GE2025 Zitto ashikiliwa na Polisi usiku wa manane Lindi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Chama cha ACT Wazalendo kimetoa taarifa kali ya kulaani kile kinachodaiwa kuwa ni uvamizi na kushikiliwa kwa muda kwa Kiongozi wake wa Chama Mstaafu, Zitto Zuberi Kabwe, na maofisa wa Jeshi la Polisi usiku wa tarehe 14 Julai 2025, akiwa katika hoteli mkoani Lindi

1752477584399.png

1752477596305.png
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara, Ester Thomas, tukio hilo lilitokea majira ya saa sita usiku, ambapo polisi kutoka wilaya na mkoa wa Lindi waliwasili katika hoteli aliyofikia Zitto na baadaye kumpeleka katika kituo cha polisi kwa mahojiano ya zaidi ya nusu saa, pasipo kufahamisha mara moja kosa lake

“Hatimaye, baada ya majibizano ya muda mrefu, polisi, majira ya saa saba na dakika nane usiku, walieleza na kubainisha kwamba wanamshikilia Kiongozi wa Chama Mstaafu kwa kosa la kutoa kauli za vitisho, kwa mujibu wa kifungu cha 89(2) cha sheria ya makosa ya jinai. Polisi hao walieleza kwamba kauli hizo za vitisho zilitokana na hotuba ya Ndugu Zitto Kabwe aliyoitoa siku ya tarehe 10/07/2025, akiwa kwenye mkutano wa hadhara Tunduru Kaskazini”, imeeleza taarifa hiyo

Zitto Kabwe ameeleza kuwa atatoa maelezo yote mahakamani na alikataa kueleza zaidi kwa polisi, akisisitiza kuwa hiyo ni haki yake ya kisheria. Aliachwa huru majira ya saa nane usiku bila masharti yoyote

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni, Zitto alitoa onyo kali kwa maafisa wa polisi na watendaji wengine wa serikali wanaoshiriki katika kile alichokiita uingizaji wa kura bandia kwenye uchaguzi, akisema chama hicho hakitasita kuchukua hatua hata kama mhusika ni askari wa vyombo vya ulinzi na usalama, onyo ambalo baadhi ya wachambuzi na wafuatiliaji wa masuala ya siasa wamelieleza kuwa ndiyo huenda imesababisha Zitto kuhojiwa Polisi

Akihutubia siku ya Alhamisi Julai 10, 2025 katika Jimbo la Tunduru Kaskazini, wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Zitto alieleza kuwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, ACT Wazalendo ilimkamata afisa wa polisi akiwa amepakia kura bandia kwa lengo la kuzisambaza kwenye kituo cha kupigia kura, akisisitiza kuwa chama hicho hakitavumilia tena majaribio yoyote ya kuvuruga uchaguzi kwa ‘mbinu chafu’ kama hizo

1752477135211.png

1752477146026.png

Soma pia: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Huyu hakushikiliwa bali alichukuliwa akapewe maagizo mapya. Simba hang'ati mkia wake hata awe mkali namna gani.
 
View attachment 3405408
View attachment 3405409
Soma pia: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Chawa ana kamatwa kama.kuigiza
 
Gvy6jSXWAAAsKxU.jpg
Gvy6jPQWgAARj7W.jpg
Gvy6jFSWsAAZ-SC.jpg

Kiongozi mstaafu wa Chama, ndugu Zitto Zuberi Kabwe, amedaiwa kukamatwa na polisi saa 6 usiku wa kuamkia Julai 14, 2025 na kisha kupelekwa kituo cha polisi Wilaya ya Lindi, lakini baadaye aliachiliwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, John Imori alipotafutwa kwa simu kuzungumzia suala hilo, hakupatikana, lakini taarifa ya ACT Wazalendo imesema Zitto amedaiw akutoa kauli za vitisho katika hotuba yake aliyoitoa Julai 10 akiwa kwenye mkutano wa hadhara Tunduru Kaskazini Mkoa wa Ruvuma.

Taarifa hiyo iliyotolewa”

kupitia mtandao wa X leo Julai 14 imesema askari polisi walivamia hoteli aliyokuwa amefikia Zitto na kujaribu kumkamata.

“Baada ya purukushani katika hoteli hiyo, Ndugu Zitto Kabwe alienda katika kituo cha polisi cha wilaya ya Lindi, huku akiongozana na polisi, wanachama na mwanasheria wa chama. Kwa zaidi ya dakika 30, Kiongozi wa Chama Mstaafu alizongwa na polisi hao pasipo kuelezwa anashikiliwa kwa kosa gani.

“Hatimaye, baada ya majibizano ya muda mrefu, polisi, majira ya saa saba na dakika nane usiku, walieleza na kubainisha kwamba wanamshikilia Kiongozi wa Chama Mstaafu kwa kosa la kutoa kauli za vitisho, kwa mujibu wa kifungu cha 89(2) cha sheria ya makosa ya jinai. Polisi hao walieleza kwamba kauli hizo za vitisho zilitokana na hotuba ya Ndugu Zitto Kabwe aliyoitoa siku ya tarehe 10/07/2025, akiwa kwenye mkutano wa hadhara Tunduru Kaskazini.”

Taarifa hiyo imesema, Zitto alitoa taarifa binafsi na kueleza kuwa maelezo mengine yote atayatoa mahakamani.

“Licha ya kueleza hivyo, polisi waliendelea kumzonga wakimtaka kiongozi afafanue ya kwamba alimaanisha nini katika hotuba yake. Hata hivyo, Ndugu Zitto Kabwe alisisitiza kwamba kama atahitajika kutoa maelezo hayo mahakamani, basi atafanya hivyo, na si vinginevyo. Hatimaye, majira ya saa nane ndugu Zitto aliachiwa kutoka kituoni hapo pasipo masharti yeyote yale.

“Chama cha ACT Wazalendo tunatangaza kwa msisitizo mkubwa, hatuko tayari kuendelea kuona misingi ya haki inakiukwa na kuendelea kushuhudia nchi yetu inaendeshwa kihuni na genge la wahuni wachache. Tunakemea na tutakemea uhuni na ukiukwaji wote wa haki kwa maneno na kwa vitendo.”
 
Chama cha ACT Wazalendo kimetoa taarifa kali ya kulaani kile kinachodaiwa kuwa ni uvamizi na kushikiliwa kwa muda kwa Kiongozi wake wa Chama Mstaafu, Zitto Zuberi Kabwe, na maofisa wa Jeshi la Polisi usiku wa tarehe 14 Julai 2025, akiwa katika hoteli mkoani Lindi

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara, Ester Thomas, tukio hilo lilitokea majira ya saa sita usiku, ambapo polisi kutoka wilaya na mkoa wa Lindi waliwasili katika hoteli aliyofikia Zitto na baadaye kumpeleka katika kituo cha polisi kwa mahojiano ya zaidi ya nusu saa, pasipo kufahamisha mara moja kosa lake

“Hatimaye, baada ya majibizano ya muda mrefu, polisi, majira ya saa saba na dakika nane usiku, walieleza na kubainisha kwamba wanamshikilia Kiongozi wa Chama Mstaafu kwa kosa la kutoa kauli za vitisho, kwa mujibu wa kifungu cha 89(2) cha sheria ya makosa ya jinai. Polisi hao walieleza kwamba kauli hizo za vitisho zilitokana na hotuba ya Ndugu Zitto Kabwe aliyoitoa siku ya tarehe 10/07/2025, akiwa kwenye mkutano wa hadhara Tunduru Kaskazini”, imeeleza taarifa hiyo

Zitto Kabwe ameeleza kuwa atatoa maelezo yote mahakamani na alikataa kueleza zaidi kwa polisi, akisisitiza kuwa hiyo ni haki yake ya kisheria. Aliachwa huru majira ya saa nane usiku bila masharti yoyote

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni, Zitto alitoa onyo kali kwa maafisa wa polisi na watendaji wengine wa serikali wanaoshiriki katika kile alichokiita uingizaji wa kura bandia kwenye uchaguzi, akisema chama hicho hakitasita kuchukua hatua hata kama mhusika ni askari wa vyombo vya ulinzi na usalama, onyo ambalo baadhi ya wachambuzi na wafuatiliaji wa masuala ya siasa wamelieleza kuwa ndiyo huenda imesababisha Zitto kuhojiwa Polisi

Akihutubia siku ya Alhamisi Julai 10, 2025 katika Jimbo la Tunduru Kaskazini, wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Zitto alieleza kuwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, ACT Wazalendo ilimkamata afisa wa polisi akiwa amepakia kura bandia kwa lengo la kuzisambaza kwenye kituo cha kupigia kura, akisisitiza kuwa chama hicho hakitavumilia tena majaribio yoyote ya kuvuruga uchaguzi kwa ‘mbinu chafu’ kama hizo

View attachment 3405408
View attachment 3405409
Soma pia: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Yeye anahojiwa tu na kuachwa...
 
Back
Top Bottom