Zitto afanye haya kurudisha umaarufu wake

​​
Nianze tu kwa kusema Ukishakataliwa na Jammiforums umekataliwa na jamii nzima ya watanzania na lazima mtu husika uwe makini na idadi ndogo (minor proportion) ya watu wanaoweza kukuhadaa eti wanakuunga mkono hapa jamvini kuliko wale wanaokupinga.

Ujumbe wako nimeishia kusoma hapa. Jamiiforums kama umefuatilia hivi karibuni imedhihirika kuwa kuna watu wengi tu ambao wanaandika mawazo "fake" ili kuvipatia maslahi vikundi fulani. ID moja inaweza kutumiwa na watu zaidi ya watano kutoa maoni. Hivyo basi kuamini kuwa maoni ya JF yanareflect uhalisia wa fikra za jamii SI KWELI.

Kuna wakati JF ilikuwa inatoa picha halisi ya fikra za jamii lakini baada ya kuvamiwa na walafi wa kisiasa hali imekuwa tofauti. Sasa hivi JF unaweza kuandika point nzuri tu lakini kwa sababu mlengo wako ni wa upande fulani, basi litaibuka kundi kubwa kukupinga. Infact kundi hilo ni kundi la ID sio kundi la members kwa sababu anaweza kuwa ni mtu mmoja tu anayetumia ID mbalimbali.

Sisi wengine tunakuja JF kwa vile ni kijiwe chetu tulichokizoea na kimekuwa sehemu ya maisha yetu, lakini genuine nature ya JF haipo tena. Siku hizi JF imekuwa sehemu ya watu kuleta habari za uongo kama ile ya mwanamke wa kimarekani aliyesingiziwa kuwa ndiye aliyekuwa na RPC wa Mwanza wakati anauwawa!

Kimsingi kuna kitu kinatakiwa kufanyika ili JF irudi kwenye hali ya kuaminiwa na kuwa sehemu ambayo akili zinapimana nguvu siyo kijiwe cha kumezeshana itikadi.
 
Mkuu hapo kwenye Bolna Red unataka awafichue ili ufanayeje kama mtanzania??? Wengine wote waliofichuliwa ulichukua hatua gani??? By the way mbona ameshawataja kwa vyeo wewe umechukua hatua gani???

Tafakari kisha chukua hatua.

Mkuu umeuliza vema, ukweli ni kwamba kwa sasa hamna hatua tunayoweza chukua lakini itoshe tu kusema mbali na uwezo tuliojaliwa wana Chadema, tunapata kuungwa mkono zaidi pale panya CCM wanapofichuliwa. Na hatua kubwa itakuwa kuwaondoa madarakani 2015.
 
Ujumbe wako nimeishia kusoma hapa. Jamiiforums kama umefuatilia hivi karibuni imedhihirika kuwa kuna watu wengi tu ambao wanaandika mawazo "fake" ili kuvipatia maslahi vikundi fulani. ID moja inaweza kutumiwa na watu zaidi ya watano kutoa maoni. Hivyo basi kuamini kuwa maoni ya JF yanareflect uhalisia wa fikra za jamii SI KWELI.

Kuna wakati JF ilikuwa inatoa picha halisi ya fikra za jamii lakini baada ya kuvamiwa na walafi wa kisiasa hali imekuwa tofauti. Sasa hivi JF unaweza kuandika point nzuri tu lakini kwa sababu mlengo wako ni wa upande fulani, basi litaibuka kundi kubwa kukupinga. Infact kundi hilo ni kundi la ID sio kundi la members kwa sababu anaweza kuwa ni mtu mmoja tu anayetumia ID mbalimbali.

Sisi wengine tunakuja JF kwa vile ni kijiwe chetu tulichokizoea na kimekuwa sehemu ya maisha yetu, lakini genuine nature ya JF haipo tena. Siku hizi JF imekuwa sehemu ya watu kuleta habari za uongo kama ile ya mwanamke wa kimarekani aliyesingiziwa kuwa ndiye aliyekuwa na RPC wa Mwanza wakati anauwawa!

Kimsingi kuna kitu kinatakiwa kufanyika ili JF irudi kwenye hali ya kuaminiwa na kuwa sehemu ambayo akili zinapimana nguvu siyo kijiwe cha kumezeshana itikadi.

Nimekusoma mkuu, hata hivyo wanaobadili ID ni masalia ambao wanahaha kujaribu kuonesha kuwa ni wengi, lakini hata hivyo hawafikii idadi ya wenye nia ya kweli na wanaoiheshimu JF. IDs nyingi kuliko watu halisi bado hawatufikii makamanda wa ukweli.
 
Ingekuwa umaarufu wake unatokana na kupigiwa vuvuzela, lisipopigwa ningekubali umaarufu wake ungeshuka, lakini umaarufu wa ZZK unatokana na ability!. Aombe msamaha kwa kosa gani, ajutie jambo gani?.

Ingekuwa jf ni wapiga kura, basi saa hizi Chadema ingekuwa Ikulu!. JF ina wanachama laki moja plus!. Hawa ndio Watanzania wote?.
ZZK bado ni maarufu vile vile tena umaarufu unazidishwa na hii Zitophobia kila siku thread 10 -10 za ZZK!.
P.

PASCO inawezekana umeharakisha kujibu, nimeweka msisitizo kuwa tulioJF ndio wapiga kampeni huko mitaani, mimi nakuhakikishia ni product ya JF na Mwanahalisi. Na hadi leo nimeweza ku-convert pro CCM zaidi ya 500.

