Ndugu zanguni wana CDM, nawaombeni sana tuwe wastaarabu. Hizi ID zetu feki humu zisitufanye tuwe wapuuzi, are we real Great Thinkers???????
Hivi ni Great Thinker gani anayekaa kumtukana kiongozi wake kama mwendawazimu?? nyie mnaojiona ndo wenye CDM hasa kuliko hata ZZK, hebu acheni kujidhalilisha, huyu ZZK si ni Naibu Katibu Mkuu wenu???
Kama mna ushahidi wa usaliti wa ZZK kwa CDM, kwa nini msiupeleke kwenye ngazi za CDM zinazotambulika ili ZZK ashughulikiwe kwa mujibu wa katiba ya CDM??
Kuna faida gani ya kuwa mnakuja humu JF na ID zenu feki mnamtukana kiongozi wenu, halafu viongozi wenzie mnaodai mnawaheshimu yaani MWENYEKITI na KATIBU MKUU wakisimama hadharani, wanasema hawana tataizo na ZZK??
Kama kweli nyie ni wana CDM wa kweli, ANDAMANENI mwende makao makuu mkashinikize ZZK atimuliwe, kama hilo haliwezekani, muwaambie hao viongozi wenu vipenzi wachague 1, kubaki kwenye chama na "msaliti" au wao wakubali kuwa ndo wana matatizo, kwa hiyo waachie ngazi.
Kwa nini wanaendelea kumuacha "msaliti" wa chama chenu kwenye nafasi ya uongozi??
Vinginevyo napata wasi wasi na uwezo wa kiakili wa nyinyi mnaojiita wana CDM, kwa nini mnachuma DHAMBI kumtukana KIONGOZI wenu humu JF kila siku kana kwamba hakuna utatuzi wa hayo mnayodhani matatizo yake?
Vinginevyo kubalini kuwa, CDM haina viongozi makini, nashindwa hata kuelewa hao viongozi wenu vipenzi kwa nini wanashindwa kujitokeza hadharani humu angalau kuwaasa muache tabia hiyo chafu ya kutukana mmoja wa viongozi mwenzao, na hii inanifanya nianze kupata wasi wasi na hawa kina KATIBU MKUU na M/KITI wa CDM, tatizo ni nini?? kwa nini wasikikemee hiki kitendo kichafu humu JF??
Kuna wakati JF inatia hata kinyaa kusoma matusi ya wanaojiita Great Thinkers.
Kwa haya matusi yanayoendelea humu JF, napata wasiwasi kama kweli sisi CDM ndio tunatarajia kutoa mustakabali mwema wa nchi yetu Tanzania, kwa nini tumegeuza matusi, uongo na unafiki kuwa ndio HOJA?