Hisia: Kuna idadi kubwa ya Watanzania wanaosumbuliwa na Stockholm Syndrome ikija kwenye kutawaliwa na CCM!

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,252
113,645
Kama kichwa cha mada kinavyobainisha, hizi ni hisia zangu tu.

Sijafanya utafiti ulio rasmi. Sina uwezo wa kiakili wala wa kiutaalamu kuweza kufanya utafiti wowote ule ulio wa kisayansi.

Ni hisia zangu kama mtu na raia mwenye busara za kawaida tu [common sense] ambaye hupenda kuangalia na kutazama mambo yajiriyo kwenye jamii na kuyachanganua kwa kadri ya uwezo wangu.

Sasa kilichonisukuma kuanzisha mada hii ni uteuzi wa aliyekuwa ‘Governor🤣’ wa Dar es Salaam enzi za utawala wa Rais John Pombe Joseph Magufuli [najua alikuwa ni Dokta pia ila nimeliacha tu hilo kwa makusudi 😉].

Siku si nyingi zilizopita, Paul Makonda aliteuliwa [au alichaguliwa?] kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa CCM.

Sijui aliteuliwa kwa sifa zipi hasa maana jamaa ni kiwanda cha pumba tupu kila afunguapo domo lake.

Katika kumfuatilia kwangu kwa ukaribu tokea aanze utumishi wa umma, sijawahi kumsikia akiongea jambo lolote lile ambalo lilinifanya nimkubali. Akifungua domo lake huwa ni pumba tu mwanzo, katikati, mpaka mwisho. Pumba.com. Undisputed, undefeated PumbaMaker champion of the world.

Kilichonistua zaidi kuhusu uteuzi wake huo, ni yale mapokeo ya taarifa za yeye kuteuliwa kushika hiyo nafasi, hususan hapa JF ila pia hata kwingineko.

Majumuisho ya uangalizi [observation] wangu huo ni kwamba, idadi ya watu waliofurahia Makonda kurudi kwenye safi za juu za kiuongozi kwenye chama chake, ni kubwa.

Nilitegemea kuwepo mapokeo yaliyo hasi. Nilitegemea uteuzi wake huo ubezwe. Nilitegemea watu watapuuzia mbali huo uteuzi.

Lakini haikuwa hivyo. Watu walionyeshwa kufurahishwa na kurudishwa kwake. Wapo waliosema kuwa yeye ndiye mtu sahihi kwenye hiyo nafasi.

Baadhi ya walioonyesha furaha ya yeye kurudi ni wale ambao wamejitanabaisha kama ni watu walio pinzani na CCM.

Hali hiyo ya mapokeo ya watu juu ya taarifa za Makonda kuteuliwa kuwa katibu mwenezi zimenifanya nijiulize endapo labda Watanzania kwa uwingi wao wanasumbuliwa na Stockholm Syndrome baada ya kushikwa mateka na utawala wa chama kimoja tokea tupate uhuru zaidi ya miaka 60 iliyopita!

Manake haiingii akilini kabisa! Iweje mtu kama Paul Makonda mwenye kashfa nyingi zihusuzo uvunjwaji na ukiukaji wa haki za kibinadamu na makandokando mengine mengi kurudishwa kwake kwenye uongozi wa chama chake kufurahiwe namna hiyo na watu?

Ni kama vile CCM imeziteka akili na hisia za watu mpaka watu hao kuona kana kwamba bila hicho chama basi hata nchi nayo haipo.

Duniani kwa kawaida, kwa mtazamo wangu, idadi ya wapumbavu na wajinga huwa ni kubwa zaidi kuliko ile ya walio werevu.

Ila kwa Tanzania, nadhani idadi ya wapumbavu inaizidi idadi ya wajinga. Na ukijumlisha idadi ya wapumbavu na wajinga, kwa makisio yangu, inafika hata kwenye 99% ya idadi yote ya watu.
 
Kama kichwa cha mada kinavyobainisha, hizi ni hisia zangu tu.

Sijafanya utafiti ulio rasmi. Sina uwezo wa kiakili wala wa kiutaalamu kuweza kufanya utafiti wowote ule ulio wa kisayansi.

Hiyo ni probability tu the reality is watanzania wamejitakia wenyewe
Only recently wameanza ku realize but safari bado ni ndefu

They have been in state of abduction by ccm for 60yrs plus
 
Hiyo ni probability tu the reality is watanzania wamejitakia wenyewe
Only recently wameanza ku realize but safari bado ni ndefu

They have been in state of abduction by ccm for 60yrs plus
Watanzania wako zaidi ya milioni 60.

CCM na wanachama wao hawazidi hata milioni 10.

Watanzania zaidi ya milioni 50 tunashindwa nini kuwaondoa CCM?

Uoga tu.
 
Nawashangaa sana wanao mponda bi mkubwa kwa kumteua Makonda. Bi mkubwa ametumia akili ya juu sana kumteua Makonda.

Kwenye mpira wa miguu kocha huwa anampanga mchezaji kwenye mechi sio kwa sababu mchezaji huyo ni hodari sana kuliko wenzake lah hasha ila anampanga mchezaji huyo kwenye mechi kwa sababu mechi hiyo ina muhitaji.

Bi mkubwa = Kocha.

Makonda = mchezaji

Leave our president alone.

# KWA Makonda na Dotto Biteko tumeshaiua Sukuma Gang.
 
Kama kichwa cha mada kinavyobainisha, hizi ni hisia zangu tu.

Sijafanya utafiti ulio rasmi. Sina uwezo wa kiakili wala wa kiutaalamu kuweza kufanya utafiti wowote ule ulio wa kisayansi.

Ni hisia zangu kama mtu na raia mwenye busara za kawaida tu [common sense] ambaye hupenda kuangalia na
U mmoja kati ya wanaompromote mtu huyo Kwa kufungua theads mfululizo kumhusu iwe Kwa mabaya au mazuri.

Tunayo mengi ya kuongelea kama Tume huru ya Uchaguzi kabla ya 2025,

Tusihamishwe.
 
Nyani Ngabu ndugu yangu Usicho kujua ni kuwa Tanzania sio sehemu salama kuishi watu wanao jielewa.

Ukishaonekana unajielewa kwenye hii nchi huitajiki ndio maana wizarani huko unaweza kukutana na mkuu wa idara wa ajabu sana ukajiuliza mara 2 mbili huyu hata ujumbe wa nyumba 10 TU hafai🤣🤣🤣.

Nilisha wahi kwenda makao makuu ya jeshi Fulani. Nilicho kutana nacho ni kioja Cha mwaka. Mkuu wa idara hata kuandika Jina lake ilikuwa mtihani🤣🤣🤣

Nikaenda kwenye kitengo kingine nikamkuta mkuu wa idara amelewa chakari muda wa kazi huku akiwa na sare.

Hii nchi ukijielewa hupati nafasi wanerithisha hata sekta binafsi na wenyewe IPO hiyo system​
 
Kama kichwa cha mada kinavyobainisha, hizi ni hisia zangu tu.
Mi nadhani CCM ni kubwa zaidi ya hisia, tafiti za kisayansi au uwezo wa kufikiri.
Hili dubwasha ni jabali kubwa la kufurahisha wengine, kutisha na kuhuzunisha wengine kwa masikitiko makubwa.
Na huo ni mwanzo tu kuelekea 2025 aisee....

Hili dude bana ukiliendea kisayansi unalo, kisiasa unalo , jino kwa jino unalo sijui utalikosa WAPI......

"IF YOU CAN'T BEAT THEM, JOIN THEM". mwisho wa kunukuu....
 
Mapokeo hasi hutoka kwa watu walio huru kifikra na kiuchumi, wanaojiweza kwa namna tofauti wasio na dalili zozote za uchawa, hawa ndio wangeweza kusimama na kuponda uteuzi wa Makonda.

Lakini kwa taifa ambalo sasa tunaona sifa kuwa chawa, tunashindana kutafuta mbinu mpya za uchawa, tena wengine wanaanzisha mpaka taasisi na kupewa pesa za kuziendesha, hayo mawazo ya kusubiri watu waponde uteuzi wa Makonda ni ndoto iliyoko mbali sana na uhalisia kwa sasa
 
Nyani Ngabu ndugu yangu Usicho kujua ni kuwa Tanzania sio sehemu salama kuishi watu wanao jielewa.

Ukishaonekana unajielewa kwenye hii nchi huitajiki ndio maana wizarani huko unaweza kukutana na mkuu wa idara wa ajabu sana ukajiuliza mara 2 mbili huyu hata ujumbe wa nyumba 10 TU hafai.

Nilisha wahi kwenda makao makuu ya jeshi Fulani. Nilicho kutana nacho ni kioja Cha mwaka. Mkuu wa idara hata kuandika Jina lake ilikuwa mtihani

Nikaenda kwenye kitengo kingine nikamkuta mkuu wa idara amelewa chakari muda wa kazi huku akiwa na sare.

Hii nchi ukijielewa hupati nafasi wanerithisha hata sekta binafsi na wenyewe IPO hiyo system​
Kabisa mkuu.

Huwa nasema kwamba

Uafrika hasa utanzania ni laana.

Waafrika hasa watanzania wana Upumbavu wa milele.
 
Back
Top Bottom