Zitto: CCM inachonganisha viongozi wa CHADEMA

Anyways haya ya kusingiziwa mara kuna watu wanachonganisha mara anaonewa yatapata majibu siku moja just a matter of time mi naamini ukwel wote utakuja kupatikana
 
Mkeshaji, umekerwa na nini kwenye thread ya CHUAKACHARA? Mtandao huu upo kwa ajili ya watu kusema mazuri na mabaya, sioni kosa lake!
Mkuu huoni thread zakumhusu mtu mmoja zina flood server za jf. Nadhani wakati mwingine si vibaya tukaunganisha mawazo yetu kwenye thread ambazo tayari zimeshaanzishwa badala ya kila mtu kuja na yake kuhusu jambo hilo hilo moja. We unaonaje?
 
Mkeshaji, umekerwa na nini kwenye thread ya CHUAKACHARA? Mtandao huu upo kwa ajili ya watu kusema mazuri na mabaya, sioni kosa lake!

Ndio maana nime-note na kumshukuru. Sioni ubaya katika post yangu. Zitto ataikuta hapa. Nimechagua hapa yeye anataka facebook, PM. If you think you can not do with this thread, you just leave the page, basi bwana/bibi? Mkeshaji
 
Mkuu huoni thread zakumhusu mtu mmoja zina flood server za jf. Nadhani wakati mwingine si vibaya tukaunganisha mawazo yetu kwenye thread ambazo tayari zimeshaanzishwa badala ya kila mtu kuja na yake kuhusu jambo hilo hilo moja. We unaonaje?

Server space inakuhusu nini, wamiliki wa JF hawajalalama. We sema unapishana na Zitto, hivyo any good comment on Zito is an insult to you!!!!
 
Mkuu naona kama alisingiziwa kwa kuwa kama hakusingiziwa na alikuwa kinara wa masalia kwa nini wasimjadili na kumfuta? Iweje wafuasi wafutwe wakati kinara na mfadhili wao bado anaendelea kuwepo chamani? Naona kama Zitto alikuwa anasingiziwa tu na hao akina Mr 8 O'clock kwani waliothibitishwa na Chama kuwa wasaliti wamepata haki yao.

Mkuu,
Mbona hili liko wazi. Hakuna aliyemsafi katika meza kuu ya CHADEMA. Kumjadili au Kumfukuza Zitto ni sawa na kuacha mlango wa nyumba wazi ili wapita njia waone kwa macho yao kilichoko ndani.

Huna haja ya kuzungusha kichwa kujenga hoja. Mambo yote yako wazi kwa kila mmoja kuona.
 
Server space inakuhusu nini, wamiliki wa JF hawajalalama. We sema unapishana na Zitto, hivyo any good comment on Zito is an insult to you!!!!
Mkuu na wewe naona unataka malumbano tu.
Thread kuhusu jambo hili zipo nyingi tu. Umeona ugumu gani kuweka post yako huko?

Hebu cheki:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-ahadi-sasa-kusomesha-watoto-kata-nzima.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...u-26-baada-ya-zitto-kufanya-mahojiano-jf.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/393403-zitto-ccm-inachonganisha-viongozi-wa-chadema.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/393256-raia-mwema-zitto-kuchukua-maamuzi-magumu.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/392924-zitto-chupuchupu-kutimuliwa-chadema.html

Kweli katika hizo zoote hakuna hata moja ambayo hoja yako inafit humo?
 
Huwezi amini kujisafisha huku kote hizi ni kampeni tu za uchaguzi wa chama unaokuja, nothing goes for nothing... Umewahi msikia hata siku moja akiwakana wale wote waliofukuzwa ambao kwa uwazi kabisa wamekuwa wakihubiri kujihusisha nae??
 
Humjui ZITTO wewe?huyu dogo ameshanunuliwa muda mrefu sana,ni ndumila kuwili,kuna watu wanamtumia huyu.
yawezekana ikawa ni kweli ...ila yawezekana ikawa ni uongo pia....kimsingi hakuna aliyefanikiwa katika hiii dunia bila kuwa na uwezo wa kuishi na wasaliti miongoni mwake......
 
hivi nikwanini alikatazwa kujieleza ? lkn wengine waliruhusiwa kusema chochote!
 
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, amekishutumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba kinachonganisha viongozi wa chama chake kwa lengo la kukidhoofisha wakati huu kinapoelekea kushika dola mwaka 2015.


Zitto alisema hayo jana alipokuwa anazungumza na viongozi wa CHADEMA wa matawi na kata zote kutoka Jimbo la Kigoma Kaskazini ukiwa ni mkakati wake wa kuendelea kukijenga chama na kujua matatizo ya kisiasa na kijamii yanayowakabili wananchi wake.


Mbunge huyo ambaye ameamua kupiga kambi jimboni humo kwa lengo la kuwazuia CCM wasipotoshe wananchi wake wakati huu wanapoadhimisha miaka 36 ya kuzaliwa chama chao, alisema kuwa licha ya maneno na uvumi kuzagaa kwamba CHADEMA Taifa inakabiliwa na mgogoro baina ya viongozi, jambo hilo si kweli.


Zitto alibainisha kuwa hali hiyo inakuzwa na watu waliopandikizwa na kutumiwa na CCM kwa ajili ya kuleta mpasuko na kukigawa chama ili kupunguza kasi yake ya kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.


“CHADEMA hakuna mpasuko wala migogoro kama inavyotafsiriwa na wengi, badala yake kuna kakundi kanataka kutuhujumu kwa kutugawa kwa kutumia itikadi za kidini, kimaeneo, kimitazamo na hata kiitikadi kama walivyotumwa na hicho chama chao.


“Ninachoweza kusema ni kwamba ndani ya chama chetu kuna majungu, fitina, kuoneana wivu, usaliti na hata kumalizana kisiasa, haya tutahakikisha tunayamaliza kikatiba kwa sababu hiyo ndiyo sheria mama inayotuongoza ili tufikie malengo tuliyojiwekea,” aliongeza Zitto.


Alidai kuwa wajibu wake ni kupigania misingi ya uwajibikaji na demokrasia ndani ya CHADEMA ili kuondokana na vitendo vya uongozi wa kutumia mabavu kama ilivyo kwa CCM, ambayo imekuwa ikitumia nguvu katika kuendesha mambo yake, sambamba na serikali iliyopo madarakani.


Hata hivyo, aliwashutumu viongozi wa jimbo lake kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo katika kujenga chama na badala yake kila kitu kumtegemea yeye kama mbunge ikiwa ni pamoja na vikao na mikutano ya hadhara.


“Ili tujenge chama chenye nguvu na heshima, ni lazima viongozi wote tushirikiane kuanzia ngazi ya matawi, kata na jimbo badala ya kila kitu kunitegemea mimi mbunge, lazima tuweke misingi imara ya chama ili mgombea ajaye wa CHADEMA asipate wakati mgumu wa kufanya kampeni,” alisisitiza.


Zitto aliongeza kuwa, wakazi wa Kigoma kwa miaka mingi wamekuwa hawana mtetezi katika ngazi za kitaifa, kiasi kwamba hoja za kuendeleza mkoa kwa kupatiwa miradi ya maendeleo zinapata upinzani mkubwa kwenye vikao vya uamuzi kama vile Baraza la Mawaziri na Bunge.


“Lazima sisi watu wa Kigoma tuwe na umoja kwa sababu tumekuwa wanyonge kwa miaka mingi, na daima nguvu ya wanyonge ni umoja baina yaoNa sisi tunapaswa kuwa na umoja kwa ajili ya maendeleo ya mkoa wetu na hata hii miradi inayoletwa Kigoma sasa ni kutokana na kelele tunazopiga,” alisema.


Aliongeza kuwa hata kama hatagombea nafasi yoyote ndani ya chama, bado ataendelea kuwa mwanachama mwaminifu na ataitumikia CHADEMA kwa vile misingi aliyoshiriki kuitengeneza kwa ajili ya ustawi wa chama hicho bado haijakamilika na hawezi kuiacha ikiwa hivyo.

JE WEWE KAMA MWANACHADEMA KINDAKINDAKI UNASHAURI NINI JUU YA HATUA YA MH,ZITO KUTAKA KUSTAAFU UBUNGE MAPEMA ANGALI BADO CHADEMA INAHITAJI WABUNGE WENGI HAPO MWAKA 1015 KWELI TUTAFIKA?.
 
yawezekana,lakini kwanini wamtumie yeye nasimtumwingine?basi anamadhaifu ajitahimini. CHADEMA inamhitaji akiwa (sane),akientertain (insanity)anakuwa hana umhimu tena.hasa katika mdahuu ambapo kila sekunde ina umhimu wake towards ujenzi wachama.

FIkiria kwamba adui hufanya utafiti na kupata weak poind ya mtu ndipo wamtumia kujenga hoja zao. Unafikiri CCM inaweza kujenga hoja na mtu kama Mchungaji Msigwa?
 
Mkuu,
Mbona hili liko wazi. Hakuna aliyemsafi katika meza kuu ya CHADEMA. Kumjadili au Kumfukuza Zitto ni sawa na kuacha mlango wa nyumba wazi ili wapita njia waone kwa macho yao kilichoko ndani.

Huna haja ya kuzungusha kichwa kujenga hoja. Mambo yote yako wazi kwa kila mmoja kuona.
Ata kama Zitto kabanishwa kwenye vikao na jasho likamtoka unadhani ataacha kutumia strategy ya kusick sympathy ya wanachadema
magazeti yaliyoaandika habari yake yeye pia huwa anaandikia huko kwa njia moja yanafanya juhudi za kumsafisha baada ya yeye kusoma mood ya wanachadema wenzake moja
Ameiingiza CCM eti inawachonganisha wakati yeye anatumikia CCM kwa namna nyingi tu kwa hiyo anaspin ukweli ili wanachama wenzake wamkubali
Anasema uongo eti alikatazwa kujieleza picha zilizotumwa hapa unamwona kaloa,karefuka kawa kama kalamu inamaana alikuwa anajieleza lakini anatafuta public sympathy anamanupulate ukweli kwa kutangaza kwamba hakusikilizwa kizuri wenzake wamemshit wamemuacha atapetape kama kuku aliyechinjwa na anajulikana kwa strategy zake za ufitini ataandika kama miezi miwili halafu story itakuwa imeisha lakini wanachama wenzake waliokuwa kwenye mkutano watakuwa wananthibitisha yale waliojadili kwenye kikao alichohudhuria
Anasema chadema hakuna haki na kuna upuuzi ndio maana hata vijana wa chadema walihamia NCCR ili kugombea ubunge lakini hasemi yeye alianzisha valangati la kuzoofisha chama Kigoma
Baada ya kikao kakimbilia kwao eti anajenga chama kwa miaka miwili nanusu alikuwa busy anaanzisha chauma chauma imebuma sasa anageuza maboya
Anasema chadema kuna ukanda lakini yeye amesikika mara nyingi akisema Raisi lazima atoke kigoma,anasema wanakigoma tuungane ili tutoe unyonge tuwe kitu kimoja sasa kama sio ukabila wake nini sasa
huyo ni head wa kubadilisha ukweli
 
Kuna kosa kubwa zaidi ya uhaini ambalo ushahidi wake umepatikana pasina shaka (beyond reasonable doubt) hata mpaka video na sauti sikilizi litakalo mfanya kiongozi aendelee na wadhifa wake achilia mbali kufukuzwa uanachama?. Kima hilo siyo kosa, basi tunaongelea sheria na taratibu ambazo haziko ndani ya chama.

You just mention a catalogue of offence the guy has committed and still committing. Hakuna hata karipio linalotoka kwa chama. What this tell us. Jamaa yuko juu ya chama na kelele za watu wala hazimzuii kutenda "maovu" mengine, ukichukulia jana tu kigoma amemwaga mengine.
 
Nadhani bado watu hawaelewi kuwa Mh Zitto anaelewa nini kinaendelea ktk siasa hizi za bongo,mnaweza dhani kuwa Mh Zitto ni mjinga kumbe la hasha,anaelewa na kimsingi ni lazima kila alifanyalo atakuwa analifanya kwa tahadhari sana maana anaelewa wapo watu wenye malengo tofauti.
 
Thank you God!

Chama kimeyashinda Mauti!

In Chadema we trust.
mkuu
nyie ambao ni mashabiki wa chama mnataka kutuambia kuwa kila jambo alifanyalo Mh Zitto halina mashiko? hivi kuna nini kinaendelea ndani ya siasa hizi,nini tatizo haswa na je mmewahi kukaa chini na kumtafuta mchawi wenu? maana haya mambo kesho yatageuka na kuna watu watayatafuna maneno yao na mwisho wa siku watatapika wasichokula.
 
Dah! tumuamini nani? Kila neno analoongea Zitto kama ni kweli vile. Tulioko nje hatujui kwa yakini ukweli ni upi na uongo ni upi. Tutajua tu
... Ndugu yangu.. siasa ni ushindani...ni ushindani wa kupata madaraka....vyama vya siasa vinashindana ili kupata madaraka ya kuongoza dola......wanasiasa ndani ya chama wanashindana ili kuongoza chama.....na siasa ni majungu, fitna na kuchafuana......
 
Back
Top Bottom