Pia wewe ni kati ya wale mnaompa tumaini ZITTO anaezidi kupotea.
 
Umaarufu upi? arudishiwe, ZZK huwezi kumtenganisha na umaarufu ktk nchi hii, kwa sababu yy ni kiongozi kijana na mzalendo kwa nchi yake, tatizo lake amejizolea maadui wa kisiasa ndani ya chama chake. kwa kuwa ni mtu wa demokrasia, wakati chama chake demokrasia ni changa. miongoni mwa mashabiki na baadhi ya wanachama hivyo wanataka uongozi au uteuzi wa wagombea ufanywe kiimla. mfano ni huu, sote tunaamini ukikataliwa jf, basi umekataliwa na watanzania wote? kwangu mimi hawa ndo wale watetea IMLA.
 
kwa akili zako unataka kutueleza CDM 2010 ilishinda uchaguzi wa uraisi mimi nahic ushabiki umekukaa kichwani vipi chama kimeshinda majimbo yasio zidi 50 na chengine kimeshinda zaidi ya majimbo 100 kipi kitaibuka mshindi wa uraisi kwa isabu ya haraka haraka ni yupi

Refer Ukwaju hapo juu amekuambia sio lazima uchague chama, unaweza chagua raisi na madiwani na mbunge wa vyama tofauti.
Kwa kuwa wewe umeonyesha uchungu sana.
Naomba Idadi ya Kura za Kikwete mshindi wa Uraisi 2010 kwa tiketi ya CCM.
 
Usitake kutudanganya hapa, kuwa ukikataliwa na Jamiiforums ndo umekataliwa na jamii nzima! Jamii gani unayoizungumzia au ndo hii ya baadhi ya watu kati ya 100,000+ wanaoshinda mitandaoni kuchafuana??
 
Tatizo kuu la Kabwe ni kutokutaka kujishusha..watanzania ni wepesi sana katika kusamehe na kuchukulia mambo easy na kuyasahau...katika hili naamini ZITTO anayo nafasi ya kusamehewa hata kama msamaha wake atauombea mdomoni tu bila kutoka moyoni........
 
Usitake kutudanganya hapa, kuwa ukikataliwa na Jamiiforums ndo umekataliwa na jamii nzima! Jamii gani unayoizungumzia au ndo hii ya baadhi ya watu kati ya 100,000+ wanaoshinda mitandaoni kuchafuana??

Ingawa sijui uchumi, kuna kitu kinaitwa multiplier effect au kwenye Maths kinaitwa exponential curve au kwenye afya kinaitwa point source, mfano ya Cholera. Hivi vinaashiria how something from one point can spread very fast. Jf ideas is a point source to spread entirely in Tz community.
 
Lazima ziwepo "Assumptions" kwanza. Niambie kwanza kwenye members 100'000+ wa JF ni wangapi hawamkubali Zitto? kama hautakuwa na hizo takwimu sidhani ka unaweza ukaja na majumuisho ya kuwa Watanzania wengi hawamkubali Zitto.
 
Ingekuwa umaarufu wake unatokana na kupigiwa vuvuzela, lisipopigwa ningekubali umaarufu wake ungeshuka, lakini umaarufu wa ZZK unatokana na ability!. Aombe msamaha kwa kosa gani, ajutie jambo gani?.

Ingekuwa jf ni wapiga kura, basi saa hizi Chadema ingekuwa Ikulu!. JF ina wanachama laki moja plus!. Hawa ndio Watanzania wote?.
ZZK bado ni maarufu vile vile tena umaarufu unazidishwa na hii Zitophobia kila siku thread 10 -10 za ZZK!.
P.

Pasco, hapa jf ndo nchi yenyewe, kama tume ya uchaguzi ingekuwa huru chadema wangekuwa ikulu. Kumbuka mpaka sasa kuna watu wanaamini kuwa chadema waliporwa ushindi wao na tume. watu laki moja ni wengi sana ukizingatia kuwa hawaishi sehemu moja na wengi wao wana ushamishi katika sehemu wanazoishi. haya ya ZK kuomba msamaha tumwachie mwenyewe atafakari na kuona kama kunastahili kufanya hivyo afanye na sio kumlazimisha kufanya ama kumkataza kama unavyotaka kufanya wewe.
 
huko Bongo mnaendeleza majungu, udini, ukabila na kila aina ya uchafu! Hamtatoka katika umasikini
 
Zitto bomu, tumesema kitambo hapa.

Kwangu hakuwa na umaarufu husika to begin with, kwa hiyo hawezi kuurudisha.

Isitoshe, umaarufu si tija, hata Hitler na shetani (the character) ni maarufu.

Sema jingine.

Kaka...

Hit under the belt!
 
Ganda la mua la jana, chungu aona kivuno!. One cannot be a hero to everybody!.
Shujaa wa mmija ni bomu kwa mwingine!.
Hata alichokifanya Osama huku wengine wakimlaani, kwa wengine ndie shujaa wao!.
Baba wa Taifa tunamuona ndiye shujaa wetu wa ukombozi dhidi ya mkoloni, wengine wanamlaumu mpaka kesho kwa kisingizio cha kuulea mfumo Kristo!.
Ukweli unabaki kuwa ZZK ni role model wa vijana kibao!.
P.

Role model wako pekee yako mpuuzi kama wewe usiwasemee wengine mkuu.
 
Naona Pro-CHADEMA JF wanajiliwaza na kujifariji...Dr Slaa ni rais wenu humu nyie Pro-CHADEMA, upande wa Tanzania ni rais kivuli wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom