudu yakasikika; bali yanayokubaliwa yasikike ni yale tu wanayolazimisha yasikike, basi watawala wanaona wana haki ya kusema wao ni malaika wanaofanya kila kitu kwa manufaa ya wanyonge. Kwa hoja hiyo, CCM wana haki ya "kutawala milele". Ni mambo ya ajabu sana kulazimisha watu wenye akili zao waamini wasichoweza kukiamini, na kwa msingi huo basi, njia za mabavu zitawavunja wasiokubali kulazimishwa waamini. Hawa wenye akili watanyamaza?
 
Aliepo hawezi kuwaza haya mambo, yeye anawaza kushinda uchaguzi wa mwaka 2020 badala ya kuwaza kuipeleka Tanzania mbele kwa kutumia rasilimali zetu.
 
Bila kupinga ushauri wako. Zitto ni mtu ambaye anajua mambo mengi kwa wastani mzuri sana. Ukija kwenye kilimo huwa anajua, ukienda kwenye uchumi humu anafahamu vyema, ukiingia kwenye siasa, huku anafahamu mpaka za kimataifa. Ukienda kwenye michezo pia anafahamu na tunaina michango yake.

Kwa sasa hapa nchini zao la michikichi Zitto analizungumzia kuliko kiongozi yoyote. Zitto pia nilimuona akizungumzia gas kwa undani. Zitto iwapo atakuwa rais wetu huko mbeleni nina hakika atakuw rais bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania na africa kwa ujumla. Iwapo atagombea hiyo 2020 na mshindani wake kuwa Magufuli ni dhahiri ataacha mwangwi mkubwa kuliko alioacha Slaa 2010 alipogombea na JK. Na ninakuhakikishia atasababisha Magufuli na ccm yake kuwa na wakati mgumu na hata kubadilisha mambo mengi kwani Magufuli ni mdhaifu linapokuja suala la siasa za ushawishi.
Ndugu wewe kumbe bado hujajua ni nini tatizo letu. Watu tunapigana kudai iwepo dira ya Taifa na kutaka wanasiasa wasijivike mamlaka ya utalaam wa kila fani katika kuongoza nchi wewe ndiyo kwaaanza unaona wapewe mamlaka ya kuvuruga na ''utaalam'' wao!
 
Mambo yetu yote uamuzi umehodhiwa na kundi dogo la watu. Uwakilishi wa wananchi bungeni upo kinadharia. Hawatoi mawazo ya wananchi. Hata wakitoa yao, huitwa kwenye kamati za vyama vyao na kutishwa.
 
Every body have sweet dreams! when you wake up the reality is ulikuwa umelala kwenye mkeka.
 
Mambo yetu yote uamuzi umehodhiwa na kundi dogo la watu. Uwakilishi wa wananchi bungeni upo kinadharia. Hawatoi mawazo ya wananchi. Hata wakitoa yao, huitwa kwenye kamati za vyama vyao na kutishwa.

Sasa tutatokaje hapa? Nimesikia hivi karibuni msemo wa ajabu kuwa "Ubunge ni mali ya chama", na sio mali ya wanaowakilishwa! La ajabu ni kwamba, mbunge akifukuzwa na chama kwa sababu za kuwakilisha matakwa ya waliomchagua, mbunge mpya atakayechaguliwa na wananchi hao anakuwa wa chama hicho hicho, na hasa kikiwa chama kinachotawala! Si maajabu hayo?
 
Ndugu wewe kumbe bado hujajua ni nini tatizo letu. Watu tunapigana kudai iwepo dira ya Taifa na kutaka wanasiasa wasijivike mamlaka ya utalaam wa kila fani katika kuongoza nchi wewe ndiyo kwaaanza unaona wapewe mamlaka ya kuvuruga na ''utaalam'' wao!

Mkuu huwa unapingia wapi? Wanasiasa ndio wanaamua kila kitu nchi hii, wataalamu wao wanaburuzwa tu. Ni mpaka atokee mwanasiasa tena rais mwenye nia njema ndio aruhusu mabadiliko ambayo wataalamu watakuwa na nguvu.
 
The first readers always mnakuwa very critic and biased. Sijui mnafikiri ndiyo model ya great thinker!
Anyway, Zitto amepresent very impressive national feasibility study.
 
Kuna nchi nyingi zinazozalisha vyuma, Mheshimiwa Zitto, hebu tupe costing za uzalishaji na namna utakavyoweza kushindana na makampuni yanayo miliki biashara hii na utakavyo shindana nazo. Naona umejiwekea uhakika wa kuwa chuma utakachozalisha kitapata soko kirahisi, jambo ambalo lina utata, you need need be having a product which very competetive in quality and pricing . How do you tackle this
Ungeanza na kuiuliza serikali ni vp dreamliner yetu itaweza kupata soko kirahisi na kushinda makampuni kongwe!
 
Ungeanza na kuiuliza serikali ni vp dreamliner yetu itaweza kupata soko kirahisi na kushinda makampuni kongwe!
Serekali haikuleta uzi hapa JF, Mheshimiwa Zitto kaleta uzi na fikra zake, nimeamua kuchangia, sasa hapo kuna lipi la ajabu.

Ndugu this is a forum na members wanabadilishana mawazo.
 
Mkuu Pasco, bado nasema mfumo wetu umetengenezwa kiasi kwamba kuna mambo yanagota bila kuhojiwa. Hapa nitakuwa wakili wa Wananchi.
Kwamba mfumo hauruhusu mwananchi kuhoji!
Atahoji wapi kabla ya kuonekana mwendawazimu au mchochezi?

Miaka michache nyuma tulikodi ndege ya ATC kwa mbwembwe zote za kupokea.
Hakuna anayejua ndege hiyo ilifia wapi. Tumehoji hapa JF lakini nani anatusikiliza?
Mfumo wetu unasikiliza Wabunge ambao sasa ni kama majoka ya ngoma, hayana meno
Hili la Bunge naomba niache nisijekuharibu karipio lako lol

Kuhusu wanahabari, ah hili nalo ni neno. Hatuna watu wanaofuatilia habari kwa udadisi.
Leo ukianzisha kiwanda cha betri waandishi wataandika kila neno tamu, hakuna atakayehoji Matushista pale Pugu road ilikufa kwasababu gani?
Hakuna anayehoji ile ndege ya kukodi iliishia wapi na kwa gharama za nani

Mfumo wetu hautoi nafasi kwa mwananchi kusema, unampa fursa ya kuikiliza tu
Haumpi mwananchi nafasi ya kupanga, unampa fursa ya kupangiwa

Kikubwa zaidi, mfumo unatoa mwanya wa 'abuse'
 
Back
Top Bottom