Zitto akera wajumbe kamati kuu CHADEMA - Tanzania Daima

Zitto akera wajumbe kamati kuu CHADEMA - Tanzania Daima

Status
Not open for further replies.
Zitto hataki kuja kwenye vikao muhimu kama hivi ili achangie mada na kukijenga chama.
Anaonekana haoni umuhimu sana wa kuhudhuria mapema ingawaje baadae anaweza kuhudhuria,hii ni kutokana na kuwa Zitto he is just an opportunist guy,hana malengo yenye nia dhabiti ya kuwa kiongozi wa juu(Raisi), au kukipigania chama chake(Chadema) kiweze kukamata dola(2015).

Lake la umuhimu ni MSHIKO TU,haujalishi umetoka upande gani,provided anahakikisha fursa na usalama wake kubakia ndani ya Chama,na at least awe na aina fulani ya uongozi kama alivyokuwa nao sasa(Naibu Katibu Mkuu)

La ajabu sasa, ngoja siku itangazwe kuwa kuna UCHAGUZI MKUU ndani ya Chadema,utamwona jinsi atakavyokurupuka......"ZITTO NATAKA KUWA MWENYEKITI WA CHAMA.....NIPENI FORM NIGOMBEE UENYEKITI".......!!! Just vikao vya maandalizi,hatakosa kuhudhuria hata kimoja,na siku hizo mambo ya udhuru hayatakuwepo kabisa. Hizo ndio zao ma-great opportunist,lakini sasa mambo ya vikao hana mpango nayo sana, na hata akija baadae anakuja kuzuga tu ili aonekane amuhudhuria,.....yeye anachosubiri kwa hamu ni lini uchaguzi utaitishwa.

Hata hivyo nataraji HEKIMA KUBWA walionayo VIOGOZI wa sasa wa CHADEMA,wataju jinsi gani ya KUMUONGOZA MTU kama huyu,mpaka hapo mwisho wake utakapofikia.
Maana ukweli maji na mafuta hayawezi kukaa pamoja siku zote,lazima vitu hivyo vitajitenga tu.
LETS MOVE FOWARD, PEOPLES PARTY-CHADEMA.
 
We are actually watching all the moves ............Wewe unaelewa vizuri sana namaanisha nini...Jamii yetu ya Kitanzania imejengwa katika misingi ya kutoulizana wewe ni dini gani na wewe ni dini gani...matokeo yake mnaleta chokochoko za kwamba sisi waislam wale wakristo...so what? kuleta hizo fikra katika jamii kwanza ni kosa kubwa ambalo nakuhaikishia as a nation hatuwezi kukubali kwa interest za maslahi yenu yawayo yote mtugawe........Watanzania wazalendo hata katika forum hii wanaona.. Ritz wewe ni moja kati ya watu mnaopenda kupandikiza migogoro katika jamii...kwa kuigawa kwa misingi ya kikabila na dini.....Kama unayafanya hayo kwa interest yako na familia yako...be careful...Wengine bado tunaipenda Tanzania..............
Mkuu haujajibu swali UDINI ni nini?
 
msaliti zitto anakalibia kufanikisha kazi aliyotumwa na CCM kuua upinzani ,,na anafanya kiufundi sana ..yetu macho.
 
Anawezeja kuwa maarufu ndani ya Chama kama hapewi nafasi. Kama hana nafasi maana yake si maarufu, Umeelewa?
 
Mwaka 2010, Sebastian Kasinge aliyeteuliwa
kugombea ubunge jimbo la Mpanda
Mashariki, alikwama kuwania nafasi hiyo.
Kisa?! Zitto.
Ilikuwa hivi, Kasinge alikwama kupata barua
ya utambulisho kutoka kwa viongozi wake wa
wilaya ya Mpanda kuwa ni mgombea.
Akaenda makao makuu ya Chadema jijini Dar
es salaam. Akakutana na Dk. Slaa, katibu
mkuu wa Chama chao, Akampa barua ya
uteuzi.
Lakini Zitto kwa kutumia kofia yake ya
unaibu katibu mkuu tena akiwa nje ya ofisi
na bila kushirikiana na wenzake wa makao
makuu, alimwandikia msimamizi wa uchaguzi
wilaya ya Mpanda kumjulisha Chadema
kutoweka mgombea jimbo la Mpanda
Mashariki. Msimamizi wa Uchaguzi mara
baada ya kupata barua ya Zitto alimwondoa
Kasinge kwenye kinyang'anyiro cha ubunge na
kumtangaza Mgombea wa CCM, Mizengo
Kayanza Peter Pinda kuwa AMEPITA BILA
KUPINGWA
Michael Makenji aliyekuwa mgombea wa
ubunge wa Chadema jimbo la Musoma
Vijijini, alijiondoa kwenye kinyang'anyiro
hicho dakika za mwisho. Nimrod Mkono wa
CCM ALIPITA BILA KUPINGWA. Hii ni baada
ya Zitto kumshawishi mgombea wa chama
chake kujitoa. Taarifa zinazomkhusu Makenji
zinasema kabla ya mgombea huyo kujiondoa
kwenye kinyang'anyiro, naibu katibu mkuu
wake alifanya mazungumzo ya kina na
Mkono.
Katika kuthibitisha hilo, Makenji alikabidhi
kwa viongozi wake wa chama ujumbe mfupi
wa sms ulioonekana umetoka kwa Zitto
kwenda kwake ukilenga kumshawishi kujitoa.
Miongoni mwa yale yaliyotajwa na Zitto
kwenye ujumbe huo ni pamoja na kwamba
Mkono yupo tayari kuongeza fedha iwapo
yeye Makenji atakubali kujiondoa kwenye
mbio za kuwania ubunge.
Josephat Isango, aliyejitosa kwenye mbio za
ubunge jimbioni Singida kupambana na
Mohamed Dewji aliwekewa pingamizi na
Wazael Nakamia, mwenyekiti wa Chama
chake, CHADEMA wilaya ya singida Mjini.
Katika pingamizi lake, Nakamia anasema
Isango hakupitishwa na Chama chake
kugombea nafasi hiyo. Alipoulizwa na
mkurugenzi wa sheria wa chama hicho,
Tundu Lissu kilichosababisha kuwekewa
pingamizi kwa ndugu Isango, Nakamia
alisema ..."ni maelekezo ya Naibu katibu
Mkuu..."
Zilitokea vuta nikuvute kadhaa ambapo
mwishowe Dk. Slaa ambaye alikuwa amelazwa
hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu
alimwandikia msimamizi wa uchaguzi barua
nyingine ya kuthibitishauteuzi wa Isango.
Rais Kikwete alipofika singida kumnadi
mgombea wa CCM Singida alimtangaza Dewji
kuwa amepita bila kupingwa, siku chache
baadae NEC ikamtangaza Isango kama
mgombea.
Tamthilia hii ya Isango, Zitto, Dewji, Nakamia
na Lissu imeelezwa mara nyingi na na Lissu
mwenyewe kwenye vikao vya CC mbele ya
Zitto wenyewe. Zitto Hakuwahi kukana.
Nakamia tayari amevulia uongozi.
Mgogoro wa Madiwani Arusha haukumalizika
bila ya kumhusisha Zitto. Kamati iliyoundwa
na chama chake kutfuta suluhu ya mgogoro
huo iligundua mkono wa Zitto katika suala
hilo. Mgogoro ule uliisha kwa kufukuzwa
madiwani watano.
Naibu katibu mkuu alishiriki kwa kiasi
kikubwa katika mgogoro huo kwa kushiriki
kuwashawishi madiwani kukiasi chama, ni
sehemu ya mkakati wake wa kupambana na
Lema na wanasiasa wenzake ndani ya chama
chake wanaoonekana kumpiku kwa umaarufu.
Uchaguzi mdogo ulipofanyika Zitto
hakushiriki hata mkutano mmoja wa
kampeni,Hkwenda Arusha siku ya
Maombolezo baada ya vifo vya wafuasi wanne
wa Chadema.
Mengi zaidi soma MAWIO, Toleo namba 0070
Alhamis November 21-27, 2013 Uk10-11

Huyu ni ADUI mkubwa wa Demokrasia Tanzania; Afrika na Dunia yote.
Siku si nyingi atavuna alichopanda.
Mungu Ibariki Tanzania
 
Sasa vita hiyo wenzako hawapmbani kwenye keyboard za internetcafe kama unavofanya wewe,huwez kushinda,

Wenzio wameshashindwa huko afghanstan na wameamua kukubaliana kusign mikataba ya amani,wewe kalubandika endelea kula viroba na kushangilia propagnda usizozielewa...:A S 39:

Eti na hili lajifanya lina uchungu na nchi yake...kweli???? Unafiki mbaya sana...Nashukuru serikali iliwaona hawa wavuruga amani kule mtwara na kuamua kuwakomalia...wewe hata hustahili kuwa raia wa tanzania...watanzania hawako kama wewe
 
Mkuu haujajibu swali UDINI ni nini?

Kila jambo likitokea kwa chadema...wewe ndio wa kwanza kuuliza ooohhh dini gani huyo...ooohhh kabila gani huyo......Mkuu.....ninyi ni watu mnaotakiwa kupigwa vita hapa Tanzania...Watanzania jhatujazoea kuongea lugha ya kuulizana dini zetu na makabila yetu...Yeyote anayeendekeza mambo hayo ni mdini na ni adui yetu..........kama wewe ulivyo.......
 
Amekacha au hajapewa barua ya mwaliko? Acheni uzushi bandugu. Zitto hajapewa mwaliko wa kikao hicho na wala hajashirikishwa kwenye maandalizi yake

Barua ya mwaliko tumpe mwanachama wa CCM?.
 
Weeeeee! Hiyo haiwezekani kwa Zitto. Ukitaka hata panya asibaki kuwa mfuasi wa CHADEMA, mpigeni chini Zitto maana yule jamaa ana nguvu sana ndani ya CDM.

Ana nguvu ipi hata sisi tuliomwamini tumeishaona ni pandikizi.
 
Mimi huwa ninasoma maudhui ya habari. Huwa sisomi magazeti kwa kutumia kigezo cha headline ambacho mara nyingi ni catchline.

Sasa kama yote yanangalia business interest, kwa nini unakataa pale ninaposema nguzo ya Tanzania Daima ni CHADEMA. Inaonekana huelewi hata maana ya neno nguzo katika msingi wa andiko langu. Tanzania Daima is embedded in CHADEMA.

Ni kweli mtu mwenye akili fupi atadhania Tanzania Daima ni CHADEMA lakini mtu mwenye fikra na mawazo pevu atatambua kuwa Tanzania Daima imesimama kwenye nguzo za CHADEMA kutokana na maudhui yake pamoja na kwamba halikuanzishwa na CHADEMA.

Huo unafiki unao uona niwa kwako na hii inatokana na mtazamo wako unaobainishwa na uwezo wako kifikra. Wewe endelea kufikiria hivyo kwa sababu huo ndiyo ukomo wako kifikra. Mimi niko huru kusema lolote na kwa wakati wowote. Sijafungwa na vyama vya siasa nadharia.

Kama unaipenda CHADEMA, endelea kuipenda kwa sababu hiyo ni haki yako kama ilivyo haki yangu ya kutokuwa mwanachama wa chama cha siasa Tanzania.

By the way, Mtu wa CCM anaonekana vipi na Mtu wa CHADEMA mwonekano wake ukoje na kikubwa zaidi, kwani kuwa mwanaCCM au CHADEMA ni kosa kisheria au dhambi kiimani?.



Thank You,

Vifaranga wanapaswa kujibiwa namna hiyo kisha wamfikishie salam mama kuku anawaolealea
 
Chadema achaneni na zitto kwani chadema ilikuwako kabla yake hata hayati baba wa taifa aliibariki kwani ina malengo na sera nzuri kwa wananchi.aidha zitto anajua anamtumikia nani(cc....) na sio siri hao ndio wapo nyuma yake bila......zitto ni mbinafsi ndio maana hujitenga daima na wengi(wanachadema
)
 
Tanzania daima ni gazeti la chadema kakini limekuwa likichochea mivutano baini ya wana chadema.

hivi wamekerwa vipi wakati mbowe kasema zitto yuko safari?

Alaf kwa nini hiyo report hisichapwe kila mjumbe akawa na hard copy?

Hivi hiyo report inatolewa kwa faida ya zitto au kwa faida ya chama na wanachama?

Hivi kwanini chadema mnapenda maneno na malumbano yasiyo na tija?

kama ni report si kunatakiwa kuwe copy ili hata asiye kuwepo apate?
 
JF Management,
Mnaweza ku-run query from your SQL server yenu ili kuonyesha nani anaandikwa sana humu JF? Huenda huyo mtu aka-qualify kuwa Miss/Mr. JF....just thinking.
 
Mkuu haujajibu swali UDINI ni nini?

wewe hata dini yenyewe huijui,mnajua mnanufaika na mifarakano na chuki mnazopandikiza dhidi ya imani zingine.ole wenu aingie rais atakaye unganisha imani zote.magaidi mtafute pakwenda
 
Tanzania daima ni gazeti la chadema kakini limekuwa likichochea mivutano baini ya wana chadema.

hivi wamekerwa vipi wakati mbowe kasema zitto yuko safari?

Alaf kwa nini hiyo report hisichapwe kila mjumbe akawa na hard copy?

Hivi hiyo report inatolewa kwa faida ya zitto au kwa faida ya chama na wanachama?

Hivi kwanini chadema mnapenda maneno na malumbano yasiyo na tija?

kama ni report si kunatakiwa kuwe copy ili hata asiye kuwepo apate?

mkuu umeelewa logic ya wanapinga absenteeism ya Kabwe
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom