Zitto Kabwe aliwafanyia kitu gani CHADEMA?

NTIGAHELA

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
362
254
Tatizo katika nchi hii Kuna kundi linajiona Lina hatimiliki ya upinzani kwenye siasa za Tanzania, wanawaona wapinzani wote ni mamluki wa watawala isipokuwa wao tu ni wazi kabisa kwa sasa hivi kwamba CHADEMA wameshindwa kufanya siasa bila kumtaja mwamba Zitto.

Tokea miaka ya 2009 Chadema wamewaaminisha Wafuasi wao kwamba Zitto ni CCM na wao ndo wapinzani, fanyeni siasa zenu.

Viongozi wa Chadema wako busy kupambana na ACT badala ya issues za kitaifa:

1. Hivi ni lini mara ya mwisho wamekaa kitako na kuchambua bajeti ya nchi, na kutoa recommendations

2. Hivi ni lini mara ya mwisho wamekaa kuchambua ripoti za CAG?

3. Sijawaona wakikaa chini na kuchambua ripoti za benki kuu na muelekeo wa uchumi wa nchi

Sasa hivi wako busy kumshambulia Kiongozi wa ACT Wazalendo, Wamesahau kuwa:

1. Chama chao ndo kinaogoza kwa viongozi wao kuunga mkono juhudi na kwenda CCM

Chadema itueleze, kama viongozi wake siyo mamluki

Inakuwaje Makatibu wake wakuu wawili wameunga mkono siasa za CCM huku Wabunge wake lukuki na wajumbe wa kamati kuu wakiunga mkono juhudi?

1. Yuko wapi Dkt. Slaa, Dr Mashinji, Nassari, Silinde, Lijualikali, Mollel, Waitara, Katambi

2. Ilikuwaje kwa Katambi mwenyekiti wao wa BAVICHA, Halima Mdee mwenyekiti wa BAWACHA, Matiko, Bulaya, Hanje?

Kwa data hizo, nani CCM zaidi yao?

By the way, Nyie ndo mlimuita mzee Lowasa kila aina ya jina baya halafu mkatoka hapo mkamfanya yeye kuwa ndiye mgombea wa chama chenu mwaka 2015-Sasa hapo mtaaminikaje?

Mwacheni kiongozi wa Chama cha ACT ndugu Zitto afanye kazi yake.

FB_IMG_1648525595297.jpg
 
Tatizo katika nchi hii Kuna kundi linajiona Lina hati miliki ya upinzani kwenye siasa za Tanzania , wanawaona wapinzani wote ni mamluki wa watawala isipokuwa wao tu
ni wazi kabisa kwa sasahivi kwamba chadema wameshindwa kufanya siasa bila kumtaja mwamba zitto tokea tokea miaka ya 2009 Chadema wamewaminisha nyumbu au Wafuasi wao kwamba zitto ni ccm na wao ndo wapinzani fanyeni siasa zenu
Mkuu kwani ZITTO kakuambiwa Alifanywa Nini na Chadema?

ZITTO ni MSALITI Mchana yupo Upinzani USIKU yupo CCM

ZITTO na Prof.Mukandala hata PROF.LIPUMBA kawashtukia
 
Ila ni kweli Chadema hujiona kuwa wao ndio wapinzani wa kweli pekee Tanzania na vyama vyengine vyote ni mamluki wa CCM,

Nakumbuka kabla ya Chadema na ACT azalendo kushirikiana ile 2020 huko nyuma Lissu aliwaita ACT kuwa wanatumika na CCM na kusema ACT hawakuwahi kuwa wapinzani na kumtaja hadi marehemu Anna mgwila kuwa alipewa kile cheo baada ya kuifanya kazi ya ccm 2015 ila nikashangaa 2020 wakashirikiana na hao hao.
 
ACT kama ingemsimamisha Lowassa 2015 nadhan Zitto Kabwe angekosa pa kuweka sura yake

Chadema ina madiwani nchi nzima wanaoshiriki Vikao vya halmashauri lakin bado hawatambui matokeo yote ya uchaguzi wa 2020

Chadema walikataa kushiriki uchaguzi wa 2019 wakashiriki wa 2020

Jamaa kweli wako serious
CHADEMA wapo serious na mambo ya msingi
 
ACT kama ingemsimamisha Lowassa 2015 nadhan Zitto Kabwe angekosa pa kuweka sura yake

Chadema ina madiwani nchi nzima wanaoshiriki Vikao vya halmashauri lakin bado hawatambui matokeo yote ya uchaguzi wa 2020

Chadema walikataa kushiriki uchaguzi wa 2019 wakashiriki wa 2020

Jamaa kweli wako serious
Amekutuma umtetee
 
Mwacheni Zitto afanye kazi yake!

KWANI CDM WAMEMSHIKA MIGUU NA MIKONO HUYO BWANA NYEPESI ILI ASIFANYE KAZI YAKE????
 
Amekutuma umtetee
Kama Wewe umetumwa kumshambulia basi nami nimetumwa kumtetea

ACT ingemteua Lowassa kuwa Mgombea Urais 2015 si pangechimbika

Hivi Zitto angekosa Ubunge 2020 halafu Mbowe na Lema wakapata sijui hali ingekuaje?


Inshallah 2025 wote Mbowe na Zitto watarudishwa Bungeni kwa udhamini wa Chama cha Mapinduzi japo wataingia kupitia vyama wanavyoongoza
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom