Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Ndugu wana JF,
Kumekuwa na mada nyingi sna humu ndani ambazo zinajaribu kuonyesha kuwa mimi ni mkosaji na kunipaka matope sana. Nimejdiliwa mno katika jf na hata kuzushiwa mambo mengi sana. Kuna wanaonisema kwa dhati y moyo wao kwamba nimekosea hapa na pale na kuna wanaoona huu ndio wakati wa kumwangusha Zitto na hivyo kuendeleza propaganda za kila namna.

Hii makala imetoka katika gazeti la Mwanahalisi la wiki iliyopita. Imeandikwa na Ansbert Ngurumo, Mhariri wa Tanzania Daima na Press Secretary wa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA. MwanaHalisi linamilikiwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa CHADEMA ndugu Antony Komu. MwanaHalisi limekuwa mstari wa mbele kunipaka matope na kutoa propaganda chafu dhidi yangu na sijui ni kwa faida ya nani.

Nadhani mmenijadili vya kutosha. Itoshe kusema nimesikia. Yale ambayo ni makosa nitajirekebisha maana mimi ni binaadamu. Yale ambayo ni uzushi, uwongo na propaganda nitayadharau.

Jambo moja nilisema na nimeshalisema huko nyuma ni kwamba, nimekuwa mwanachama wa CHADEMA toka nikiwa nina umri wa miaka 16 na sasa nina miaka 35, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote cha siasa. Sitegemei kuwa mwanachama wa chama kingine chochote cha siasa tofauti na CHADEMA. Sijawahi hata siku moja kusaliti chama changu na wala sitajaribu kufanya hivyo. Nina utii kwa Katiba ya chama changu na kwa chama kama Taasisi (Asasi). Pamoja na kutofautiana kimawazo na viongozi wenzangu (wote hatuwezi kufikiri sawasawa) sijawahi kukiuka maamuzi halali ya vikao vya chama kwa mujibu wa Katiba.

CHADEMA ni taasisi inayokua na hivyo changamoto zinaongezeka kila siku. Ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunazikabili changamoto hizi bila kuathiri kazi iliyombele yetu ya kujenga Tanzania yenye demokrasia ya kweli na yenye watu wenye fursa ya kuendeleza maisha yao.

Siasa za kupakana matope. Siasa za kumalizana. Siasa za maji taka, hazitasaidia nchi yetu wala chama chetu. Ifikapo mwaka 2015, wanachama wataamua nani atabeba bendera ya chama kwa njia za kidemokrasia. Hakuna sababu ya kuanza kumalizana sasa. Tukajenge chama wilayani na vijijini ili ifikapo uchaguzi ujao tuwe na mawakala kila kituo, walinde kura zetu na tuweze kushika Dola na kuongoza.

Watanzania mtusaidie katika jukumu hili. Jumamosi njema

Umewaudhi wapenda mageuzi, hata wapigakura wako, kwa tabia yako ya kuonekana kigeugeu, kwa kuwa umejitokeza, tunachokuomba uyafanye mambo kwa vitendo kuturudishia imani. Vile vile kama kuna tofauti kati yako na uongozi, take action to solve, tuendeleze CHADEMA yetu. Ndani ya CHADEMA hakuna udini, kama ulipitiwa siku unahojiwa TBC, ifute ile kauli yako humu. Asante sana kwani kidogo nimeanza kupata imani na wewe.
 
Bw Zitto,
Majibu kuwa mwandishi wa makala ni katibu wa nani na ni mhariri wa gazeti la nani hayakusaidii wewe mwenyewe wala chama chako. Tujuze kama ni kweli umefanya vikao na fisadi Lowasa, na kama ni kweli, vikao hivyo vilikuwa kwa maslahi ya chama chako au kwa maslahi binafsi. Tunajua kuwa pamoja na kuwa kiongozi wa chama, lakini pia unayo maisha yako binafsi na haki ya kukutana na yeyote wakiwemo the so called fisadis.
 
Sijafanya kikao chochote na Lowasa. Kulikuwa na kikao cha Lowasa na Mbowe ambacho mimi nilishiriki kama Naibu wa Mbowe Bungeni. Hata hivyo sijafanya kikao kingine chochote.

Makala hii imeandikwa kwa lengo baya na ndio maana mwandishi kaficha jina lake. Kama ana guts aweke jina lake wazi na aje na ushahidi wa haya aliyoyaandika.
 
Umewaudhi wapenda mageuzi, hata wapigakura wako, kwa tabia yako ya kuonekana kigeugeu, kwa kuwa umejitokeza, tunachokuomba uyafanye mambo kwa vitendo kuturudishia imani. Vile vile kama kuna tofauti kati yako na uongozi, take action to solve, tuendeleze CHADEMA yetu. Ndani ya CHADEMA hakuna udini, kama ulipitiwa siku unahojiwa TBC, ifute ile kauli yako humu. Asante sana kwani kidogo nimeanza kupata imani na wewe.

Sijawahi kusema mahala popote kuwa ndani ya CHADEMA kuna udini. Ninaomba clip ya TBC iwekwe hapa jamvini na mtu anionyeshe wapi nimesem kuwa ndai ya CHADEMA kuna udinni. Tafadhali usinywe sumu unazopewa.
 
Sijafanya kikao chochote na Lowasa. Kulikuwa na kikao cha Lowasa na Mbowe ambacho mimi nilishiriki kama Naibu wa Mbowe Bungeni. Hata hivyo sijafanya kikao kingine chochote.

Makala hii imeandikwa kwa lengo baya na ndio maana mwandishi kaficha jina lake. Kama ana guts aweke jina lake wazi na aje na ushahidi wa haya aliyoyaandika.

Mmetangaza mlichozungumza?

Maana msipotangaza mnaacha mwanya kwa speculations zote pamoja na kuwanyima wanachama wenu kujua uongozi unafanya nini.

Mmejadiliana nini na Lowassa ?
 
Sijafanya kikao chochote na Lowasa. Kulikuwa na kikao cha Lowasa na Mbowe ambacho mimi nilishiriki kama Naibu wa Mbowe Bungeni. Hata hivyo sijafanya kikao kingine chochote.

Makala hii imeandikwa kwa lengo baya na ndio maana mwandishi kaficha jina lake. Kama ana guts aweke jina lake wazi na aje na ushahidi wa haya aliyoyaandika.

Tumekusikia mkuu
Kitu kinacho wauma watu ni yale mahojiano na TBC1 ungenyamaza aaah roho kwatu
 
ila kunamengine Zitto ukubali kuwa unakosea kwanini watu wamakujadili wewe sana ndani ya CHADEMA wakati wapo wengi pale? kwanini hasiwe Mdee?
 
Hii makala imetoka katika gazeti la Mwanahalisi la wiki iliyopita. Imeandikwa na Ansbert Ngurumo, Mhariri wa Tanzania Daima na Press Secretary wa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA. MwanaHalisi linamilikiwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa CHADEMA ndugu Antony Komu. MwanaHalisi limekuwa mstari wa mbele kunipaka matope na kutoa propaganda chafu dhidi yangu na sijui ni kwa faida ya nani.

Kweli Chadema kumekucha.

Waswahili wanasema Nyani akimaliza miti huingia mwilini. Chadema imeamua kuvaana wenyewe kwa wenyewe?

Mara Regia Mtema na Kitila (I swear I am not picking on her, mwenyewe kaja kutoa dukuduku hapa) mara Zitto na Komu, hayo ni ma beef yanayo leak hapa tu, huko ndani wenyewe wanaokujua sijui kukoje.
 
Ile ilikuwa mbaya. Bora hata hii, mwandishi kaficha jina.

Wanaaibisha jina la chama tu.

Hivi mpaka Zitto aje ajitetee na kujaza information zote hizo kuwa linamilikiwa na nani na kuonyesha ugomvi ndani ya chama?

Angejitetea bila ya kutaja majina ya watu wa ndani ya chama angepungua wapi?
 
Sijafanya kikao chochote na Lowasa. Kulikuwa na kikao cha Lowasa na Mbowe ambacho mimi nilishiriki kama Naibu wa Mbowe Bungeni. Hata hivyo sijafanya kikao kingine chochote.

Makala hii imeandikwa kwa lengo baya na ndio maana mwandishi kaficha jina lake. Kama ana guts aweke jina lake wazi na aje na ushahidi wa haya aliyoyaandika.

Kama hayo unayoyasema ndivyo, endelea kupiga mzigo. You have my support na usichelewe sana kuyatolea ufafanuzi
 
Ile ilikuwa mbaya. Bora hata hii, mwandishi kaficha jina.

Wanaaibisha jina la chama tu.

Hivi mpaka Zitto aje ajitetee na kujaza information zote hizo kuwa linamilikiwa na nani na kuonyesha ugomvi ndani ya chama?

Angejitetea bila ya kutaja majina ya watu wa ndani ya chama angepungua wapi?

Yaani jamaa wanaendesha chama cha kitaifa kama watoto wa shule fulani hivi.

Hiki ndicho chama mbadala kweli ? Prima donnas kibao.
 
Sijawahi kusema mahala popote kuwa ndani ya CHADEMA kuna udini. Ninaomba clip ya TBC iwekwe hapa jamvini na mtu anionyeshe wapi nimesem kuwa ndai ya CHADEMA kuna udinni. Tafadhali usinywe sumu unazopewa.

Pole sana Zitto kwa madongo unayotupiwa, tambua tu umekuwa ni mwanga na tumaini kwa vijana wengi (mimi mmoja wapo) lakini kwa siku za hivi karibuni tumaini la vijana hawa limeanza kufifia hata kufikia kusema kwamba Tanzania mabadiliko hayawezekani iwapo hata Zitto "kanunuliwa". Mie sina ushahidi wa hayo unayotuhumiwa na sidhani kama kuna mtu yeyote mwenye ushahidi 100% isipokuwa dhamira yako wewe mwenyewe ndio inayojua ukweli ni upi, brother, you are one of the icons of the Tanzanian youths, a hope to the young ones, hakuna pesa utakayopokea kutoka kwa mafisadi itakuwa na thamani kubwa kuliko imani yetu sisi kwako. Lisemwalo lipo, kama halipo linakuja, tafakari na uchukue hatua, kama ulipotoka, huo ni ubinadamu, rudi kwenye mstari tuendeleze mapambano.

Take all these allegations thrown against you as an incentive to work hard and get rid of your controversial moves which of recent have made most of us suspicious about your trustworthness and intergrity!
 
Mwandishi wa makala ni press secretary wa mwenyekiti Mbowe, mmiliki wa gazeti lililochapa makala ni mhazini wa CHADEMA taifa Anton Komu, Zitto anasema ifikapo 2015 wanachama wenyewe wataamua nani apeperushe bendera ya chama kuelekea kwenye mafanikio.

Picha ninayopata ni kuwa tofauti zilizopo kati ya Zitto na mwenyekiti wake ni kubwa sana kwamba hata kuzielezea inakuwa ngumu. Hali hii isiporekebishwa mapema, chama kitakuwa na hali mbaya sana kiasi kwamba hata kumpata huyo mpeperusha bendera 2015 itakuwa ndoto.
 
Yaani jamaa wanaendesha chama cha kitaifa kama watoto wa shule fulani hivi.

Hiki ndicho chama mbadala kweli ? Prima donnas kibao.

Watanzania imekula kwetu, viongozi tunaowategemea hawaoni hata maneno yao yatachukuliwaje na jamii.

Hapa tukifungua thread tukamnukuu, tukaanza kujadili kwa nini Zitto anahujumiwa ndani ya Chadema atakuja kusema "thread sikuanzisha mie na maneno hayo nilikuwa najibu thread nyengine kwa hiyo yasitumiwe" au?

Hebu fikirini kidogo kabla ya kuja kupayukwa ya ndani ya chama huko.
 
Mara Regia Mtema na Kitila (I swear I am not picking on her, mwenyewe kaja kutoa dukuduku hapa) mara Zitto na Komu, hayo ni ma beef yanayo leak hapa tu, huko ndani wenyewe wanaokujua sijui kukoje.

Why are you so obsessed with Ms. Mtema? Regina hajawahi kulalamika juu ya Kitila.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom