Zitto Kabwe ameeleza kuwa ni kweli walipiga kura na kukubaliana watoke wakati Rais akizungumza, lakini wao walipinga na ndiyo maana aliamua bora asiingie ndani ya Bunge, mesema kuwa yeye kama Zitto na wenzake aliona ni bora kutoingia kuliko kuingia na kutoka wakati Rais ambaye ndiye alama ya Bunge na Amiri jeshi mkuu akiongeaa.
Kwa vile kutoka ulikuwa msimamo wa chama, basi yeye na wenzake wamekosea na hilo ni swala la Chama kwani wanaweza kuadhibiwa na chama kwa vile kura za kukubaliana kutoka ilishinda.
Zitto alisema kuwa wanasubiria hatma yake katika chama na kusema kuwa hiyo ndiyo gharama ya Demokrasia. Ila amekanusha kuwa jambo hilo lisifikiliwe ni mgawanyiko bali mtazamo tofauti wa mawazo.
Source: TBC 1 News Bulletin
Huyu Mh huwa simuelewi at times, hii information ni ya kubomoa chama na sioni mantiki ya yeye kuisema hadharani. Zitto ni liability kubwa kwa Chadema. At times simuelewagi maamuzi yake anayatoaga wapi na anashauriwa na nani.