Zimbabwe Election: Progress & Results

Mugabe ni kiongozi ambae kwa kweli sitmuonea aibu usoni mwake iwapo nitaonana nae ! Nina guts kweli kweli juu ya huyu mzee !

i cant even put words into sentences maana nina mengi ya kusema juu ya huyu mzee !

Acha unafiki we kijana. CCM ifanye madudu unasema sawa leo Mugabe unasema hutamwonea aibu kwa lipi tofauti na CCM??
 
KWA KWELI MAONI MENGI YAMETOLEWA KUHUSU ZIMB.....YANGU NI HAYA......!
ZIMB NI NCHI HURU NA INAFANYA UCHAGUZI WA KIDEMOKRASIA......!
DEMOKRASIA KTK UCHAGUZI NI KUKUBALI MATOKEO NA SIO PALE TU UPANDE MMOJA UNAPOSHINDA...UPANDE HUO UKUSHINDWA UTASIKIA UTASIKIA UCHAGUZI HAUKUWA HURU NA HAKI.......!
WAZUNGU HUTAKA KUONGOZA KWA REMOTE(puppet leaders/regimes),IKITOKEA UKAWA AGAINST NAO WEWE UTAKUWA HUFAI,ADUI,DIKTETA(they will call you names)........!
HIVI HATUSHANGAI KWA NINI WAZIMB WENYEWE BADO WAPO NA ZANU-PF?SHUTUMA NYINGI ZINATOKA NJE YA ZIMB NA SIO NDANI TOFAUTI NA NCHI NYINGI......!(ukikuta shutuma za ndani ya zimb ni zile za vibaraka wachache)......!
AFRIKA INATAKA WATU KAMA MUGABE.....(sio viongozi yes boss)....WENYE KUJUA KUWA UINGIREZA IAMUE MAMBO YAKE,NA ZIMB NAYO IAMUE MAMBO YAKE......! SIO SYSYTEM YA CHAKO CHANGU CHANGU CHANGU......!
I HATE MUGABE....BUT I LOVE HIS POLICIES......!SIPENDI MUGABE AONGOZE ZIMB LAKINI KWA CANDIDATES WALIOPO MUGABE ASHINDE.....BTN THE TWO EVILS...CHOOSE THE LESSER....."
 

Ninakubaliana na kukuunga mkono kwa yote isipokuwa hayo niliyoyapa wino mwekundu.
Mimi pia namkubali Mugabe lakini ni vizuri pia akaelewa busara na ujanja wa karne yake imepita, hana nafasi tena kishafanya mazuri,inabidi aiachie damu changa.Akina Nyerere na Mandela walipoamua kuachia ngazi, si kuwa walikuwa wajinga lakini waliona wazi kuwa Dunia ya sasa ni tofauti na ile ya wakati wao. Kati ya watu Milioni 13 siamini kama Mugabe pekee ndo kichwa, na kuwa ndo pekee mwenye mbinu barabara za kupambana na Westerner.Mugabe ana msimamo mzuri lakini hana akili ya kubuni mbinu muafaka na bora zinazoendana na karne hii. Ukosefu huo wa busara ndo unaosababisha nchi ya Zimbabwe kuwa hoi.

Kulazimisha kushinda, kwa kuandikisha watu na vituo hewa ni kuwanyima Wananchi wa Zimbabwe haki ya msingi ya kufanya maamuzi yao kwa njia ya kura.
 
Bongolander, hata yule adversary wa Mugabe marehemu Smith yupo kwenye register book, halafu tukiambiwa sisi tuna matatizo tunavimba!

Kweli Kitila inasikitisha sana, wakati mwingine naona wasio na akili ya kujua haya wananafuu. Kwa sababu ukiwa na akili ya kujua mabaya na yanayokudhalilisha yanakuumiza, lakini kama huna akili ya kuyajua unaona poa tu. Lakini ajabu ni kuwa kuna wengine naona hata Mugabe mwenyewe anaowaona kuwa ni wajinga. BOB amekwisha kabisa he is no use to anyone, except washikaji zake kama 100 hivi.
Kibaya zaidi ni kuwa ni sisi watanzania tuliomwingiza madarakani.
 
Wakimbizi wengi wa Zimbwabwe na hasa ambao wapo ulaya pamoja na kumchukia Mugabe, wanapenda ashinde ili waweze kuendelea kuwa wakimbizi...

Mkuu,

Lakini usisahau kwamba wazim wengi waliopo Ulaya wataalam mbalimbali kama madaktari na manesi ni wengi sana na walikuja kwa vibali kufanza kazi.

Halafu kuna wanafunzi wengi ambao walikuja wakati Zimmbabwe haijawekewa viza (hao ndio wengi.)

Na mwisho ndio wakimbizi ambao walikuja baada ya Zimbabwe kuwekewa viza na kushindwa mambo mengi.

Unajua huyu jamaa alisomesha sana wazimbabwe na matokeo yake amebaki na wajinga ambao hawaelewi nini haki zao na namna ya kuchambua kati ya politiking and it manipulation na real democracy na fair elections.

Mugabe anajaribu kuwapiga mkwara wananchi kwamba wasipomchagua atawanyima chakula, huu ni uungwana kweli!
 
Mahesabu,
Tatizo la Zimbabwe hata kama mimi ningekuwa mwananchi wa nchi hiyo sijui kura yangu ningempa nani!..
Wagombea ni BOMU, kila mmoja wao ana matatizo yake na yule aliye bora zaidi huyo SIMBA hana nafasi kabisa ya ushindi kutokana na chama chake kutokuwa na mvutio kwa wananchi yaani hakijulikani nje ya miji mikubwa ya Harare na Bulawayo...
Hili neno Demokrasia na tafsiri zake bado kabisa haliingii akilini.. Utata mkubwa unakuja pale kamati kuu ya chama inapoteua mgombea bila wananchi wanachama wa vyama hivyo kushirikishwa kumchagua mgombea kwa tiketi ya chama. Na utaratibu huu unanipa shauku ya kuuliza hivi kweli nini hasa maana ya Uanachama ikiwa uchaguzi wa mgombea hutolewa na watu wachache kisha mnasisitizwa kumuunga mkoni ktk uchaguzi mkuu hata kama wananchi sii chaguo lao la kiongozi ndani ya chama chao. Lini wananchi wananchama wa tuseme CCM walipewa nafasi ya kumchagua kiongozi wa chama chao?..
Nadhani taratibu za uchaguzi wa viongozi wetu ngazi za rais inabidi ubadilishwe kabisa..
Pili, hili swala la kiongozi kama Mugabe kutunga sheria ya kumwezesha tena kugombea Urais ni Udikteta wa hali ya juu sana kwani nina hakika wapo watu ndani ya ZANU PF wenye msimamo kama wake isipokuwa wanaweza kuwa na mbinu tofauti na safe kulinda Uhuru wao wanapo deal na wazungu. Haiwezekani kuwa yeye tu ndiye mwenye msimamo thabiti.
 
Vote-counting procedure


Four million Zimbabweans living outside the country are not allowed to vote. (Hiyo ni approx. asilimia 25% ya population ya Zimbabwe.



Kwa mpango huu naona Robert atakuwa na kazi kubwa ya kuiba huu uchaguzi ingawa turnout siyo kubwa kama wengi walivyotegemea.
 
Sasa mimi ndio najiuliza, sisi wabongo (Waafrika) tuna matatizo gani hasa kwenye mambo haya ya kuchaguana?

Je, tunahitaji nadharia (theories) maalumu kwa ajili ya kuelewa siasa za Afrika?

Kitila,

Ndivyo tulivyo..Que Sera Sera!
 



Queues formed early at many of Zimbabwe's polling stations as
Robert Mugabe, in power since 1980, faced his most serious
electoral challenge in years.






Dzingai Karidza, 46, cast his vote in Highfields Township,
the heartland of nationalist politics in Zimbabwe.






Zimbabweans have become accustomed to waiting in line -
facing food shortages and hyperinflation in recent years.






Mr Mugabe is standing for his sixth term in office at the
age of 84 as his country's economy reels.





Veteran opposition leader Morgan Tsvangirai
is challenging Robert Mugabe again.





This vote has added interest because a former Mugabe ally,
Simba Makoni, is now also standing against him.





On the eve of polls, cameras recorded Zimbabweans illegally escaping
into South Africa from their troubled homeland.






Hundreds of people attempt to cross the border
each year in a desperate bid to escape Zimbabwe's woes.

Pictures Credit: BBC News
 
Pole pole watu wataanza kuelewa kuwa ndivyo tulivyo!!!
 
Pole pole watu wataanza kuelewa kuwa ndivyo tulivyo!!!

Acha utani bana! Kwani unafikiri hawalijui hilo?

Wengi hapa ni porojo tuu..but deep down we know Mugabe is just a garbage..useless animal! Zimbabwe is bleeding than hell!
He has taken the whole nation at Ransom. We all know!

Bwana waafrika ndivyo tulivyo! Tutaenda wapi, kelele nyingi..but ukweli tunaujua kuanzia vijijini kwetu tunakotoka mpaka huko majuu mliko! ukweli upo na mnauona......

Mi nadhani hata wazungu tuwalaumu kwa kutuambia kwamba definition ya democracy ni moja world wide..nadhani inabidi kila nchi/bara iwe na standards zake..especially Africa. Tujue kabisa kwamba we are unique....
 
Kweli bana nadhani wengi wetu deep down ukweli tunaujua lakini tupo kwenye denial tu!!
 
..binafsi napenda kuona Simba Makoni anashinda uchaguzi huu.

..kwasababu hana chama basi kuna uwezekano mkubwa akaleta usuluhishi, umoja, na mshikamano, Zimbabwe.

..i am tired of MDC vs ZANU bickering.
 
Mimi nimechoka kuona Wazimbabwe wakihangaika kimaisha! Kuna mtu kabandika picha hapa ya mama na mwanae wakivuka mpaka wenye barbed wire kwenda Afrika Kusini...Jamani huyu Mugabe mwenye miaka 84 bado anataka kuwa raisi kwa nini? Na kwa nini watu wamchague....aaaghhh yaani hawa Wazimbabwe wangekuwa wanafikiria kama mimi maisha yao yangekuwa na nafuu kushinda yalivyo sasa chini ya Mugabe
 
Nyani Ngabu,

..tuko pamoja. Zimbabweans should give this Simba guy a chance.

..lakini nilipomuangalia Mugabe nimeona kama wamefanana na huyu wa kwetu Mizengo Pinda. Lakini at 84 Mugabe anaonekana yuko fiti zaidi. sijui kama wewe mwenzangu umeliona hilo.
 

Yaa Mugabe naona ana genetics nzuri maana kama kwa umri wa miaka 84 ameweza kuhimili mikikimikiki ya kampeni basi jamaa yuko fit!!

Na kweli kuna resemblance flani hivi na Pinda...
 

Nafikiri tofauti ipo kichwani maana pamoja na matatizo yote Mugabe ukimpa nafasi ya kuongea anaua, ila huyo wa kwetu uhuuu!

Makoni ni distractor hawezi kushinda. Isitoshe hatujui hasa anasimamia nini maana kaingia juzi kwenye kinyang'anyiro. Wengine wanasema alitumwa ili aharibu vote za MDC, lakini inasemekana baada ya kuanza kampeni akawa anaharibu zaidi za Mugabe. Sasa huyu ni spoiler tu, usitarajie atapata kura za maana. Morgan amepambana sana na kwa kweli amekuwa akishinda. The guy is so resilient and I admire him for that.

Sasa NN, hiyo nani yako ya ndivyo tulivyo, tunatakiwa tuifanyie kazi, tusikubali tu kwamba basi kwa kuwa haya majamaa ya CCM na ZANU-PF yanafanya yanavyofanya basi tubaki hivyo hivyo tu. We can decide to be part of the struggle rather than to just wait for success to fall freely from heaven, which is unlikely to happen!
 
Hivi nani anaweza kuelezea kuanguka kiuchumi kwa Zimbabwe-kutoka ilivyokuwa chini ya wakoloni hadi walipopata uhuru na miaka michache baada ya uhuru na ilipo sasa bila ya kurudi kule kule kwa Waafrika Ndivyo Tulivyo? Yaani hawa Waafrika walipochukua madaraka wameichukua Zimbabwe kutoka moja ya nchi zenye uchumi mzuri Afrika na kuipeleka kuwa moja ya nchi vichekesho na sasa wameifikisha kuwa moja ya nchi zinazotia huruma duniani. Jamani nani anaweza kunieleza nikaelewa hii safari ya kinyume nyume?
 

Kaka, kweli Mugabe ana mdomo! Kwa hilo tu namvulia kofia. Lakini kama nisemavyo kila siku humu maneno yasiyoambatana na vitendo ni sawa na upepo tu.

Pia nakubaliana na wewe kabisa kwamba tusibaki hivyo hivyo tu bila kufanya kitu. Ugumu unakuja pale ambapo nyie mnaotaka kufanya kitu mnapojikuta mko wachache. Hebu chukulia huyu Mugabe...amekuwa madarakani miaka 27 au 28. Uchumi/ hali nzima ya Zimbabwe inatia huruma. Nini atakachokifanya huyu Mugabe sasa hivi kubadilisha hiyo hali kama alishindwa kwa miaka yote hiyo? Lakini pamoja na kushindwa vibaya kuitawala hiyo nchi lakini eti kuna mijitu bado inamuunga mkono. Where is the common sense...? It is not complicated at all to figure out that this guy can't do jack....it's time for change. He doesn't deserve another term let alone the nomination....What are these people expecting from him...especially those who support him?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…