Nadhani wewe una matatizo makubwa. Hii sio habari ya kuandika, usidhani ni Kigoma tu wanachagua watu na sio Chama, kama unadhani ndivyo basi umekosea sana. Zito kama angekuwa na akili kama unavyosema angeliingia bungeni na kukaa kumsikiliza mshikaji wake JK. Kitendo cha yeye kutokufika bungeni ni unafiki wa hali ya juu na kiuongozi ni usaliti. Ingekuwa Chadema ni chama cha kijeshi, angeshapigwa risasi siku nyingi
Zito in all aspects ni mvurugaji wa chama, kuna mambo anafanya ambayo sidhani kama yanamsaidia. Lakini kiongozi makini ni yule mwenye msimamo na asiyekubali kuyumbishwa, sioni kama hilo analo Zito. Kuna kipindi alisema hatogombea tena ubunge, mara atachangua jimbo la kugombea, mara akagombea, mara niko shule. He can not be trusted. Wakati kampeni za uchaguzi zinaendelea, alitangaza kugombea uraisi 2015 very strange, bila kujua outcome ya uchaguzi huu. Zito alishaweka kichwani kuwa Dr Slaa hatoshinda, na ndio maana haoni kama kilio cha Chadema kina maana.
Hili na kupiga kura ndani ya chama sidhani kama alipashwa kulileta mitaani, anajikosha kwa watu, na anataka kugombea uraisi 2015, kweli, kwa mazingira haya haya, au anadhani bila pressure mambo yatakuwa tofauti, loh, amekosa weledi wa kutambua hii hali yote
Kwa wanaokumbuka kilichoivuruga NCCR ni kila mmoja kati ya Mbatia, Marando na Mrema, Selasini kuwa wasemaji wa Chama. Zito hakupaswa kukimbilia kwenye vyombo ya habari na kuteta kilichofanyika katika vikao vyao vya ndani. Huko ni kukosa kuheshimu mamlaka husika ndani ya chama na nadhani Chadema wanapaswa kumchukulia hatua kali. Hujamsikia mjumbe wa kamati kuu ya ccm akienda kwenye mtanzania daima na kueleza kilichotokea ndani ya kamati kuu kumuengua Sitta.
Nakubaliana na wanaosema kuwa Zito ni wa kumuangalia sana, he is cheap and he can easily be seduced. He has tried several times kupingana na mwenyekiti wake, na nadhani ana bifu na Mbowe. I think the best way watanzania watamheshimu ni kwa yeye kuondoka Chadema kwa amani kama hakubaliana na mwenyekiti wake na viongozi wenzake, kuliko kukivuruga chama. Asingojee kupewa adhabu, kwa kuwa ndicho anasubiri kifanyike, Chadema, dont waste time na huyu mtoto, wala hakuna haja ya kumchukulia hatua, kwani mtakuwa mmefanya kile anachokitaka, cha msingi ni kumsideline, kwa kuwa hawezi kutunza siri za chama, basi awekwe pembeni tu, this time is critical na sidhani kama kuna muda wa kupoteza na huyu mlimbwende Zito