acha kufananisha mawili; kuhusu kuuza nyumba ni wizi, na sihafiki ukimya, naweza kumuunga mkono Waziri anayetoka nje ya kikao cha cabinet na kupinga hata kama amezidiwa kura na msimamo wa serikali maana that's is good citizenry cum patriotism! ila suala la Zitto+wenzie siliafiki maana sidhani kama amefurahishwa na matokeo na sidhani kama hatua iliyochukuliwa na chama chake ilikuwa mbaya kwa maana ya kuvunja sheria kiasi cha kuwa na utovu wa nidhamu na kuamua kutohudhuria akiwa na wakina Ndesamburo na mwanae Owenya na wakina Prof. Kahigi (niko disappointed kwakweli)! huo ndo tunaouita ukosefu wa togetherness na nina uhakika CHADEMA had a strong cause to present by what they did! Zitto ni wazi anakuwa in dilema situation maana kwa hali inavyoendelea ni wazi urafiki wake na wabunge wa NCCR-Mageuzi unamweka katika a compromise situation akidhani anaweza kuwaunganisha na CHADEMA for his own gain na hapo ndo atakapojimaliza maana hiyo heroism he wants to show itawapa chance CCM kumvuruga na CHADEMA na natabiri ataingia NCCR-Mageuzi na huo ndo utakuwa mwisho wake! Mwana siasa makini ajaribu kuangalia what happened to the likes of Dr Kabour! na ajifananishe na anachotaka kufanya! nathani atakuwa smart politician kama ataona nguvu ya CCM behind the scene katika kubomoa Upinzani na kuacha chokochoko zisizo na mpango na nathani CHADEMA wanapaswa wawe waangalifu saana na hawa watu wasio na nidhamu na kuleta chochoko kila siku! sasa si muda wa mavurugu ila kujipanga na ku-set goals of what they wanna achieve before the next election!HATARI: Nyoka kaingia ndani ya CHADEMA
Tumepata taarifa kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia CHADEMA, Zitto Kabwe, akiongea na TBC1 amesema kuwa yeye ni miongoni mwa Wabunge wa CHADEMA waliokuwa wanapinga ile walkout isifanyike Bungeni Alhamisi iliyopita wakati Kikwete anahutubia.
Watu wametoa mawazo mbalimbali kuhusu suala hili. Kuna waliosema ameonesha ukomavu wa kisiasa na demokrasia ndani ya CHADEMA.
Mimi nina mawazo tofauti sana. Kitendo alichofanya Zitto Kabwe ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu kwa uongozi wa CHADEMA.
Yeye kama mwanachama wa CHADEMA, Mbunge, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni anapaswa kuelewa kuwa maamuzi yote yanayofanywa na chama yanakuwa ndiyo msimamo wa mwisho wa chama. Hapa kuna suala la collective responsibility.
Alichokifanya Zitto kwa kuongea na TBC1 ni sawa na waziri ambaye anatoa siri ya vikao vya Cabinet kwa vyombo vya habari.
Mfano, kwenye cabinet kunatokea mvutano kuhusu suala fulani, let's say uuzwaji wa nyumba za serikali. Mawaziri wanajenga hoja zao halafu serikali inafikia uamuzi wa mwisho kuwa itauza nyumba za serikali kwa vigogo wa serikali.
Then atokee waziri mmoja aseme hadharani kwenye media kuwa yeye alipinga mpango wa kuuza nyumba za serikali kwenye Cabinet lakini akazidiwa kura na mawaziri wengine. Huyo mtu angefukuzwa kazi mara moja.
Ni jambo la kustusha sana kuona kuwa Zitto amekiri hadharani kuwa yeye alipinga jambo hili na kulikuwa na mvutano ndani ya CHADEMA. Kwa matamshi haya, ametoa siri za vikao vya ndani vya chama.
Uamuzi unapofikiwa na chama hata kama wewe binafsi haupendi unakuwa ni wa mwisho na lazima wewe uukubali, uunge mkono na uutekeleze.
Nadhani kama kiongozi wa CHADEMA, Zitto ameonesha utovu wa nidhamu kwa chama, amevunja kiapo cha kutunza siri za chama na ameonesha kukosa maadili.
Tena Zitto alienda mbali zaidi na kusema kuwa yeye aliamua kutokwenda kabisa Bungeni kwa kuwa hajakubaliana na walkout. Hili ni kosa kubwa sana la kupingana na maamuzi halali ya chama.
MASWALI YA KUJIULIZA:
1. What is Zitto Kabwe trying to achieve?
Je, anataka kuonesha umma wa Watanzania kuwa kulikuwa na mgawanyiko kwenye CHADEMA juu ya hili jambo na yeye hakuunga mkono uamuzi huu? Au pengine huenda anataka kuwaonesha vigogo wa CCM kuwa kazi waliyomtuma kuzuia walkout aliifanya kwa bidii na jitihada zote lakini akashindwa.
Kwa ufupi, kitendo cha Zitto si jambo childish tu, bali kinazidi kujenga zile hisia zilizopo mura mrefu kuwa yuko karibu mno na vigogo wa CCM na ni mtu ambaye huwa anatumiwa tumiwa hovyo kulinda maslahi fulani ya watu wachache.
CHADEMA ijihadhari na nyoka huyu hatari.
Mheshimiwa ZITTO unajua kuwa Rasilimali za nchi zinaporwa na wageni kwa msaada wa Mafisadi.
Kura za uraisi zimeibwa na wewe unajua, wewe ZITTO unategemea tutapataje Tume Huru na Katiba Mpya bila kuchukua maamuzi magumu??
Mikataba feki ya madini na vitalu vya uwindani Tanzania -Viongozi wa Si CM wanajineemesha na familia zao. Inakuaje kwenye madini tupate 3% na wageni wachukue 97%???? Je sisi watanzania ni vipofuuu??
Kura zimeibwa mchana kweupe, ushahidi wa kutosha upo. Tume ya uchaguzi imechakachua kura kwa maelekezo ya UDikteta wa CCm. Mh ZITTO yote haya huyajui? Kura za wananchi umezipata kwa sababu wananchi wanataka ukombozi, uhuru wa kiuchumi.
Zitto tunakuheshimu sana usiwe mnafiki, usitafute umaarufu wa Si CM.
It is soo sad kwa kaka yangu mpenzi Zitto. Anapaswa kukaa kimya... Yuko juu ktk media, alikua juu kwa mema na sasa anakoelekea atakua juu kwa mabaya. Asidhani hii hali ni nzuri kwake hata kidogo maana anakua kamna amerogwa, atakwisha kabisa kisiasa na hatakuwa tena Zitto anayekubalika na jamii. Nadhani Zitto the only way ya kutoka tena ni kutafuta BUZWAGI nyengine bungeni Anne Makinda amfukuze apate ujiko na iwe issue atakayowalipua mafisadi akiwamo RA, Lowassa na Chenge, na hata JK ili kurudisha imani ya wananchi kwake, vinginevyo anakoelekea wananchi wataendelea kuaminishwa na kuamini kwamba amenunuliwa na akienda CCM ama NCCR atakua kama Mbatia, Tambwe Hiza ama Salum Msabaha.

Nyinyi munapenda Zitto aseme yes sir! kila wakati? Anayo haki ya kukataa kuunga mkono kitu kama hawafikiani nacho na huo sio usaliti.

Usaliti ni ile kujidai umekubali kumbe rohoni mwako hupendi kile kinachofanyika.

Jaribuni kufikiri nje ya boksi jamani!
Bintimkongwe, unaweza kuwa ni shabiki wa Zitto na tunaelewa ana mashabiki wengi. Lakini usiwe shabiki kipofu. Kwa vyovyote vile, lazima ukiri kuwa Zitto amekosa maadili kwa kutoa siri za chama hadharani. Alikuwa na kila haki ya kupinga uamuzi huu akiwa ndani ya vikao vya chama. Lakini uamuzi wa mwisho ulipochukuliwa, alitakiwa kukaa kimya. Hata kamati kuu ya CCM wenyewe ilipoamua kumfukuza Spika Samuel Sitta kulikuwa na mvutano mkubwa. Je, umemsikia Bernard Membe kwa mfano kujitokeza hadharani na kusema yeye alipinga uamuzi wa kumfukuza Sitta?
Kwa kweli Zitto lazima alaaniwe kwa kujaribu kuleta mtafaruku ndani ya CHADEMA, ambacho ndiyo chama sisi Watanzania tunakitegemea kituokoe kwenye janga la utawala wa CCM.
Kwa maslahi ya taifa, tuweke ushabiki wa majina ya wanasiasa fulani pembeni na tuangalie masuala kwa upana wake.
Zitto anasema wabunge walipiga kura. The majority won. Huo ndio ukweli. Usijaribu kupindisha eti yalikuwa maamuzi ya Mbowe.Yalikuwa si maamuzi ya chama, alipinga maamuzi ya Mbowe, kuwa mkweli.
Tina,It is soo sad kwa kaka yangu mpenzi Zitto. Anapaswa kukaa kimya... Yuko juu ktk media, alikua juu kwa mema na sasa anakoelekea atakua juu kwa mabaya. Asidhani hii hali ni nzuri kwake hata kidogo maana anakua kamna amerogwa, atakwisha kabisa kisiasa na hatakuwa tena Zitto anayekubalika na jamii. Nadhani Zitto the only way ya kutoka tena ni kutafuta BUZWAGI nyengine bungeni Anne Makinda amfukuze apate ujiko na iwe issue atakayowalipua mafisadi akiwamo RA, Lowassa na Chenge, na hata JK ili kurudisha imani ya wananchi kwake, vinginevyo anakoelekea wananchi wataendelea kuaminishwa na kuamini kwamba amenunuliwa na akienda CCM ama NCCR atakua kama Mbatia, Tambwe Hiza ama Salum Msabaha.