Ntaendelea kuamini Zitto na Mbowe ndo msingi wa uimara wa Chadema, nakubaliana na zitto kwamba Chadema ikivunjika leo itachukua miaka 20 mingine mbele kwa watu kukiamini chama cha upinzani kufikia imani hii waliyonayo leo kwa Chadema..
Ni rahisi sana kukipasua Chadema kuliko wengi wanavyodhani, ukitaka kukimaliza hiki chama fukuza kati ya hawa wa3, Zitto, mbowe au dr slaa, basi! Umeshinda.
Mie niko kijijini na pia nazungumza sana na vijana juu ya siasa za Chadema kwahyo nafahamu nguvu ya hawa watu kwenye fikra za vijana wengi wasiotumia mitandao na tv, kwao siasa za upinzani ni Chadema ya Zitto,slaa na mbowe..
Ondoa mmojawapo umeua upinzani kwa nusu ya wapenda mabadiliko nchini..