Mwaka 2010, Sebastian Kasinge aliyeteuliwa
kugombea ubunge jimbo la Mpanda
Mashariki, alikwama kuwania nafasi hiyo.
Kisa?! Zitto.
Ilikuwa hivi, Kasinge alikwama kupata barua
ya utambulisho kutoka kwa viongozi wake wa
wilaya ya Mpanda kuwa ni mgombea.
Akaenda makao makuu ya Chadema jijini Dar
es salaam. Akakutana na Dk. Slaa, katibu
mkuu wa Chama chao, Akampa barua ya
uteuzi.
Lakini Zitto kwa kutumia kofia yake ya
unaibu katibu mkuu tena akiwa nje ya ofisi
na bila kushirikiana na wenzake wa makao
makuu, alimwandikia msimamizi wa uchaguzi
wilaya ya Mpanda kumjulisha Chadema
kutoweka mgombea jimbo la Mpanda
Mashariki. Msimamizi wa Uchaguzi mara
baada ya kupata barua ya Zitto alimwondoa
Kasinge kwenye kinyang'anyiro cha ubunge na
kumtangaza Mgombea wa CCM, Mizengo
Kayanza Peter Pinda kuwa AMEPITA BILA
KUPINGWA
Michael Makenji aliyekuwa mgombea wa
ubunge wa Chadema jimbo la Musoma
Vijijini, alijiondoa kwenye kinyang'anyiro
hicho dakika za mwisho. Nimrod Mkono wa
CCM ALIPITA BILA KUPINGWA. Hii ni baada
ya Zitto kumshawishi mgombea wa chama
chake kujitoa. Taarifa zinazomkhusu Makenji
zinasema kabla ya mgombea huyo kujiondoa
kwenye kinyang'anyiro, naibu katibu mkuu
wake alifanya mazungumzo ya kina na
Mkono.
Katika kuthibitisha hilo, Makenji alikabidhi
kwa viongozi wake wa chama ujumbe mfupi
wa sms ulioonekana umetoka kwa Zitto
kwenda kwake ukilenga kumshawishi kujitoa.
Miongoni mwa yale yaliyotajwa na Zitto
kwenye ujumbe huo ni pamoja na kwamba
Mkono yupo tayari kuongeza fedha iwapo
yeye Makenji atakubali kujiondoa kwenye
mbio za kuwania ubunge.
Josephat Isango, aliyejitosa kwenye mbio za
ubunge jimbioni Singida kupambana na
Mohamed Dewji aliwekewa pingamizi na
Wazael Nakamia, mwenyekiti wa Chama
chake, CHADEMA wilaya ya singida Mjini.
Katika pingamizi lake, Nakamia anasema
Isango hakupitishwa na Chama chake
kugombea nafasi hiyo. Alipoulizwa na
mkurugenzi wa sheria wa chama hicho,
Tundu Lissu kilichosababisha kuwekewa
pingamizi kwa ndugu Isango, Nakamia
alisema ..."ni maelekezo ya Naibu katibu
Mkuu..."
Zilitokea vuta nikuvute kadhaa ambapo
mwishowe Dk. Slaa ambaye alikuwa amelazwa
hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu
alimwandikia msimamizi wa uchaguzi barua
nyingine ya kuthibitishauteuzi wa Isango.
Rais Kikwete alipofika singida kumnadi
mgombea wa CCM Singida alimtangaza Dewji
kuwa amepita bila kupingwa, siku chache
baadae NEC ikamtangaza Isango kama
mgombea.
Tamthilia hii ya Isango, Zitto, Dewji, Nakamia
na Lissu imeelezwa mara nyingi na na Lissu
mwenyewe kwenye vikao vya CC mbele ya
Zitto wenyewe. Zitto Hakuwahi kukana.
Nakamia tayari amevulia uongozi.
Mgogoro wa Madiwani Arusha haukumalizika
bila ya kumhusisha Zitto. Kamati iliyoundwa
na chama chake kutfuta suluhu ya mgogoro
huo iligundua mkono wa Zitto katika suala
hilo. Mgogoro ule uliisha kwa kufukuzwa
madiwani watano.
Naibu katibu mkuu alishiriki kwa kiasi
kikubwa katika mgogoro huo kwa kushiriki
kuwashawishi madiwani kukiasi chama, ni
sehemu ya mkakati wake wa kupambana na
Lema na wanasiasa wenzake ndani ya chama
chake wanaoonekana kumpiku kwa umaarufu.
Uchaguzi mdogo ulipofanyika Zitto
hakushiriki hata mkutano mmoja wa
kampeni,Hkwenda Arusha siku ya
Maombolezo baada ya vifo vya wafuasi wanne
wa Chadema.
Mengi zaidi soma MAWIO, Toleo namba 0070
Alhamis November 21-27, 2013 Uk10-11