Zimbabwe Election: Progress & Results


Kuna watu watakwambia hiyo yote ni kwa ajili ya UK na USA!!
 
Nyani Ngabu,
Zimbabwe was OK yaani walikuwa vizuri kiuchumi hadi mwaka 2000 pale Mugabe alipochukua ardhi za wazungu... Hilo ndio kosa kubwa la Mugabe kulingana na mtazamo wa nchi za magharibi yaani Mugabe ni racist kinamna bila kujali kwamba hao wazungu walishika asilimia 70 ya ardhi yenye rutba.
Tatizo jingine ambalo nimekuja ligundua ni kwamba siku zote mazao yote ya chakula Zimbabwe yalikuwa yakitokana na modified seeds toka South ambazo tayari zilikwisha badilisha rutuba ya udongo kiasi kwamba huwezi kupanda mbegu nyingine yoyote ile ikaweza kuota vizuri...Hivyo wamekwama hata kwa chakula.
Waswahili akina ndivyo tulivyo hawana access ya mbegu hizo isipokuwa kupitia kwa Kaburu ambaye ndiye kachukuliwa ardhi na kibaya zaidi ni vikwazo walivyopewa Zimbabwe kiuchumi kiasi kwamba mimi binafsi nilitaka kununua kitu toka Zimbabwe nilikataliwa na benki ya hapa kuwa hakuna business transaction yoyote inayoruhusiwa na Zimbabwe.
Kwa hiyo mkuu unaweza pima hawa jamaa zetu walipo simama na tatizo kubwa naloshindwa kuelewa ni kwamba hata huyo Simba akichukua je atarudisha ardhi kwa wazungu?...na akikataa hivyo vikwazo vitakwisha kwa sababu Mugabe hayupo madarakani!
Nikikumbukia Cuba Marekani walisema akiondoka Castrol wataweza kurudisha uhusiano wao na Cuba lakini kilichotokea ni kwamba sababu mpya zimevutwa kuhusu mdogo wake kuwa hawa ni ndugu..Kwa hiyo kazi sii ndogo hata kidogo...
Nikirudi ktk swala la Wazimbabwe mkuu hakuna haja ya kuwaonea huruma kwa sababu FMES kesha sema viongozi wetu ni reflection yetu sisi, hivyo kuna kina Mugabe kibao wamejaa Zimbabwe, hawakubaliani na matakwa ya nchi za magharibi...PIGA, UA.
Na ndio sababu kubwa inayompa kura.. hawa jamaa zetu ni maskini jeuri kama Mugabe mwenyewe!
 
Mimi bado naamini kuwa Mugabe atashindwa hapo kesho.... Kinyume cha hapo inabidi Kikwete ajiandae.....

I beg your Pardon!!!
Mw.WK,Could you please Re-phase that Statement:-"Mimi Bado naamini kuwa Mugabe atashinda hapo kesho...na inabidi Kikwete ajiandae kwenda kwenye Sherehe za kuapishwa kwake"

**That's African Rulers for You!!
 
I beg your Pardon!!!
Mw.WK,Could you please Re-phase that Statement:-"Mimi Bado naamini kuwa Mugabe atashinda hapo kesho...na inabidi Kikwete ajiandae kwenda kwenye Sherehe za kuapishwa kwake"

**That's African Rulers for You!!

Mimi naweza kukubaliana na MwK maana jeshi liko tayari kuua watu wakishinda na kuwaua pia wakiingia mtaani kama Kenya .
 

Kitila usisahau wizi wa kura pia ambao sasa hivi unashamiri katika nchi nyingi duniani hata za Magharibi. CCM wameshaiba chaguzi. Kenya uchaguzi wao wa December, 2007 pia kulikuwa na wizi wa kura ambao ulisababisha maafa makubwa katika nchi hiyo, Kichaka mwaka 2000 na 2004 aliiba kura pia katika uchaguzi wa Marekani. Hivyo tusishangae pia kuona Mugabe anaiba kura ili aendelee kuwa madarakani.
 
Habari za uhakika kutoka kwa observours wamekuta majina ya wapiga kura 8000 kwenye kituo kimoja ambayo ni ya uongo.



Ukitaka kujua jinsi Mugabe alivyoiharibu Zimbabwe ni lazima uelewe jinsi alivyoingia madarakani, jinsi alivyoua wale ambao walionekana ndio wangechukua ukanda na baada ya kupata, jinsi alivyoendelea kuua hususan Matebeleland. Atakaa kwenye madaraka kwa njia yoyote ile hadi afe. Hawezi kuachia Madaraka hata akishindwa kura. MARK MY WORD.
 

Asante kwa ukweli ulioandika. Waafrica wengi tunasahau asili yetu haraka sana na hasa baada ya kuishi nje ya nchi aka ulaya na marekani kwa muda mrefu.

Ukoloni mambo leo bado upo duniani hivyo ni muhimu sana kuwa makini na hawa watu wa mataifa ya magharibi ambao kila kukicha wanatafuta mbinu mpya ya kutuibia na kuhamisha mali na utajiri wetu.
 

Watanzania wangapi wanazamia Africa kusini kila siku? Watanzania wangapi wanakosa hata mlo mmoja kwa siku?.Kwa kuwa wewe upo hapo unabofya ki-board unafikiri watanzania wenzako pia wana maisha mazuri? maana angalau wewe kama umeweza kubofya kiboard lazima uhakika wa mlo mmoja unao.

Leo hii Tanzania ni tegemezi kwa zaidi ya 40% katika bajeti tu mbali na misaada mingine kupitia taasisi zisizo za kiserikali je hao jamaa leo wakikata misaada unafikiri hii Tanzania itakuwaje? jibu unalo itakuwa mbaya kuliko Zimbabwe ingawa hapa Mugabe hayupo.

Matatizo ya Zimbabwe hayawezi kuondoka hata kama Mugabe akiondoka mpaka hao makaburu wapate wanachotaka maana yake ni kwamba hao wazimbabwe waendelee na utumwa kwenye mashamba ya wazungu ndiko wanakostahili na sio wao kumiliki ardhi.

Kuna mtu anasema Mugabe ni racist,si kweli suala la ardhi ni makubaliano ya siku nyingi kati ya Uingereza na Zimbabwe,serikali ya Uingereza ilitakiwa kutoa fedha za fidia kuwafidia raia wake walioko Zimbabwe ili ardhi igawiwe kwa Wazimbabwe wasio na ardhi lakini Waingereza wamekuwa wanapiga chenga tangu mwaka 1980 hadi mwaka 2000 Mugabe alipoamua kufanya kweli.

Matumaini waliyonayo Waingereza ni kuwa wakifanikiwa kumtoa Mugabe wakaweka mtu wao tatizo la ardhi litaisha,hawatalipa fidia na ardhi wataendelea kuimiliki.

Nawaombea wazimbawe maana wanapita wakati mgumu lakini heri yao maana mwishowe watapata suluhu ya matatizo yao wakati sisi tutaendelea kuwalamba miguu wazungu wakishirikiana na viongozi wetu kutufisadi
 
Kuna watu watakwambia hiyo yote ni kwa ajili ya UK na USA!!

Uchumi mzuri ni neno tata.Hapa JF kuna nchi iliongelewa nafikiri ni Equetorial guinea kuwa na GDP ya dola 30,000 lakini watu wake wanaishi katika umaskini wa kutupa.Juzijuzi tulikuwa tukisikia pongezi kwa Tanzania kuwa uchumi unakua kwa 7% lakini ukienda kwa Wananchi unakuta umaskini umeongezeka.
Sasa unapozungumzia Zimbabwe kuwa na uchumi mzuri wakati 70-80% ya watu wake hawana ardhi wote hao ni peasants kama walivyo watanzania wengi ni lazima uwe mwangalifu.
 

Kula tano za chapchap...
Kuanguka kwa Mugabe itakuwa ni ushindi wa hypocrisy za UK na Marekani.Watu wengi hawaangalii issue ya Zimbabwe from both sides.
Mugabe kabla hajagusa interests za UK( kwa kuwanyang'anya mashamba wazungu)aliitwa kiongozi safi na mtu ambaye anajua kuleta maendeleo nchini mwake.Ila tu alipothubutu kuchukua mashamba yale ndipo alipoanzwa kupachikwa kila aina ya majina na isitoshe UK na Marekani zikaanza kupeleka mabilion ya pesa kwa wapinzani ili kuungusha utawala wa Mugabe.Na Mugabe alipoamua kupambana ndipo UK na mshirika wake Marekani wakatangaza vikwazo vya kiuchumi na pia kuwashurutisha EU kufuata mkondo.
Ni lazima tutambue kuwa vikwazo vya kiuchumi siyo lelemama! ndiyo hasa vinavyosababisha uchumi kudorora siku hadi siku! na ndiyo maana Marekani na washirika wake wanataka pia Irani iwekewe vikwazo vya kiuchumi ili kulidhibiti taifa hilo la kiislamu.
Sasa basi tujiulize nini kwanini Zimbabwe na siyo DRC? maana kila kukicha watu wanauliwa DRC na hatusikii lolote toka kwa Marekani na mshirika wake UK..au ni mimi tu ndiye ninayeona kuwa demokrasia pia inahitajika DRC na tena muda huu!! Hii inatoa jibu kuwa demokrasia inayopigiwa mbiu na UK na Wamarekani huwa tu pale interests za wazungu zinapoguswa na si vingenevyo!.
Leo hii kama unabisha jaribu kupeleka mabilion ya pesa kwa watu weusi walioko UK na Marekani ili kuwamobilize kuziondoa serikali hizo madarakani uone jinsi nchi hizo zitakavyo react kwa nguvu zote za dola!! na tena pengine kufungua guantanamo nyingine!
Kumbe basi tunapata jibu kuwa Mugabe yuko vitani...anapambana na hizi sera potofu za UK na Marekani za kuwakandamiza watu weusi kwa kuwanyima haki zao za kumiliki ardhi na mali kama wazungu au watu wengine.

-Wembe
 
Zimbabwe in cross-road

 


Mimi nasapoti kabisa kitendo cha Mugabe kugawa ardhi kwa kwa waafrika.Asilimia 80 ya ardhi katika nchi yoyote ile haiwezi kuwa chini ya minority 2 % ya population.Kwa wale ambao wanabisha angalia southafrika, land reform yao inaenda polepole sana,na mkisikia kunawaka moto msishangae.

Hata hivyo nafikiri Mugabe sasa inabidi apumzike.He has done the dirty work,and land reform is irreversible, lakini ni bora sasa hivi awaachiwe vijana kama simba makoni waendeleze pale alipoacha, hasa uchumi.
 

Nyani:

Swali lako ni la msingi sana. Laiti kama tungepata jibu la swali hilo, tungeweza kuelewa ni kwa nini Zimbabwe ilivyo hivyo leo.

Mimi sina jibu, lakini ngoja nijaribu kutoa changamoto fupi, labda itatuelekeza kwenye wenye majibu.

Kwanza, chukua mfano wa Tanzania kabla ya Azimio la Arusha. Tunafahamishwa kuwa uchumi ulikuwa ni mzuri tokea 1961 na miaka iliyofuata. Tulikuwa na ushirikiano mzuri tu na mataifa yote ya kibepari - hususani watawala wetu Uingereza, Marekani na wengineo. Kutaifisha mali za mabepari, nia ikiwa ni kuwanufaisha raia walio wengi maskini hakukumpa Nyerere sifa; na tokea hapo inaelezwa kuwa uchumi wetu ulianza kuporomoka hadi leo hii.

Pili, angalia mfano wa Kenya. Wao hawakuwabughudhi mabepari - hasa hasa walowezi waliokuwa na mashamba makubwa ya Chai, wenye viwanda, makampuni ya utalii, mabenki, n.k; wengi wa hawa wakiwa ni raia wa Uingereza. Wananchi wachache, hasa waliokuwa kwenye siasa wakajichukulia ardhi nyingi iliyokuwa imerudishwa kwa kulipiwa na serikali ya Uingereza, (hii ni tofauti na yaliyotokea Zimbabwe). Kwa hiyo hapa hapakuwepo na matatizo tunayoyaona Zimbabwe leo. Kwa vile viongozi wa Kenya waliamua kufuata amri za wakubwa hukusikia na hutasikia kelele hizo kutoka Uingereza au Marekani. Hata hivyo, kuwaridhisha wakubwa bila ya kuwanufaisha wenye nchi, matokeo yake ni hayo tuliyoyaona juzi baada ya uchaguzi.

Tatu, Zimbabwe kabla ya mashamba ya wazungu kuchukuliwa, hapakuwa na matatizo makubwa kiuchumi, na wala Mugabe alikuwa haonekani kuwa shetani mkubwa, pamoja na kwamba hali ya wananchi wa kawaida ilikuwa siyo ya maendeleo makubwa. Ahadi zilitolewa kabla ya uhuru, kwamba Uingereza ingetoa pesa kulipia mashamba ambayo yangekuwa yananunuliwa toka kwa wazungu ili wananchi nao wapate ardhi. Uingereza hawakutimiza ahadi hii; na Mugabe akaamua kuanza kuwashughulikia. Hii ilikuwa ni ahadi ya wapiganaji wa ukombozi kwa wananchi wao, kwa hiyo ililazimu waitimize.
Mugabe alipofanya haya, akawa shetani.

Hitimisho:Naomba niazime msemo wako - 'Ndivyo Tulivyo.'
Naomba unielewe kwa nini nasema hivi, pamoja na kwamba sikubaliani na msemo huo:

1. Nyerere alipotaifisha viwanda na kujenga vingine vingi na vizuri tu: Mwatex, Mutex, Moshi Machine tool; Ubungo farm implements; Morogoro Canvas; Mang'ula Machine tool; Mbeya Paper; Urafiki Textiles; Twiga Cement; Tanga Fertilizer; Kioo; Tanga Cement, n.k.
Tazara ikajengwa, Kilimanjaro International Airport,n.k. Mmmmh niendelee mpaka wapi?
Ndivyo Tulivyo- nikiwa na maana ya kwamba baada ya Mugabe naye kuchukua mashamba ya wazungu, waliogawiwa mashamba hayo hawakuwa na uwezo wa kuyatumia kama hao walionyang'anywa, kwa sababu mbalimbali, baadhi yake zikiwa za 'Ndivyo Tulivyo," na baadhi ya sababu zikiwa nje ya uwezo wa Zimbabwe- kwa mfano kuhujumiwa na wakubwa ikiwa pamoja na kuwekewa vikwazo.

Nikirudi Kenya - kwa vile walioshikiria uchumi waliendelea kuwa wale wale, hapajatokea msukosuko kama Tanzania na Zimbabwe walivyo.

Ndivyo Tulivyo?- unataka kufanya majaribio Nyani? Mwambie Mbeki au Zuma awavuruge wazungu pale kwao leo hii, halafu tukutane miaka miwili ijayo tuelezane matokeo.

Matokeo tunayoyaona Zimbabwe na Tanzania, lakini sio Kenya wala Afrika Kusini - Yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na sisi wenyewe wananchi kwa (Uhujumu wetu? au kutokuwa na uwezo kuendesha mambo yetu, kama uchumi vizuri. Matatizo yanazidi kuwa makubwa tunapoanza kutumiwa kama mifano na hao wakubwa, huku wakitumia kila hila tuonekane kuwa hatuwezi.

Kenya wakianza kugusa maslahi ya wakubwa, tutakuwa nao pamoja.
 
Kalamu umeniacha hoi kichizi ndugu yangu...
Ndio bana nataka nifanye majaribio kama kweli ni Ndivyo Tulivyo au la...?

Hivi uchumi wa Afrika Kusini sasa hivi ukoje ukilinganisha na enzi za kabla ya utawala wa walio wengi?

Kinadharia tu...tuseme leo hii Mbeki anawatimua wazungu na kuwarudisha kwa Uholanzi au popote walipotokea...je Afrika Kusini itaendelea kuwa economic powerhouse?

Kati ya Afrika Kusini na Nigeria ni ipi yenye maliasili nyingi na ipi imeendelea kuliko nyenzake?

Na kuna mtu humu ndani anayeamini kuwa Afrika Kusini bila kuwepo na wazungu ingeendelea kama ilivyoendelea hivi sasa?
 





Do you wanna fight?



Will Zimbabwe be free of Robert Mugabe? Stricken nation reaches polling day
 

By the end of the day some results will come out.
 
Wana-JF,
Hatima ya Zimbabwe ipo mikononi mwa wananchi wa Zimbabwe wenyewe, wana haki ya kumchagua yeyote yule ambaye wanamtaka, hata kama ni Robert Gabriel Mugabe. Yanayotokea Zimbabwe chanzo chake wote tunakijua ni ubeberu wa nchi za Magharibi dhidi ya rasilimali za nchi ya Zimbabwe. Mugabe alikuwa amefikia mahali ambapo mikuki miwili imeelekezwa kwake. Mkuki wa kwanza alitakiwa akubaliane na matakwa ya nchi za magharibi au akatae na kutekeleza matakwa ya wananchi wake. Alichokifanya Mugabe ni kuwakatalia 'wakubwa' na kujali maslahi ya wananchi wake kwa kugawa ardhi iliyokuwa inamilikiwa na weupe wachache.

Namalizia kwa kusema kuwa 'kitanda usichokilalia huwezi kujua ubaya wa kunguni wake'.

Wazimbabwe kama Mugabe anawafaa, tafadhalini mrejesheni madarakani na nitawapongeza kwa hilo kwani haki yenu ya kidemokrasia kumchagua yeyote mnayemtaka bila ya kulazimishwa na nchi yeyote.
 


Kaka, ubaya wa Mugabe sasa hivi huko Zimbabwe hauhitaji kuhubiriwa na US au UK. Kila mzimbabwe anaujua isipokuwa aliye waziri wa serikali ya Mugabe na familia na ndugu zake wa karibu sana. Hebu jaribuni kuongea basi na hata wa Zimbabwe; piga simu kwa mtu yeyote ZImbabwe. Uzuri kupiga simu Zimbabwe ni very cheap.

Jamani, tutaacha lini kuwalaumu wazungu kwa matatizo yetu? Halafu hawa wazungu kwa nini wanakuwa wabaya tu pale wanapotukosoa lakini hatuachi kutega mikono yetu kwao? Haya mashamba aliyoyachukua Mugabe aliyapeleka wapi? Kwa nini uzalishaji ulishuka? Kwani hawa US na UK walienda huko wakawataza wananchi wasilime? Hawa US na UK ndio wamepeleka njaa Zimbabwe? Hivi, ni hawa US na UK wanaomwambia Mugabe awape waduasi wake tu mahindi na awanyime wale ambao wanampinga? Hivi ni US na UK waliowaambia wananchi wamchukie Mugabe? And, kwa nini ni Mugabe, ina maana hakuna mtu mwingine anayekubaliana na sera za chama chake na anayeweza kuzisimia zaidi yake? Kwa nini mtu mmoja aruhusiwe kuiharibu nchi nzima kwa kiasi kile kisa aliwanyang'anya wazungu mashamba? I mean, kwa nini hata sisi ambao tunafikiri ni kizazi kipya katika bara letu tunashindwa kukubali kuwajibika kwa kushindwa kwetu kutekeleza wajibu wetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…