SoC03 Zijue taratibu za kisheria katika kudai malipo kutoka kwenye kampuni ya bima baada ya kumpoteza ndugu kwenye ajali

Stories of Change - 2023 Competition
May 9, 2023
18
13
UTANGULIZI
Tumekuwa tukishuhudia ajali nyingi nchini Tanzania zinazokea mara kwa mara ambapo kupitia ajali hizo wapendwa wetu huweza kupoteza maisha, wengine huweza kupata vilema vya kudumu. Jambo la kusikitisha wengi wetu hatuna elimu au uelewa wa kisheria kuhusu hatua zipi zichukuliwe na mhanga wa ajali baada ya kumpoteza ndugu yake kwenye ajali iliyosababishwa na vyombo vya moto. Hivyo kupitia jukwaa hili napenda kuuelimisha umma iwapo ndugu, jamaa, na rafiki akiwa mhanga wa ajali basi afuate utaratibu wa kisheria ambao nimeueleza kupitia jukwaa hili.

Malipo ya bima baada ya ajali;
Huusisha fidia kwa mhanga aliyepata ajali iliyosababishwa na chombo cha usafiri ambacho kimekatiwa bima. Malipo hayo yanaweza kuwa fidia kuhusu gharama za matibabu, gharama za mazishi n.k.

KESI ZINAZOHUSIANA NA MADAI YA BIMA YA AJALI YA BARABARANI
Inapotokea ajali barabarani anayewajibika akiwa wa kwanza ni dereva alafu anafuatia mmiliki wa chombo kilichosababisha ajali, ikitokea mmiliki wa gari hilo ndiyo dereva basi atawajibika mwenyewe. Zipo aina mbili za kesi katika kudai malipo ya bima ambazo ni
1. Kesi ya kitrafiki( traffic case); aina hii ya kesi hufunguliwa na askari dhidi ya dereva aliyekuwa akiendesha gari wakati wa ajali.
2. Kesi ya madai ambapo mhanga wa ajali hufungua kesi ya madai mahakamani dhidi ya dereva kama mshitakiwa wa kwanza na mmiliki wa gari kama mshitakiwa namba mbili akidai fidia kutokana na madhara aliyoyapata. Baada ya mmiliki kushtakiwa anaweza kuiambia mahakama kwamba gari lake lilikuwa na bima hivyo anaomba kuuunganisha hiyo kampuni ya bima kwenye kesi na akikubaliwa kampuni ya bima itakuwa mshitakiwa namba tatu kwenye kesi. Ikiwa mdai atathibitisha madai yake na mahakama kumtia mmiliki hatiani basi ile pesa inakayoamriwa kulipwa na mmiliki italipwa na kampuni ya bima.

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUDAI MALIPO YA BIMA BAADA YA KUMPOTEZA NDUGU KWENYE AJALI
Katika kudai malipo ya fidia ya bima baada ya kumpoteza ndugu kwenye ajali mwenye jukumu la kudai hizo fidia ni msimamizi wa mirathi na siyo mtu yeyote yule, na ili mtu awe msimamizi wa mirathi kuna taratibu za kufuatwa kama ilivyoainishwa kupitia sheria ya Usimamizi wa Mirathi sura namba 352. Kwamba lazima awe ameteuliwa na ukoo baada ya kikao cha ukoo kufanyika, au kama ametajwa kwenye wosia ulioachwa na marehemu,

Msimamizi wa mirathi baada ya kuchaguliwa na ukoo au wosia anatakiwa kwenda mahakama ya mwanzo au mahakama kuu kuomba kuteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi na ikiwa hakuna pingamizi lolote juu ya kuteuliwa kwake basi mahakama itamteua kubwa msimamizi wa mirathi. Mahakama itatoa fomu za usimamizi wa mirathi Fomu namba IV na mwembaji ataambatanisha na fomu nyingine kisha kuendelea na utaratibu wa kuandika barua ya madai ili kuipeleka bima.

