Zitto Kabwe: Kama ningepata mamlaka ningefanya tofauti

Zitto Kabwe: Kama ningepata mamlaka ningefanya tofauti

Eti sisi tunakomaa na Stiglers Gorge ambalo kesho tu linajaa tope na hatuna guarantee na Mungu kwamba tutaendelea kuwa na mvua za kutosha, vipi nchi ikikumbwa na ukame?
Ishu ya mvua za kutosha nimekua nikijiuliza sana mkuu!! Hivi haya mabadiliko ya tabia nchi hawayaoni? Sijui wanatumia nini kufikiri hawa jamaa [emoji29] [emoji29] [emoji29] ?
 
Tunahitaji dira ya maendeleo ya taifa ambayo inaandaliwa na wadau wote wakiwemo wananchi wenyewe. Tukishampata kiongozi wetu basi tunamwapisha kwa kitabu cha dini na mpango huu wa dira ya maendeleo ya taifa ili atekeleze.

Vinginevyo tutegemee mengine mapya kabisa tukimpata kiongozi mwingine.
 
Ni rahisi sana kusema lakini sio kutenda.

Turudishe mpira kwako Mbunge wa Kigoma mjini: Huko kwako umefanyaje nje ya sera ya serikali kuu?
We ulitaka afanyeje?kwani yeye ndo anaekusanya kodi za wananchi hadi we umuulize hivyo?
 
Kusikika kulikuwa na Tija gani wakati huo? Kulimsaidia nini Mtanzania wa kawaida?
Kwa hakika NINGEFANYA TOFAUTI na alichofanya Zitto Kabwe. Shame on him!
Muda utaongea.
Jadili hoja, sio mtoa hoja
 
sheria mbovu or migodi + ardhi vilivyomilikishwa kwa wageni kinyemela
Mkuu, sheria mbovu ni za kujitakia bunge ndio linazitunga, migodi + ardhi sheria zake ni bunge hilohilo, kama wapinzani wanaziona wakati wa kuzitunga mpaka wanasusia kikao kujitenga na hizo sheria, ina maana wanaopitisha wanajua wakifanyacho, mwaka 1999 Lisu alikamatwa na kuwekwa ndani kwa kupinga sheria hizi akiwa sio mbunge, Mkapa alijimilikisha mgodi wa Kiwira je umesahau madudu ya meremeta nk? hao mnao waita wabunge wetu walipigia makofi sheria hizi na kuzomea wapinzani, wao wanajali ubunge wao zaidi kuliko chochote, ndio maana miaka hiyo walipigia makofi sheria mbovu halafu wakapigia tena makofi makinikia, yaani watu wa ajabu mno! hebu angalia hoja za humu jf, mtu badala ya kutoa hoja anamshambulia mtoa hoja hii ni kiroja, hicho usemacho si kweli hawa viongozi wana nia ovu, tena hawa wa sasa ni sifa binafsi tu, ni ushamba wa kutaka sifa tu, nimekulia dar, msemo wa ushamba wa kisukuma ni maarufu sana, zamani nilikua nauchukulia msemo wa utani tu wa kuchekesha, hapana sasa naushuhudia kwa masikio na macho yangu eeh Mwenyezi Mungu tunusuru!
 
Kuna kitu nimegundua katika mambo ya uongozi
Ukikaa pembeni unaona kiongozi flani anavyokosea na kuharibu lazima utamuona mjing/mzembe sana maana unaona anafeli kirahisi sana kwa maswala yanayohitaji akili ndogo tu kujiongeza
Lakini kiuhalisia ukipewa hicho kijiti ndipo utakapogundua how complex it is
Pale kila jambo linakuja mezani likisubiri wewe ndio ufanye maamuzi
Hapo unajua fika kila mtu anakuangalia wewe anangoja ukosee tu aite press conference akuchane
Kama huwezi kucalm down na kutumia hekima na busara iamue unaweza ukajikuta unavuruga kila kitu.
Tuwaombee sana hawa viongozi wetu maana wana changamoto nzito ambazo its almost killing them inside
Especially kwa wale wazalendo wa kweli

Ukiona mtu anapata shida kutoa maamuzi ya kiuongozi ujue sio mtu sahihi wa nafasi husika. Huu ugumu unaousema wanakutana nao viongozi waliongia madarakani kwa kutumia udhaifu wa sheria za uchaguzi. Lakini kwa kiongozi aliyeingia madarakani kihalali atachukua ushauri wa yoyote kwa faida ya nchi yake.
 
Ni rahisi sana kusema lakini sio kutenda.

Turudishe mpira kwako Mbunge wa Kigoma mjini: Huko kwako umefanyaje nje ya sera ya serikali kuu?


Hivi vichwa hivi!!!

Hivi mbunge kuna hazina ambayo iko chini ya mamlaka yake?

Zitto ameongea kama msomi mwenye fikra pana ila watu wanamjia juu!
 
Huu ushambenga wa aina hii uwe unapendelea kujadili na Gyno wako wakati wa standard check ups zako. Siku njema.
Mjadala sio saizi yako kaendelee kusoma after four thirty ya Ngugi wa Thiong'o ndio unachoweza!
 
Je wapi unapata umeme we kuzalisha chuma liganga na mchuchuma?
Tuanzie hapo


..msome vizuri mtoa mada.

..ameeleza kuwa eneo la MCHUCHUMA kunapatikana MAKAA YA MAWE ambayo yanaweza kutumika kuzalisha UMEME.

..vilevile mtoa mada ameeleza kwamba eneo la LIGANGA kuna hazina kubwa ya madini ya CHUMA, VANADIUM, na TITANIUM.
 
Mda aliotumia kuandaa hili kwanini asitumie kuandaa desa ni jinsi gani kama mbunge atawasaidie ili wanufaike na zao la chikichi?
 
ongozi hawa wanawaza zaidi kuchukua fedha kutoka hazina kufanya mambo yatakayowapa umaarufu wa kisiasa kuliko kuwaza kufanya mambo yatakayotengeneza fedha za kupeleka hazina
Mradi gani ambao usingekuchukua fedha Hazina,
 
Yaani Zitto kila kitu wewe unajifanya unajua zaidi. Duh.

Don't be naive, Zitto katoa njia mbadala iwapo yeye angekuwa rais angafanyaje. Hakuna popote alipolazimisha kujifanya anajua kila kitu. Ww tetea au onyesha wazo lako badala ya kumuona anajifanya mjuaji. Tatizo la Zitto hapa ni huu mchezo wake wa kuja na wazo kisha kulibwaga hapa bila kurudi na kutoa ufafanuzi wa baadhi ya post hata chache.

CC: Zitto
 
Chuki na undumi la kuwili ndo unao kusumbua Zitto

Ikitumika/Akitumia njia A, kesho yake lazima ibuke na kusema angelitumia tu njia B
Hakika umenena, angeanza na mchuchuma au Liganga ungesikia wamefanya sivyo..

Zitto aliwahi kutoa ushauri sukari ya nje isiingie ndani (vibali vifutwe) serikali mpya ilipoingia madarakani ikafuta vibali vyote sukari ikawa adimu, ghafla wakaanza oooh wamekosea sukari imeadimika na Bei imepanda sana
 
Back
Top Bottom