Zitto Kabwe: Kama ningepata mamlaka ningefanya tofauti

Zitto Kabwe: Kama ningepata mamlaka ningefanya tofauti

Zitto Kabwe, uko vizuri sana kinadharia. Ningependa kuamini kuwa ungeweza kuyasimamia mambo haya kiutekelezaji pia. Sijui hstoria yako vizuri ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika majimbo uliyowahi kuyaongoza. Kwa hiyo siwezi kukuhukumu kwa hilo.

Mimi kama Kalamu1, nakubaliana kabisa na dhana yako juu ya huo mradi wa makaa ya mawe na chuma, na hasa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi inayoendelea nchini na mingi inayofanyika barani Africa na kwingineko. Tuna chuma na makaa ya mawe, tuna graphite na madini mengine yanayohusika katika utengenezaji wa 'grade' mbalimbali za 'stainless steel,' ambazo zingekuwa msingi wa viwanda vyetu vingi, kama utengenezaji wa vipuli vya magari yanayounganishwa Rwanda na Kenya. Ungekuwa msingi wa kukuza uwezo wetu kiteknologia na 'skills' kwa vijana wetu ambao ndio wangeliendeleza taifa hili.
Tukiacha hiyo chuma na makaa ya mawe, tunafurahia kuuza madini yetu ya msingi nje, kama hiyo graphite. Inakuwaje tunao uwezo mkubwa wa kuwapata wawekezaji wanaokuja kuchimba na kusafirisha madini ghafi lakini hatuna uwezo wa kuwaalika akina Philips, Siemens, Medtronic, n.k. waje waunde vifaa vyao, kama Magnetic Resonance Imaging (MRI) hapa hapa hapa kwa kutumia helium na madini hayo; nasi tukiambulia kupata ujuzi na kuibia teknologia? Kwani ni mahospitali mangapi yatakayohitaji mashine hizo hapahapa kwetu na Afrika nzima inavyozidi kupiga hatua katika maendeleo.
Kwa nini tunapenda sana uwekezaji wa rahisi rahisi tu wa kuchimba na kusafirisha na kuachiwa mashimo?

Nisiwachoshe. Ule uwekezaji katika viwanda waliokuwa wanaufanya Mwalimu na wenzake, ulikuwa ni uwekezaji makini sana. Kwa bahati mbaya sana wakati wake ulikuwa bado. Leo tunao vijana wengi kabisa na wazuri wa kuendesha mapadiliko katika nchi hii. Kinachotakiwa tu ni uongozi wenye nidhamu, dira sahihi na mikakati madhubuti ya kutupeleka mbele kimaendeleo. Vyuo vyetu vipovipo tu, mchango wake katika kuleta mabadiliko nchini hakuna kabisa, lau kama unahesabu hao maprofesa wanaokwenda kujaza matumbo yao kwenye siasa.

"Introspection' yangu ingeniongoza katika kuweka 'priority' ya kudumu katika kilimo kwa wananchi walio wengi. Elimu, ya kutuwezesha kama taifa kusimama kwa miguu yetu wenyewe katika kila nyanja ya maendeleo. Vipaumbele vya kwaida kila mwaka wa mipango ya maendeleo vingikuwa kama hivyo vilivyopo sasa, ujenzi n.k.

Mwisho: Zitto, umesema vyema kuhusu 'kujipa muda/nafasi ya upweke-------' Bila shaka kuna mengi uliyowahi kuyafikiria yanayokuhusu wewe mwenyewe binafsi na nafasi yako katika siasa za nchi hii. Hayo unayajua mwenyewe. Oh, so much potential, and yet---!

Eti anasimamiaje utekelezaji wa mambo ktk majimbo aliyowahi kuyaongoza, ni kumuonea tu Zitto kutaka akujibu swali hili....

Na inawezekana labda hutambui kazi na majukumu ya Mbunge.....

Kukusaidia tu japo kiduchu, mbunge ni mwakilishi tu wa wananchi wa eneo dogo fulani....

Mbunge hana maamuzi wala nguvu ya kupanga na kuutekeleza mradi wowote wa maendeleo ktk jimbo lake....

Maamuzi yote ya nini kifanyike ktk jimbo la mbunge fulani, siku zote hutegemea mipango ya serikali kuu na bajeti yake....

Na kwa mfumo wa siasa za kukomoana za Tanzania, ni ngumu sana kwa jimbo la linaloongozwa na mbunge wa nje ya chama kilicho madarakani kupata miradi ya kimaendeleo unless ktk mazingira fulani fulani tu ya kimkakati zaidi....

Labda mbunge ktk eneo hili aweza kutumia strategies zake binafsi nje kabisa ya mfumo wa kiserikali wa kibajeti kufanya miradi ya kimaendeleo mfano kutafuta wafadhili binafsi nk
 
Mkubwa mwenzangu Zitto

Hilo ni jicho la kisiasa, kiuhalisia haliwezekani hata robo. Sayansi ya viwanda haiku kama unavyofikiri na haitakuwa hivyo. Kwanza niseme kitu kimoja ambacho kinaziumiza nchi zinazoendele kuwa ni wanasiasa, waweza waita watawala ili upinzani uonekane hauhusiki, lakini wote ni wale wale na wana lao moja. Mikataba mnayoingia ndo huwa inaharibu kila kitu hata kabla ya uzalishaji wenyewe. Mbaya Zaidi huwa mnafanya makusudi kwa kujua asilimia 100. Mfano mzuri ni nyumba za bei nafuu mlizojenga, sijui unafuu mliangalia watu wa kipato kipi. Hivyo waweza kuta chuma kutoka china kikawa na bei nafuu kuliko chuma cha mchuchuma na liganga, sababu ikiwa ni virushwa wakati wa kuingia mikataba.

Nije kwenye mada:
moja:
Chuma na makaa ya mawe tayari ni viwanda viwili. Mwekezaji haweza wekeza kwenye makaa ya mawe kwa ajili ya kulisha kiwanda kimoja cha chuma pekee, atapata hasara.
Kiwanda cha chuma hakiwezi kujengwa kwa kuangalia soko la reli pekee, ambalo huwa halizidi hata miaka kumi linakuwa limetosheka. Hapo yawezekana ndo anaanza kurudisha faida. Hii na hapo juu ni kwa sababu bei za za makaa ya mawe na chuma huhitaji uzalishaji mkubwa ili kutengeneza faida, ndiyo maana viwanda vingi bongo hutumia vyuma chakavu.

mbili:
Kiwanda cha chuma mchuchuma na liganga hakitakuwa na uwezo wa kuzalisha chuma cha pua (pure iron). Kupata chuma cha pua ni kiwanda kingine tena ambacho kitahitaji uhakika wa soko, (si reli pekee kama hapo juu)
Kiwanda cha chuma cha pua hakitaweza tengeneza mataruma ya reli, nacho kitahitaji soko tena Zaidi ya reli kuweza simika kinu cha kusafisha chuma kuwa PURE IRON.
Huyu wa pure iron hataweza tengeneza mataruma yareli, hivyo hicho ni kiwanda kingine ambacho kinahitaji uhakika wa soko kiweze kusimikwa.

tatu:
Kuna chemikali ambata na spea (reagents and spares) ambazo hatuna kiwanda cha kuzizalisha humu nchini, mwekezaji atahitaji uhakika wa kuzipata kwa bei nafuu na kwa wakati (SUPPLY CHAIN isiyo na longolongo wala rushwa!!)

nne:
Hivyo vyote wakati wa mwanzo vitahitaji wataalamu wa kuja kuwafundisha wazawa ambao huwa ni fly in/fly out katika muda mfupi mfupi

tano:
Ukiangalia mlolongo hapo juu, lazima kimoja kianze kistawi kiweze vutia cha pili yake, hivyo si swala la miaka mitano mtu aje azalishe pure iron baada ya mchuchuma kuanza.
Wa pure iron akianza, wa mataruma naye atachukua muda kupata uhakika wa soko kuanza kuzalisha tena.
Kwa mlolongo huo waweza ona kama una nia ya kujenga reli kwa chuma chako utachukua si chini ya miaka 15 mpaka huo uwezo upatikane.

Kuna mambo mengi, wanasiasa wanasema yaliyofichika, lakini yapo wazi hivyo ni bora kununua chuma na kujenga reli kuliko kusubiri viwanda ambavyo huna uhakika vitakamilika lini, hili la kusubiri laweza kuwa chanzo cha kuwabembeleza wawekezaji kwa kuwa kuna uhitaji, hivyo wakatupiga kama buzwagi na wengineo

MIMI NINGEFANYA KAMA MAGUFULI NA SERIKALI YAKE !!
Hoja hii. Mheshimiwa Zitto unaweza ukaipitia au kuitolea maelezo kama yapo.
 
Ni rahisi sana kusema lakini sio kutenda.

Turudishe mpira kwako Mbunge wa Kigoma mjini: Huko kwako umefanyaje nje ya sera ya serikali kuu?
Serikali imempa sh ngapi ili afanyie hayo?
 
Eti anasimamiaje utekelezaji wa mambo ktk majimbo aliyowahi kuyaongoza, ni kumuonea tu Zitto kutaka akujibu swali hili....

Na inawezekana labda hutambui kazi na majukumu ya Mbunge.....

Kukusaidia tu japo kiduchu, mbunge ni mwakilishi tu wa wananchi wa eneo dogo fulani....

Mbunge hana maamuzi wala nguvu ya kupanga na kuutekeleza mradi wowote wa maendeleo ktk jimbo lake....

Maamuzi yote ya nini kifanyike ktk jimbo la mbunge fulani, siku zote hutegemea mipango ya serikali kuu na bajeti yake....

Na kwa mfumo wa siasa za kukomoana za Tanzania, ni ngumu sana kwa jimbo la linaloongozwa na mbunge wa nje ya chama kilicho madarakani kupata miradi ya kimaendeleo unless ktk mazingira fulani fulani tu ya kimkakati zaidi....

Labda mbunge ktk eneo hili aweza kutumia strategies zake binafsi nje kabisa ya mfumo wa kiserikali wa kibajeti kufanya miradi ya kimaendeleo mfano kutafuta wafadhili binafsi nk

Kitaturu, ninakubaliana kabisa na haya uliyoyaeleza hapa kuhusu kazi za mbunge katika uwakilishi wa jimbo. Nisipokubaliana na wewe ni nini nafasi ya mbunge kama kiongozi wa wananchi jimboni kwake. Sijui kama utanielewa utofauti ninaouzungumzia hapa juu ya kofia hizi mbili anazoweza kuzivaa mbunge. Maendeleo ya jimbo ni zaidi ya kutegemea pesa inayotolewa na serikali, na hata wafadhiri uliowataja.

Hata hivyo, katika kukurupuka kunijibu mimi, umeamua kutoweka maanani kauli yangu ya kuwa sina taarifa ya anayoyafanya Zitto jimboni kwake na kwa sababu hiyo nisingeweza kumhukumu kwa hilo.
 
hata mimi naamini wabunge kusubiri kuwa funded na serikali kwenye miradi ya maendeleo ni kupoteza muda,

serikali inaonyesha kabisa iko biased,

resources zote zinapelekwa hukoooo…..wanakojua wenyewe…

.inabidi wabunge wabuni miradi peke yao,

wachukulie ubunge kama wazazi/walezi wa familia,

waje na strategies za kuwainua wananchi wao…

.kutafuta wafadhili ni moja ya njia,

pili ni kutafuta wataalam waje kuexplore opportunities and invest kwenye jimbo lako...
 
Kakaangu na school mate wangu wa Tosa, Mh zitto!!, Andiko lako ni zuri sana na kiukweli linajaribu kuleta tofauti japo tafakari yako juu ya ambayo ungeyafaya kama ungekuwa wewe ndio mwenye mamlaka haijashiba. Imeeleza kijuujuu tu bila hata kutuambia gharama halisi ambayo ungehitaji kuinstall plant nzima ya kuprocess hayo mawe kuwa goods kama mataaluma ya reli itagharimu kiasi gani!!!, hujaelezea uwekezaji wa mtambo wa kufua umeme kwa makaa ya mawe pia kwa MW ulizoelezea hapo juu ungepata wapi pesa za kutosheleza kukamilisha!!!!.
Kiufupi andiko lako limajaa tu yale ambayo watanzania wengi tunapenda nchi yetu ifikie lakini tutafikiaje hapo hujaelezea kwani hata ziara yako na kamati ya POAC kama link uliyoambatanisha hapo juu inaonyesha namna mlivyotembelea migodi nakupewa mikakati ya kwenye makaratasi lakini hamkua na initiative mpya zozote, KWAHIYO ENDELEA TU KUTAFAKARI labda mbele utaweza kuja na hitimisho zuri la Tafakari yako litakalo kuwa na muonekano mzuri wa hadhi yako.
Umegonga kwenye tatizo! Kwani Afrika hasa Tanzania tulishaishiwa mipango mizuri? La hasha! Tuna wanasiasa wengi sana ambao wana mipango mizuri sana kusikiliza. Tatizo letu liko kwenye utekelezaji. Na ni kwa sababu wanasiasa ndiyo wanajitwisha kila utaalam ulio dunia hii. Ndio wapanga mipango kwenye mambo yote. Alichoandika Zitto kwangu siyo kitu kipya bali ni nadharia kama nadharia nyingine nyingi ambazo nimewahi kusikia kutoka kwa wanasiasa wetu. Mimi nadhani wazo kama hili bado liko kwenye stage ya mwanzo kabisa. Linatakiwa lipelekwa kwa wataalam walifanyie reaserch ya kutosha na waje na mpango wenye gharama, muda na kila kitu kinachotakiwa kifanikisha mpango kama huu. Tena niseme nasikitika labda hatuna wataalam wengi wenye uwezo wa ku-research mpango kama huu, hivyo pengine itabidi tuajiri wageni kwa kutumia akili. Vinginevyo mimi naona haya ni mawazo kama mawazo mengine mengi waliyowahi kupangwa na hayakuleta manufaa yoyote. Mwanasiasa anajifungia chumbani, anapanga mipango yake na akiingia ofisini kwesho yake analazimisha ifuatwe.
 
hata mimi naamini wabunge kusubiri kuwa funded na serikali kwenye miradi ya maendeleo ni kupoteza muda,

serikali inaonyesha kabisa iko biased,

resources zote zinapelekwa hukoooo…..wanakojua wenyewe…

.inabidi wabunge wabuni miradi peke yao,

wachukulie ubunge kama wazazi/walezi wa familia,

waje na strategies za kuwainua wananchi wao…

.kutafuta wafadhili ni moja ya njia,

pili ni kutafuta wataalam waje kuexplore opportunities and invest kwenye jimbo lako...

Kazi kubwa ya uongozi ni pamoja na kubuni na kuwahamasisha wananchi wajiletee maendeleo katika yale madogo yaliyo ndani ya uwezo wao. Mathalani, wananchi hawawezi kusubiri serikali iwaletee pesa za kujenga vyoo safi katika makazi yao; kuwahimiza wataalam wa kilimo wawasaidie wananchi katika kilimo bora, n.k, n.k.
Miaka mitano ni muda mzuri sana kwa kiongozi yeyote kuonyesha uwezo alionao katika kubadili mwelekeo wa maisha ya wananchi anaowaongoza. Hata kule kuwatia hamasa na kubadili misimamo juu ya hali ya maisha yao, ni kazi tosha kabisa kwa kiongozi kuifanya. Ni wananchi ndio wanaoleta maendeleo wenyewe, viongozi ni nyenzo tu, kama pesa.
 
Mkubwa mwenzangu Zitto

Hilo ni jicho la kisiasa, kiuhalisia haliwezekani hata robo. Sayansi ya viwanda haiku kama unavyofikiri na haitakuwa hivyo. Kwanza niseme kitu kimoja ambacho kinaziumiza nchi zinazoendele kuwa ni wanasiasa, waweza waita watawala ili upinzani uonekane hauhusiki, lakini wote ni wale wale na wana lao moja. Mikataba mnayoingia ndo huwa inaharibu kila kitu hata kabla ya uzalishaji wenyewe. Mbaya Zaidi huwa mnafanya makusudi kwa kujua asilimia 100. Mfano mzuri ni nyumba za bei nafuu mlizojenga, sijui unafuu mliangalia watu wa kipato kipi. Hivyo waweza kuta chuma kutoka china kikawa na bei nafuu kuliko chuma cha mchuchuma na liganga, sababu ikiwa ni virushwa wakati wa kuingia mikataba.

Nije kwenye mada:
moja:
Chuma na makaa ya mawe tayari ni viwanda viwili. Mwekezaji haweza wekeza kwenye makaa ya mawe kwa ajili ya kulisha kiwanda kimoja cha chuma pekee, atapata hasara.
Kiwanda cha chuma hakiwezi kujengwa kwa kuangalia soko la reli pekee, ambalo huwa halizidi hata miaka kumi linakuwa limetosheka. Hapo yawezekana ndo anaanza kurudisha faida. Hii na hapo juu ni kwa sababu bei za za makaa ya mawe na chuma huhitaji uzalishaji mkubwa ili kutengeneza faida, ndiyo maana viwanda vingi bongo hutumia vyuma chakavu.

mbili:
Kiwanda cha chuma mchuchuma na liganga hakitakuwa na uwezo wa kuzalisha chuma cha pua (pure iron). Kupata chuma cha pua ni kiwanda kingine tena ambacho kitahitaji uhakika wa soko, (si reli pekee kama hapo juu)
Kiwanda cha chuma cha pua hakitaweza tengeneza mataruma ya reli, nacho kitahitaji soko tena Zaidi ya reli kuweza simika kinu cha kusafisha chuma kuwa PURE IRON.
Huyu wa pure iron hataweza tengeneza mataruma yareli, hivyo hicho ni kiwanda kingine ambacho kinahitaji uhakika wa soko kiweze kusimikwa.

tatu:
Kuna chemikali ambata na spea (reagents and spares) ambazo hatuna kiwanda cha kuzizalisha humu nchini, mwekezaji atahitaji uhakika wa kuzipata kwa bei nafuu na kwa wakati (SUPPLY CHAIN isiyo na longolongo wala rushwa!!)

nne:
Hivyo vyote wakati wa mwanzo vitahitaji wataalamu wa kuja kuwafundisha wazawa ambao huwa ni fly in/fly out katika muda mfupi mfupi

tano:
Ukiangalia mlolongo hapo juu, lazima kimoja kianze kistawi kiweze vutia cha pili yake, hivyo si swala la miaka mitano mtu aje azalishe pure iron baada ya mchuchuma kuanza.
Wa pure iron akianza, wa mataruma naye atachukua muda kupata uhakika wa soko kuanza kuzalisha tena.
Kwa mlolongo huo waweza ona kama una nia ya kujenga reli kwa chuma chako utachukua si chini ya miaka 15 mpaka huo uwezo upatikane.

Kuna mambo mengi, wanasiasa wanasema yaliyofichika, lakini yapo wazi hivyo ni bora kununua chuma na kujenga reli kuliko kusubiri viwanda ambavyo huna uhakika vitakamilika lini, hili la kusubiri laweza kuwa chanzo cha kuwabembeleza wawekezaji kwa kuwa kuna uhitaji, hivyo wakatupiga kama buzwagi na wengineo

MIMI NINGEFANYA KAMA MAGUFULI NA SERIKALI YAKE !!
At least Magufuli amejaribu kuhusu MAKINIKIA. Wewe unaturudisha nyuma kabisa kwenye karne ya kumi na tisa kwa 'excuses' hizi ulizoziweka hapa kwa nini hatuwezi kuendeleza chuma na makaa ya mawe yachangie katika uchumi wetu. Na kwa hoja kama hizi, ni kwamba hakuna lolote ambalo tunnaweza kulifanya kwa sababu moja au nyingine. Tuendelee tu hivi hivi ilivyo sasa. Tukisema tuanzishe 'Chemical Industry' utakuja na sababu hizo hizo, Pharmaceutical Industries, hivyo hivyo!
Mawazo potofu kabisa haya kwenye karne hii. Hao waChina wamejenga SGR hapo Kenya, akina Manu Chandaria walikuwa tayari kutoa vyuma vya mataluma ya ujenzi wa reli ile, tena kwa viwango. Leo unatuambia hatuwezi?
Sasa kama waChina wanatengeneza chuma kwa bei ya kutupa, kwani teknologia hiyo haipatikani popote. Si waChina tunao hapa chungu nzima. Ni kipi kinatuzuia waje wajenge hapa watumie makaa yetu na chuma chetu kuzalisha hivyo vya thamani hapa hapa! Unasema soko. Wao wanauza wapi?
Sijui ni yapi ambayo Magufuli anafanya ambayo na wewe ungeyafanya, maanake naona wewe uko kinyume kabisa na yale ambayo angependa kuyafanya.

Zitto anahoja. Lililopo ni kuifanyia kazi hoja hiyo, sio kukatisha tamaa.
 
Mkuu hukunielewa
Mimi naunga mkono hoja kiwanda cha chuma, lakini si kwa kulenga standard geji. Kwa std geji ndo maana nikasema ni bora kununua chuma kuliko kuzalisha cha kwetu maana kuna viwanda vingi mpaka ufikie mataruma

NITAFANYA KAMA MAGUFULI NA SERIKALI TAKE
 
Nimekuelewa sana, hata kabla ya kurudia kusoma hoja zako baada ya kusema sikukuelewa. Achana na mawazo hayo ya 'hatuwezi' aisee! Acha wenye uthubutu wafanye, usiwakatishe tamaa. Kazi ya mwanasiasa mzuri ni ku'encourage' ili 'vision' yake itekelezeke. Yeye haielekezi wataalam wenye nyanja mbalimbali watatekelezaje 'nitty gritty' ya miradi inayohusika katika 'vision' yake. Yeye anatoa 'broad view', watekelezaji wanajua watatekeleza vipi.
 
Zitto , baada ya kusoma bandiko lako yapo ninayokubaliana nawe na nisiyokubaliana nayo

Nianze kwa nisiyokubaliana nayo.
Kauli kwamba 'ningepewa mamlaka ningefanya abcd' si sahihi.

Kauli hiyo inatoa 'uhalali' wa mwingine kusema nina mamlaka nafanya abcd

Pengine ungesema ningepewa mamlaka ningeshauriana na wenzangu kuhusu abcd

Utamaduni wa kushaurian umetoweka na Mwalimu. Ukirudi nyuma, kulikuwa na mipango ya maendeleo ya kitaifa 'vision' kuanzia ule wa mwaka 1963 na kuendelea.

Mipango hiyo imeacha alama unazoweza kuziona kote nchini hadi leo.
Si barabara, maji, umeme,Shule, Hospitali, viwanda, kilimo n.k.

Kwasababu ya kupoteza vision ya kitaifa, mipango ya maendeleo imekuwa kama hadithi
Nimeshangaa tumeondoka kwenye gesi ya Mtwara katika miaka 2 tu sasa ni stigler gorge

Nauliza, tulikuwa na vision ya kitaifa kuhusu nishati? Na kama ilikuwepo ni ya miaka mingapi?Na kwa utaratibu gani tumeweza kubadili gia ghafla kiasi hicho?

Pili, tulipoacha reli kama ile ya kaskazini ikaota nyasi tulikuwa na vision ya kitaifa ya infrastructure? Kama ilikuwepo kwanini tunarudi kwenye reli tena ikiwa tuliachana nayo?

Tatizo ni moja, mfumo wetu wa kujitawala una matatizo.
Hatuna sera za kitaifa kama dira, tunasera za vyama.

Hivi ni vitu viwili tofauti ingawa hatujui. Sera za kitaifa zinaeleza 'vision' ya taifa
Kwa wenzetu sera za kitaifa hazibadiliki hata kama mifumo ya kisiasa inabadilika.

Sera za vyama zinabadilika katika kueleza tunafikiaje malengo ya dira ya Taifa 'vision'

Hili utaliona Bungeni Ulipo.
Masuala ya kitaifa yanajadiliwa kivyama, utapataje vision ya taifa kwa mfumo huo?
Mipango ya maendeleo inafikishwa na kujadiliwa kivyama tena bila tathmini ya uliopita

Kutokana na mfumo mbovu unaoanzia bungeni, hakuna mijadala ya sera za nchi
Ubovu huo unapelekea kuwepo kwa Elimu kwanza, Kilimo kwanza, Viwanda kwanza n.k. kwa kofia ile ile uliyosema 'ningekuwa na mamlaka, au nina mamlaka nitafanya abcd'

Ningekuwa au nina, si mbadala wa tungefanya . Kwa hilo unadhani tutafanikiwa?

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Tatizo kuu la Tanzania sasa ni ccm.Hawapendi kabsa mwananchi akomboke iwe ki elimu,uchumi hata kijamii.Ufukara na ujinga wa Watanzania kwa ccm n mtaji mkubwa.Hvyo hiki chama ni laana mpaka kitapotoka nadhan watanzania tutapata uhuru wa pili na wa kweli.
 
NingefanyaTofauti

Na Zitto Kabwe

KWA miaka mingi nimekuwa mtu ninayeamini katika kujipa muda wa upweke na kutazama dunia iliyonizunguka na kujiuliza maswali ama kunihusu mimi binafsi au kuhusu nchi yangu na Afrika. Waingereza wangesema self reflection lakini ninapenda kutumia neno la lugha ya Kiswahili; kutafakari. Ninaamini kwamba ni muhimu kwa kiongozi kupata muda huu muhimu.

Siku chache zilizopita, nilijipa muda huo wa utulivu kwa ajili ya tafakari. Swali kuu nililokuwa nikijiuliza ni hili; kwamba kama ningekuwa nimepewa mamlaka ya kuongoza Tanzania nini ningefanya tofauti na wanaoongoza sasa?

Katika tafakari hii nilikumbuka safari niliyofanya wilayani Ludewa mwaka 2011 kukagua na kutoa nguvu kwa uwekezaji wa kimkakati wa uchimbaji wa madini ya chuma na makaa ya mawe na kuweka msingi wa viwanda mama nchini kwetu. Unaweza soma chapisho la blogu ya safari hiyo hapa An Eye Opener Week-long Visit to South Tanzania 1500MW Electricity Complex. Nadhani ningeanza na mradi huu kabla ya kitu kingine chochote. Nina sababu za kufikia hitimisho hilo.

Mchuchuma na Liganga ni nini?

Madini ya chuma na makaa ya mawe ndio msingi wa maendeleo ya viwanda duniani kote. Nchi yetu ina madini haya yote kwenye eneo moja, wilayani Ludewa mkoa wa Njombe. Hakika Mungu alitupenda, maana aliumba dunia na akaisanifu Ludewa na kuiweka Tanzania ili iwe chanzo cha viwanda mama.

Katika eneo la Mchuchuma kuna mashapo yenye tani bilioni 1.2 makaa ya mawe yenye uwezo wa kuzalisha Umeme 600MW kwa miaka 150. Makaa hayo pia hutumika kuyeyusha chuma na kuzalisha chuma cha pua. Vilevile eneo la Liganga lina mashapo ya madini ya chuma tani bilioni mbili ambayo ndani yake kuna madini yenye thamani kubwa ya Titanium na Vanadium.

Ujenzi wa kilometa moja ya reli unahitaji chuma cha pua (steel) chenye ubora wa hali ya juu kiasi cha tani 40 mpaka 60. Tanzania tunajenga kilomita 1200 za reli kwa sasa hivi na baadaye zitaongezeka kwa vipande vya Tabora - Kigoma, Kaliua - Mpanda - Karema, Uvinza - Musongati na miradi mingine kama Mtwara - Mbamba Bay, Ruvu - Tanga, Tanga - Musoma - Kigali nk. Kwahiyo basi, Tanzania itahitaji sio chini ya tani 500,000 za chuma cha pua (steel) katika kipindi cha miaka michache ijayo.

Afrika nzima inajenga reli za kisasa na zote zinahitaji chuma kwa ajili ya kujenga njia za reli. Kenya na Ethiopia wamemaliza hatua za kwanza za reli zao ambapo Kenya imeshajenga kilometa 485 kutoka Mombasa mpaka Nairobi na Ethiopia kilometa 760 kutoka Addis Ababa mpaka Djibouti. Miradi yote hii mataruma ya reli yameagizwa kutoka nje na kuletwa Afrika na hivyo kuzalisha ajira huko kwenye nchi hizo (ambazo mataruma hayo yamezalishwa ).

Fedha za miradi hii zitakwenda nje ya nchi, Waafrika hawatafaidika kabisa. Tanzania nayo inakwenda njia hiyo hiyo licha ya kwamba ina madini ya chuma na makaa ya mawe ya kuzalisha chuma cha pua ambacho huzalisha mataruma ya reli na bidhaa nyingine kadha wa kadha za ujenzi wa reli. Tanzania ingeamua, ingeweza kulisha miradi yote ya reli chuma kutoka Ludewa katika nchi za Kongo, Zambia, Angola, Uganda na Rwanda ambao wote wana miradi ya ujenzi wa reli na wamepanga kuagiza chuma kutoka China na kwingineko.

Bei ya tani moja ya chuma kwenye soko la dunia ni dola za Marekani 600 mpaka 1000. Kwa hiyo Tanzania ikizalisha chuma tani milioni moja tu kwa mwaka, inaweza kupata mapato ya fedha za kigeni kati ya dola milioni 600 mpaka dola bilioni moja kwa mwaka. Kwa mashapo yaliyopo Tanzania, tunaweza kuzalisha kiwango hicho cha chuma kwa miaka zaidi ya 2000 na chuma cha Ludewa kisiishe.

Kwa hakika mahitaji ya chuma yatakuwa ni makubwa na tunaweza kuzalisha na kuuza nje mpaka tani milioni tano kwa mwaka. Hivi sasa nchi ya Australia ndio inaongoza duniani kwa kuuza chuma kingi zaidi. Mwaka 2017 waliuza tani milioni 49 za chuma na kupata dola za marekani bilioni 49.

Jambo kubwa sana ambalo Tanzania imebahatika ni kwamba mashapo ya chuma yana madini mengine yenye thamani kubwa zaidi. Kwa mfano Vanadium ya Ludewa inauzwa tani moja dola 50,000 katika soko la dunia. Katika kila tani milioni moja ya chuma kutoka Ludewa, kuna tani 80,000 ya Vanadium. Tukiuza madini haya tunapata fedha za kigeni dola za kimarekani bilioni nne kwa mwaka.

[HASHTAG]#NingefanyaTofauti[/HASHTAG]

Unapokuwa na mamlaka ya uongozi wa nchi unakumbana na changamoto nyingi sana na moja ya changamoto ni kuamua uanze na nini katika vipaumbele vya nchi ili kupiga hatua za kimaendeleo. Kiongozi mwenye maarifa huanza na mambo ambayo yatamwezesha kupata rasilimali fedha ili atekeleze majukumu mengine. Ni dhahiri hapa Tanzania tuna changamoto ya miundombinu ya usafirishaji, reli, barabara na hata usafiri wa anga.

Viongozi wetu wa sasa wameamua kuanza na hayo kwa kutumia fedha za kodi au mikopo ghali yenye riba kubwa kutoka mabenki ya biashara ya nje. Wameanza na ujenzi wa reli wa dola bilioni saba, ununuzi wa ndege wa zaidi ya dola bilioni moja ( Dreamliner ‘Terrible Teen’) imenunuliwa kwa dola milioni 224 na hata ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Rufiji maarufu kwa jina la Stiglers Gorge litakalogharimu dola bilioni 3.5.

Yote haya yanahitaji kukamua kodi wananchi na kuchukua mikopo inayokuza Deni la Taifa. Yote haya yanasababisha mzunguko wa fedha nchini kuwa mdogo kwa sababu fedha zinatoka nje ya nchi kulipia wakandarasi na kununua malighafi kama chuma.

Ningekuwa na mamlaka ningeyafanya haya yote, lakini kabla ya kufanya hayo, ningeanza kwanza kwa kufanya jambo moja kubwa ambalo lingenipa fedha za kufanya hayo. Ningefanya tofauti.

Ningeanza na mradi wa Mchuchuma na Liganga kwa kuhakikisha kuwa uwekezaji unaanza mara moja na uzalishaji wa chuma na makaa ya mawe unafanyika bila kuchelewa. Ningehakikisha kuwa ndani ya miaka 2 tunaanza uzalishaji wa chuma, Vanadium na Titanium.

Mauzo ya Vanadium peke yake ni sawa na dola bilioni nne kwa mwaka ambapo kwa kuwa haya ni bidhaa ambatana na chuma maana yake 80% ya mapato haya yangekuwa ya nchi. Kwa hiyo mwaka wa kwanza tu wa uzalishaji ningeweza kupata dola bilioni 3.2. Kwa fedha hizo, tungejenga reli kuanzia Dar mpaka Dodoma kwa mara moja bila kuungaunga na kubakia na chenji ya dola bilioni moja ambazo ningeweza kujenga hospitali tano kubwa kama Mloganzila katika kanda tano za nchi; Mbeya, Mtwara, Mwanza, Kigoma na Arusha.

Ningeweza kujenga vyuo vya VETA kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa nchini ( Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji ) kwani unahitaji shilingi bilioni 750 tu kujenga vyuo hivyo vilivyokamili na vifaa vya kutosha vijana kupata mafunzo.

Ningeweza kujenga vyuo vikuu vipya vitatu aina ya UDOM kwani UDOM moja ina thamani ya shs bilioni 800 tu. Haya ni mapato ya mwaka wa kwanza tu. Kumbuka kuwa tunaweza kuendelea kuchimba chuma tani milioni moja kwa mwaka kwa miaka 2000!

Tungeamua kuzalisha tani milioni tano kwa mwaka maana yake mapato ya Vanadium peke yake kwa mwaka yangekuwa dola bilioni 16 ambazo ni sawa na kumaliza reli yote mpaka Kigoma na Mwanza na kuiwezesha Air Tanzania kuwa na ndege kubwa na ndogo sawa na Shirika la Ndege la Ethiopia na hata kuzalisha umeme zaidi ya 10,000MW ndani ya miaka mitano kwa kutumia makaa ya mawe, geo thermo, gesi asilia, upepo na jua – yote hayo bila kuathiri hifadhi ya Selous.

Kwa kuzalisha tani milioni tano kwa mwaka tungezalisha chuma, Vanadium na Titanium kwa miaka 400 mpaka kumaliza mashapo yote tuliyonayo. Kwanini hatuwekezi Mchuchuma na Liganga?

Kungoza nchi kunahitaji MAARIFA. Hakika [HASHTAG]#NingefanyaTofauti[/HASHTAG]
Kaka Zitto, hakika wewe ungekuwa kiongozi wetu tungepiga hatua kubwa sana sana kiuchumi, unajua mno kaka. Nilishawahi kuandika hapa kwamba wewe haswa ndio kiongozi ambaye ungepata nafasi ya kuiongoza nchi hii miaka michache tu wakenya tungewakalisha kiuchumi na mifuko ya watu ingenenepa mno.
Sasa tunaongozwa na mkemia mambo ya uchumi ndio hajui kabisa na kwa bahati mbaya zaidi hapokei ushauri matokeo yake hajui kabisa ainvest wapi fedha ya nchi ili kama nchi tupate utajiri wa haraka. Sasa badala ya kufanya miradi kama hiyo ya Liganga na mchuchuma ananunua ndege ambazo ni liability tu, lile shirika halijawahi kuingiza faida hata mara moja, lakini hatukatai kuwa na ndege lakini kama nchi tuna utajiri wa asili kama huo wa chuma na madini ambapo tukiwekeza tunavuna mahela kufuru ya kununua madege, kujenga hospital, vyuo na miundombinu kadha wa kadha.

Sasa badala hela ya kodi aipeleke kwenye uzalishaji wa mambo mazuri kama hayo ili tusiwe tunategemea kodi kujenga miradi ya nchi, anajenga sgr na kununua ndege kwa hela za kodi na mikopo duh ama kweli this time tutashindia chai kwa mluzi

Kaka endelea kutupa madini kama haya, Mungu si athumani inaweza ikatokea namna tu huko mbeleni ukapata nafasi ya kuongoza ndani ya miaka kumi yako wasouth tutawapumulia kisogoni.

Kila La kheri kaka
God bless u
God bless Tz
 
Ni rahisi sana kusema lakini sio kutenda.

Turudishe mpira kwako Mbunge wa Kigoma mjini: Huko kwako umefanyaje nje ya sera ya serikali kuu?

Kwanini usiiulize serikali ya CCM yenye dhamana ya kutumia pesa za Watanzania.
 
Upo sahihi ni ushauri mzuri sana wa kuzingatiwa...

Ila ujue kuongea au kuandaa mipango ni tofauti sana na utekelezaji...

Ni sawa na mtoto pale anapoona kwa nini baba yake hafanyi jambo fulani kama baba wa wengine na kujisema ngoja na mimi niwe baba nitafanya vyote na zaidi... ila nae akija kua baba ndiyo ugumu na changamoto anaziona...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom