Kwa habari hii gazeti la CCM/serikali mgao mkubwa wa umeme unakuja

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,269
675
Hii serikali inaendeshwa KIHUNI, HII HABARI IMETUGWA KUTUAMINISHA ILI MGAO WA UMEME UANZE HUKU WAKIMTETEA PROF MUONGO


muhongo6_300_172.jpg

UTEKELEZAJI wa shinikizo la kuvuliwa madaraka kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, linaloendelea kutolewa na wabunge na baadhi ya wanasiasa kwa Rais Jakaya Kikwete, huenda ukaacha masononeko kwa wananchi walionufaika na kipindi kifupi cha uongozi wa waziri huyo.

Profesa Muhongo aliyejitengenezea uadui kwa wafanyabiashara na wanasiasa, kutokana na misimamo yake ya kulinda maslahi ya umma na kuzungumza ukweli, huku akijiamini kulikotafsiriwa kuwa ni dharau, hatima ya uongozi wake ipo mikononi mwa Rais Kikwete, ambaye ameshauriwa na Bunge kutengua uteuzi wake.

Katika azimio la saba, kati ya maazimio manane ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lililomalizika mwishoni mwa mwezi uliopita, kuhusu utoaji wa fedha katika akauti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mamlaka ya uteuzi wa Profesa Muhongo, imeshauriwa kutengua uteuzi huo.

"Bunge linashauri na kuazimia Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mwanasheria Mkuu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, wawajibishwe na mamlaka ya uteuzi itengue uteuzi wao," limeeleza azimio hilo la saba.

Usambazaji umeme

Kama Rais Kikwete atatekeleza ushauri huo wa Bunge na shinikizo la wanasiasa na wafanyabiashara, uongozi wa muda mfupi wa Profesa Muhongo takribani miaka miwili, utakumbukwa kwa umahiri wa kusambaza umeme vijijini.

Kabla ya kuteuliwa kwa Profesa Muhongo, Watanzania asilimia 14 tu ndio waliokuwa wakitumia nishati ya umeme, kati yao asilimia 12 walikuwa watumiaji wa mijini na asilimia mbili tu, ndio walikuwa watumiaji wa vijijini.

Kwa mujibu wa takwimu za Serikali, kati ya mwaka 2007 na mwaka 2010, kulikuwa na ongezeko la asilimia nne tu la watumiaji wa umeme, hali iliyoonesha kuwa ongezeko la Watanzania waliokuwa wakipata umeme, lilikuwa asilimia moja kwa mwaka.

Lakini baada ya kuteuliwa kwa Profesa Muhongo katika nafasi hiyo, katika muda mfupi wa uongozi wake, idadi ya Watanzania wanaotumia umeme iliongezeka na kufikia asilimia 36 katikati ya mwaka huu.

Kwa hatua hiyo, uongozi wa Profesa Muhongo ulivuka malengo ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambayo ndio msingi wa utekelezaji wa malengo ya Serikali, iliyotaka Serikali kuhakikisha ifikapo mwaka 2015, asilimia 30 ya Watanzania wawe wanapata umeme.

Baada ya kupita malengo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Profesa Muhongo aliamua kuweka malengo mapya, ambapo alitarajia ifikapo 2015, asilimia 45 mpaka 50 ya Watanzania wawe na fursa ya kutumia umeme.

Miongoni mwa Watanzania wanaokiri hilo ni Diwani wa Kata ya Manga wilayani Tarime, Omolo Ochola ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa madini kutoka Rorya.

Ochola alipozungumza na gazeti hili wiki hii, alisema Waziri Muhongo amefanya kazi kubwa, amesambaza umeme vijiji vingi hapa nchini na kudhibiti ubadhirifu uliokuwepo hapo awali.

Mbali na Ochola, Mbunge wa Ntera, Livingston Lusinde (CCM), alisema yeye hawezi kuona aibu kuzungumzia mafanikio ya uongozi wa Profesa Muhongo, huku akitoa mfano wa Tanesco kupigia simu wateja ili ikawaunganishie umeme, kuwa haikuwahi kutokea kabla ya uongozi wake.

Bei ya uunganishaji

Katika kutimiza malengo hayo, uongozi wa Profesa Muhongo, ulitangaza punguzo la gharama za kuunganisha umeme majumbani kutoka Sh 177,000 za awali hadi Sh 27,000 vijijini.

Awali, punguzo hilo lilitolewa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara, ambako bomba la kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam limeanzia na limepita, lakini baada ya muda gharama hizo zilishushwa kwa vijiji vyote nchi nzima.

Profesa Muhongo mwenyewe alisema gharama hizo zitahusu miradi inayosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA), katika kipindi ambacho wakandarasi watakuwa wakiendelea na awamu ya pili ya miradi iiliyoanza Machi mwaka huu na kutarajiwa kukamilika kati kati ya mwakani.

Profesa Muhongo alisema kuwa katika awamu ya kwanza ya miradi iliyomalizika Desemba mwaka jana, wanavijiji walilipa gharama kubwa, hivyo uongozi wake uliamua kupunguza malipo hayo, ili huduma hiyo ya nishati iwafikie watu wengi zaidi.

Kufuta mgawo

Kuhusu suala la mgawo wa umeme, Profesa Muhongo mwaka 2012 alisema mgao wa umeme hautakuwepo tena na haukubaliki kamwe.

Profesa Muhongo alisema hadi Juni 2012 uwezo wa mitambo ya kufua umeme (installed capacity) ulikua megawati 1,375.74 (gesi asilia ikiwa ni asilimia 40, maji asilimia 41 na mafuta asilimia 19).

Alifafanua kuwa uwezo huo, ulikuwa ni ongezeko la megawati 367 sawa na asilimia 36 ikilinganishwa na uwezo wa megawati 1,013.74 uliokuwepo Juni, 2011.

Alisema mahitaji ya juu ya umeme kwa mwaka 2011/12 yalifikia wastani wa MW 820.35 ikilinganishwa na MW 730 kwa mwaka 2010/11. Tangu wakati huo, hakujatokea mgawo mkali wa umeme kama uliotokea mwanzoni mwa mwaka 2011, na miaka ya nyuma ya hapo.

Tanzania kabla ya uongozi wa Profesa Muhongo, ilikuwa ikikabiliwa na mgawo wa umeme wa mara kwa mara, ambao mbali na kuathiri maisha ya watu wa kawaida kutokana na kusababisha mfumko wa bei, pia uliathiri sekta ya viwanda ambapo baadhi vilitishia kufunga.

Kutokana na mgawo wa mara kwa mara, mwanzoni mwa mwaka 2011, Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), liliwahi kutoa taarifa ya kutishia kufungwa kwa viwanda 50 kati ya 280, huku vingine vikitishia kupunguza uzalishaji, kutokana na makali ya mgawo wa umeme.

Wamiliki hao walidai kupitia CTI kwamba, hawana uwezo wa kutumia jenereta kwa ajili ya shughuli za uzalishaji viwandani, kwa vile umeme wa jenereta utawalazimu kulipia gharama za matumizi ya nishati hiyo maradufu, tofauti na ile inayozalishwa na Shirika la Umeme (Tanesco).

Walitoa mfano kuwa wakitumia umeme wa Tanesco kwa kila kilowati moja, wanalipia senti za dola ya Marekani nane mpaka tisa, lakini wakitumia umeme wa jenereta, kwa kila kilowati moja, wanatumia senti za dola ya Marekani 18 mpaka 20.

Mbali na hao, CTI ilieleza pia kuwa asilimia 15 ya wanachama walitishia kuongeza bei ya kuuzia bidhaa wanazozalisha na athari yake kwa mapana, ilielezwa kuwa viwanda vitakosa mapato, ajira kwa watumishi wa viwandani zitapotea na Serikali pia itakosa mapato yanayotokana na kodi za viwanda.

Aidha Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ilieleza kuwa mfumko wa bei ulipanda na kufikia asilimia 6.4 kutoka asilimia 5.6, sababu kubwa ikiwa ni mgawo wa umeme.

Ofisi hiyo ilitoa mfano wa bei ya vyakula na vinywaji baridi, kwamba ilipanda kutoka asilimia 2.9 na kufikia asilimia 6.7 kutokana na mgawo wa umeme.

Kushusha bei ya umeme Baada ya kufanikiwa kufuta mgao wa umeme, kusambaza umeme kwa wananchi na kuunganisha umeme kwa wananchi kwa gharama nafuu, mwanzoni mwa mwaka huu, Profesa Muhongo, alitangaza kusudio lake la kushusha bei ya umeme.

Diwani Ochola wa Manga wilayani Tarime, alisema Profesa Muhongo alikuwa amejiandaa kushusha zaidi gharama za umeme mwakani.

Naye Musa Onyango, mchimbaji mdogo kutoka Rorya, alisema gharama za umeme zilikuwa zikipanda kila mwaka na kuwakatisha tama Watanzania ikilinganishwa na kipindi cha mwaka mmoja wa Profesa Muhongo ambapo kumekuwa na ahueni kubwa ikilinganishwa na wakati wa viongozi waliotangulia Kusudio hilo la kushusha bei, lilitarajiwa kuanza kuonekana mara bomba la gesi kufika jijini Dar es Salaam na mitambo ya umeme kuanza kutumia gesi badala ya mafuta mazito.

Uongozi wa Profesa Muhongo, uliweka wazi kuwa wafanyabiashara wanaouzia umeme Tanesco, wanauza uniti moja kwa kati ya Dola ya Marekani senti 33 na 50.

Bei hiyo ya umeme kwa Tanesco kwa mujibu wa takwimu za Serikali, ni kubwa kuliko bei ya umeme ambayo shirika hilo linauza kwa Watanzania wanaotumia umeme mdogo wa majumbani, umeme wa kati kwa wafanyabiashara, umeme wa kati wa viwandani na umeme mkubwa kwa viwanda vikubwa, na kubwa kuliko bei ya umeme ya mashirika ya umeme ya nchi za Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa Takwimu za Tanesco, wateja wa majumbani, uniti moja ya umeme wanauziwa kwa dola ya Marekani senti 19, wateja wa biashara senti 13 na viwanda vya kati na vikubwa senti 10.

Umeme wa taa za barabarani ni senti 19, wakati Tanesco inanunua kwa senti 33 na 50. Profesa Muhongo alisema bei ya umeme iliyopo, ni kwa muda tu na itashuka sana bomba la gesi likikamilika, kwa sababu hata mitambo ya kufua umeme inayotumia mafuta nayo, itatumia gesi na mitambo mipya ya gesi italetwa.

Alisema Serikali inataka umeme mwingi utokane na gesi, jua, upepo na joto ardhi, lakini wapo wanaokataa bomba lisije Dar es Salaam na nyuma yao, wapo wafanyabiashara ambao wanahofia kuwa mwisho wa biashara yao ya kuuzia Tanesco umeme kwa bei ya juu umefika.

Msimamo huo wa Profesa Muhongo, uliwahi kuungwa mkono na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliyesema mwishoni mwa Januari mwaka huu alipokuwa Mtwara, kuwa Serikali imedhamiria kuachana na umeme huo wa mafuta na kama wafanyabiashara hao watataka kuendelea na biashara hiyo, ni vyema wabadilishe mitambo yao iwe ya gesi na sio ya mafuta kama ilivyo sasa hivi.

Wataalamu wa gesi

Kutokana na ugunduzi mkubwa wa gesi uliofanyika nchini, Profesa Muhongo pia alianzisha utaratibu wa kusomesha Watanzania wengi zaidi katika vyuo vya nje ya nchi katika masuala ya gesi na mafuta, ili wananchi wasimamie rasilimali hiyo kwa manufaa ya taifa lao na vizazi vyao.

Lengo la Profesa Muhongo katika hilo, ni kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya kwanza yenye wataalamu wengi wa mafuta na gesi, katika nchi za bara la Afrika, baada ya miaka mitano ijayo kwa kuwa na wataalamu zaidi ya 300 watakaokuwa wamesomea masuala hayo nje ya nchi.

Pia amefanya juhudi kushawishi watanzania ambao ni wataalamu mafuta na gesi zaidi ya 10 wanaofanya kazi nje ya nchi hususani nchini Canada na Uingereza, mpaka wakakubali kurejea kufanya kazi hizo nchini.

Utata wa kumwajibisha

Hatua ya Bunge kutaka Profesa Muhongo awajibishwe, imetokana na maoni ya Mwenyekiti wa Bunge wa Kamati ya Fedha za Serikali (PAC), Kabwe Zitto, kuwa fedha hizo Sh bilioni 321 ni za umma na utoaji wake na kwamba hatua ya kulipwa kwa kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), iligubikwa na harufu ya ufisadi.

Hata hivyo, Profesa Muhongo katika utetezi wake, alisema wakati wa kufunga akaunti hiyo kulikuwa na Sh bilioni 182.77 tu, wakati deni baada ya kupiga hesabu, lilikuwa Sh bilioni 275.20 na zote ni fedha za IPTL, zilizotokana na mauzo ya umeme wake katika Shirika la Umeme (Tanesco), na hivyo bado kampuni hiyo inaidai shirika hilo la umeme Sh bilioni 123.90.

Mbali na kueleza kuwa kampuni hiyo ya IPTL bado inaidai Tanesco, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, ambaye naye anatakiwa kuondolewa, alisisitiza kuwa akaunti ya Escrow haikatwi kodi, ila kodi hiyo hukatwa kwa mpokeaji wa fedha hizo na kutaka Mamlaka ya Mapato (TRA), kwenda kudai kodi yake kwa IPTL.

Profesa Muhongo na Werema mpaka sasa msimamo wao ni kwamba fedha hizo si za umma, huku Profesa Muhongo akisisitiza kuwa mbali na kuwa si za umma, pia Serikali bado inadaiwa Sh bilioni 123.90.

Lakini hata taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), hajathibitisha kuwa fedha hizo ni za umma, bali ilieleza kuwa kuna uwezekano kuwa katika fedha hizo, kuna fedha za Tanesco, fedha za Serikali kwa maana ya kodi na fedha za IPTL, ambazo ni mauzo ya umeme kwa Tanesco.

Chanzo:Habarileo

DSC06650.jpg
 
Hivi bado kuna watu wananunua gazeti hili. Afadhari umenisaidia nimeona linavyofanana.
 
Watanzania muwe mnaona na upande wa pili pia. Pamoja na tuhuma za kashfa za kifisadi, huyu ndugu kapiga kazi.

Hili ndio tatizo kubwa ka baadhi yetu, mtu kafanya kazi yake mnataka abebwe au nini??!!!
Kapiga kazi ipi ambayo ni exceptional??!!
Mmezoea non performing figures so mkiona "kawaida" sasa inaitwa "zaidi" mtu anaoewa kila zuri hapa duniani kwa nini asifanye kazi wakati kuna watu wanaenda kazini kwa mguu tena mbali vitendea kazi hakuna na hawaonekani achilia mbali uhakika wa pensheni akistaafu!!!!!

Kama ana makosa anyanyuke tu!!!
 
Back
Top Bottom