Zitto: CCM inachonganisha viongozi wa CHADEMA

Zitto: CCM inachonganisha viongozi wa CHADEMA

Karibuni masijala

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Posts
409
Reaction score
135
Wanabodi heshima kwenu,

Mhe. Mbunge na Naibu Katibu Mkuu kwa taarifa zilizonukuliwa na vyombo vya habari na Mitandao ya Kijamii kuhusika kukihujumu chama. Ambazo zilijadiliwa na Mkutano kwa agenda ya Mengine amezijibu kwa kusema ni mbinu ya CCM kuwachonganisha ili Kuivuruga CHADEMA.

Source: Magazeti ya leo
Zitto awasha moto mpya CHADEMA

Imeandikwa na Bakari Kimwanga, Kigoma | Mtanzania | Jan 31, 2013

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), amevunja ukimya kuhusu hatima yake ya kisiasa ndani ya chama hicho. Amesema kwamba, hivi sasa ndani na nje ya Chadema kuna kundi la watu ambalo limekuwa likipika fitna na majungu ya kuwagombanisha viongozi wa chama hicho.

Kwa mujibu wa Zitto, kundi hilo limekuwa likifanya mradi huo kwa lengo la kutaka kutimiza maslahi yao binafsi kuliko kukisaidia chama.

Zitto, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, aliyasema hayo mjini hapa jana, alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Cine Atlas, Ujiji, mkoani Kigoma.

Pamoja na uwepo wa makundi hayo, alisema nia yake ya kugombea urais mwaka 2015 itabaki kuwa ndani ya Chadema na siyo chama kingine kama baadhi ya watu wanavyosema.

"Hakuna ugomvi ndani ya Chadema, bali kuna kupishana mitazamo na hili ni jambo la kawaida katika taasisi yoyote ya kisiasa inayoamini katika misingi ya utawala bora.

"Nataka kuwaambia kwamba hakuna migogoro Chadema, ila kuna watu wachache ambao wamekuwa wakiwagombanisha viongozi wa chama chetu. Binafsi sina ugomvi na mtu yeyote, ila kutokana na ubinafsi wa baadhi ya watu, watu hao wanakiweka chama katika taswira ambayo haijengi.

"Kama ni urais wa Zitto, Mungu akipenda utatokana na Chadema na hautatoka nje ya chama hiki. Kama kuna matatizo ya ndani ya chama, tutayamaliza na kama kuna jambo zito, nitarudi kwenu wananchi wangu ili mniambie ni nini cha kufanya.

"Katiba yetu imeweka misingi mizuri sana, hasa katika kutatua matatizo yetu na hii tutaitumia katika kuyamaliza, ingawa zipo juhudi za watu ambao wamekuwa wakipandikiza chuki.

"Leo Chadema ikipasuka kwa migogoro, nawaambieni wana Kigoma wenzangu, kwamba katu hakitatokea chama kingine cha upinzani chenye nguvu kwa muda wa miaka ishirini ijayo.

"Kama urais upo, basi utatoka ndani ya chama hiki nilichopo na siyo nje, hasa kwa kusukumwa na mipango ya Mungu," alisema Zitto.

Akizungumzia maendeleo ya Mkoa wa Kigoma tangu upinzani ulipoingia, alisema hatua hiyo imekuja kutokana na wananchi wa mkoa huo kuyakubali mageuzi ya dhati.

Alisema kwamba, baada ya wananchi kuyakubali mabadiliko ya kisiasa, Serikali ya CCM ilihakikisha inafanya kila jitihada za kutaka kuwagawa wananchi wa mkoa huo, kwa kuwa iliamini ndiyo njia ya kuwafanya wakipende chama hicho.

"Upinzani ni asili ya Kigoma, ila ninataka kusema hata hawa wabunge wa NCCR-Mageuzi wote walikuwa ni vijana wa chama chetu. Lakini kutokana na ugomvi wetu wa kipuuzi, wakaona ni bora watafute ubunge kwa kukimbilia NCCR-Mageuzi.

"Hata hivyo, pamoja na Serikali kuifungua Kigoma kimaendeleo, hali hii imetokana na uwezo wetu wabunge wa mkoa huu bila kujali itikadi za vyama vyetu, kwani kila mara tumekuwa tukiwabana mawaziri kwa lengo la kuharakisha huduma za maendeleo katika mkoa wetu," alisema.

Katika hatua nyingine, alitangaza mbele ya mkutano huo, kwamba atawalipia ada wanafunzi wote waliofaulu kwenda kidato cha kwanza katika shule za Serikali, hasa wa Kata ya Kagera, ambayo inaongozwa na Chadema.

"Niliahidi kwamba, kama kuna kata itafanya vizuri kwa kuwa na viongozi wote wa Chadema kuanzia mtaa hadi udiwani, nitatoa zawadi na leo hii ninatangaza kulipa ada kwa wanafunzi wote wa kata hii kwa mwaka mzima," alisema Zitto na kushangiliwa.

Wanajamvi kuna Ukweli katika hili? Mhe. Anasingiziwa?
 
yawezekana,lakini kwanini wamtumie yeye nasimtumwingine?basi anamadhaifu ajitahimini. CHADEMA inamhitaji akiwa (sane),akientertain (insanity)anakuwa hana umhimu tena.hasa katika mdahuu ambapo kila sekunde ina umhimu wake towards ujenzi wachama.
 
Ina maana Mr Eight Oclock alikuwa anamsingizia na hata maelezo ya wana P7

Mkuu naona kama alisingiziwa kwa kuwa kama hakusingiziwa na alikuwa kinara wa masalia kwa nini wasimjadili na kumfuta? Iweje wafuasi wafutwe wakati kinara na mfadhili wao bado anaendelea kuwepo chamani? Naona kama Zitto alikuwa anasingiziwa tu na hao akina Mr 8 O'clock kwani waliothibitishwa na Chama kuwa wasaliti wamepata haki yao.
 
Ndugu zangu sasa mtailaumu CCM kwa kila tatizo litakalotokea kwenu? Kama kweli basi mnawambia watu kwamba CHADEMA siyo chama makini kama kinaweza kuingiliwa na kuvurugwa kiasi hiki.
 
inaoneka yoote yanayoletwa hapa kuhusu Zitto ni uongo.
ndio maanaake.kama wana ukweli wowote wa tuhuma zao mbona wameshindwa kuuweka wazi kwenye kikao,badala yake wanakuja JF na ID fake kumchafua Zitto!
Tumesha washtukia na hatutaki ungese wao, Ben Saanane na kundi lake waache kutumiwa kiakili mwisho wake mtatumiwa kimwili na upumbavu wao
 
Last edited by a moderator:
Yeye kila sehemu ana maadui? Ndani ya CHADEMA anasema maadui na nje ana maadui,basi aendeleze CHAUMMA yake
 
whatever,..hata ku-make headlines kila siku ni mbinu za kisiasa kwa huyu kipenzi cha WanaCCM
 
Kijana smart kama Zitto hawezi kujipata katikati ya hekaheka za kutumiwa na CCM ili aiyumbishe CHADEMA bila yeye mwenyewe Zitto kujua. A smart politician, technical strategist Zitto mwenye mbinu za medani zilizopea ili abaki salama kwenye siasa za USHINDANI (achana na siasa za majitaka) inabidi achague upande, ama kujenga chadema akiwa ndani yake ama kutimkia CCM badala ya kutumia uoni wake makini kuibua na kujenga makundi ndani ya chadema ili kukidhoofisha.

Kuyumba kwa msimamo wa Zitto juu ya nini afanye ndani ya Chadema ndiko kunamuweka matatani, kwa kiswahili rahisi tunasema "Zitto anajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe."

Nimtakie Zitto afya njema.
 
Zitto anajaribu kuruka kimanga. Unategemea akubali kuwa anakisaliti chama au lazima atafute wa kumbebesha mzigo. Nadhani angeelezea uhusiano wake na jamaa wa Usalama wa Taifa ingeleta maana.
nyinyi mnao mtuhumu ndio mlitakiwa ndio mlitakiwa hizo tuhuma aka upumavu wenu muuwasilishe kwenye kikao halafu yeye ndio atajibu. Zitto hawezi kujibu majungu ya JF, Zitto ni mtu makini sana,ndio maana majaribio yenu yoote ya kumuangusha yameshindwa.
 
Last edited by a moderator:
Kwa sisi wataalamu wa kugundua tabia za watu wakiongea ukweli, hapa Zitto kasema ukweli...lkn alitakiwa aendlee mbele kidogo tu kusema ni kwanini CCM wamemlenga sana yeye na si mtu mwingine..pia ni wakati sasa aseme wazi uhusiano wake na Jack Zoka ulikuwa katika misingi gani ilhali inaaminika wazi kuwa TISS inatumika kuihujumu CDM ? akisema hilo na tutamuelewa....lkn pia awe mkweli?
 
Hapo kuna ukweli mkubwa kwa kuwa sisiemu siku zote ni kusambaratisha upinzani[rejea NCCR-Mageuzi kati ya Masumbuko na Mrema ambao wote walikuwa masisiemu].

Kwa hivi sasa sisiem inawawia ngumu kuisambaratisha CHADEMA kwa sababu ya viongozi makini akiwemo ZZK mwenyewe kwani anauvumilivu sana kutokana na mbinu chafu anazofanyiwa na sisiem. Kule Tanga kwa mfano kuna tuhuma kwamba ZZK ni swahiba wa January Makamba ndiyo maana akienda ziara za Tanga hapandi Lushoto.

Pia kunatuhuma kwamba sisiem wanamtumia ZZK kueneza sera ya rais ajaye awe kijana ili kuleta sintofahamu na kupoteza malengo ndani ya CHADEMA na mengine mengi ili mradi tu CHADEMA ISAMBARATIKE,KUMBE CHADEMA NI MIXTURE YA KISIKI CHA MPINGO NA MFUPA ULIOMSHINDA FISI.

NINI KIFANYIKE KWA NDUGU ZZK:
Aeleze wazi juu ya tuhuma hizo na nyingine anazozifahamu ili arudishe wafuasi wake wa ndani na nje chama chake waliopotea kutokana na mambo hayo.

NINI KIFANYIKE NA CHADEMA:
Kuendelea kutompa nafasi Shibuda kwani ndiye kirusi kikubwa,Kuendelea kumpa ushauri ZZK ili awe adulty kwa kulitumikia taifa.

Naishia hapa ili na wengine waendelee.
 
Zitto anajaribu kuruka kimanga. Unategemea akubali kuwa anakisaliti chama au lazima atafute wa kumbebesha mzigo. Nadhani angeelezea uhusiano wake na jamaa wa Usalama wa Taifa ingeleta maana.

Mbowe si alimzuia asijielezee? Au ulitaka agombanie Mike kama enzi zile za Mrema na Marando? Hao walokwambia ana uhusiano na watu wa System mbona hawapeleki tuhuma Rasmi kwenye vikao vya chama? Mbona hilo hujiulizi?
 
Dah! tumuamini nani? Kila neno analoongea Zitto kama ni kweli vile. Tulioko nje hatujui kwa yakini ukweli ni upi na uongo ni upi. Tutajua tu
 
TEMILUGODA

hizo ulizojitutumua kusema kishakwambia ni tofauti za kimtazamo na haziepukiki kwa chama chochote cha Kidemkrasia we unataka watu wooote wafanane mawazo?

Hata kwenye kugomea Urais wa JK aliwapinga wenzie akiwaeleza hawawezi kuendesha siasa bila ya kumtambua mimwita anatumiwa lakini mlivyotuliza akili mkajua mmekosea mkaanza kumtambua Jk kimya kimya mpaka Nyumbani kwake mnaenda kumtembelea mpaka usiku. Hata kwenye Ngazi ya familia tofuti za kimtazamo zipo!
 
Last edited by a moderator:
magamba ni noma...remember NCCR mageuzi ya Mrema,hawa wana mbinu chafu kama waganga wa kienyeji.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom