Sikiliza wewe Mbulumundu, mgao wa umeme ulikuwepo 2005 wakati Kikwete anaingia madarakani, ukawepo 2006, 2007, 2008, 2009, 2010, 2011, 2012 na sasa 2013. Wewe unaongelea siku 11 zipi? Mgawa wa siku 11 unavumilika kwa watu kama wewe mnaotegemea umeme kwa kuwashia taa mpate mwanga wakati mnaKapuya, sisi mafundi welding ni siku 11 za njaa na mateso, sisi vinyozi ni siku 11 za jehanamu, sisi wauza samaki wabichi ni siku 11 za kilio. Kwa kweli nyie MaCCM aliyewaroga amekufa. Kila siku mnajifariji na ahadi zenu za kuvumilika na sasa ni miaka 50 nchi haina kitu hata kimoja cha kujivunia.