Je ni kweli 10% ya kwa vyama inatija?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Nimejiuliza sana na kutafakari maoni ya watu wawili ambao wote nawaheshimu kama wadau wenzangu japa jamii forums kwa muda mrefu na sio vizuri kukaa bila msimamo kwenye mijadala kama hii yenye tija.

Zitto anaweza kuwa sawa kwamba 10% ni muhimu kwa taifa letu kwenye kukuza demokrasia

Lakini P, naye anaweza kuwa sawa kwamba uongozi kwenye vyama vya siasa ni wakujitolea.

Mawazo yangu ni haya. Swali la msingi je tuko kwenye nyakati gani kwenye mfumo huu wa demokrasia mfano kwa demokrasia changa ambayo ndiyo inaanza Zitto yupo sawa kwamba ni muhimu kuwa na ruzuku ili tuweze kuibuia mawazo na kupata vyama vyenye ushawishi na matokeo yake kusaidia taifa. Lakini hatuwezi kuwa na mfumo wa ruzuku bila ukomo. Demokrasia ikikuwa na vyama vinatakiwa kupungua na ushindani ya kisiasa unatakiwa kuwa mkali
Zaidi na ndiyo maana nchi za demokrasia huwezi kuona vyama vinashinda kwa zaidi ya 60%.

Sasa ukweli ni kwamba Tanzania tayari tuna zaidi ya miaka 25 toka vyama vingi. Kwa mawazo yangu tatizo la Tanzania kwa sasa kubwa ni katiba na sheria nzuri na hakuna ushahidi kwamba idadi ya vyama inasaidia hili. Lowassa aliweza kupata kura karibu 40% na kwa mawazo yangu ingekuwa sasa angeweza kupata si chini ya 45% kwa mazingira kama yale kwa sasa. Hivyo Tatizo sio kukuwa kwa demokrasia lakini tatizo ni sheria mbaya za kukandamiza demokrasia. Demokrasia ikikuwa upinzani unakuwa karibu na 50%.

Pili sioni faida ya kuwa na idadi kubwa ya vyama Tanzania badala yake kuwe na vyama vichache vyenye nguvu na idara imara. Vyama vya kununuliwa au kutegemea ruzuku sana vimekuwa kero kwa demokrasia badala ya kuwa msaada.

Kwa tulipo kwa sasa na kufunguka kwa Watanzania kwa mawazo yangu Tanzania ingenufaika kama tungebaki na CCM, Chadema na ACT badala ya vyama ambayo havisaidii na mara nyingi vinatumia kama kukandamiza demokrasia.

Cha maana kubadilishwe sheria za kuchangia vyama bila kuogopa serikali. Vyama viruhusiwe kuwa na miradi au hata share kwenye makampuni.

Hivyo naungana na P kwenye hili kwa njakati hizi anachosema kina tija kuliko zitto ingawa Zitto ana nia nzuri na kwa njakati nyingine za huko nyuma angekuwa sawa. Nawaheshimu wote lakini kwenye hili nakubaliana na P lakini kuwe na sheria rafiki za kuchangia pesa vyama bila kutishiwa.
 
Pia sioni faida ya kuwa na idadi kubwa ya vyama Tanzania badala yake kuwe na vyama vichache vyenye nguvu na idara imara.
Idadi itapungua endapo ofisi ya msajili ingelikuwa makini katika kusoma mirengo ya vyama (ideologies) , maono ya vyama (vision) na malengo ya vyama (goals). Halafu ikawa inalinganisha, ili ikitokea Kuna chama kinakuja kujisajili lkn kina maono, mirengo na malengo sawa na ya chama kilichodajiliwa tayari kisisajoliwe.
 
Nimejiuliza sana na kutafakari maoni ya watu wawili ambao wote nawaheshimu kama wadau wenzangu japa jamii forums kwa muda mrefu na sio vizuri kukaa bila msimamo kwenye mijadala kama hii yenye tija.

Zitto anaweza kuwa sawa kwamba 10% ni muhimu kwa taifa letu kwenye kukuza demokrasia

Lakini P, naye anaweza kuwa sawa kwamba uongozi kwenye vyama vya siasa ni wakujitolea.

Mawazo yangu ni haya. Swali la msingi je tuko kwenye nyakati gani kwenye mfumo huu wa demokrasia mfano kwa demokrasia changa ambayo ndiyo inaanza Zitto yupo sawa kwamba ni muhimu kuwa na ruzuku ili tuweze kuibuia mawazo na kupata vyama vyenye ushawishi na matokeo yake kusaidia taifa. Lakini hatuwezi kuwa na mfumo wa ruzuku bila ukomo. Demokrasia ikikuwa na vyama vinatakiwa kupungua na ushindani ya kisiasa unatakiwa kuwa mkali
Zaidi na ndiyo maana nchi za demokrasia huwezi kuona vyama vinashinda kwa zaidi ya 60%.

Sasa ukweli ni kwamba Tanzania tayari tuna zaidi ya miaka 25 toka vyama vingi. Kwa mawazo yangu tatizo la Tanzania kwa sasa kubwa ni katiba na sheria nzuri na hakuna ushahidi kwamba idadi ya vyama inasaidia hili. Lowassa aliweza kupata kura karibu 40% na kwa mawazo yangu ingekuwa sasa angeweza kupata si chini ya 45% kwa mazingira kama yale kwa sasa. Hivyo Tatizo sio kukuwa kwa demokrasia lakini tatizo ni sheria mbaya za kukandamiza demokrasia. Demokrasia ikikuwa upinzani unakuwa karibu na 50%.

Pili sioni faida ya kuwa na idadi kubwa ya vyama Tanzania badala yake kuwe na vyama vichache vyenye nguvu na idara imara. Vyama vya kununuliwa au kutegemea ruzuku sana vimekuwa kero kwa demokrasia badala ya kuwa msaada.

Kwa tulipo kwa sasa na kufunguka kwa Watanzania kwa mawazo yangu Tanzania ingenufaika kama tungebaki na CCM, Chadema na ACT badala ya vyama ambayo havisaidii na mara nyingi vinatumia kama kukandamiza demokrasia.

Cha maana kubadilishwe sheria za kuchangia vyama bila kuogopa serikali. Vyama viruhusiwe kuwa na miradi au hata share kwenye makampuni.

Hivyo naungana na P kwenye hili kwa njakati hizi anachosema kina tija kuliko zitto ingawa Zitto ana nia nzuri na kwa njakati nyingine za huko nyuma angekuwa sawa. Nawaheshimu wote lakini kwenye hili nakubaliana na P lakini kuwe na sheria rafiki za kuchangia pesa vyama bila kutishiwa.
Asante sana Mkuu Kamundu , this is still debatable, thanks for standing by me.
P
 
Siasa ni sehemu ndogo tu ya kuendesha nchi.

Siasa ni sera tu, na hata Kama sera ni nzuri namna gani lakini mifumo ni dhaifu hakuna faida.

Mifumo ndio moyo wa nchi.

Sasa kupeleka 10% ya fedha kwenye siasa pekee badala ya kuimarisha mifumo na kufanya miradi ya kimkakati ni upunguani.
 
Sasa kupeleka 10% ya fedha kwenye siasa pekee badala ya kuimarisha mifumo na kufanya miradi ya kimkakati ni upunguani
Hii hoja ya 10% ya bajeti ya nchi iende kwa vyama mmeitoa wapi? Alichosema Zitto ni kwamba 10% ya ruzuku iende kwa vyama vidogo ambavyo havina wabunge, madiwani n.k ili visitegemee wenyeviti waliovigeuza mali binafsi kisa vyama viko hoi kifedha na havina sources of income.
 
Tanzania kuna vyama vingi sana na bado vinaendelea kuanzishwa, ushauri wake hauwezi kufanyiwa kazi.
 
Hii hoja ya 10% ya bajeti ya nchi iende kwa vyama mmeitoa wapi? Alichosema Zitto ni kwamba 10% ya ruzuku iende kwa vyama vidogo ambavyo havina wabunge, madiwani n.k ili visitegemee wenyeviti waliovigeuza mali binafsi kisa vyama viko hoi kifedha na havina sources of income.
10 % ya ruzuku??

Kwani utaratibu wa kutoa ruzuku ukoje??
 
10 % ya ruzuku??

Kwani utaratibu wa kutoa ruzuku ukoje??
Utaratibu wa ruzuku ni kura za ubunge na madiwani plus namba ya wabunge na madiwani. So vyama visivyo na wabunge au madiwani mfano CHAUMMA, UPDP,DP, Jahazi Asilia, APPT Maendeleo n.k havipati ruzuku.

Hoja ya Zitto ni kwamba umaskini wa hivyo vyama ndio unasababisha wenyeviti wa kudumu maana pesa yake binafsi ndio inaendesha chama.

Ndio ana suggest 10% ya ruzuku mfano kama ruzuku ni billion 10 kwa mwaka basi billion 1 igawiwe kwa vyama visivyo na wabunge/madiwani ili viwe na uhuru wa kiuchumi na visiwe vyama vya "mfukoni".

Ooh wait.... watu wataanzisha vyama ili wapate ruzuku? Yeye Zitto anasema masharti yawe ushiriki kwenye chaguzi mbili za kitaifa. Hii itazuia wajanja kufungua vyama kiholela.
 
Back
Top Bottom