Zitto afanye haya kurudisha umaarufu wake

Acha Uvivu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
524
Reaction score
131
​​Wanajamvi, sio kusudi langu kuingilia mtazamo wa mtu yeyote, ila kwa nia ya dhati na uelewa kuhusu uhuru wa kutoa maoni unaolenga kujenga na sio kubomoa, nimeona vema nitoe Ushauri kwa Mkuu Zitto na Kundi lake.

Nianze tu kwa kusema Ukishakataliwa na JammiForums umekataliwa na jamii nzima ya watanzania na lazima mtu husika uwe makini na idadi ndogo (minor proportion) ya watu wanaoweza kukuhadaa eti wanakuunga mkono hapa jamvini kuliko wale wanaokupinga. Na hasa ukijua kuwa wanachama wa JF ndo wapiga kampeni huko mitaani kuhusu Chama na mwanasiasa binafsi (kumbuka hofu ya Pinda-CCM) juu ya JF.

Kwa kutambua mchango wako (Zitto), achana na hao walala hoi wanaojipendekeza, wakiwemo CCM wanaotaka kukutumia kama tissue, ningeomba haya uyafanye kutoka kwangu kama Mtanzania mpenda mabadiliko na mchukia wanafiki:
KWANZA; Ujutie kile ulichokuwa unakifanya maana huenda ulikuwa hujui ulitendalo.

PILI; Jishushe tu tuombe radhi Watanzania ambao kwa idadi kubwa ni wakulima na wafanyakazi na ambao tunaomba usiku na mchana kuona nchi yetu imekombolewa toka mikononi mwa CCM. Haimanishi ufanye mkutano wa hadhara lakini JF inatosha tu kutupa jibu nasi tutakurudisha kundini, maana kama nilivyo sema hapo juu; UKIKUBALIWA NA JAMIIFORUMS UMEKUBALIWA NA WATZ WOTE. Na kwa kinachoendelea ndani ya chama chako, ambacho umewahi sema huna mpango wa kukihama, onyesha ushirikiano na baada ya kuyamaliza huko ndo uje kwetu.

TATU; Baada ya hayo hapo juu kufanyika, tufichulie wote walioficha mpunga (fedha) huko Uswisi kama ulivyoanza vema na usikate tamaa. Na lazima hili lifanyike baada ya hayo hapo juu kwa sababu hili likitangulia bado halitakurudisha kwenye level yako ya awali. Hakika ukiyafuata haya na ukatuambia wezi tulionao nguoni mwetu tutakurudisha kwenye form fasta.

Ni mtazamo wangu wanajamvi.
 
Ingekuwa umaarufu wake unatokana na kupigiwa vuvuzela, lisipopigwa ningekubali umaarufu wake ungeshuka, lakini umaarufu wa ZZK unatokana na ability!. Aombe msamaha kwa kosa gani, ajutie jambo gani?.

Ingekuwa jf ni wapiga kura, basi saa hizi CHADEMA ingekuwa Ikulu!. JF ina wanachama laki moja plus!. Hawa ndio Watanzania wote?.
ZZK bado ni maarufu vile vile tena umaarufu unazidishwa na hii Zitophobia kila siku thread 10 -10 za ZZK!.
P.
 
Eti ukikubaliwa na JF umekubaliwa na watanzania wote??? Kwe kwe kwe kwe kwe kwe kweeeeeee.....acha nichekeee mieeeee
 
Ingekuwa umaarufu wake unatokana na kupigiwa vuvuzela, lisipopigwa ningekubali umaarufu wake ungeshuka, lakini umaarufu wa ZZK unatokana na ability!. Aombe msamaha kwa kosa gani, ajutie jambo gani?.

Ingekuwa jf ni wapiga kura, basi saa hizi Chadema ingekuwa Ikulu!. JF ina wanachama laki moja plus!. Hawa ndio Watanzania wote?.
ZZK bado ni maarufu vile vile tena umaarufu unazidishwa na hii Zitophobia kila siku thread 10 -10 za ZZK!.
P.
great thinkers 100000 sio kitu cha kubeza! Of course wapo mizigo wachache na pia wapo wazee wa vibahasha pia.
 
Ingekuwa umaarufu wake unatokana na kupigiwa vuvuzela, lisipopigwa ningekubali umaarufu wake ungeshuka, lakini umaarufu wa ZZK unatokana na ability!. Aombe msamaha kwa kosa gani, ajutie jambo gani?.

Ingekuwa jf ni wapiga kura, basi saa hizi Chadema ingekuwa Ikulu!. JF ina wanachama laki moja plus!. Hawa ndio Watanzania wote?.
ZZK bado ni maarufu vile vile tena umaarufu unazidishwa na hii Zitophobia kila siku thread 10 -10 za ZZK!.
P.
Mkuu kuna mamilioni ambao sio member humu na wanamchukia zitto kichizi mfano thread inaweza kuwa na member 20 lakini guest 1000 sasa huoni hiyo ni Noma
 
Zitto bomu, tumesema kitambo hapa.

Kwangu hakuwa na umaarufu husika to begin with, kwa hiyo hawezi kuurudisha.

Isitoshe, umaarufu si tija, hata Hitler na shetani (the character) ni maarufu.

Sema jingine.
 
​​Wanajamvi, sio kusudi langu kuingilia mtazamo wa mtu yeyote, ila kwa nia ya dhati na uelewa kuhusu uhuru wa kutoa maoni unaolenga kujenga na sio kubomoa, nimeona vema nitoe Ushauri kwa Mkuu Zitto na Kundi lake.

Nianze tu kwa kusema Ukishakataliwa na Jammiforums umekataliwa na jamii nzima ya watanzania na lazima mtu husika uwe makini na idadi ndogo (minor proportion) ya watu wanaoweza kukuhadaa eti wanakuunga mkono hapa jamvini kuliko wale wanaokupinga. Na hasa ukijua kuwa wanachama wa JF ndo wapiga kampeni huko mitaani kuhusu Chama na mwanasiasa binafsi (kumbuka hofu ya Pinda-CCM) juu ya JF.

Kwa kutambua mchango wako (Zitto), achana na hao walala hoi wanaojipendekeza, wakiwemo CCM wanaotaka kukutumia kama tissue, ningeomba haya uyafanye kutoka kwangu kama Mtanzania mpenda mabadiliko na mchukia wanafiki:
KWANZA; Ujutie kile ulichokuwa unakifanya maana huenda ulikuwa hujui ulitendalo.

PILI; Jishushe tu tuombe radhi Watanzania ambao kwa idadi kubwa ni wakulima na wafanyakazi na ambao tunaomba usiku na mchana kuona nchi yetu imekombolewa toka mikononi mwa CCM. Haimanishi ufanye mkutano wa hadhara lakini JF inatosha tu kutupa jibu nasi tutakurudisha kundini, maana kama nilivyo sema hapo juu; UKIKUBALIWA NA JAMIIFORUMS UMEKUBALIWA NA WATZ WOTE. Na kwa kinachoendelea ndani ya chama chako, ambacho umewahi sema huna mpango wa kukihama, onyesha ushirikiano na baada ya kuyamaliza huko ndo uje kwetu.

TATU; Baada ya hayo hapo juu kufanyika, tufichulie wote walioficha mpunga (fedha) huko Uswisi kama ulivyoanza vema na usikate tamaa. Na lazima hili lifanyike baada ya hayo hapo juu kwa sababu hili likitangulia bado halitakurudisha kwenye level yako ya awali. Hakika ukiyafuata haya na ukatuambia wezi tulionao nguoni mwetu tutakurudisha kwenye form fasta.

Ni mtazamo wangu wanajamvi.

Mkuu hapo kwenye Bolna Red unataka awafichue ili ufanayeje kama mtanzania??? Wengine wote waliofichuliwa ulichukua hatua gani??? By the way mbona ameshawataja kwa vyeo wewe umechukua hatua gani???

Tafakari kisha chukua hatua.
 
hapa unampigia mbuzi gitaa. Ilithibitika kwenye forum hii kuwa yeye ni mmoja wa wahusika, tena wahusika wengine ni jamaa zake wa karibu. Hii ilikuwa pri emptive move kudanganya watanzania
 
Mkuu hapo kwenye Bolna Red unataka awafichue ili ufanayeje kama mtanzania??? Wengine wote waliofichuliwa ulichukua hatua gani??? By the way mbona ameshawataja kwa vyeo wewe umechukua hatua gani???

Tafakari kisha chukua hatua.
Mkuu kutaja vyeo vyao, ndiyo kutaja majina yao?
 
Ingekuwa umaarufu wake unatokana na kupigiwa vuvuzela, lisipopigwa ningekubali umaarufu wake ungeshuka, lakini umaarufu wa ZZK unatokana na ability!. Aombe msamaha kwa kosa gani, ajutie jambo gani?.

Ingekuwa jf ni wapiga kura, basi saa hizi Chadema ingekuwa Ikulu!. JF ina wanachama laki moja plus!. Hawa ndio Watanzania wote?.
ZZK bado ni maarufu vile vile tena umaarufu unazidishwa na hii Zitophobia kila siku thread 10 -10 za ZZK!.
P.

Yes, uwezo wake unatokana na ability yake, lakini ability ipi? Kuwa kinyume na wenzake? Ability ya kuunda makundi na hoja ya kugawa watanzania kwa dini, ukanda, kabila na hata mikoa? Yes, ni zamu ya vijana na zamu ya kigoma kwani wao wanaweza.

A good thing about JF we easily expose our ideaologies and people we highly esteem. However your esteem to ZZK is contrary to your ideologies, but still he is and will remain a friend , come rain or sun
 
Zitto bomu, tumesema kitambo hapa.

Kwangu hakuwa na umaarufu husika to begin with, kwa hiyo hawezi kuurudisha.

Isitoshe, umaarufu si tija, hata Hitler na shetani (the character) ni maarufu.

Sema jingine.
Ganda la mua la jana, chungu aona kivuno!. One cannot be a hero to everybody!.
Shujaa wa mmija ni bomu kwa mwingine!.
Hata alichokifanya Osama huku wengine wakimlaani, kwa wengine ndie shujaa wao!.
Baba wa Taifa tunamuona ndiye shujaa wetu wa ukombozi dhidi ya mkoloni, wengine wanamlaumu mpaka kesho kwa kisingizio cha kuulea mfumo Kristo!.
Ukweli unabaki kuwa ZZK ni role model wa vijana kibao!.
P.
 
Ingekuwa umaarufu wake unatokana na kupigiwa vuvuzela, lisipopigwa ningekubali umaarufu wake ungeshuka, lakini umaarufu wa ZZK unatokana na ability!. Aombe msamaha kwa kosa gani, ajutie jambo gani?.

Ingekuwa jf ni wapiga kura, basi saa hizi Chadema ingekuwa Ikulu!. JF ina wanachama laki moja plus!. Hawa ndio Watanzania wote?.
ZZK bado ni maarufu vile vile tena umaarufu unazidishwa na hii Zitophobia kila siku thread 10 -10 za ZZK!.
P.

Yaani huwezi hata kuficha unafki wako
 
Ganda la mua la jana, chungu aona kivuno!. One cannot be a hero to everybody!.
Shujaa wa mmija ni bomu kwa mwingine!.
Hata alichokifanya Osama huku wengine wakimlaani, kwa wengine ndie shujaa wao!.
Baba wa Taifa tunamuona ndiye shujaa wetu wa ukombozi dhidi ya mkoloni, wengine wanamlaumu mpaka kesho kwa kisingizio cha kuulea mfumo Kristo!.
Ukweli unabaki kuwa ZZK ni role model wa vijana kibao!.
P.

Ukweli unabaki vijana kibao wanahitaji exposure. Kwa hiyo hata wengi wakiwa na role model wao mbaya, wingi wao haumaanishi kwamba role model ni mzuri. January Makamba alishawahi kuwabeza Watanzania kwa kukubali uongozi wa CCM kwa kunukuu msemo wa "A Million Flies eat shyt, they can't be wrong" sarcastically.

Tell me about merit for merits sake, don't justify merit by popularity.

Ukweli unabaki in the land of the blind the one eyed is king.

Ukweli unabaki, role models wa kweli hawajulikani, wanaojulikana si role models. Kwa sababu process ya kujulikana ilivyokaa inaua characters zote nzuri za role models. Regardless of party. Mi naona Mnyika anafanya mambo vizuri na ana discipline, lakini huwezi kusema ni role model kwa sababu sasa hivi kapewa kazi ya kuwa mouthpiece wa CHADEMA, na ku spin mambo kwa party line, tayari kashapata taint kwa lawyerly obfuscation. Angebaki grassroots activist huko Ubungo, labda angeweza kuwa role model, lakini angebaki huko tusingemjua nationally. A paradox.

Ukweli unabaki the whole idea of a role model is outdated and a top heavy, individual focused fantasy, we need to focus on the grassroots and ideals, not individuals.
 
Mkuu ni kweli ukikataliwa na Jf ndo umma umekukataa?
 
Back
Top Bottom