Zitto Kabwe, Mbowe, Lissu hamuioni ripoti ya CAG?

JackisonDubai

JF-Expert Member
Mar 27, 2023
537
1,274
Ni masaa sSasa yamepita toka report ya CAG isomwe mbele ya Rais na kuibua madudu kibao lakini mpaka Sasa wanaojiita wachambuzi na wapinga ufisadi wa Serikali ya awamu ya tano wako kimya.

Twitter Zitto Kabwe yuko kimya kabisa au ndiyo kusema asali tamu sana?
 
Ni masaa Sasa yamepita toka report ya CAG isomwe mbele ya Rais na kuibua madudu kibao lakini mpaka Sasa wanaojiita wachambuzi na wapinga ufisadi wa serikali ya awamu ya tano wako kimya.
Twita Zito Kabwe yuko kimya kabisa ,au ndiyo kusema asali tamu sana?

Katatue matatizo yako uliyo nayo
 
Unataka waichambue kwa halaka au unataka waichambue, wape muda imeandikwa kitaalamu huwezi kuichambua kwakukurupuka.
 
Ni masaa Sasa yamepita toka report ya CAG isomwe mbele ya Rais na kuibua madudu kibao lakini mpaka Sasa wanaojiita wachambuzi na wapinga ufisadi wa serikali ya awamu ya tano wako kimya.
Twita Zito Kabwe yuko kimya kabisa ,au ndiyo kusema asali tamu sana?
Sikiliza wewe sisi ndio wataalamu
 
Ni masaa Sasa yamepita toka report ya CAG isomwe mbele ya Rais na kuibua madudu kibao lakini mpaka Sasa wanaojiita wachambuzi na wapinga ufisadi wa serikali ya awamu ya tano wako kimya.
Twita Zito Kabwe yuko kimya kabisa ,au ndiyo kusema asali tamu sana?
Huu ujinga ukiendelea hivi hatufiki.
Yote uliyosema yanapaswa kufanywa na wananchi. Wananchi wapaze sauti Kila Kona!
Vyama vya siasa vinatakiwa kuja na sera mbadala tena kwa maandishi na si porojo za mkumbo!
Tofauti na hapo vitaparamia hoja na vitaishia kutoa mawazo ambayo yatatumiwa na ccm kubaki madarakani!
Mawazo watoe wananchi. Vyama vije na sera mbadala (well thought after)
 
Ni masaa Sasa yamepita toka report ya CAG isomwe mbele ya Rais na kuibua madudu kibao lakini mpaka Sasa wanaojiita wachambuzi na wapinga ufisadi wa serikali ya awamu ya tano wako kimya.
Twita Zito Kabwe yuko kimya kabisa ,au ndiyo kusema asali tamu sana?
Mbona una haraka hivyo!? Ripoti kama hiyo inahitaji utulivu ili kuweza kuipitia na kuichambua vizuri.

Hebu na wewe tupe tathimini yako kuhusu ripoti hii na hayo ambayo unasema madudu kibao. Ila ni lazima utambue siyo kila ambacho kinaonekana kama kasoro katika sura ya awali ya "auditing query" humaanisha kuwa madudu yamefanyika.

Kasoro nyingine hutokana tu na kukosekana kwa viambatanisho husika katika kipindi ambacho ukaguzi wa kimehasabu unafanyika. Kasoro kama hizi huja kufutwa baada viambatanisho hivyo kutolewa.

Kwa hiyo mtu makini ni lazima avute subira mpaka kasoro zilizoainishwa na wahusika watakapopata wasaa wa kurekebisha kasoro zilizoibuliwa wakati wa uchunguzi wa kimahesabu zitakapopata majibu. Zile ambazo hazitapata majibu ya kuridhisha ndizo hasa zinapaswa kuitwa madudu.
 
Back
Top Bottom