Zitto amsifu Ngeleja amshauri ahame CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto amsifu Ngeleja amshauri ahame CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Dec 9, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  Zitto msifu Ngeleja amshauri ahame CCM

  Na Said Mwishehe

  NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Bw. Kabwe Zitto 'amemfagilia' Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja, na kusema anafurahishwa na uchapakazi wake ambapo amewapongeza wananchi wa Sengerma kwa kuchagua kuwa mbunge wao.

  Akizungumza na wananachi juzi katika mkutano wa hadhara 'Operesheni sangara' uliofanyika katika Wilaya ya Sengerema ikiwa ni sehemu ya mikutano Kanda ya Ziwa, Bw Kabwe alisema wananchi walifanya uamuzi mzuri kumchagua Bw. Ngeleja ambaye amekuwa akifanya vizuri katika shughuli zake za uongozi.

  Bw. Kabwe alisema tangu Bw. Ngeleja alipoteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini, amefanya kazi zake vizuri na kwa umakini mkubwa jambo ambalo linaleta matumaini makubwa kwa kuwa na viongozi wa aina hiyo.

  “Ndugu zangu wa Sengerema naomba niwashukuru kwa kumchagua Ngeleja kuwa mbunge wenu, yuko makini na anajua anachokifanya katika shughuli zake na tunaweza kusema ni moja kati ya viongozi makini wa CCM. Unapoona kiongozi anafanya vizuri lazima usifie ndiyo maana nimeona ni vema nikaawaeleza,” alisema Bw. Kabwe.

  Alisema amepunguza baadhi ya matatizo ambayo yalikuwa yakitokea katika wizara hiyo kwa mawaziri waliopita ya kuingiza nchi katika mikata mibovu lakini yeye amekuwa makini na kuhakikisha serikali haingii katika matatizo kama ya Richmond.

  Bw. Zitto alisema kitu ambacho kinaweza kumkwamisha Bw. Ngeleja kufanya kazi zake vizuri, ni chama alichokuwepo ambacho kitamfanya asiweze kuendelea na kuchapa kazi kama ilivyokuwa sasa na kumshauri aondoke huko na kutafuta chama ambacho kitamfanya aendelee kuwajibika vizuri.

  “Ngeleja ni mchapa kazi mzuri lakini kwa kuwepo kwake CCM kutamharibia na kumuweka katika wakati mgumu hivyo anapaswa kuondoka na kwenda chama ambacho kitamfanya aendelee, kiongozi kijana anawajibu wa kupima chama gani akienda ataweza kuendelea na majukumu ya kuwatumikia wananchi,” alisema.
   
 2. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Haya ndio ya Zitto haya.

  Mchana anatupigania kwa jasho na machozi. Usiku analala nao!

  Zitto Kabwe amekubali, ame endorse jinsi Kikwete administration inavyo handle masuala ya mali asili za Tanzania. Amepitisha, amebariki, mwelekeo mzima wa mining policy ya Kikwete administration kwa kupasisha na kusifia kazi ya kiongozi wa wizara ya madini.

  Now, Hon. Zitto, you have every right to - and you could be absolutely right in - your assesment of Ngeleje's work. After all, since you wrote that presidential report you are probably more privy on all issues on the mining front than most experts are.

  Lakini sasa, mheshimiwa mbunge, lakini sasa, tusije tukasikia, tusisome mahala, tusije tukakuona sehemu, bungeni, ama Ikulu, ama mitandaoni, ama kwingine kokote kule kwa siri unapokutana na viongozi wa CCM, tusisikie umetamka kukosoa, kuswalisha, kubeza au kudai maelezo ya chochote na lolote lile lililopo chini ya portfolio ya William Ngeleja.

  Ahsante kwa kutuwekea wazi msimamo wako.

  Malcom X, mwanaharakati wa kimarekani wa karne iliyopita, aliwahi kusema kwamba ana heshima zaidi kwa mtu anaemwambia aliposimama, hata kama hayuko sawa, kuliko yule anaekuja kama malaika lakini ndani hana unje wa vazi la kondoo. Kwa hilo, ahsante tena.

  Ok. Tusonge mbele. Nani aliyebaki sasa ? Tuna nani mwingine? Nani ataahidi kulinda mali za Watanzania ? Yana mwisho!
   
 3. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2008
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Kingozi Kuhani, Salaam Mkuu;

  Kwanza asante sana kwa uchambuzi yakinifu wa hoja mbalimbali zinazokuja hapa jamvini.

  Sijaelewa bado ni hoja gani unayotaka kuiweka bayana katika post yako hapo juu.
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Dec 9, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Juzi Juzi tu Jakaya kaamshambulia Ngeleja kwa ugoigoi wa wizara yake kubadilisha mitambo ya kuzalisha umeme ili itumie gesi asilia. Leo bwana kabwe anakuja na mpya kumsifia huyo huyo bosi wake alieonyesha kutorudhika na utendaji wake. Zitto ni vyema ukawa mkweli tujue uko upande gani ili usitupotoshee harakati za kuikomboa nchi yetu.
   
 5. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Allien, umemuelewa Bulesi ?

  Hata huyo Kikwete mwenyewe, did you hear him, Bulesi anakwambia hata huyo Kikwete mwenyewe anamgombeza gombeza Ngeleja hadharani.

  Leo Kikwete kagomba kuhusu bei za mafuta, kasema kamuagiza huyu Ngeleja afanye a do something.

  Kikwete alishawahi kumwambia hadharani Ikulu kwamba inaonekana huyu Ngeleja ha make time kusoma documents muhimu. Remember that ?

  Kikwete mwenyewe is not happy with this official, anam lambast in public kama kitoto kidogo all the damn time.

  Halafu mpinzani aliyekuwa anapiga kelele kuhusu wizi wa mali asili za umma anakuja kum endorse, baada ya kuanza kualikwa alikwa kwenye cocktail parties za Magogoni. Na kuandika ripoti ambazo baadae anakuja kutuambia hawakua na nguvu ya kufufua kila yaliyofichika - including the names of who own which mine - kwa sababu hawakuwa na nguvu za ku subpoena watu na documents. Tume ya Rais haina subpoena authority!!! Sasa kwa nini ulikubali kuingia kwenye kitume kisicho na nguvu ya ku find out nani anamiliki mgodi ati kwa vile hawana power of subpoena ? Rais kwani hana nguvu ya ku grant subpoena power ? Please, usanii mwingine bana.

  Bulesi, that was a trenchant point there.
   
 6. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2008
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Kuhani, nakupata sasa Kiongozi;

  Siasa wakati mwingine zinaweza kuwa ni za ajabu sana, isije ikawa Bwana Zitto anafanya elimination ya mawaziri vijana ili kuifanya public ifocus kwa waziri kijana, msomi na anyeongoza wizara nyeti aliyetoa siku saba. Vinginevyo, sioni Mantiki ya yeye kumfagilia mtu ambaye performance yake ni questionable.

  Sina uhakika kama Mh. Ngeleja ana chembechembe au harufu yoyote ya ufisadi. Shida yake inaweza kuwa katika performance (Efficiency and Effectiveness). Mawaziri wote vijana wamepandishwa vyeo kutoka manaibu mawaziri kuwa mawaziri kamili katika kipindi kifupi tu cha miaka mitatu. Kwa mtu asiye na experience na uongozi, hii ni changamoto kubwa. Labda tumpe muda tuone kama performance itakwenda juu.

  Sina uhakika na Waziri kijana Kamala . . . Naona kule suala la EAC na ardhi yetu analisimamia vizuri . . .
   
 7. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #7
  Dec 9, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280


  Mkuu,

  Zitto kama mwanasiasa Liberal ana haki ya kusifia mazuri.Si kila siku kukandia tu,ingawa kwako wewe mkuu na viongozi wengine wa CCM wanaliona hili kama lugha ya kigeni.

  Huu ndio ustaarabu wa kisiasa.Sasa sijui unapomkataza zitto kufanya hayo uliyodai,unamaanisha nini?

  Zitto amemsifia Ngeleja,zitto hataki kuwa mnafiki.Kesho akimlima Ngeleja itakua ni haki yake
   
 8. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #8
  Dec 10, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  "Mwanasiasa Liberal" maana yake nini ?

  Tusije tukawa tunaokotaokota mawazo na maneno kutoka mifumo ya siasa za sehemu nyingine halafu maelezo ya ki-mushkeli mushkeli yanafanya tusielewane.

  Unataka kusema siasa za mrengo wa kushoto? Tanzania tunacho hicho kitu? Mashoga wanakubalika Tanzania? Wasioamini Muumba wanachukuliwaje Tanzania ? Kuna uhuru wa kusema unachotaka ? Unaweza kusema "Rais ana malengelenge" ? Sijui unanielewa ? Hakuna liberalism Tanzania!!

  "Mwanasiasa Liberal ana haki ya kusifia mazuri," kwa hiyo ndio kusema conservatives hawana haki ya kusifia mazuri ?

  Una maana gani "Mwanasiasa Liberal" ?

  Una maanisha independent politician ? Zitto ni independent yule? Unayo voting record ya Zitto ? Ni kwa kiasi gani Zitto ame vote kwa kuji align na CCM au ku endorse platform ya CCM ? Sijui hata unanielewa? "Mwanasiasa Liberal" ?

  Unaongelea haki kwa mujibu wa nini, haki za Kikatiba za kufyatua unachotaka al muradi hujasema Rais ana malengelenge, ama ?

  Unajua tofauti kati ya the right to say something na being right in what you said ?

  Signature issue iliyojenga political career ya Zitto Kabwe ni ufisadi wa mali asili za Tanzania. Leo ametoa ringing endorsement kwa kazi ya mkuu wa serikali mwenye portfolio ya sekta ya madini Tanzania.

  Sasa asije kusikika akipiga yowe tena kuhusu usimamizi na undeshaji wa sekta ya mali asili za Tanzania.
   
 9. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #9
  Dec 10, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280

  Mkuu,

  Acha kukurupuka,ungekua unaelewa maana ya kuwa Liberal politician usingekurupuka kushangaa Zitto kumsifia Ngeleja au kutoa maonyo hayo ya ajabu ajabu

  Wewe una mawazo mgando ya kuwa mtu akishakua upinzani au chama flani basi ni wa kukosoa tu,na akisifia inakua dhambi kwa jinsi unavyoonekana
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Dec 10, 2008
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mheshimiwa Zitto Kabwe ni miongoni mwa wanasiasa wachache waliotokea kunikuna sana hasa katika kipindi hiki, lakini mh.Zitto Kabwe wakati mwingine anakwenda nje ya mstari kabisa sijui ni ujana au uchanga katika medani za siasa.Mheshimiwa Zitto hiyo si miongoni mwa kazi zako wala chama chako hakijakutuma kwa shughuli hiyo.

  Habari ya kumsifia Ngeleja wakati anajua fika jamaa kashindwa kwa kiwango cha kutisha kuisimamia wizara nishati na madini ni jambo lingine linalonifanya nimwangalie Zitto kwa jicho la mashaka.Bei ya mafuta katika soko la dunia imeshuka sana lakini bei ya mafuta katika soko la ndani imebaki ile ile au imeshuka kidogo sana,Ngeleja kama angekuwa hodari tungeona bei za mafuta zikishuka sambamba na bei inavyoshuka katika soko la dunia.Muungwana juzi kwenye baraza la Idd kamtolea uvivu.Hii si mara ya kwanza kwa mh.Zitto kunichefua kwa hoja zake dhaifu,najua wa jf mtakumbuka mchango wa mh.Zitto katika kikao cha bunge kuhusu Tanzania kujiunga na EAC fast tracking sina haja ya kuelezea jinsi alivyotofautiana na mamilioni ya watanzania kwani kila mtu aliyekuwa akifuatilia mjadala alibaki kinywa wazi.
   
 11. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #11
  Dec 10, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Zitto anacheza sana tu hapo, na hajafanya homework yake, na alikuwa anacheka cheka na watu kisiasa.

  Mgombea wa CHADEMA atapata tabu kwenye hilo jimbo.Hata kama tunaongelea post partisanship, you do not get on your opponents you know what.

  Siasa za Tanzania bado sana.
   
 12. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #12
  Dec 10, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nini maana ya "Liberal politician" ? Una maana siasa ya mrengo wa kushoto ? Kwa hiyo ma conservatives ndio huwa hawasifii wapinzania wao ? Liberal ni mrengo wa kisiasa. Sio haki ya kusifia!! Kama unataka kusema mwanasiasa asiyejifunganisha kijumla na itikadi au chama fulani sema independent au maverick!

  Hata hivyo ma concept hayo na mirengo hiyo kwetu haipo!! Tanzania unaweza kujua votting records za Mbunge ili utathmini itikadi wanazofungamana nazo? Huwezi. Bongo kuna mambo ya mivutano ya liberalism vs. conservatism ?Hakuna!!! Unaweza kufanya abortion ? Kukubalika na jamii kua shoga ? Kusema unachotaka bila kukamatwa kama vile "Rais ana malengelele" ? Huwezi. Hakuna free speech Bongo. Mkuchika akihojiana na Mwanakijiji alisema Tanzania huruhusiwi kusema "Rais ana malengelenge"!!! Tanzania kuna migongano ya kiitikadi juu ya separation of church and state ? Kuna migongano ya kiitikadi kuhusu property rights na gun rights ? Hakuna liberalism vs. conservatism Bongo. !!! Sio unaokotaokota ma-concept kwenye mifumo ya nchi nyingine unataka kui apply sehemu usiyohusika!

  Nimetoa sababu kwa nini Zitto anashangaza anaposifia sifia hapa. Signature issue iliyo m-propel Zitto to prominence ni ufisadi wa migodi na madini. Hii sekta bado ina matatizo lukuki, na wizara ya Ngeleja bado ina mitafaruku na ishu kila kukicha, kuanzia kwenye mikataba ambayo haijapitiwa, bei za mafuta, mapungufu ya nishati, ufisadi wizarani, na mengine kibao, tena Ngeleja ni waziri pekee ambae Kikwete huwa anam lambast lambast hadharani. Halafu leo Zitto anakuja ku endorse kazi ya Waziri. Zitto anatakiwa sasa hivi awe out there pressing and pushing for his report's recommendations to be implemented. Sio kumu endorse Waziri ambae hata bosi wake Kikwete kalalamika kwamba Ngeleja hata hasomi documents muhimu za wizara yake.

  Wengine mko hapo mnazugwa eti "mwanasiasa Liberal" ana haki ya kusifia, mnaona kama ni uungwana ungwana fulani wa kisiasa. You don't get it. Yeyote anasifia, lakini husifii abject failures.
   
 13. m

  mboje Member

  #13
  Dec 10, 2008
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh, yamekuwa hayo tena Hon.Kabwe?
  Ni haki yako lakini usji ukala matapishi yako tena, hatutakuelewa!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 14. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #14
  Dec 10, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Exactly, thank you.
   
 15. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #15
  Dec 10, 2008
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,144
  Likes Received: 1,234
  Trophy Points: 280
  Inwezekana huyo aliyemshutumu ndiye goigoi, kuchelewa kuibadilisha hiyo Mitambo ndiyo umakini wenyewe ambao Zitto kaungelea. Hauwezi uka damp hela ya Umma kwenye mitambo ambayo ina mgogoro ambao haujaamuliwa na mahakama hadi sasa. Aliyemshambulia Ngeleja hayupo makini na ndio maana Zitto akamtaka aondoke kule kwani Umakini wake unakwaza
   
 16. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #16
  Dec 10, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kusifia kwa Zitto kuna maana mbili

  1. Ana skendal na Masha ( amemuwasha kweli Mwanza pale); anamtofautisha kijana mwenzake na mwingine- divide and rule pale kafanya ( mjanja huyu) lakini kawaambia perfomance yake haiko sawa kwa sababu yuko ktk mfumo ulio hoi wa CCM.

  2. Politically kumsifia mtu ni kumuweka karibu na wewe; lakini ni muda muafaka sasa kutafuta namna ya kunvuta kiukweli u kweli; sengerema itakwenda chadema 2010 expected maana lile lilikuwa na Masha mzee sasa amestaffu kumpisha kijana so lazima chadem ichukue ukanda ule ( majimbo ya wapinzani hawajajua tu)

  Mie what liberal what conservative lakini politics lazima uwe mkweli; ufocus na uwe objective; hope zitto hajatoka ktk mstari

  :: asije tu akayafanya haya yote kwa sababu kweli kuna kitu pembeni; itakuwa aibu ingawa sio siri namwamini bado Zitto anavyotupigania kuliko wanaoandika tu hapa wakiwa ughaibuni
   
 17. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #17
  Dec 10, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Good observation Bill,
  Nashangaa sana watu kutumia mashambulizi ya JK kwa Ngeleja publically kwamba ni kuonyesha Ngeleja kashindwa kazi ama ni goi goi katika utendaji wake, just open the book, dont judge it from its cover!

  Yawezekana umakini wake ndicho chanzo cha kushambuliwa na kuonekana hafanyi kazi!, Yawezekana kutokubali tupa pesa za walala hoi katika vitu visivyo na tija, na pengine kutokubali kimbia na mihuri ya serikali hotelin Londoni ndicho chanzo chake yeye kuonekana kashindwa kazi!

  Umakini unatakiwa pote si wa kumuona Zitto kakosea lakini pia wa kuchunguza uhalali wa JK kumshambulia publically mara kwa mara Ngeleja!
   
 18. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #18
  Dec 10, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Okay, Rwabugiri,

  Sasa kama inawezekana Kikwete anamshambulia Ngeleja hadharani kwa sababu Ngeleja hataki kufuja hela za walalahoi ni kwa nini huwa Ngeleje anaitikia "ndio mzee" ?

  Kama anapogombezwa gombezwa hadharani ni kwa vile anachukia ufisadi ni kwa nini then ana turn around kwenda kutekeleza maagizo ya kifisadi ya Rais ?
   
 19. M

  Mundu JF-Expert Member

  #19
  Dec 10, 2008
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hivi katika baraza zima la mawaziri wa Muungano, hakuna hata mmoja ambaye anafanya kazi zake vizuri na kustahili kusifiwa? Mbona anaposifiwa Ngeleja tena kwa hoja zenye nguvu za Zitto, wengine hupinga tu tena kwa hoja dhaifu kama... asije akabadilika na kumkandia tena siku zijazo; mara mbona Rais amekuwa akimgombeza tena mbele ya kadamnasi.

  Hivi hatuwezi kuja na Hoja mbadala zenye nguvu kumhusu Ngeleja na ndipo tuweze kusema kuwa Zitto ameropoka? kama hatuna hizo hoja tusikurupuke tu na kutoa maangalizo yasiyo na kichwa wala miguu.

  Hivi ukifananisha utendaji kazi wa karamagi na NGELEJA katika Wizara hiyo iliyokuwa imeharibika; huwezi kusema kuwa kijana anajitahidi? Give credits when due! after all if you don't have facts, you have the right to keep your mouth shut!!!!!
   
  Last edited: Dec 11, 2008
 20. M

  Mama JF-Expert Member

  #20
  Dec 10, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Hivi Zitto ni Waziri?
   
Loading...