huyo kijana hafai kuwa kiongozi kama maamuzi ya chama yaliyopigiwa kura na wanachama wengi wakakubali alafu m2 anakwenda media kuongea pumba hawezi kuwa ni kiongozi bali ni mnafiki nadhani anataka ki2 kutoka ccm tayariameshahongwa na mafisadi bora achape mwendo.na ni kweli cku zake zinahesabika hana tofauti na mremakafara
Wengi tunataka katiba mpya ingawa wengi hatuijui hata hii iliyopo wakiwemo zaidi ya asilimia hamsini ya wabunge wetu...
Lakini je, hatua ya wabunge wa chama chenye wabunge 47 kutomtambua RAIS aliyepata kura zaidi ya asilimia sitini ama tuseme hata hamsini tu na kiongozi wa chama chenye wabunge zaidi 260, ni hatua itakayoweza kutupatia hiyo katiba mpya??? Hivi kutoa ishara za kutothamini ama kuheshimu UTAWALA mbele ya jamii ambayo asilimia 45 ya waliopiga kura wanasema wameshawishiwa na kuthamini AMANI na haswa katika taifa lenye kutishiwa na mgawanyiko wa kijamii huku tukijua wazi matokeo ya migawanyiko ya aina hiyo, ndio njia muafaka wa kufanikisha kupatikana kwa katiba mpya?
Zitto unasema wewe ni democrat na unapenda kuongea unaloliamini na unapenda uwazi na ukweli. Lakini yanayojiri kwenye vikao vya chama ni siri ila matokeo ya hivyo vikao sio siri. Hivi ulivyokwenda TBC 1 na kubwabwaja yaliyojiri ndani ya vikao vya chama ulikua unataka wananchi wakueleweje? Kuwa utoto unakusumbua mpaka uropoke kila unachokijua bila ya kupima unaongee na nani na nini unakiongelea? Kuwa wewe umekua kimwili tu na sio kimawazo? Naomba nikupe mfano. Hivi wewe Zitto ukiingia chumbani kwa mama yako na bahati mbaya ukamkuta anavaa nguo, utatoka na kuwaambia watu kuwa umemwona mama yako akiwa mtupu?
katika kuonesha hali ya masikitiko mh zitto zuberi kabwe amepingana na kitendo cha chadema kutoka nje ya bunge, akiongea na tbc leo zitto amesema yeye kama yeye hakubali kitendo cha chadema kuwalk out
big up zitto :lock1::lock1:hapo umeonesha ukomavu wa siasa
karibu chamani:clap2:
<br />
<br />
hatukatai yeye kuwa na mawazo tofauti, tunachopinga ni kwamba kulikuwa na ulazima gani kwa yeye kwenda kwenye media kusema alikuwa hakubaliani na uamuzi wa wengi? Binafsi naona ni kujipendekeza kwa jk na ccm. Niliwahi kusema hapa kwamba binafsi namuona zitto kama mtu mwenye tamaa sana na madaraka. Si mtu unayeweza kumuamini kujenga na kuimarisha chama. Hata mchango wake kwenye kampeni ya dr. Slaa ulikuwa kama hakuna kabisa na alionekana akimtetea sana jk kama kafanya kazi nzuri sana!
Kumfukuza Zitto itakuwa ni kukubali kwamba CHADEMA haina utamaduni wa kukubali tofauti ya mawazo chamani.
Kwa chama kinachotaka kuleta demokrasia zaidi Tanzania, ambacho jina lake linabeba neno demokrasia, jambo hili litakuwa baya sana.