Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Tulishawambia kuwa hafai hata kuongoza kambi ya upinzani bungeni lkn mkasema kuwa chadema wana ukabila leo mmepata majibu kuwa waliona mbali.

Asante kwa kukubali.
 

Heshima mbele Mkuu.....ujumbe murua kabisa huo
 
I have said it many times that Zitto is a loose cannon....now you all are starting to see it.
 
Zitto alianza kuonyesha tofauti kubwa baada ya Kuchaguliwa katika ile kamati ya Bomani ya madini sijuhi ni nini kilitokea huko lakini hakuwa tena yule Zitto aliyekuwa anaweka mijadala mizito kama ule wa Buzwagi uliomfanya awekwe bench Bungeni,

Wapo Wanaosema Zitto ni Mwanasiasa makini na sio mkurupukaji, lakini ukiangalia issue ya Dowans na ile mitambo yao, Zitto na I Rashid walwatisha Watanzania kuwa lazima tutaingia Gizani, Zitto alidiriki hata kutaka kuipita Sheria ya manunuzi ya serikali, watu walipiga kelele na kutaka kujua credibility ya Zitto,

Hili la sasa kwa kweli sijuhi tumweke wapi Mh Zitto
ukitaka kuchunguza makini katika hili Zitto alikuwa anataka kuwaonyesha (?) kuwa yeye japo yupo Chadema, lakini ana misimamo yake na hayuko kinyume na wao (?)

Kuna kitu inabidi Zitto awe makini, kama ana lengo la kuitingisha Chadema basi inambidi afanye haraka, kwa maana Tangu ile issue ya Dowans umaarufu wake umeshuka kwa baadhi ya wanachama na wapenzi wa Chadema, sasa hii issue itazidi kumshusha na mwisho wa siku hata akitoka watu hawatashituka kwa sababu watakuwa wamesha mjua kuwa si mwenzao na wala Chadema Haitayumba
 
OOOOH my..kijana kaanza kuzeeka, anadhani yeye ndo kila kitu, anafanya mabo ya ovyo ovyo... ananifanya nianze kuamini kale kacheo ka kamati ya madini bungeni kali mcorrupt... tunafauatilia yendo zake..... ni mapema sana kumpa hukumu.. tutajua ukweli tu..
huyu jamaa ( zittokabwe ) na SHIBUDA ... jamani tuwaangalie kila move wanayofanya , maana roho yangu hanipi imani kwao kabisaa
 
halo wana jf,
sijaandika muda mrefu ila kwa hili sitaweza kunyamaza! Hivi huyu bwana mdogo ana nini hasa?! katumwa au? yawezekana ana pepo limemwingia anahitaji kuombewa! najua yawezekana yeye anasoma humu au rafiki yake wa karibu, mwambieni tafadhali sana asituvuruge, watu bado tuna machungu, kama amechoka siasa aache aende kwenye field yake ya kufundisha kama alivyowahi kutamka. Na pia ajue yuko pale kwasababu ya chadema na si vinginevyo! Zitto, 'usichukue chakula cha watoto na kuwarushia mbwa'
 

Mbona unachanganya mambo na kukariri sana bila ya kutumia commonsense. Ina maana watu wakipiga kura ya kwenda kuchoma moto nyumba ya mpinzani wewe ukatoa sababu zako zikiwa kwamba it is not moraly right tusifanye hicho kitendo ni kosa. Na nyie ambao mna oppose mkija shindwa lazima mkachome hata kama hamkuona ni sawa in the first place eti kwa sababu wengi wape hii sijui itakua akili gani.

Were then is the self autonomy, its not like expressing hatred is part of chadema main manifesto au labda mtufahamishe na wengine. Kutoa adhabu hapo ni demonstration of an authoritatian leadership, si kama mtu kapigia kura kitu au policy ambayo wao hawaikubali au la hata huko kwenye liberal democracies now and then politicians do not agree with all their parties ideas.

Sasa kama wao wameona hii si sawa (kwa sababu zao wao wenyewe) si ndio namna yao walioichagua kuto participate in the walk out kwa kutokwenda bungeni in the first place (by the way its their right as they never voted for it in the first place) . Je wangeingia na wasitoke si ndio mge pata aibu zaidi. Hebu tuongeze mawazo na kutokuwa one dimensional thinkers.
 
Mheshimiwa ZITTO unajua kuwa Rasilimali za nchi zinaporwa na wageni kwa msaada wa Mafisadi.

Kura za uraisi zimeibwa na wewe unajua, wewe ZITTO unategemea tutapataje Tume Huru na Katiba Mpya bila kuchukua maamuzi magumu??

Mikataba feki ya madini na vitalu vya uwindani Tanzania -Viongozi wa Si CM wanajineemesha na familia zao. Inakuaje kwenye madini tupate 3% na wageni wachukue 97%???? Je sisi watanzania ni vipofuuu??

Kura zimeibwa mchana kweupe, ushahidi wa kutosha upo. Tume ya uchaguzi imechakachua kura kwa maelekezo ya UDikteta wa CCm. Mh ZITTO yote haya huyajui? Kura za wananchi umezipata kwa sababu wananchi wanataka ukombozi, uhuru wa kiuchumi.

Zitto tunakuheshimu sana usiwe mnafiki, usitafute umaarufu wa Si CM.
 
Hata mtoto mdogo kabisa angekuwa na busara zaidi ya zitto kwa hili asingeweza ku-act namna hii.
Hii ilikuwa ni Ishu sensitive sana ilikuwa inahitaji umakini wa hali ya juu ku-andle na kuangalia wananchi wanavyolipokea.
Sasa hata pale ambapo bado tunajaribu kua-absorb ishu nzima ya hawa makamanda kufikisha ujumbe kwa kikwete kwa njia
ya kishujaa,njia ya kihistoria katika siasa za nchi yetu,anatokea huyu Zitto na ushenz wake.
Am really disappointed with this dude.Zitto kitu kimoja anatakiwa ajue ni kuwa there is only two ways here kama ana lengo la
kuwa kiongozi mwenye wafuasi wengi katika nchi,labda kama ana ndoto za kugombea urais wa nchi hii baadae.
Either awe kushoto au kulia(CCM/CHADEMA).
Lakini akitaka kotekote,ajue kuwa haendi popote,huwazi kuwaridhisha mabwana wawili,kwa maana hiyo huwezi ku-act kama CUF na
ukategema kuongoza nchi hii,never forget about.

I am more than convinced that this dude can't be trusted.
He has let us down.
 

Sawa jamaa hajapinga yeye kukataa..hiyo ni demokrasia pia... Hapa kiapo cha kutoa siri za chama amekiuka... Sijui sisi tukijua hilo tunafaidika vip??? au hapendi maamuzi ya wengi waliomua kutoka bungeni?? Tukishajua inamsaidia nini au alitumwa sasa anakiri hadharani akapate 10 pasee yake??
 
kwa mimi huyu ZITTO NILISHAMFUTA ZAMANI TANGU ALIPOANZA KUTOA TAMKO LA DOWANZ

HILI NDO TATIZO LA KUWA NA WASIASA VIJANA WENYE NJAA

DOGO KAINGIA KWENYE SIASA AKIWA NA NJAA SASA MAFISADI WA3NA#MG4EU5ZA NYUMA NA MBELE
 

ZITTO anahitaji uenyekiti wa kamati hasa ile ya hesabu za mashirika ya uma. Sasa atafanyaje ili asipewe mtu wa NCCR au CUF ni kujifanya kuwa yeye haungi mkono mamabo yanafanywa na CHADEMA. Anapenda vyeo sana huyu jamaa kwa hiyo huwa anafanya lolote kwa maslahi yake binafsi ya kupata vyeo. Ni bora angenyamaza kimya ingawaje kutokwenda pia ni credits kwa CHADEMA kuliko angeenda halafu angebaki bungeni wakati wenzake wameendoka ingekua more worse.
 
ZITTO ni kijana asiye na maadili na ni mjinga anashindwa kujua chama ndo kimemfanya ajulikane...Huyu ni wa kufukuza tu aende huko CCM

Nimefuatilia THREAD zote hizi na kugundua kuwa TANZANIA si ile niliyoijua hapo kabla. Watu hawaangalii nani kasema nini, alimradi ALUTA CONTINUE. Nionavyo mimi hata Slaa akitokea akasema kinyume na matakwa ya WaTanzania, THEY WILL WALK OUT! Hii inatufundisha kuwa muda wa KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI UMEFIKA.

Sikudhani kama Zitto anaweza kushambuliwa hivi naye.....COME DEMOCRACY COME, COME TRUE PEACE COME, COME TANZANIANS TOGETHER COME, ......
 

Yalikuwa si maamuzi ya chama, alipinga maamuzi ya Mbowe, kuwa mkweli.
 
nahisi ufahamu wake umeshachakachuliwa na mafisadi/ na ameshakuwa mbinafsi sasa
 

Yalikuwa si maamuzi ya chama, alipinga maamuzi ya Mbowe, kuwa mkweli. Kama ni chama hata Zitto ni mwana chama tena safu ya uongozi, nae alikuwa na maamuzi yake.
 
HIZI SIASA ZA BWANA MDOGO HAZINA MSHIKO

ANGEKUWA NCHI ZA WENZETU WATU WANGEMIMINIKA MADUKANI KUNUNUA GUN:laser: ILI WAANZE NAYE

CDM SIO CHAMA CHA ZITTO NI CHAMA CHA WANANCHI HUWEZI KUKURUPUKA TOKA SHIMONI UKATOA TAMKO

HUYU DOGO ATAKUFA KIFO KIBAYA
 
Ushauri kwa viongozi wa CHADEMA,mpuuzeni Zito. Wala msicomment chochote ambacho amekisema katika vyombo vya habari. Mwacheni alopoke but at the end of the day ataona kila mtu anamuignore na hapo ndio utakuwa mwanzo wake wa kufa kisiasa. Hata maandiko matakatifu yanasema usijibishane na mtu mpumbavu. Zito ni mpumbavu.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…