NAMNA YA KUANDIKA BARUA YA MADAI KWA AJILI YA KULIPWA FIDIA NA KAMPUNI YA BIMA BAADA YA KUMPOTEZA NDUGU KWENYE AJALI.
Wengi wetu hatujui barua ya madai huandikwaje hivyo kujiandikia tu pasipo kujua athari zake kwa kushindwa kuainisha aina ya madai. Katika barua ya madai, madai yamegawanyika katika makundi mawili ambazo ni
1. Gharama halisi ulizoingia kwa kugharamia msiba na ni lazima uambatanishe na risiti za gharama ulizotuma mfano gharama za jeneza, usafiri, sanda, viti, vyakula,. Katika kuandika aina hiii ya madai epuka kughushi nyaraka kwa lengo la kujipatia fedha.
2. Madai ya kumpoteza mpendwa wako; sehemu hii ni muhimu katika barua ya madai na inshauriwa ukiwa unaandika kumbuka yafuatayo
- kipato cha marehemu ikiwa marehemu alikuwa na kipato kikubwa basi atalipwa fidia kubwa na ni muhimu kuambatanisha uthibitisho wa kipato chake.
- Elimu ya marehemu ikiwa marehemu alikuwa na kiwango cha juu cha elimu basi atalipwa fidia kubwa na ni muhimu kuambatanisha vyeti vya elimu kama uthibitisho
- Umri wa marehemu
- wategemezi ikiwa marehemu ameacha wategemezi basi atalipwa fidia kubwa na inabidi kuonyesha uthibitisho wa wategemezi aliowaacha.

JE, KUNA USUMBUFU AU UBABAISHAJI KATIKA MALIPO YA BIMA BAADA YA KUMPOTEZA NDUGU KWENYE AJALI
Watu wengi katika jamii zetu wana mitazamo hasi kuhusu malipo ya bima kutokana na kile wanachodai kwamba kuna usumbufu na ubabaishaji au masharti mengi kwa upande wa bima. Ila ukweli ni kwamba hakuna usumbufu labda kama wadai wengi hawana elimu juu ya taratibu za kisheria za kudai malipo na nyaraka zipi inatakiwa kuwa nazo.

Kabla haujafika katika ofisi za bima kudai fidia inakupasa kufahamu nyaraka za muhimu ambazo hutolewa na mamalaka za serikali ambazo ni
a) fomu inayoonyesha matokeo ya kesi. PF115
b) fomu ya matibabu PF3
c) hati ya kifo
d)hati ya mazishi
e) Taarifa ya uchunguzi wa marehemu
f) hukumu ya kesi dhidi ya dereva aliyesababisha ajali
g) hati ya mashtaka ya dereva aliyesababisha ajali
h) fomu namba IV kutoka mahakamani inayokupa uhalali wa kuwa msimamizi wa mirathi
i) barua ya madai
J) fomu ya ukaguzi wa gari iliyosababisha ajali
k) kadi ya gari pamoja na PF90

Mara nyingi nyaraka hizi hupatikana polisi na hupelekwa kwenye kampuni ya bima ili wahanga waweze kufidiwa kutokana na ukubwa wa madhara waliyoyapata.

HITIMISHO
Kwenye madai ya kifo ya kumpoteza mpendwa wako kwenye ajali inakupasa kabla hujajipanga kwenda kwenye kampuni ya bima kudai kuelewa kwamba wewe huna mkataba na hiyo kampuni ya bima bali unadai kwa mjibu wa sheria kwa kutumia bima ya aliyesababisha ajali.

Ahsanteni 🙏 imeandaliwa na frolian M. matungwa (Mwanasheria)
 
umefanya vema bro nimeandika pia unaweza kupitia chapisho langu
 
Shukrani sana

Vipi kuhusu basi public transport kupata ajali (umeumia labda umevunjika mguu au mkono kwa ujumla utakuwa tegemezi shuguli zako zimesima au ulikuwa muajiriwa kazini ndo basi tena)
Taratibu ni hizo hizo au ni tofauti?
 
Procedure ni zile zile ila tofauti ni kwenye nyaraka utakazozipeleka bima. Hususan zile zinazohusiana na Fomu za usimamizi wa mirathi maana hapa hii procedure kwenye scenario uliyoisema hakuna kifo.

Pia hakutakuwepo na maombi ya kusimamia mirathi kwakuwa mhanga bado yupo hai.

Nazani umenielewa mkuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom