VoiceOfReason
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,194
- 1,375
Sijawahi kuomba Kikwete aongezewe muda. Tanzania Daima waliandika habari hiyo kwa lengo maalumu na nililalamika rasmi kwa Mhariri mtendaji. Unaona sasa unanihukumu kwa habari iliyotungwa? Ndio maana nimetaja Tanzania Daima na Mhariri wake maana hii ni scheme ya muda mrefu na nimelalamika sana kimya kimya. Hata suala la mimi kutangaza nitagombea 2015 liliandikwa na Tanzania Daima peke yake tena kati kati ya kampeni. Hakuan aliyejiuliza ni kwa nini gazeti linalomilikiwa na Kiongozi wa CHADEMA linaweza kuandika kitu kama kile katikati ya kampeni.
Sijawahi kusema mahala popote kuwa ndani ya CHADEMA kuna udini. Ninaomba clip ya TBC iwekwe hapa jamvini na mtu anionyeshe wapi nimesem kuwa ndai ya CHADEMA kuna udinni. Tafadhali usinywe sumu unazopewa.,Umewaudhi wapenda mageuzi, hata wapigakura wako, kwa tabia yako ya kuonekana kigeugeu, kwa kuwa umejitokeza, tunachokuomba uyafanye mambo kwa vitendo kuturudishia imani. Vile vile kama kuna tofauti kati yako na uongozi, take action to solve, tuendeleze CHADEMA yetu. Ndani ya CHADEMA hakuna udini, kama ulipitiwa siku unahojiwa TBC, ifute ile kauli yako humu. Asante sana kwani kidogo nimeanza kupata imani na wewe.
Brother, hakuna mgogoro CHADEMA!
Huwezi kutegemea ufanye makosa kisha usiandikwe kwa sababu tu gazeti linamilikiwa na mwenyekiti wa chama
Na kama unaona kuna tatizo kwenye hilo ulitakiwa uwasiliane na mwenyekiti wa chama na mjadiliane mpaka mpate suluhu. Kama msimamo wake ni hasi kwako, kwa faida ya chama unatakiwa umezee tu ufe kisabuni.
Hii ya kuja kuweka malalamiko ya kuonyesha kuwa kuna mvurugiko kwenye chama is not a good look kwako wala chama chako.
Si kweli tukio lili ripotiwa na TBC1 ukiongea.Sijawahi kuomba Kikwete aongezewe muda. Tanzania Daima waliandika habari hiyo kwa lengo maalumu na nililalamika rasmi kwa Mhariri mtendaji. Unaona sasa unanihukumu kwa habari iliyotungwa? Ndio maana nimetaja Tanzania Daima na Mhariri wake maana hii ni scheme ya muda mrefu na nimelalamika sana kimya kimya. Hata suala la mimi kutangaza nitagombea 2015 liliandikwa na Tanzania Daima peke yake tena kati kati ya kampeni. Hakuan aliyejiuliza ni kwa nini gazeti linalomilikiwa na Kiongozi wa CHADEMA linaweza kuandika kitu kama kile katikati ya kampeni.
Na wanakuhujumu kwenye magazeti mara kwa mara kwa sababu wanakupenda!
Kaka zitto fanya kazi wananchi walokutuma achana na majungu, na kama hukukubaliana na mgomo wa Wenzako ungekuwa mwenye akili kama ungekaa kimya than kupayuka TBC, ulichemsha kaka hapo, ulionekana Kiherehere mbele ya CCM na Makamba au JK mwenyewe, ulionekana KIKOMEDY fulani kwa wanamageuzi halisia kama wewe, ulionekana nadhamilia kusema CHIZI kwa walio wengi wetu tunaokufahamu ndugu MPIGANIA ZITTO WA KABWE...TUBU MTU WANGU na ukubali ulichemsha otherwise hatutakuelewa hapo
Si kweli tukio lili ripotiwa na TBC1 ukiongea.
sikufanya makosa. Nimesema nimeandikwa ndivyo sivyo. Ningekuwa nimefnya makosa magazeti mengi zaidi yangeandika lakini liliandika moja tu. Sijaja kuweka malalamiko hapa JF. Kufa kisabuni yaweza kuwa ushauri mzuri lakini nimeukataa. Kufa kisabuni ni unafiki uliozidi kipimo. I am sorry for that.
Nashukuru sana kwa ushauri wako. Wakati mwingine ukikaa kimya maadui zako huona kama ndio umekiri. Nimekaa kimya sana sana. Nilisimama kabisa kuja hapa nikadhani itapunguza chuki za watu. Hata hivyo haikukoma. Hata hivyo ushauri wako nimeuchukua kwa mikono miwili. Asante sana sana
Kama bahati tu.
Mh.Zitto huo ushauri huyo bwana kwa kweli ukiusoma unaoneka kutoka moyoni.
Napenda kuongezea kuwa si humu JF tu ambapo unafaa kuchunga na kuwa makini kuongelea mambo ya Chama Chako au ya kwako binafsi hasa pale ambapo unadhani yanaweza husishwa na Chama au status yako ya Kisiasa bila ya kuyapima kwa umakini mkubwa.
Sisi wengine unatuumiza na hasa wanachama wa Chama Chako pale ambapo unakuwa mbele kuliko chama chako katika kutoa habari kwa vyombo vya habari ili hali Chama kama Taasisi bado haijatoa habari husika.
Ni kweli kuwa tunafaa kuwa na Uhuru wa kusema lakini tunafaa kuwa makini kupima tunayosema maadui zetu wanafaidika namna gani au tunaendelea kuwabomoa kiasi gani
Asante na endelea kuwatumikia wana Kigoma na TZ kwa uadilifu mkubwa na Mungu akujaze hekima na busara ili Mafisadi wasikuchote na kukuweka kwenye hima yao.
Basi usilalame tukikunukuu kuwa umesema kuna mvurugiko ndani ya chama kwa sababu ndo ulichokisema leo.
Kuwa huwezi kufa kisabuni kwa hiyo umeamua ufe pamoja na wengine.
Umeamua kusema kuwa kuna watu wanaokuhujumu, tena ni watu wa karibu sana na mwenyekiti wako, ili usitupiwe lawama peke yako, bora 'uoza' wa chama wote uuanike nje.
Hao mentors wako ndo walivyokufundisha hivyo? Kuwa faida na image yako lazima iwe mbele, chama baadae?
Zito
kumbuka upinzani hata wale wa canada, Norway, Australia bado kazi yao ni kukosoa serikali.
Je una mipango gani yenye priority kwako kuhusu mfuko wa jimbo ?
je katika serikali hii utajikita kuban utendaji wa wizara gani hasa? Tunaweza kukusaidia kukupa baadhi ya data za kuhoji
Otherwse nakutakia U MP mwema
Basi usilalame tukikunukuu kuwa umesema kuna mvurugiko ndani ya chama kwa sababu ndo ulichokisema leo.
Kuwa huwezi kufa kisabuni kwa hiyo umeamua ufe pamoja na wengine.
Umeamua kusema kuwa kuna watu wanaokuhujumu, tena ni watu wa karibu sana na mwenyekiti wako, ili usitupiwe lawama peke yako, bora 'uoza' wa chama wote uuanike nje.
Hao mentors wako ndo walivyokufundisha hivyo? Kuwa faida na image yako lazima iwe mbele, chama baadae?
Mwaka 2010 - 2011 nimeamua kujikita kwenye Rural Growth, Gas and Petroleum sub-sectors and Leadership Ethics. Rural growth kwa ajili ya kusukuma nguvu katika cutting poverty levels vijijini. Bado ukuaji wa uchumi wa Taifa letu haufiki chini na hivyo hauendani kabisa na kupungua kwa umasikini. Ajenda hii imesahaulika sana sana. Baada ya kupata sheria mpya ya madini (bado ina mapungufu kidogo), napeleka nguvu kwenye kuhakikisha kuwa Gesi Asilia na Mafuta yanafaidisha nchi yetu. Lengo ni kusukuma kuwe na Sheria mpya ya Gesi na Mafuta ili kuepuka yaliyotukuta kwenye sekta ya Madini. Nina muswada wa sheria nilioandika ili kubadili sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Serikali kukataa kuuchapisha. Ninadhamiria kuhakikisha kuwa muswada ninaurudisha Bungeni. Lengo ni kutenganisha Biashara na siasa kwa kuanzisha blind trusts. Pia lengo ni kufanya sheria ya maadili iwe effective na wananchi wawe na uhuru zaidi wa kukagua mali za viongozi wao.
Mabo mengine ni masuala ya chama mfano suala la Katiba mpya nk.
Gaijin
Zitto akioga wengine wanachafuka na wengine wakioga uchafu unamrukia zito.
Sioni tatizo kwa zitto kujaribu kujisafisha. mradi tu uwe ukweli. Kama akijisfishakwa ukwelihtakama mwenyekiti atachafuka ni haki yake. Ila jambo lililo wazi vyombo vya habri tanzania vinatumika na vinatumiwa vibaya. few days back i saw one faceof zitto 2 day I see anaother face. Huruma inanijia kwa zitto na CHADEMA. ila sijajua ukweli