Zitto akera wajumbe kamati kuu CHADEMA - Tanzania Daima

Zitto akera wajumbe kamati kuu CHADEMA - Tanzania Daima

Status
Not open for further replies.
in no time moderators will merge this thread with the later
 
Mwaka huu CCM mtavaa chupi vichwani. Chadema imekuwa mwiba mkali sana kwenu!!
 
Naunga mkono hoja ila ungeeleza na sababu na jinsi anavyovuruga chama ili wanajukwaa wakuelewe
 
Magamba mbinu zenu zimekishagundulika! CDM haiendeshi kwa hila za magamba...
 
Wangejua kua yeye ni muhimu na ni msaidizi wa katibu mkuu wao, wasinge tuma vifaranga kuja kumchafua huo wote ni unafiki.. hao jamaa ni wa ajabu sana wanafikiri zitto ni kichwa maji...
 
Ni kuhusu Zitto kabwe, huyu kijana anakivuruga sana chama kwa mwenendo wake anao ufanya ndani ya chama, unaopelekea kukidumaza chama. Kiukweli zito ni kirusi kinacho kimaliza chama.Hivyo mimi binafsi naomba kamati kuu kuchukua maamuzi magumu dhidi ya zito

toa sababu wakuelewe.
 
Yanayo kutoka kinywani yanadhihirisha upeo wa fikra zako. huu si uwanja wa matusi bali hoja. kama huna ARGUMENT TORERANCE sepa
 
Zitto ambaye katika siku za hivi karibuni aliibua mjadala kwenye vyombo vya habari, hasa alipoingia kwenye malumbano na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amekacha kikao hicho na badala yake ametoa taarifa ya kusafiri nje ya nchi.
Mara nyingi CHADEMA na Tanzania Daima huwa wanapenda kutengeneza habari lakini bila kufahamu kuwa katika habari hiyo kinachoumia ni chama na mlengwa wa habari.

Kulikuwa kuna umuhimu gani kuweka hii paragraph katika habari hii na kutoa hitimisho kwa kusema amekacha kikao.

Kwanza Kamati Kuu ina wajumbe zaidi ya 35, inakuwaje kukosekana kwa Mh. Zitto kuwakele wajumbe wakati yeye hata siyo Mwenyekiti au Katibu wa Kikao hicho.

Hata hayo mahesabu yanayodaiwa kufanywa, kwani mpaka awepo kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA ndiyo ayaone?. Kiutaratibu na kisheria, anapokuwa bungeni anakuwa siyo mbunge wa wanaCHADEMA na hata anapokaa kwenye kikao cha Kamati huwa hayuko pale kutetea maslahi ya CHADEMA bali ya wananchi bila kujali itikadi zao. Ajenda za Kitaifa haziwezi kupunguzwa na kubakia ndani ya vikao vya CHADEMA. Vipi mahesabu ya CCM, CUF nayo aende akahudhurie kikao chao kuupata ukweli?. Hizi ni hoja za kitoto!.

Haya ndiyo majungu yanayokiumiza chama kwa sababu kama kuna wajumbe wamekeleka, kwa nini wasitoe dukuduku lao ndani ya kikao na kama Mwenyekiti ataona kuna umuhimu wa kulijafili basi lijadiliwe ndani. Inawezekana ikawa hizi ndizo ajenda za kwenye vikao vya Jf kama ilivyo jadi kwa sasa kwa viongozi wa CHADEMA. Ofisi na vikao vyao kwa sasa vimehamia Jf.

All in all hata kama watatumia nguvu nyingi kukanusha lakini ukweli ni kwamba, CHADEMA kuna makundi hai yanayohatarisha misingi na ajenda endelevu ya chama.

CHADEMA lazima kichukue maamuzi magumu kwa faida ya mstakabali wake na kinyume cha hivyo, viongozi wataendelea kujificha kwenye ajenda za CCM ndiyo mchawi, mchawi, mchawi.
 
na mimi naanza kupata wasi wasi na mienendo ya zitto! Huyu mbona ni kama fisi ndani ya zizi la kondoo?
 
Zito alisha nunuliwa na magamba siku nyiiingiiii.


Zitto Zuberi Kabwe kwa sasa ni dhahiri kabisa inaonyesha ni tatizo ndani ya chama. Huu ni ukweli mchungu kwa Zitto lazima akubaliane nao na dalili zote zinaonyesha hivo!Ni kichekesho kama siyo kihoja kwa N/Katibu Mkuu wa CDM kutohudhuria kikao muhimu cha Kamati Kuu yeye akiwa kiongozi mwandamizi na Mjumbe muhimu wa kikao husika! Hili haliingii akilini hata chembe!!!!!!

Haiwezekani CC ya CDM ikae kwa ajili ya kujadili maswala nyeti na muhimu yanayohusu chama halafu yeye awe na Ziara zake binafsi ambazo hazihusiani moja kwa moja na CDM! Hii ni dharau na ni ishara mbaya sana kwa Zitto.

Zitto alishavimba kichwa kwa umaarufu ambao nina hakika unaenda kumwangamiza kisiasa. Tunajua kabisa yuko karibu sana na baadhi ya Viongozi wa CCM akiwemo rais Kiwete. Lazima kwa namna fulani kwa nyakati fulani Zitto anatumiwa na Serikali ya CCM kuivuruga CHADEMA, hili halina ubishi na Zitto analijua hilo kule ndani ya nafsi yake!!!

Chokochoko zote hizi za Zitto,sijui amechafuliwa sana,amepigwa mishale sana,amezushiwa sana na Viongozi ndani ya Viongozi wenzake ni vurugu za kutaka kukisambaratisha chama. Kuna mambo yako wazi kabisa kuhusu huyu dogo ambayo yana ashiria kuwa hayuko pamoja na Uongozi wa Juu wa chama:

  1. Kuna hili la kutaka KUGOMBEA kuwa Mwenyekiti wa CDM,ili hali chama kina Mwenyekiti anayeongoza vizuri tu. Hili ni tatizo. Kuna mawili hapa aidha ni TAMAA ya madaraka au ni NJAMA za kuvuruga chama.
  2. Kuna hili la POSHO za Wabunge.Kwamba Zitto hataki kupokea posho ambazo ziko kwa mujibu wa sheria na kanuni za Bunge. Sasa huwa simwelewi Zitto anapokataa posho ambazo ziko kisheria anataka kumfurahisha nani? Je,ni mbinu zake za kisiasa kutaka kujimbanua na viongozi wenzake ndani ya CDM au nini? Kwanini basi hapeleki muswada wa kupinga hizi posho kama anaona hazina umuhimu badala ya kulumbana na kina Lema kwenye mitandao?
  3. Kuna hili la RUZUKU ya Serikali kwa vyama vya siasa ambapo Zitto anasema vyama hivi vyote ikiwemo CDM hawajawahi kuwasilisha hesabu zilizokaguliwa na CAG tangu mwaka 2009. Zitto anadai hivo kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge lakini wakti huohuo yeye ni N/Katibu wa CDM. Swali ni: Yeye alikuwa wapi miaka yote hii kuhusiana na Mahesabu ya CDM??? Huu ni UNAFIKI wa Zitto kwa chama.
  4. Kuna matukio yanayohusu CHADEMA ndani na nje ya Bunge ambapo Zitto mara zote ameonekana kutoungana na Viongozi wenzake katika kupinga mambo hayo. Mosi ni hili la msimamo wa CDM kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya. Wakti viongozi wa CDM wakipinga uchakachuaji wa rasimu hiyo Zitto hakuwepo kabisa wala hakuwa na habari. Kuna mlipuko wa Bomu la Soweto kule Arusha, Zitto Kabwe hakuwepo wala hakuguswa na tukio hilo kwa vile hakuna mahali popote aliwahi kulizungumzia tukio hilo kana kwamba halimuhusu!!!Hili ni tatizo kwa Zitto.
  5. Mwisho ni hili la MABILIONI YA FEDHA zilizoko ughaibuni ambazo bila shaka zimetoroshwa na MAFISADI wachache wenye uroho na utajiri wa harakaharaka. Bwana Zitto ameligeuza swala hili kama swala BINAFSI na hataki kabisa kukihusisha chama. Sasa simwelewi huyu jamaa anataka sifa au ni mbinu zake za kisiasa za kujizolea umaarufu wakti akizidi kukididimiza chama!!! Mimi namkumbusha Zitto Kabwe kuwa kidole kimoja hakivunji chawa! Arejee kumbukumbu zake kuhusu isseu ya EPA. Swala la EPA lilitikisa nchi kwa vile kina Dr. Slaa na kina Mbowe waliungana pamoja kimkakati kwa kutaja ile LIST OF SHAME na ikazaa matunda!

Tunamshauri Zitto aache ulevi na tamaa ya madaraka na sifa kwani zitamporomosha vibaya sana kisiasa labda kama ana mpango wa kuhamia huko kwa watu wa Magamba-CCM.

Wasalaamu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom